wadau leo nawatambulisha mdau mastablasta wa helsinki ambaye amefungua kurasa mpya wa kuchana mbavu kila siku kwenye globu hii ya jamii. ameahidi kila siku kuibuka na moja akianza na hiyo ya hapo chini...

Mwalimu wa darasa la kwanza akimuuliza swali mwanafunzi wake Juma.
Mwalimu: Juma tuambie ukiwa na shilingi mia tano na ukimuomba baba shilingi mia saba , jumla utakuwa na shilingi ngapi?
Juma: nitakuwa na shilingi mia tano.Mwalimu:
Jaribu kuhesabu tena, ukiwa na shilingi mia tano na ukimuomba baba shilingi mia saba , jumla utakuwa na shilingi ngapi?
Juma: Nitakuwa na shilingi mia tano.
Mwalimu: Juma naona wewe hujui hesabu.
Juma: Mwalimu naona humjui baba!
Mastablasta Helsinki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...