VIONGOZI WA DECI WAKIWA MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI KISUTU LEO, WAKIKABILIWA NA MASHTAKA MAWILI.
1. KUENDESHA NA KUSIMAMIA MRADI WA UPATU
2. KUPOKEA AMANA KUTOKA KWA UMMA BILA LESENI
DHAMANA YAO IKO WAZI HADI TUNAINGIA MITAMBONI WALIKUWA BADO SELO MAHAKAMANI KISUTU.
HABARI KAMILI
VIONGOZI watano wa Deci wamepandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar, wakikabiliwa na mashtaka mawili.
Viongozi hao walipamdishwa ni Jackson Mtalesi, Dominic Kigendi, Timotheo Saiguran Ole Loitg’nye, Samwel Mtares na Arbogast Kipilimba.
Baada ya kupandishwa kizimbani, walisomewa mashtaka yanayowakabili, ambapo katika shtaka la kwanza wanakabiliwa na tuhuma za kuendesha na kusimamia mradi wa upatu.
Katika shtaka hilo washtakiwa hao wanadaiwa kwamba kati ya mwaka 2007 na Machi, 2009 katika makao makuu ya Taasisi hiyo, pamoja na maeneo mengine ya nchi walisimamia na kuendesha mradi wa upatu kwa kukusanya fedha kutoka kwa umma, kwa ahadi ya kuwapa matumaini ya kumiliki fedha zaidi, ambazo katika mazingira ya kibiashara ilikuwa ni kubwaa kuliko mtaji.
Shitaka la pili ni la kupokea amana kutoka kwa umma bila leseni. Wanadaiwa kuwa katika kipindi cha mwaka 2007 na Machi, 2009 wakiwa katika ofisi za taasisi hiyo na maeneo mengine nchini, walipokea amana kutoka kwa umma bila leseni.
Hata hivyo, walikana kuhusika na mashtaka hayo waliyosomewa, ambapo walipelekwa mahabusu baada ya upande wa mashtaka katika kesi hiyo kuiomba mahakama kutotoa mashari ya dhamana kwa sasa kwa madai kuwa Mpelelezi Mkuu wa kesi hiyo aliomba hivyo.
Kesi hiyo iliahirishwa hadi Juni 17, mwaka huu itakapotajwa mahakama hapo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 12, 2009

    Hapo ndio kipimo cha upendo kaka

    Mdau.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 12, 2009

    Dunia imeisha kweli Watu wa Mungu wanapelekwa Mahakamani!!!!, sijui niamini mchungaji gani!!!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 12, 2009

    Ndugu Anon 12 june 3:50 sikuelewi una maana gani kuwa hapo ndiyo kipimo cha upendo?

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 12, 2009

    kaka hao watani zetu matepeli sana hawana utu sasa si hela zipo watulipe sasa watz ilitumalize ugomvi wezi hao.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 12, 2009

    Noma Kweli Huchelewi Kufunguwa BLOG ukamuona Mzazi wako Kwenye Benchi la Mahakama Mbona suuuuuuu. Baba Zao watu jamani. mtaumiza familia zenu kama hamna kosam ungu atawasaidia kama mnalo kosam ungu pia atawasaidia mbadilike sasa sio freshi ufisadi jamani. Kiminyio.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 12, 2009

    Nawauliza wanasheria mlioko kwenye globu hii hivi itakuwaje sasa tuliopanda tutapata pesa zetu?
    Nionavyo ndio basi tena mpaka mahakama itoe uamauzi nishaurini wandugu!!1

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 13, 2009

    Hapo waliopanda mbegu ndio wameshalipwa tayari, waondoe matumaini. Kesi itaenda maana siamini kama hawakuwa na leseni maana ndio naona kosa la msingi. Lakini sheria inasemaje kutokuwa na leseni ufungwe miaka kumi? Sidhani.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 13, 2009

    jamani tafadhalini tusi wajaji hao watu kabla ya kesi. hatujui kama hawa watu wana makosa au la. hawa ni watu wa mungu na kazi yao haina makosa. kama hawa watu wametenda mabaya ni lazima tuwa samehe kwasababu ya kazi yao muhimu walio pewa na mungu.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 13, 2009

    Wakuu tunaomba data:
    1: DECI ilikuwa na kiasi gani cha pesa kwenye akaunti yake?

    2: Pesa hizo zipo benki gani?

    3: DECI ilisajiliwa kivipi?

    4: Hatima ya pesa za DECI nini? Wawekezaji watarudishiwa au pesa zitakuwa "frozen"?

    5: Sababu zilizoifanya serikali kuikamata DECI baada ya miaka ya huduma zilikuwa zipi?

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 13, 2009

    afu ubane hii...

    naongeza
    1.ao waliokuwa wanachukua fweza na kununulia dividends je??
    2.miaka 3 inaendeshwa,mlikua mwataka adi kiweje?nahisi harufu ya kutafuta umaarufu na kupoteza mwelekeo wa EPAzzz zile.
    3.kwa kosa gani aswa watumishi wa watu?
    4.watu sii waliweka kwa hiari yao tu bila kutojua kwao/kupembua pumba na mchele?
    5.kuna watu na visa na visilani kukomoa wezao?

    mshindwe ktk jina la Mola

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 13, 2009

    yani wamewafunga wazee hawa mahabusu bila dhamana??

    kwa lipi aswa???

    haki ya nani kuna uonevu wa hali ya juu sana,ivi kesi zile NZITO zimefikia wapi?

    ngojeni

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 13, 2009

    Waendeshaji wa DECI wamefanya utapeli gani kwa wanachama wao? Sidhani kama ni vema kuwatia hatiani kwa kisingizio cha utapeli, litafutwe kosa lingine nje ya "UTAPELI KWA WANACHAMA" Hakuna mtu aliyelalamika kutapeliwa na watu hao ni hisia tu kuwa LABDA baadae kuna mtu angetapeliwa (kwa kisingizio cha uzoefu)Mpaka sasa TAPELI katika hisia zangu ni yule aliyezuia pesa za wanachama ambazo wengi wao wameathirika kwa kuzuiwa na siyo kwa kutapeliwa. Kwangu mimi hilo ni ZENGWE tu ili maskini azidi kuwa maskini na tajiri azidi kumkandamiza maskini

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 16, 2009

    sitaki kuamini...uonevu huu

    anyway tutafikiana tu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...