DARSA YA RAMADHANI KWA
WAKAZI WA LEICESTER

Assalaamu Alaykum Wa Rahmatul Lah
Bismaillahir Rahmanir Raheem

Ramadhan Kareem imekaribia sana, Tunapenda kuwaarifu wakazi wa Leicester UK kuwa Inshaallah tutaendelea na utaratibu wetu wa kuendesha Darsa za Mwezi wa Ramadhani kwa utaratibu ufuatao:

SIKU: Jumamosi na Jumapili, baina ya Alasiri na Magharibi.
FUTARI: Kama kawaida, tutafanya futari ya pamoja. Tafadhali tushirikiane kwa kuleta vyakula ili kufanya futari ya pamoja. Tujihimize katika kunufaika na thawabu za kumfunguza mwenye kufunga katika mwezi huu.
Darsa ni kwa Wanawake na Wanaume
Darsa itaongozwa na Sheikh Saleh bin Juma
KITABU: Bustanul Waidheena & Riyadhus Samieen
Shime tuhudhurie Darsa zetu tupate kujikumbusha tunayoyajua na kujifunza mapya tusiyoyajua ili kunufaika na fursa ya Mwezi wa Ramadhan.
OMBI RASMI: Tafadhali tuusambaze ujumbe huu kwa ndugu na wapenzi wetu katika imani katika mji wa Leicester.
PAHALI: First Floor, 60 Malabar Road, Leicester, LE1 2PD, UK
Kwa maelezo tafadhali wasiliana nami kwa email au simu 07982124581 au
Sheikh Saleh 07529693934.
Ahsante sana.
Khamis Sahal

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Allah bless us all. welcome Ramadhan Kareem.

    ReplyDelete
  2. ule muda wa kutubu yale tuliyoyafanya miezi kibao iliyopita ndo muda wake huu.Mnaopenda kwenda kunywa mipombe,kufanya washerati nk muache angalau kwa MWEZI MMOJA, LOL.

    ReplyDelete
  3. Assalaam alikhum,

    Ni vizuri sana kukumbushana katika mambo mazuri yenye faida ya milele. Nawatakia Ramadhan njema wana Leicester na waislam wote.

    ReplyDelete
  4. Kama kuna mambo ambayo JUMUIYA zingetakiwa kuanzisha (kule ambako hayapo) na kuendeleza (kule ayalipo) ni taratibu kama hizi. Hii ni BARAKA kuubwa saana kwa wakazi wa Leicester kuendeleza utaratibu wa kufunzana na kukutana nyakati hizo kuendeleza masomo mbalimbali.
    Nawatakia MFUNGO MWEMA na pia ikiwezekana hata mara moja kwa mwezi baada ya mfungo ili kuimarisha mafunzo mnayopeana wakati wa Ramadhan.
    Wasalaam

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...