ndugu na jamaa wakijiandaa kuzika kwenye kaburi la nyota tano...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 30 mpaka sasa

  1. Mazishi kama hayo yakifanyika Bongo lazima watu wahakikishe kwamba kaburi linawekewa sege la nguvu, maana vibaka lazima warudi kufukua na kuondoka na vitu vilivyo ndani ya hilo kaburi!

    ReplyDelete
  2. NYOTA 5 !!!???? Mie sijaelewa labda mie ni mshamba naomba wenzangu mnieleweshe huyo nyota 5 nina ni nani? kaka michuzi nisaidie ujue blog yako yasomwa na waloerevuka na washamba, wasomi na walalahoi hebu nitoe tongo tongo mwenzangu, maana humu nimefaidika na mengi nitasikitika kama hili litanipita kaka.

    Ila akili nyingi huondoa maarifa!!! sasa hao wenzangu wanaamini huyo mtu atanyanyuka na kuangalia T.V. na kujipamba na kuvifanyia kazi vitu vyote walivyomuwekea??? Hiki ni kichekesho na hao ndo wanaosifiwa wana akili nyingiiii sasa akili zao huondoa maarifa matokeo ndo hayo wanatembea uchi, wanamzika mtu na T.V. na dressing Table haya wabongo na nyinyi igeni utaratibu huu maana sisi kwa kuiga tunaongoza, na mkifanya hivyo kila siku mtakuta maiti zenu zimefukuliwa, nawapa tahadhari.

    ReplyDelete
  3. who is this nyota Tano pls?

    ReplyDelete
  4. Nyie anony hapo juu, jamaa ana maana kama kulivyo na five star hotel (Hotel ya hadhi ya nyota tano)hili kaburi ni la hadhi ya five star vile vile!!!

    Ila kama ni kutafuta utofauti jamaa wamezidisha sasa! wameniudhi!!

    ReplyDelete
  5. Jamaa ana maana kama vile kulivyo na Hotel zenye hadhi ya nyota tano (Five star hotel), basi hili ni kaburi la five star rank!!

    Lakini hata kama ni kutafuta utofauti huu sasa ni ujinga!! Kuna watu wanaweza kuiga kweli bongo!!

    ReplyDelete
  6. kaazi kweli kweli hapo......naona jamaa wanaelekea kule kwa wa-Masri, Pharaoh akifariki basi mpaka vimwana wake na anatumbukizwa nao ndani ya piramidi lake.....kweli hujafa hujaumbika manake jamaa mpaka mvinyo wamemuwekea akitaka kupoza baada ya kuangalia tv kaburini!!!!!

    Michuzi, lete nondoz manake haya ndiyo mambo yenyewe haya baada ya uchovu wa siku mzima!!!!

    ReplyDelete
  7. Kaburi ni kaburi na mauti ni mauti tu hata ufanye na utakuta mtu huyo mwisho wake ni finarri jahannam fihaa.

    ReplyDelete
  8. Jenga hilo kaburi pale kinondoni uone labda wakati wa kusali msifunge macho hiyo plasma itatoweka. Hata hapo kuna ndugu wa marehemu wana tamani vitu hapo.

    Hizi kufuru sasa

    ReplyDelete
  9. kama alivyosema anony wa kwanza hapo juu nami namuunga mkono kwamba waswahili kwa kuiga hatujambo. igeni na hiyo sataili ya nyota 5 basi kama mnazo pesa? maana mswahili akiamua kuiga kuimba kama beyonce jinsi atakavyokuwa akiubinua huo mdomo kwa madiodo basi utadhani ni beyonce wa kweli (aliyepakwa kiwi).
    utawakuta wanafunzi wanashindwa kufuatilia masonmo shuleni ila kila waendapo utawakuta wamebeba vitafutali uchwara vilivyosheheni mashairi ya nyimbo za kizungu wakizikariri bila kuchoka ila ukiwaambia wakariri masomo aka!utachoka. hicho kiswaenglish watakachoongea utalia. sisi ni wepesei tu wa kukariri lakini hatuko creative na tutaendelea kuiga kila kitu cha mzungu mpaka tutakapokuwa wajinga kupindukia.

    ndimi Tpaul(Agent)
    naomba toa hoja.

    ReplyDelete
  10. KUFURU TU!... Kama walozikwa ki 5* wakaangalie pyramids za ma firauni wa Misri, leo hii maiti zao ni vivutio vya utalii tu. Ukishakufa ushakufa... hata uzikwe na jeneza la dhahabu, Mwili utaoza, utanuka na mafunza watatoka katika mwilini!

    Heri yao wanaozikwa kwa sanda!

    ReplyDelete
  11. What a waste?Watu can't afford a daily bread wengine wanarudisha hela ardhini,jamani?

    ReplyDelete
  12. Kaka Michu aaa aah!! Hao sasa wamekufuru, si bora tu wangeweka ka-TV kaelfu 50 angalau kuliko hizo za kisasa zitutoazo udenda!! Hata mimi naingia mshawasha wa kulifukua. Labda atafufuka awe anaangalia ze comedy, ila mawimbi ya tv hayataingia kaburini. Je Umeme watampa au... sijawai ona hii ndi mara ya kwanza, mdau J.

    ReplyDelete
  13. Five star grave sawaa...but the furnitures and other items?? why??? Hana ndugu waliobaki wa kuenzi mali zake hata kama wanazo nyingi? Au alikufa katika kutafuta izo vitu mpaka wameona it wont be fair wakimzika wakati hajavitumia?? Au wana ndugu wanaogopa watavigombania wacha aende navyo mwenyewe?? Kaka Michuzi assistance please

    ReplyDelete
  14. Huu ni ujinga wa mwisho kabisa ...

    ReplyDelete
  15. duh wamemuwekea kitanda na screen kubwa , utadhani kama ataamka vile, mambo mengine i dont c the point.

    ReplyDelete
  16. a..........aaaaaaaaaaa!i dont mind ufujaji wa hela kwenye hilo kaburi is their money anyway they can spend the way they like but who is nyota tano ?msichana au mvulana ?mtanzania au?maana hata simjui.

    ReplyDelete
  17. DUH! Sasa tuseme ndo marehemu atafufuka na kuanza kuishi mle kaburini kama vile alivyokuwa hai? Sasa hao waliozikwa kwenye nafasi ya kubana tight spaces, wanajisikiaje? Ni kupoteza hela kwa kweli, lakini kama marehemu alikuwa nazo mwache azifaidi hata kwenye kifo. Na kama jamaa alivyosema hapo juu waweke walinzi kwenye hiyo kaburi.

    ReplyDelete
  18. jamani hao watu wanaitwa magipsy au mazingara au chigana.hawa hawajulikani ni watu wa nchi gani.wanaishi mipakani mwa nchi za ulaya.wana pesa kuliko akili zao na ni wezi mwisho.wao shule sio muhimu na wala hawana nyumba,wanaishi ktk macaravan.kama wakichoka kuishi sehemu wanaamia kwingine.na mtu akifa wanafanya sherehe kubwa sana hasa akiwa mtu mzima.na mazishi yao ni kama hivyo.wanatumia pesa nyingi ktk mazishi kwa kununua vitu vipya vya kuweka kaburini na pia watu wanywe na kula.

    ReplyDelete
  19. Hivyo vitu vyote ni mali ya marehemu kwani kuna tamaduni nyingine za Mashariki ya Kati mtu akifa anazikwa na vitu vyake vyote. Aliyesema nyota tano amesherehesha tu.

    ReplyDelete
  20. Hiyo ni kufuru ya hali ya juu sana! Wanadamu sasa tunaelekea pabaya...! Lakini si la kushangaza sana maana hao wanaofanya hivyo ni wahindi. Wahindi wanaabudu miungu ya ajabu... Wanaabudu ng'ombe...Panya wanawaheshimu... So siwashangai kufanya kufuru ya namna hiyo. Wao wasubiri kwanza wala siyo kiyama... Shughuli itaanzia hapa duniani maana vibaka kwao hiyo tayari ni dili...! Ngoja walijue hilo kaburi lilipo... Mini wakiniletea hiyo Plasma ntainunua!

    ReplyDelete
  21. Dunia kula kukicha inakwenda mbele na maendeleo yake, nafurahi kuona watu wamekuwa wabunifu kwa kuleta kitu kipya, inafurahisha.
    Suala la kuiga, kupoteza pesa nk, nk, nadhani hiyo ni mitazamo ya kutoka mtu moja hadi mwingine. Kitu muhumu hapa ni ubunifu wa jambo ambalo ni tofauti na kabisa na tulivyozoea.
    Big up, Michu teremsha nondoz tuone vitu na ideas tofauti, labda nasi siku moja tunaweza kuja kuiga kuwa wabunifu maana wadau wengi wanasema wabongo ni waigizaji na sio waagizaji.

    ReplyDelete
  22. Hii ni kufuru kwa mwenyezi mungu na misuse of Limited Resources, Yaani kwa akili yao hao wanadhani ndio wamemtengenezea PEPO, Ha hebu wasubiri wiki walifungue waone watakuta nini ndani. Halafu vile vile ni kutudhalilisha sisi tusie na uwezo wa kupata hivyo vitu, maana yake "Anakushinda hata mfu analala pazuri", Takbiiiiiiiiiirr,

    Kila nafsi itaonja mauti na siku ya mwisho ataulizwa ewe mwanadamu dhalili nduguzo walikutengezea kaburi la nyota tano, ila leo napitisha hukumu yangu mara mbili. Hapo wanazidishia adhabu ya Kaburi, Baada ya kuja "malaika wa mauti peke yake, si kuna nafasi atakuja na wapambe wafanye shughuli yao kwa nafasi

    ReplyDelete
  23. kweli sie wa-tz ni wajinga sanaaaaaaaaa...hii picha am sure mi-supu umeitengeneza! ila kwa kuwa mi-bichwa yetu haifikiri basi tunaendaa tuu km ma-bata mizinga!!!...kuna mtu anazikwa na tv na kitanda cha kulalia? nyie watu wacheni upumbavu!!! na anzeni kufikiri eboh???

    ReplyDelete
  24. Jamani TUMIENI AKILI KIDOGO!!
    Hili ni pango alilokamatwa SADAM hussein.Hapo ni wakati wakiliandaa.Hamuoni ni waarabu tupu wamejaa hapo?Hakuna Mzungu hata mmoja hapo.

    ReplyDelete
  25. Anon hapo juu chukua Tano.
    Kwanza hao watu waliozunguka kaburi hawaonyeshi kama wanafagilia maziko ya namna hiyo. Hao jamaa mtu akifa asubuhi jioni wanazika..mda wa kutengeneza kaburi la zege wanapata wapi.

    ReplyDelete
  26. hii ni kufuru tu na roho ya ubinafsi, hata mimi nitasubiri tu wafiwa waondoke nichimbue nitoe ntakavyo halafu nifunuke kaburi nikitoe na plazima hilo. haklafu ukute watamvika marehemu juweris na saa bei mbaya. ujinga mtupu na ubinafsi.

    ReplyDelete
  27. Mazishi namna hii sio kufuru wala nini. WaTanzania wengi labda hamjui kuwa machifu wengi wa hapa bongo walizikwa namna hii, yaani na mali zao kama vile viti vya kifalme & vigoda, silaha aliyokuwa anatumia, nguo zao majoho yake ya wanyama, chombo cha kulia chakula, chanuo etc etc yaani all personal possesions. Afrika ya kusini hususan wa Nguni wafalme wao walizikwa wakiwa wamekalia viti vyao vya kifalme - Chaka Zulu na Lobengula wamezikwa hivyo hivyo.

    Hapa nyumbani pia kama sikosei Mirambo, Horombo na wengine pia walizikwa hivyo. Mtwa Munyigumba wa wahehe alizikwa hivyo hivyo - labda Mliakuvana atutolee mwanga kidogo kutueleza zaidi juu ya mazishi ya Munyigumba na machifu wa kihehe kabla yake.

    ReplyDelete
  28. Jamani hilo ni duka nyie, hammuoni huyo baba anayevuta sigara hapo anapokea pessa kutoka kwa huyo jamaa , jamaa kashanunua plazma hiyo, ohooo

    ReplyDelete
  29. MWANZO NILIPOONA MFUNIKO WA JENEZA PEMBENI NA SANAMU LA YESU NIKAAMINI NI KABURI, LAKINI MNGEACHA UZUZU WABONGO HUU NI MFANO TU WAMAHANDAKI YA IRAQ, HAWA NI WAKRISTO WA IRAQ WANAISHI CHINI KWA CHINI WAISLAMU WENYEWE KWA WENYEWE WANAMALIZANA WATASALIMIKA WAO,WAMECHOKA KUISHI KWENYE VUMBI WAME(REALIZE)VITA HAIISHI LEO,INABIDI KU UPGRADE LIVING CONDITIONS.HAPO ANALIPA PESA YA BATI LA MAWE,BILA KUSAHAU KUNUNUA KABISA JENEZA UNAWEKA NDANI KAMA VILE WENGI WETU TUNAVYO NUNUA SANDA TUKAWEKA NDANI HAIMAANISHI TUMEKUFA. true story

    ReplyDelete
  30. Mazingara;kama ilivyosemekana ni kabila la hao wafiwa hapo juu,ni wahamaji(nomads) waliotokea India na kuingia nchi za Ulaya mashariki mfn:Romani nk,miaka mingi sana iliyopita.
    Wana pesa sana lakini elimu na makazi ya hadhi hawana sababu ya uhamajihamaji wao.
    Si wizi tu bali ni wasomaji mikono,kuona mambo ya mbele.Na ni hata ombaomba na waiba/wauza watoto.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...