Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Sekondari Lupanga ya Manispaa ya Morogoro wakiwa nje na madarasa yao jana ( Machi 23) wakiendelea na mgomo wa kutoingia madarasani wakisulutisha kwanza walimu watano wa kiume wa shule hiyo waliokubuhu kwa vitendo vya ngono na baadhi ya wanafunzi wa kike wa waadhibiwe kwanza.

Mkuu wa Shule ya Sekondari Lupanga ya Manispaa ya Morogoro, Pascal Mlimbo, akielezea jambo kwa waandishi wa habari ( hawapo pichani) leo ofisini kwake kufuatilia sakata la wanafunzi wa shule hiyo waliogoma kuingia madarasani kwa madai ya kuwatuhumu baadhi ya walimu wao wakiume kufanya ngono zilizokubuhu na baadhi ya wanafunzi wa kike. Ili kurejesha amani Mwalimu Mkuu huyu ameamuru ipigwe kura ya siri ya maoni kabla bodui ya shule haijajua ifanye nini. Picha zote na mdau wa mji kasoro bahari John Nditi


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. hahahahahahah Bongo kweli mambo safi yaani kuna migomo hata ya mapenzi na walimu mashuleni, huku hotel zinaungua , Hhuku walimua wanafanya mapenzi na wanafunzi mmmh Tanzaniaa-Tanzaniaaa yangu

    ReplyDelete
  2. Bora mmeamua kugoma, nadhani siku hizi fisadi wa aina yoyote (haijalishi ni fisadi wa ngono au wa EPA) inabidi atumie akili kweli ili kufanikisha ufisadi wake!!! Endeleeni kuwaumbuaaa

    ReplyDelete
  3. I just love this..watoto mmenifurahisha...naomba shule zote za sekondari na hata primary ziige mfano huu..nategemea kusikia migomo zaidi..wamezidi hao kutuharibia watoto wetu badala ya kuwa wakufunzi wanakuwa waasi mafisadi wakubwa hao...tunataka majina yao hadharani ili wasije wakaajiriwa na mtu mwingine kwenye shule yoyote..!!

    ReplyDelete
  4. Kura hapo za nini tena? mwalimu mkuu atakuwa basi na hizo Tabia kama akiwapa nguvu walimu wenzake, Lazima iwekwe kikao zitizamwe sheria gani wamevunja hao walimu wachukuliwe hatuwa na wanafunzi waliofanya hivyo waulizwe maswali na Polisi ndio wajue nini kifanywe Tatizo kubwa lipo pia kwa hao wanafunzi sababu wakisema hakujatokea kitu hicho itakuwa ngumu. lakini kama tukio limetokea wamelazimishwa kwa nguvu yani hapo bila mjadala mahakamani sheria ichukuliwe wapigwe fine yan guvu na ndani. Musa.

    ReplyDelete
  5. Hawa wanafunzi wanaleta mapinduzi mazuri katika elimu. Walemiu wengi wa kiume hupenda kunyanyasa wanafunzi wa kike na kuwafelisha makusudi kama hawatoachia. Rushwa_ngono inatakiwa iishe. Haimkomboi mwanamke kielimu kujamiiana na kupewa maksi za bure au kupata vijisamaha vya kutodeki darasa au adhabu za kuchelewa.

    Mwacheni binti ajitahidi masomoni na asidiwe kimasomo bila masharti ya ngono. Na apewe usawa katika mafanikio (kufaulu) na maanguko (adhabu).

    Msichana asionekane kama kiumbe kutoka Venus bali wa hapa na jamii inahitaji mchango wake wa hali na mali.

    MVULANA NA MSICHANA WOOTE WANA HAKI SAWA KWA MOLA.

    ReplyDelete
  6. Duuuu kazi kwelikweli,tunasubiri majina yao!

    ReplyDelete
  7. Hiyo kura ya siri nani atakayeisoma? Si ajabu huyo mwalimu mkuu mwenyewe anahusika somehow...iundwe tume ambayo ni independent...hii mambo zenu za Kesi ya nyani kumpelekea tumbili mnatoa wapi? acheni uhuni...na nataka hao watoto wasije wakahojiwa kabisa na mtu yeyote ambaye anafanyakazi hapo. Si kuna Wakaguzi wa Shule..ndo wafuatilie hilo...!!

    ReplyDelete
  8. Go Girls go, ni kweli baadhi ya walimu wa kiume wamekubuhu kubaka watoto wa kike, huu ni mfano wa shule moja ila ziko zaidi ya hii. Watoto wasikilizwe wana mengi ya kuileleza jamii. Mgomo wao ni halali na wanadai haki yao ya msingi. Hawa ni watoto wa kuigwa katika jamii. go Girls go

    ReplyDelete
  9. Huyu mwalimu mkuu nae..sasa hapo kura za nini...au iundwe tume ya nini...kitu simple...polisi wachukue statements kutoka kwa wanafunzi wanaodai kufanya ngono na hao walimu...na wahusika kukamatwa, kesi kupelekwa mahakamani..end of story....anadai kura zipigwe wakati watuhumiwa wanajichimbia. Safi sana wanafunzi kazaneni hivyo hivyo mpaka kieleweke..

    ReplyDelete
  10. Jamani Tanzania tumepiga hatua, tena hawa ni wanafunzi wa kijijini......well done girls!!! Give these teachers run for there money!!! wamalizeni kabisa, hivi ni vitendo vibaya ambavyo vimeendelea kwa muda sasa Tanzania, its about time zitokomezwe. Bravo Girls Bravo!!!

    ReplyDelete
  11. TAMWA wanasemaje?

    ReplyDelete
  12. Mojawapo ya faida ya uhuru wa kugoma ndiyo hii ya kukataa kudhulumiwa kwa sababu tu ya maumbile na tamaa za wasio na uwezo wa kujizuia. Kila wakiiona sketi miili inawachemka sababu ya kukumbatia pepo la ngono!

    ReplyDelete
  13. Serikali haioni hii mpaka wanafunzi wenywe wameona wajioko...where is our govt? inahalalisha haya mambo kweli....?????????

    We need to pray for our little gals ...they sure want to live and see their kids growing up too....Wamechoshwa na maukimwi kuambukizwa na walimu

    ReplyDelete
  14. What a shame! Hadi kufikia hatua ya wanafunzi kugoma ina maana hata mkuu wa shule naye yumo, awe wa kwanza kujiuzulu. Hivi ni lini watanzania tutathamini kazi zetu na kuwajibika pale inapobidi kufanya hivyo?! Naomba jina la kiongozi wa mgomo huu kwani anastahili pongezi na zawadi (Mama Kikwete take action)!

    ReplyDelete
  15. Aisee hawa watoto wasichana ni wanamapinduzi na mashujaa,Kitendo walichokionyesha ni ushahidi kwamba sio watu wakuchezewa.Naomba TAMWA mkawaunge mkono hawa watoto wasije wakaishia kutandikwa viboko ili kuziba madhambi ya walimu. Sasa na wewe mkuu wa shule Pascal Mlimbo watoto wameshakuanikia maovu unachelewa nini kuchukua hatua zinazohitajika??

    ReplyDelete
  16. Hivi serikali na hata bunge liko wapi kutoa hata statement ya kusashifu vitendo hivyo? Wizara ya Elimu haisemi chochote ni kwasababu gani? Wako wapi watu ambao kisheria walipaswa kutoa statements kuhusu tukio hili? Katika hii kesi, Mkuu wa Shule ni Mtuhumiwa pia..yeye atafanyaje utafiti? Hii ni jinsi ya kuficha ukweli na tunaitaka serikali iingilie kati...sisi si ndio tumewaajiri? Wao ni watumishi wa Umma si wanakaa kimya na mambo kama haya...lazima watoke kauli haraka iwezekanavyo. "KESI YA NYANI TUSIMPELEKEE TUMBILI" NARUDIA TENA HILI JAMANI...!!Halafu vyombo vya habari vimekaa kimya havilipi tukio hili uzito linaostahili...!! Haya ndo mambo ambayo waandishi wetu wanapaswa kuyafanyia "independent investigation" kwavile at times hatuna uhakika kama hata upelelezi utafanyika wa haki...ninyi waandishi wa habari..mmoja alivalie njuga suala hili tunataka kujua mwisho wake..!!

    ReplyDelete
  17. Huyu mwalimu mkuu mbona yanki,handsome na bado anaonekana yupo enegertic.Usikute na yeye anashiriki katika kuibanjua hiyo "amri ya 6" na hao watoto.Sasa hapo najua yupo roho juu kwenye hizo kura za maoni zinazopigwa.

    Mkulima-kijijini Gezaulole.

    ReplyDelete
  18. Nyie mnaosema polisi wachukue statements angalieni sana.Tatizo la Bongo ni kwamba the whole system is corrupt.Hao polisi hawawezi kuchukua hizo statements hadharani,kwa usalama wa hao watoto,ni lazima wawaweke kwenye usiri ndipo wachukue hizo statements.Huko kwenye privacy nako,hao polisi nao wanaweza wakawatongoza vile vile,ha ha ha ha ha ha ha haha!

    Huyo mngine anaesema TAMWA wakowapi kwa kweli sijui nimsaidiaje.Unakumbuka yule Bosi wa TAMWA (Leila Shekhe) alivyoacha kazi TAMWA akaenda TACAIDS.Akanyanyaswa kijinsia na bosi wake MAJ.GEN HERMAN LUPOGO,alipoenda kushtaki kwa DAP,DAP akamjibu,aaaaaaaaaah,na wewe umezidi kuwa mzuri bwana,hebu ondoka hapa!!ha ha ha ha ha ha ha haha.Bongo tambarareeeeee!!

    mkulima-kijijini Gezaulole.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...