MWENYEKITI WA JUMUIYA YA WATANZANIA TAMIL NADU AKIWASILISHA HOTUBA YAKE MARA BAADA YA UCHAGUZI ULIOMUWEKA MADARAKANI.

WATANZANIA WA TAMIL NADU WANA FURAHA KUWATANGAZIA UZINDUZI WA JUMUIYA YA WATANZANIA KATIKA JIMBO LA TAMIL NADU, INDIA, ULIOFANYIKA TAREHE 26 DISEMBA 2008.
MGENI RASMI KATIKA UZINDUZI HUO ALIKUWA BALOZI WA TANZANIA NCHINI INDIA, MH. JOHN KIJAZI.
UZINDUZI HUO ULITANGULIWA NA KONGAMANO LILILOJADILI UMUHIMU WA KUZINDULIWA KWA JUMUIYA, NA KUPITISHA KWA AZIMIO MOJA KUUNDA JUMUIYA HIYO KWA KATIBA ILIYOJADILIWA NA KUKUBALIWA NA WOTE.BAADA YA KONGAMANO HILO LA SIKU NZIMA, WATANZANIA WALIPATA NAFASI YA KUJUMUIKA PAMOJA KWA CHAKULA CHA JIONI KILICHOANDALIWA KWA HESHIMA YA NCHI YETU KWENYE HOTELI YA ARUNA, CHENNAI.
TUNAWASHUKURU WOTE WALIOCHANGIA HALI NA MALI KUFANIKISHA UZINDUZI HUU.TUNAWAKARIBISHA WATANZANIA WOTE NDANI YA JIMBO LA TAMIL NADU, AMBAO HATUNA MAWASILIANO NAO WAFANYE HIMA KUWASILIANA NASI KUPITIA:
WENU KATIKA UJENZI WA TAIFA,
MKURUGENZI WA MAWASILIANO

WASHIRIKI WA KONGAMANO KWENYE PICHA YA PAMOJA BAADA YA CHAKULA CHA JIONI

WASHIRIKI WA KONGAMANO LA WATANZANIA TAMIL NADU KATIKA PICHA YA PAMOJA NA BALOZI


WATANZANIA WA TAMIL NADU WAKATI WA CHAKULA CHA JIONI




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Hongereni. Nakuona Bwn Ndima! Piga kitabu.

    ReplyDelete
  2. Nasikia hao ndugu zetu wa Tamili nadu (yaani watu wa asili kule) rangi yao ya ngozi inafanana na mmatumbi na mdengeleko wa hapo kwetu...kwa hiyo wabongo huko hamta pata taabu ya kubaguliwa wanazopa wabongo katika sehemu nyingi ulimwenguni!!!hata kule kwa ibilisi mkubwa nasikia maniga pia yanawadharau wabeba maboksi ya kiafrika!!!

    ReplyDelete
  3. Hi!! Your blog are very nice and more info. I hope follow my blog and please click my google ads.

    ReplyDelete
  4. duh naona wanatamil-tz ss mpo poa,kuna watu wangu siwaoni hapo,akina freddy,the Rock,aron,amonson,,...MMH Najua Morin hawezi kumiss,namuona hayupo nyuma nae,nakuona mzee deus minywele,komaa na barozi hapo akuachie hata buk la kuwezesha co-oparaxn...mzee salah alikuwepo?au alikkuwa kwenye night part?....mbona madem wa ooty siwaoni,Erode kuna watz pale nao siwaoni au hawakutoa mchango....BGUP SANA WAZEE.

    ReplyDelete
  5. naja CHENNAI,ntawatafuta adi ubalozini kwetu Tanzania
    TAMIL NADU=TAMIL TIGER??????just curiosity

    ReplyDelete
  6. haya ndio yanayokubalika kwa walio nje ya tanzania jumuia za WATANZANIA. watanzania wanajiweka pamoja bila na kusaidiana bila kujali rangi dini wala siasa, sio ufunguzi wa matawi ya ccm amabayo kwa upande mmoja ni kama kuwagawa wengine. ukiwa sio mwana ccm huwezi kuhudhuria vikao vyao nk

    ReplyDelete
  7. Hahaaa sina mbavu...jumuiya nyingine..Watanzania wa nje kweli mmeishiwa...hivi nyie hamjifunzi kwa wenzenu wa nchi hizo. Jumuiya hizi ni kupiga siasa tu...hakuna utendaji wowote humo.

    ReplyDelete
  8. Hongera Deus kwa kuchaguliwa Mwenyekiti wa watanzania.

    ReplyDelete
  9. Nilikuwa nina kiji swali kimoja. Mda wa mtu nje ya Tanzania ni pesa sana. J
    e, kuna faida gani kiuchumi ya kuhudhuria mikutano kama hii, iwe ya CCM au Jumuiya? Naweza kusaidiwa nikibanwa kifedha? au ni kula kababu na kupiga story za home?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...