mawazo yanazidi kubaribishwa juu ya namna ya kupunguza ama kuondoa raha hii ya foleni dar

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 29 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 29, 2009

    sii mchezo,ndipo ninapochoka kuja dar

    hakuna ahueni wether gari yako au daladala

    roads toka ukoloni?????

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 29, 2009

    Foleni ina raha zake, maana kila siku tunachelewa kurudi nyumbani kwa kisingizio cha foleni

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 29, 2009

    Nafikiri kuwepo kwa taa za kuongoza magari kwenye hii "round about".

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 29, 2009

    solution ni congestion charge tu!

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 29, 2009

    Dawa ni kuhama tuuu.... Ndio mtajua kwa nini wengine tulianza zetu kiwanja tangu 90s. Sababu we predict this crap, and we knew we couldn't take it... So, if your disappointed njoo zako kwenye lane 8 kwenda 8 kurudi... easy. Hakuna Fisadi wa kisadi....

    Karibu America.

    And I'm proud to be an American Where at least I know I'm free
    And I won't forget the men who died
    Who gave that right to me
    And I gladly stand up
    next to you and defend her still today
    cause there ain't no doubt I love this land

    God bless the USA

    Mdau wa Dallas

    ReplyDelete
  6. Kosa la viongozi wa Tanzania ni kutumia uchumi tegemezi ambapo sera zinapelekea watu wote kuhamia Dar.

    Kwa hiyo chanzo cha matatizo ya msongamano hapo Dar ni hicho.Kuondosha kero hili ni lazima sera nzima ya uchumi ibadilike, aliezaliwa Tabora na mikoa mengine ajengewe mazingira ya kuweza kusoma, kufanya kazi, kupata matibabu na mambo yote ya lazima ili aweze kuishi huko Tabora bila ya kuwa na umuhimu wa kuhamia Dar.

    Kama watu wote wa Tanzania hawataweza kuishi mikoa mengine, msongamano huo utaendelea hapo Dar.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 29, 2009

    kwanza kabisa wenye magari wajifunze proper driving nikimaanisha kujua uendeshaji na sheria za barabarani, maana Tanzania hakuna sheria za barabarani kila mtu anayewza kushika usukani na kukanyaga accelerator anaingia barabarani matokeo yake ni vurugu mechi barabarani.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 29, 2009

    Hapo mie ningekuwa na KIbajaji nakatiza Kati kati tu Shwaaaaaaaaaaaaaaa hahahahaha!.

    ReplyDelete
  9. Al MusomaJune 29, 2009

    Hiyo raha ya foleni ililetwa na msomi au wasomi walioamua kuifanya Samora One Way

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 29, 2009

    Ofisi zote za Serikali hamishia Dodoma ili shughuli zipungue hapo katikati ya Jiji, vinginevyo hiyo miradi ya eti magari yaendayo kasi ni ulaji wa fedha tu. Hayo magari yaendayo kasi yatapita hewani!!!!

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 29, 2009

    tatizo la foleni Dar City Centre, si rahisi ku-solve in isolation. Wazee wa jiji, sijui hata kama wanafanya assessment baada ya kuchukua measures fulani fulani hapo jijini e.g checking of travel time during peak hours,
    1.Origin Destination study zinatakiwa kufanyika hapo jijini
    2.Revie ya junctions zile ambazo ni critical kwenye network inabidi zifanywe kuangalia capacities
    3.Zuia all unnecessary Right turns which are close to the critical junctions analysed

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 29, 2009

    hii picha nzuri na mada ambayo inahitaji kujadiliwa kwa kina hasa katika kiwango cha serikali ya dar na serikali kuu. ninaishi nje ya nchi na ugonjwa wangu mkubwa ni homesick. lakini kila nikitua dar kero ya foleni (kupoteza saa 3 hadi 4 kila siku ndani ya foleni)hunitamanisha kurejea kwenye ukimbizi wangu!! juzi nilikuwa dar na nilipambana na kero hiyo kila siku. ukionyesha kushangaa, wabongo wanakushangaa kwa kushangaa!!! hilo nalo ni tatizo. pamoja na katikati ya jiji KERO BAKUBWA iko pale ubungo makutano ya barabara ya morogoro road na barabara ya mandela road. izingatiwe kwamba hii ndio njia kuu ya kutokea na kuingilia katika jiji kutoka mikoani na wakati huo huo inatumiwa na wenyeji. inatisha. pale ni sindimba!!!serikali haijalipa kipaumbele suala la msongamano wa magari jijini dar. linahitaji mkakati maalumu, ikiwezekana iundwe idara ama kitengo maalum katika wizara ya miundombinu kushughulikia tatizo hili. kupanga ni kuchagua alisema jkn.

    ReplyDelete
  13. Tatizo ni kwamba mtume athaaminiki kwao.
    Tumetowa wasomi wa ardhi wangapi tokea tupate uhuru ?
    Hakuna cha ajabu chochote kuhusu plani za miji.
    Wewe unadhani tungepanga plani nzuri za kutumia wasomi wa ndani ya nchi kubuni mbinu za miji mipya bora hili swala lingekuwepo?
    Kila mtu anataka kwenda Posta mpya kuna nini kule?Si kwasababu plani ya mji ni mbovu.
    Tanzania inawasomi wengi na kama hatutawatumia basi nchi nyingie zitanufaika nao.
    Rushwa inatokana na ulimbukeni wa kutoaminiana,tukiaminiana na kuamuwa kujenga nchi hakuna litalotushinda.
    Nyumbani ni nyumbani hata kama kichakani.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 29, 2009

    sasa wizara ya transportation . kila familia gari mbili

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 29, 2009

    Nilikuwepo Dar hivi karibuni na kukumbwa na dhahama za foleni. Sehemu kubwa ya matatizo yanaanzia kwenye makutano. Ni kama ile hadithi ya Esopo ya mbuzi waliokuwa wanahitaji kupishana kwenye njia nyembamba.
    Njia za haraka haraka za kupunguza tatizo ni:
    1. Kufuata kanuni za uungwana tukiwa tunaendesha. Nikitoa mfano, huku US kuna makutano utakuta yana alama za Stop 4 way. Maana yake ni kwamba kila anayefika pale anatakiwa asimamishe gari lake, aangaze kila upande kabla ya kuendelea na safari. Mkikutana watu kadhaa pale mnapishana kutegemeana na nani alitangulia mpaka wote mnaenda. Huwezi kukuta gari limeziba njia zote.
    2. Trafiki kutoona hiyana kutulima wakitukuta tumefanyiana usenene.

    Kwa muda mrefu suala hili linarudi kwenye mambo ya mipango miji. Tunajenga maghorofa katikati ya jiji bila kujenga maegesho wala kuimarisha miundombinu mingine. Mvua ikinyesha inakuwa mtafutano. Ukienda mjini unaweza kuendesha mji mzima unatafuta egesho. Yote hiyo ni kuongeza foleni tu. Kuna kampuni inayodaiwa kumilikiwa na familia ya kigogo fulani inakula hela kwa kukusanya tozo za maegesho kwa kuegesha magari kwenye maegesho yaliyojengwa kwa pesa za walipa kodi. Kwa nini wasijenge maghorofa ya kuegeshea magari halafu wakaanza kula hela kutokana na magari yanayoegeshwa humo?
    Tupo kwenye ulimwengu pepe. kwa nini lazima mtu ufunge safari mpaka ofisi ya serikali kulipia ada ya nini sijui?

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 29, 2009

    The only solution to this is construction of Flyovers, nashangaa mpaka leo wanajenga barabara wanaweka lane mbili tu na round about hapo kungekua na flyover mgeona hayo magari Dar ni 1/8 tu ya magari yaliyo kwenye miji mikubwa wangekua na barabara za namna hiyo kuna siku watu wangeacha magari barabarani wakaenda nyumbani kwa miguu,watu wanakua kama hawaendi kwa wenzetu wakati kila siku wako safari ina maana haziwasaidii

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 29, 2009

    Hiyo mini roundabout haifai kuwa sehemu bize kama hapo. Bomoa weka robot

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 29, 2009

    POINT YA SERIKALI KUHAMIA DODOMA NI YA MSINGI MANAKE MAGARI YAO NA YA WAFANYAKAZI WAO YATAPUNGUA SAANA COZ NI MENGI NA MANENE,YA PILI YA KUBORESHA MIKOANI ILI WATU WASIKIMBILIE DAR NAYO NI MUHIMU SAAANA MANAKE UKIANGALIA MITAA HII YA KWA OBAMA KILA JIMBO NI HATARI NA KILA KITU KIPO LABDA KAMA MTU NI MSHAMBA NA UNATAKA MAGOROFA NDIO UENDE NY AU CHIGACO BILA SABABU,PIA MADEREVA KUFUATA SHERIA NAYO NI MUHIMU SABABU BONGO MADEREVA WEHU WENGI SANA NA NIMECHEZA NAO SANA KABLA SIJATIMKA HAPO.KINGINE CHA ZIADA,ETI NI LINI BONGO KUTAKUWA NA MAGARI USED YA MAANA KAMA HUKU STATES?KWENYE PICHA HAPO NAONA PRADO/LEXUS HERE NDIO AT LEAST YA MAANA MENGINE YOTE NDIO YALE NILIYOYAACHA(COASTER,MARK 2,CHASER,RAV4 ETC) DAAAAMN!!HIVYO BADO MNAKUBALI BONGO KUWA DUMP YA USED CAR ZA MIAKA YA TISINI TU??AKUNA CHOICE KABISAAAA ZA MAGARI YA WALALA HOI MITAA HIYO,MAY BE KILA MTU ANATAKIWA ANUNUE GARI JIPYA KAMA VIGOGO NA FISADIZ,LMAO!!

    NI HAAAYO TU!!

    ReplyDelete
  19. AnonymousJune 29, 2009

    tatizo la foleni linachangiwa na mpango mbaya wa mji.
    1.CITY CENTER-kutokana na kuwepo kwa center ya mji ambako huduma zote za maana ndiko zinapatikana,watu wanalazimika kuelekea huko asubuhi na kutoka huko jioni kwa wingi,matokeo yake=MSONGAMANO aka FOLENI.
    SULUHISHO=decentralization ktk huduma,maofisi mbalimbali na huduma mbalimbali zitawanywe ktk sehemu tofauti na kule posta.yaani ktk maeneo mapya kama mbezi,pugu kajiungeni,mbezi beach n.k

    2.ujenzi wa vijumba vidogovidogo vinavyo hifadhi watu wachache na luka space kubwa.
    hii inachangia kumaliza nafasi katikati ya mji,nikimaanisha maeneo yote yaliyo ndani ya radius toka kariakoo hadi kimara kisha ufanye mzunguko wa duara.
    SULUHISHO= kujenga majengo marefu(gorofa) yatakayotoa huduma ya makazi kwa wakazi wengi ktk sehemu kidogo.hii pia itarahisisha kupata sehemu zilizo wazi kwa bustani,kujenga shule,masoko madogo na zahanati hapohapo karibu,kupunguza nguzo za kusambaza umeme na mabomba,na kuweka vituo vya polisi karibu wananchi ikiwa ni pamoja na kupata nafasi ambazo magari ya zimamoto yanaweza kuifikia nyumba ikiwa inawaka moto.

    UKIDHANI KUPANGA MJI NI GHARAMA,fikiria GARAMA UNAYOITUMIA KWA KILA 1minute inayopotea njiani bila kufaniwa kazi inaliingizia taifa hasara kiasi gani.

    mdau masomoni ughaibuni.

    ReplyDelete
  20. AnonymousJune 29, 2009

    Mm naona baathi ya maofisi yangeanza kuamishwa nje kidogo ya jiji... Mji uanze kukua, Office zisambazwe especially za serikali.

    Kila Office ipo ktk jiji ndio mana inakuwa kero.
    Tatizo la Tanzania everything is located in one place.

    Halafu Taa za barabarani, watu waanze kuzingatia taa za barabarani na sheria zake. Utoaji wa leseni huwe kwa anayejua gari, tuache mambo ya rushwa.

    Bwana Michuzi, Sisi huku tupo wasomi wengi sana...Kwanzia Associates, Masters, Bachelors na PHD...Tunaomba wazee waanze kutuachia ngazi vijana wa kazi tujenge nchi. Mambo yao ya kizamani tumechoka. Tunahitaji nguvu mpya isiyolala ovyo bungeni.
    But i beleive Kikwete is on right track, Nimesikia interview zake mbili tatu alipokuwa DC.

    Watanzania inabidi tuanze kuwa pamoja, tujenge taifa kwa pamoja kwa vijana wetu wa kesho...

    Kuna mambo mengi yananiumiza moyo:
    1.Tuna Tanzanite vipi?
    2.Mlima Kilimanjaro nasikia umekuwa wa wakenya.
    3.Mtu wa miaka 39 badala afanye jambo la maana anaenda kuanzisha zeUtamu hlf ni msomi.
    4.Rushwa
    5.Ubinafsi: mtu badala atekeleze kazi yake, unakuta anajinufaisha mwenyewe.
    6.Elimu inabidi iboreshwe.

    It takes time to make all these things happen, bt we got to start. Kiwete anajitahidi sana, inabidi tumsaidie. ni wajibu wa kila mtanzania kusaidiana. Tuache majungu na tuwe kitu kimoja.

    ReplyDelete
  21. AnonymousJune 29, 2009

    mdau masomoni ughaibuni,
    kujenga majengo marefu(gorofa) yatakayotoa huduma ya makazi kwa wakazi wengi ktk sehemu kidogo ndiyo chanzo cha msongamano huo sasa huo mtindo ukiongezeaka si magari yatapandana?

    ReplyDelete
  22. Sioni sababu ya hayo magari kuingia city center ndio maana vitambi,maradhi ya moyo na sukari haziishi.Lazima tujizoeshe kutembea angalau hapo city center.

    ReplyDelete
  23. AnonymousJune 29, 2009

    Ndugu zangu kwakweli niambie how do you feel ukiona ujinga kama huu unaendelea nyumbani??? This makes me sick in my damn stomach..
    Watu wanasema serikali ihamie Dodoma, ohh kwahiyo tutoe tatizo Dar. tulipeleke Dodoma arafu baada ya miaka ishirini tutahamia wapi??
    We have to be honest with ourselves, hili tatizo ni uongozi usiokuwa na upeo, logistical issue zinahitaji plan za muda mrefu sana...the least is 20 to 50 years.
    Ukienda City of Dar kuwauliza plan za barabara za mji kwa miaka hata ishirini ijayo I doubt kama watakuwa nazo.
    On short term basis, fufua treni toka tegeta, mbagala, mbezi(ubungo), na airport kuja mjini. Hiyo itakata haraka vipanya. Then wakati unapanua barabara unaweka toll za magari yaendayo mjini ili kudiscourage magari kuwa mengi mjini.
    Hela inayopatikana inaingia kwenye mfuko wa kupanua barabara. Tatizo kubwa ni RUSHWA RUSHWA RUSHWA RUSHWA. Kila mpango watu wanafikiria jinsi ya kuiba

    ReplyDelete
  24. AnonymousJune 30, 2009

    nitumie road road network ya City na Traffic volumes zake tuwafanyie kazi hao wazee wa jiji

    tuma kwenye hii email ukiweza
    fmloka@yahoo.ca

    ReplyDelete
  25. Chacha MusaJune 30, 2009

    Nitaanza na solution then nitatoa yaliyo moyoni....
    Mimi ningeshauri kuwe na utaratibu mzuri wa kuwezesha yafuatayo;
    1. Kujengwa maeneo ya kuegesha magari(nje ya City center), halafu kuwe na mabasi special yakutoka kwenye maegesho hayo na kurudi.
    2. Kuwe na ushuru wa kuingiza gari kwenye city center hii ni kui-re-enforce point#1.
    3. Huduma muhimu za jamii kama vile Mahakama,posta,benki,hospital,ofisi za bandari,TRA, you name it.. zipanuliwa na kupeleka matawi kwenye makazi ya watu. Mbezi,ubungo,kigamboni,osterbay..nk
    4. Watanzania lazima tuwe na ustaarabu kwani misongamano mingine tunasabisha madereva..(nilikuwa huko last year haki ya Mungu yaani hatuna ustaarabu hata chembe...mtu anaziba njia au junction bila sababu..daladala wafuate sheria na kuzingatia vituo.
    5. Viongozi wetu waaachane na Rushwaaaaaaaaa... tujenge na kuendeleza infrasture.
    Jazba..
    1. Wenzetu hawaongelei tena msongamano wa mgari wanaongelea Global warming..namna ya kuboresha magari ili kuprotect mazingira.. Serikari ya marekani inatoa Dollar 4,500 bure kama ukinunua gari yenye kutumia mafuta kidogo huku ikitunza mazingira free money.
    2. Haya yote viongozi wetu wanayajua kwani wameshatembea nchi zilizoendelea na kuona ubora tena kwa kutumia our tax money...
    3. watanzania tuache ushamba kwani ukinunua gari na ukapanda daladala hamna ubaya sio mpaka kila mtu ajue unagali.. kama daladala lipita mlangoni kwako mpaka unapokwenda kwanini uchome mafuta, kuharibu mazingira,na kuweka msongamanoooo... Damn.
    5. Sio mpaka uende makao makuu ndio ujue umepata huduma bora naaminiu hata matawi yanatoa huduma kama utakayopewa makao makuu tena bila msongamano.
    6. Watanzania tuwe na kiu ya maendelea bila uchoyo, tamaa, selfishness......

    ReplyDelete
  26. wewe unayesema karibu karibu USA una akili kabisa haba swali ni nini kifanyike toa mawazo yako yatusaidie sio tuame nchi kama wewe unavyojidai sasa tukiama wote nani atabaki je? itakuwa nchi kwa kifupi zipo ideas nzuri kwanza uwepo public transport za kutosha na kwa wakati.pili gharama za parking katikati ya mji ziwe kubwa zaidi ili kupunguza magari yasiyo na lazima kama ilivyo Tokyo Japani tatu kuboresha miundo mbinu ili kukizi mahitaji ya miaka hamsini ijayo ni tu. tukubali kwamba serikali yetu haina uwezo huo kama kama mnavyodai nini kipewe kipao mbele barabara ya mkoa hadi mkoa au wilaya hadi wilaya ndo sera ya sasa baada ya hapo tusubiri ni hayo kaka.

    ReplyDelete
  27. AnonymousJune 30, 2009

    mdau wa Dallas (I proud to be an American idiot) you are sooooooooo funny .nyie ndo wale mmekimbia migomigo familia zenu zinateseka hata mlo wa siku ni sheshe wewe unakazana kushop na kujisheua eti "God bless USA"
    Kweli duniani kuna watu na viatu lol!!!

    ReplyDelete
  28. AnonymousJuly 01, 2009

    Bro Michuzi, hiyo siyo priority, priority ni Chalinze - Segera!

    ReplyDelete
  29. AnonymousJuly 31, 2009

    Fadhily(MN U.S.A)

    Jinsi ninavyoona tatizo sio magari kuwa mengi nyumbani Tanzania.Hapa marekani state kama ya MN kuna magari mengi zaid kuliko Tanzania yote lakini foleni sio kubwa kama ya nyumbani.Tatizo lililopo ni kuwa na ufinyi wa barabara.
    Viongozi wengi wa serikalini wanakuja kutembea nchi za nje na wanajionea jinsi barabara zilivyojengwa huku lakini cha kushangaza hawatumii exposure ya nje kujenga bara bara nyingi Tanzania.Serikali ina uwezo wa kujenga barabara nzuri tatito wengi wa viongozi wetu nyumbani sio wabunifu na wanajifikiria wenyewe badala ya wananchi wa Tanzania.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...