Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda (pili shoto) akitazama uyayushaji wa vyuma katika karakana ya Shirika la Nyumbu (TATC) mkoani Pwani wakati alipotembelea shirika hilo leo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Wapi safety precautions (protective gears)?. Ninajua kuwa wanajua melting point ya steel ni more than 1370 degrees of celcius, which means any blust there none will survive the melting Iron.

    Wangempatia miwani, helemet na hata boots waziri mkuu. Hii kitu lazima sasa itungiwe sheria mambo ya kazi ya mungu sasa tuyaache.

    Hao wafanyakazi wanakuwa exposed kwenye very high toxic and dangerous environment hivi ni vitu vinavyochangia wastani wa maisha kwa watanzania kushuka.

    ReplyDelete
  2. Maendeleo ya kiviwanda na hasa viwanda vizito au viwanda mama (heavy industries) ya nchi yeyote yako katika utumiaji na ukuzaji wa teknolojia ya kufua chuma hadi kuwa steel. Hivi Tanzania ingekuwa wapi kimaendeleo kama teknolojia ingepewa kipaumbele kama alivyofanya Mwalimu Nyerere. Bila shaka tungekuwa tunatengeza magari yetu wenyewe, na vitu vinginevyo vinavyohusiana na ujenzi na kilimo vitokanavyo chuma. orodha ni ndefu. Hongera sana Waziri Mkuu kwa kuyaona haya.
    Hebu fikiria kiwanda cha kuunganisha redio za National kama kingeendelezwa bila shaka tungekuwa tunaunganisha kompyuta na television kama si kuzitengeneza sisi wenye. Kiwanda cha UFI, Kiwanda cha BORA naamini NIKE ingekuwa inatengenezwa hapo DAR. Viwanda vya nguo bila shaka vingekuwa katika ustawi wa hali ya juu na kuwavutia wawekezaji wa kigeni kama ilivyo kwa India, Bangladesh au Mauritius. Viwanda ni vingi na orodha ni ndefu.
    Naamini mapinduzi ya kilimo yaliyoanzishwa tena na serikali ya awamu ya nne yatakwenda sambamba na mapinduzi mengine ya kuvihuisha tena viwanda. Kwa kufanya hivyo tutaweza kufanikiwa kuutokomeza umaskini na pia kuikomboa nchi yetu kiuchumi kwani bado tuko katika mfumo wa uchumi wa kikoloni (Colonial Economy).

    ReplyDelete
  3. Hawa jamaa bado wanatengeneza nyumbu?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...