Jamani ehh, kuna mtu wa SUA anaitwa Dk. Misinzo alituambia mwezi uliopita ana defend PhD Thesis yake live kwenye internet. Hatukuweza kuiona live hiyo defense yake sisi wengine. Tunaomba atuambie tena nini matokeo ya defense yake. Pia kuna taarifa kwamba ame-patent kirusi cha Nguruwe. Je ni yeye ka-patent au ni University yake aliyosoma? Nani ana-own hiyo patent What next baada ya kupata patent ya hicho kirusi cha Kitimoto?
Tupe habari ili tuweze kumchomea mishikaki ya mahindiz.....

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa mdau aliyetaka kujua juu ya matokeo ya utetezi wa uzamivu (Ph.D. defence) yangu. Nilifaulu na kupewa hiyo Ph.D., Mungu/Molla apewe sifa. Siku ilifana sana. Napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru wale wote waliojumuika nami siku hiyo. Shukrani nyingi kwa watanzania wote waishio Ubelgiji waliofurika kwa wingi sana siku hiyo. Shukrani za kipekee kwa wale waliotokea Ujerumani kuja kunipa sapoti. Nilijisikia faraja na confidence ya juu pale nilipowaona watanzania. Shukrani pia kwa wale walioweza kuangalia defence kwa kupitia Video conference pale SUA au katika mtandao. Kwa wale wenye slow internet connection walioona kwa kutumia webcam ya skype. Nilidefend 26.11.2007, nilisafiri kuja Tanzania 28.11.2007. Nimemaliza likizo fupi mie na familia yangu. Nimeibuka leo na kuikuta hii post, asante Michuzi.
    Kuhusu patent, unaweza kusoma zaidi hapa: http://www.freepatentsonline.com/20070184544.html au gonga HAPA. Kwa ufupi, wagunduzi wa patent hii ni 1. bosi wangu Nauwynck, Hans (Zomergem, BE), 2. mie kama mwanasayansi niliyefanya kazi na kugundua Misinzo, Gerald (Sengerema, TZ) na 3. afisa haki miliki wa kitivo Arnouts, Sven (Bertem, BE). Patent tumeiuza kwa kampuni moja ya kutengeneza chanjo, nastahili asilimia 25 ya mauzo.
    Hivi karibuni ntapandisha kitabu changu cha thesis ili wenye nia ya kuisoma wasome. Michuzi soma Acknowledgements, nimekushukuru kwa blogu yako maridhawa iliyokuwa ikinipa nguvu kila mara nilipoona nipumzishe akili. Watakaohitaji CD ya thesis waniandikie.
    Naomba kuwasilisha.

    ReplyDelete
  2. Wewe Misinzo ulipita pale Kibaha SEcondary? Nafikiri ulinitangulia mwaka mmoja. Ulikuwa CBA pale na Kina Ibrahimu Mahumi?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...