Mchezaji , Mohamed Mkangara wa timu ya wanaume ya kuvuta kamba ya Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo (HUM) ( wa kwanza mbele kushoto) akiwaongoza wenzake kuwavuta wachezaji wa timu ya Bunge katika uwanja wa Jamhauri wa mjini hapa ambao Bunge ilishinda kwa duru 2-1 na kuiondoa Habari kuendelea hatua ya nusu fainali ya mashindano hayo ya SHIMIWI.
Picha na habari na John Nditi,

Morogoro

TIMU 16 za kuvuta kamba za wanaume na nyingine za wanawake kutoka Wizara na Idara Serikali katika mashindano ya shimiwi zimefanikiwa kuingia hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo yanayofanyika Mkoani Morogoro.

Timu hizo zilizofanikiwa kuingia hatua ya nusu faunali baada ya kuzitoa timu pindani katika michezo uliyofanyika jana ( Okt 31) katika uwanja wa Jamhuri wa mjini hapa.

Katika michuano hiyo, timu nane za kila upende zilifanikiwa kusonga mbele kufuatia mchuano mkali ulioonyeshwa na washiriki wa timu hizo.

Kwa upande wa wanaume timu zilizofanikiwa kusonga mbele ni Maendeleo ya Jamii kwa kuwafunga Makamu wa Rais, Ofisi ya Waziri Mkuu kuifunga Ukaguzi na Hazina kupata ushindi dhidi ya Sayansi.

Timu nyingine ziliofanikiwa kusonga mbele katika hatua ya nusu finali ni Bunge kwa kuifunga Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo, Wizara ya Kilimo kwa kuifunga Haki za Binadamu, Mahakama kuwafunga Mambo ya Nje, Afya kuibuka na ushindi dhidi ya Viwanda na Ikulu kupata ushsindi mbele ya Tume ya Mipango.

Kwa upande wa timu za wanawake, Miundombuinu iliweza kupata ushindi dhidi ya RAS Mkoa wa Shinyanga, Ofisi ya Waziri Mkuu kuibuka washindi mbele ya RAS Mkoa wa Ruvuma na Bunge kuweza kuifunga Wizara ya Habari.

Timu nyingine kwa upande wa kuvuta kamba wanawake zilizofanikiwa kusonga mbele ni Hazina kwa kuifunga Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia , Mambo ya ndani kuifuga Elimu na Mahakama kupata ushindi mbele ya RAS Mkoa wa Iringa.

Nyingine zilizofanikiwa kusonga mbele katika hatua ya nusu fainali ni pamoja na RAS Mkoa wa Dodoma kwa kuwafunga wenzao wa RAS Mkoa wa Arusha na Ikulu kuweza kuwafunga Tume ya Mipango.

Wakati huo huo, timu riadha na kupokezana vijiti ya RAS Mkoa wa Arusha imeweza kuambulia nafasi ya tatu kwa wanariadha wake kunyakua media saba za shaba katika mashindano ya mbio za umbali wa mita mbalimbali.

Katika mbio za mita 200 na 100 mwanariadha Anna Ombay aliweza kutwaa medali mbili za shaba, ambapo kundi la wanariadha wazee , timu hiyo ilipata medali moja ya shaba kutoka kwa mkimbiaji wake, Gerald Mainda kushinda mbio hizo.

Akizungumza na Mwaandishi wa habari hizi jana ( Okt 31) mjini hapa, Katibu wa timu hiyo, Flora Assey na Mwenyekiti wake Edimund Kamala, kwa nyakati tofauti walisema ushindi huo ni wakujivunia kwa vila hivyo ni mara ya pili kwa Mkoa huo kushiriki mashindano hayo ya SHIMIWI.

Kwa mujibu wa Katibu wa timu ya RAS ya Mkoa huo, aliwataja washindi wa medai hizo kwa upande wa mbio za mita 400 kupokezana vijiti kwa wanaume ni Daudi Mwakatobe, Godfrey Munis, Sixbert Hangoli na Tumain Julius.

Hata hivyo alisema RAS Mkoa huo unatarajia kupata ushindi katika michezo mingine ya jadi ya Karata na Draft ambayo ilitarajiwa kuanza jana ( Nov mosi) mwaka huu .

Alisema timu ya Mkoa huo imepata mafanikio makubwa kwa mwama huu tofauti na mwaka jana ambapo ilikuwa ni wageni wa mashindano hayo ya Shimiwi.

“ kusema kweli mwaka huu tumepata maendeleo makubwa tofauti na mwaka jana licha ya kufanya vizuri lakini ugeni wa michezo hii ilichangia tusiweza kuonyesha uwezo wetu” alisema Assey

Hivyo alisema watajiandaa vyema katika michezo ya mwaka ujao ili kuweza kutoa upinzani na kushinda michezo mbalimbali waliyoshiriki mwaka huu ikiwemo ya soka na netibali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. jamani kaka michuzi mimi nipo mbali huku ughaibuni na dada yangu sasa hivi yupo morogoro naye yupo kweye timu ya kuvuta kamba ya wanawake ikulu please ukifanikiwa kupata picha za timu hiyo wakiwa wanavuta kamba naomba uiweke i'll be so happy mungu akubariki

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...