asante mdau nine kwa ujumbe huu
hii sasa inakuwa too much sasa..... arghhhh!


Huyu bwana anatufaa kweli?
Angalizo: Hii ni mada ya kifamilia na inawahusu wadau
wa bwawa la maini tu. sawa jamani??? ohooo...
watu tunashindwa hata kula daku hapa....






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 52 mpaka sasa

  1. Ni kukimbiza wote, hao maco-owners na benitez

    ReplyDelete
  2. pole sana kaka michuzi...asiyekubali kushindwa si msindani kubali matokeo mlizidiwa kimchezo.

    ReplyDelete
  3. dah michuzi kweli wewe ni mmatumbi mbona unafanana na John Mashaka kwanza nimeipenda sana speech yake, heeh hii game imekwisha niliacha ni 2-1? Ok i sent you email kuhusu ujamaa na capitalism vipi mbona sijaiona? Basi msailimie kaka yako Mashaka mmefanana sana kama sungura.

    ReplyDelete
  4. Hatufai!!! It's time for him to move on!!! 3 points out of 9!!!

    ReplyDelete
  5. Kutufaa anatufaa Swali ni kwamba je Liverpoolfc Tuna Player ambao wanacheza Game to win?

    Katikati asingemleta Aquilani angemleta Diego alienda Juventus wanahitaji Winger wa Kulia wa nguvu na Stiker Jarmaine Beckford wa Leeds Rahisi kama hawawzi kumpata David Villa.

    Hawa ndio wachezaji wakuleta na sio kuleta

    Wakuleta:

    David Villa-(striker) anacheza mpira wa ushindi akifungwa inamuuma.

    Jarmaine Beckford(striker)- anacheza mpira wa ushindi

    Arron Lenon au Ashley Young(winger)

    Siowakuleta:

    David Silva: Wasimlete kabisa liverpool, jamaa good player ila laini na hachezi game kwakushinda game yake kwakujionesha hafai kabisa wasipoteze pesa hapo.

    Voronin auzwe Babel kama hatochezeshwa Striker auzzwe wasimuharibie Mpira.

    Mwakani tujitaarishe kwa SG kuondoka.

    Mdau mwenye machungu Pazi.

    ReplyDelete
  6. Teh teh teh teh teh!!!Liver bwawa MMEFULIAAA msitafute visingizio.Na bado sasa,mwaka wenu huu.Michuz usinibanie comment yangu maana we nawe hasira zako duh!!

    ReplyDelete
  7. Kaka nipo liverpool hapa kijivekesheni nikitokea edinburgh. lengo hasa la kupiga kambi hapa ni sababu mimi ni mwanachama hai wa liverpool mwenye kadi kabisa. nilinunua season ticket pound 350kwa ajili ya klabu yangu hii. nimetoka anfield sahivi lakini yaliyotukuta uwanjani tulitamani tusingekwenda kabisa. inauma sana yani timu imecheza fyongo sana leo, hawa aston villa hawakucheza soka la kutisha sema walicapitalize on our silly mistakes. torres leo alikuwa nalenale sana hakucheza ile ngangari, kacheza kilegevulegevu utadhani nae yuko kwenye swaumu bwana!!!!
    Anyway ni mapema kumlaumu kocha sababu hata last season tulivyocheza vizuri bado kocha alikuwa yeye, nadhani timu inamuangusha kwani yeye hawafundishi wacheze legelege namna ile. inauma kupigwa 3 home ukizingatia chelsea ndo hawana hata dalili ya kupoteza michezo. sijui, ngoja tusubiri lakini kwa jinsi timu ilivyocheza tunahitaji mabadiliko ya haraka sana ki-morali na kiuchezaji. halafu msisahau tuna pengo la attacking mieldfielder tangu aondoke Alonso pale kati pamekuwa sio kabisa yani! lucas anachemsha na leo kapiga OG(own goal), ni bora vilonim angekuwa anaanza kuliko kuingia kama sub! mr. dullacell naye sio yule tumjuae, we really need to do something. it's down to the coach to boost team morale and see how we can pick up in future games. the way we are now we don't look like real title challengers.
    anyway ndo soka lets hope for the best in coming fixtures.
    kaka michuzi kama unataka jezi original sema nikutumie kaka bureeee!! na kadi ya uanachama kama huna basi ongea nikukatie manake ushabiki bila kuwa mwanachaama inakuwa howcome kaka
    Mdau wa Liverpool, UK.

    ReplyDelete
  8. Benitez simlaumu kwenye Timu namlaumu kwenye kununuwa Kanunuwa Vibaya.

    Glen Johnson £17m wamewapa Posthmouth £10m na £7m walikuwa wanawadai za Crouch wameongeza.
    Ok Glen Ni Mchezaji Mkali hapo simlaumu. £10m katumia.

    Kaleta £15m Aquilani si £20m kama wanavyosema.

    £25m hizo zimetolewa kabla hata Alonso hajauzwa £30 KWahiyo kuna Pesa Wamarekani za Msimu huu hawajampa Benitez,

    Aquilani kaja kwa Pesa za Keane £12 na Alizouzwa Leto £3m. Kwahiyo Kapewa £10m tu kwa Johnson Mwaka huu na YUle Mgiriki £2m ambazo kuna Youth kama Nne wameuzwa kwa Nusu Millioni Nusu Million.

    £30M je zinaenda kwenye madeni yao? Wamarekani au? Kama timu imewashinda waiuze kwa bakharesa bwana. Sio Hockey hii. Benitez pia asingetumia £15m kwa Aquilani angegawanya £8 kwa Striker Na £7m kwa Winger Ambao wakali Haina haja Kutumia pesa Nyingi mtu mmoja. Bwawa Litakauka naona Bora tushuke Daraja tuwe nafasi ya 5 au 6 ndio tutatia akili. Ukweli Chelsea anachukuwa Hata arsenal wakibana. MZ.

    ReplyDelete
  9. Bring Van Der Vaart na Striker Basi kwisha msijitie Homa Benitez bado yupoyupo bado hakuna kukata tamaa mapema Mnooooooooooo. Wasiwasi wangu mie sehemu moja tu Kuyt Watafute mtu wa kulia Kuyt wamsukume mbele. Riera lazima acheze kushoto Benayoun kulia Kuyt mbele Steven Gerrad arudi Nyuma wakileta Van Der vaart anacheza Na Torres, Kuyt Bench. Villa nawapa Pongezi Ndio vizuri kutokea vile michuzi tuchange tununuwe timu. TZ KOp.

    ReplyDelete
  10. Pengo la Alonso halijazibwa. Ukiangalia mechi za msimu uliopita England, Alonso alikuwa mchezaji anayeongoza kwa kuchezewa rafu mbaya zinazosababisha mtu apewe kadi nyekundu. Alikuwa hakamatiki. Hata huyo Aquilani nina mashaka naye. Wachezaji wa Italia pata potea, ndio kina Dossena hao. Viungo wanatokea Spain...Alonso, Xavi, Iniesta, Guti, Fabregas, Marcos Senna (japo ni mbrazil kiasili). Msimu huu yaelekea Liverpool itapambana na kina Portsmouth kubaki ligi kuu.

    ReplyDelete
  11. duh pilipili ya ma-scouser inawawasha nyinyi wamatumbi? kujipendekeza tuu

    ReplyDelete
  12. Mtakoma mwaka huu, top four sahau, mtamkumbuka sana alonso

    ReplyDelete
  13. Bwawa la majonzi mwaka huu kazi mnayo, na saumu hii duh!!!!

    ReplyDelete
  14. Kama mdau kufa kupona wa bwawa la maini kama utakumbuka katika msimu uliopita uliuliza kwa nini huyu asitimuliwe nilikuunga mkono mikono na miguu kwenye post moja uliipouliza kwa nini asitimuliwe. Huyu jamaa hafai hata kwa kuumangia anapaswa kutipiwa virago mara moja. Tatizo wamiliki wenyewe ni wale wanaoita handball footbal. He has to go ASAP. Kocha gani anaacha wachezaji muhimu waondoke? Refer Robie Keane na Alonso hata Mziray kama anataka ushindi angewang'ang'ania nasikia kutapika.

    ReplyDelete
  15. MDAU TARIMEAugust 25, 2009

    HII KITU BADO MBICHI,NIMAPEMA MNO KUANZA KUFUZANA,LIGI YA UKEREWE HAITABIRIKI NA USISAHAU ANAECHEKA MWANZO,HATA DUMU,ATAKAECHEKA MWISHO NDIO MCHEKAJI,BRO MICHU USIKONDE

    ReplyDelete
  16. Benitez anatufaa sana sema tuuu naona kama anaanza kufulia kiutaalamu na tactics..daaaaa goli 3 inatia uchungu sana jamaaniiii

    ReplyDelete
  17. KUDADADADADADAKIIIIIIIIIIIIIIIIIII! WALAHI,Huo ndio mwanzo kama msimu uliopita kwenu mwateleza na badooo!
    kUONDOKA KWA ALONSO HAMNA KIUNGO NA MMEKWISHA. KUDADEKIIIIIIIIIIIII1

    ReplyDelete
  18. Yaani hapa nilipo hata kuftari nimeshindwa..homa juu dah!!....hata kuongea. Pale katikati bila Alonso ni uozo mtupu...sijui hata nianzie wapi....ninauchungu sana..

    Mdau Toronto.

    ReplyDelete
  19. Hii inaonyesha na jinsi gani MAN U watachukua ubingwa kirahisi.Arsenal ni kawaida yao kuanza league kwa mkwala wacheck baada ya mechi nne or tano. Man U huwa wanaanza slow. Chelsea hawatupi tabu. liverpool walikuwa wanapiga kelele sana kabla ya league kuanza

    ReplyDelete
  20. I have finally lost faith in our manager and truely believe he has to go now. He has had the time and the money and we are looking worse than under Houllier. It seems that the other teams have worked usout and as we have no plan B,C or D like United and Chelsea have.......Look at our bench or lack of it..... all the money he has had, every commentator and supporter saying we need another quality striker and Rafa thinks he knows better. Well, if Lucas, Voronin and Babel are better then we will struggle to get into the top 6. What will his excuse be?? He will blame the Referee as he always does and he can blame the owners for not giving him more money to waste but he will never blame his poor judgement in players and his inability to change tactics and break teams down. I am sickened to think that another year will go without the titleand probably without a trophy. We dont look like winners and so its time for change.

    ReplyDelete
  21. Hili Bwawa lina chunusi! Kunyweni maji au yamwageni!

    Kaka Gee, AR.

    ReplyDelete
  22. mmmh na nyie LIVERFOOLS vipi tena,juzi tu hapa mmesema mmesha ANZA ligi,leo tena HATUFAI,inakuaje wajameniiii,ile ni timu ni ya watu wawili tu,hata babu yao FERGIE alisema,this year mtawajua,kwani wanajua janja yenu,kamata GERRO na yule mtoto laini TORRES basi kwishneiii,poleni

    ReplyDelete
  23. Poleni sana wapenzi wa Liverpool, hasa kwa mzee mwenyewe wa blogu ya jamii, Starring: Mr.Michuzi. Kwa kweli iki kipigo ni kikubwa sana hasa kwa timu inayotarajiwa kushinda ubingwa wa EPL hapo mwakani.Halafu nyumbani kwenu, mbele ya washabiki wenye kelele kuliko wote uingereza. Hakitasahaulika. Ila sishangai sana kwani wakati timu nyingine zinagombana hadi kufikia hatua ya kupelekana mahakamani juu ya wachezaji katika Transfer window, nyinyi mmelala tu kuridhika tu. Inawezekana ikawa ni ubahiri wa owners, na siyo kosa la Benitez. Angalia muarabu wa Manchester City anavyomwaga maela....Duhh!

    ReplyDelete
  24. Eti ninasikia Gerard, Torres, Kuyt, Benayun na nyota wengine hawakucheza ndiyo maana Liver wamefungwa. tena nasikia magoli yenyewe yamefungwa kwa taabu sana hata hivyo Liver wangeondoka na ushindi mnono sana.

    ReplyDelete
  25. Ni kisa cha mbwa kula mbwa!!!!!

    ReplyDelete
  26. aliokata mtu gerald sio benitez...aliejifunga lucas sio benitez..kona wameshindwa kukaba waliocheza sio benitez....

    ReplyDelete
  27. gme bado...tumpe muda Benitez....kufukuza kocha sio suluhisho....

    msukuma asilia....

    ReplyDelete
  28. No salamaelkum BENITEZI, pole naona mmewaachia nafasi ya 4 arsenal

    ReplyDelete
  29. Benitez lazima atimuliwe. Tena mapema mapema kabla chomba hakijaenda mrama. Nadhani wachezaji pia washachoka nae. Hana mpya huyo

    ReplyDelete
  30. You will never crawl alone!!

    ReplyDelete
  31. Watani hoyeeee!!!!! You will never walk alone...kazi kweli kweli

    ReplyDelete
  32. Bado mapema Mpeni match tatu za mbele ndio akichemka ndio mtamtimuwa. ndio kwanza ligi inaanza . kama Man U Mwaka jana alianza kwa kusuwasuwa.Jamani Timu zimejianda msimu hakuna cha lelemama na Cha history hapa

    ReplyDelete
  33. Kamakawa mgonjwa hakatai dawa!Yaani jana ile picha linaanza tu stering anakufa kwenye Maua! we unategemea nini tena! Big Up to Reo coker! na badooooooooooo! Ila kaka michuzi mbona jamaa waliharibika sura sana? ama walichokoza ugomvi baa? maana Carragher, Torres wote inaonekana kama walichezea sana za uso!
    Teh teh teh, Ila sio kosa lenu, unajua Tottenham walisifia kwamba Jogoo mtamu tena ukipata na mba! mwalongo mwe! we issa we, mwanchembe kabakaba!

    MANUTD-DIE-HARD-FAN.

    ReplyDelete
  34. ahaaaaa BALOZIIII,Mbona una IMANI haba ...umesahau maneno ya nabii wetu...hata Simba SC walianza ivi ivi...Poleni ndio Ukubwa..

    ReplyDelete
  35. mwishowareliAugust 25, 2009

    INANIUMA SANA....TATIZO LA KOCHA WETU RAFA MANENO MENGI NA SISI TUNATAKA VITENDO.NI VYEMA HAONDOKE MAPEMA.

    ReplyDelete
  36. Na bado safari ndio kwanza inaanza,mliwazarau sana wenzenu na kujipa ujipa ujiko kuwa huu ni msimu wenu LIVERPOOL.Na kwa mchezo huo sidhani hata kama kweli mtaingia ktk 4 bora.Michuzi sasa tunakukaribisha ujiunge na vijana wa emirate.
    Mdau wa Arsenal.

    ReplyDelete
  37. NA BADO SAFARI HII MTAFULIA SANA,, MMEMUUZA ALONSO (MZEE WA RULA) SASA MNAONA MNAVYOJINYEA???? NA BADO.. POLE SANA MKUU WA NANIHII NDO UKUBWA HUO ILA MSIKATE TAMAA MWAKA HUU UBINGWA NI WETU..

    ReplyDelete
  38. teh teh ..kwe kwe kwi kwi..sasa liverfool si mmezoea kufungwa..maana mwaka wa 19 hamjachukua kombe la england..sa mlitaka mshinde ili iweje na wkt hamchukuagi hili...

    WALTER MEZZAH,TKM

    ReplyDelete
  39. - chambilecho cha mwafrika, uwanja wa taifa:'ndege KOKO ana ukimwi!!!'..ukipenda badilisha ndege, tia jina la mnyama mwingine pia-

    - mdau mmoja hapo juu unasema Kuyt nje?..tazama mpira vizuri..Mdachi yuko class moja na SG na Carragher kwa kitu kinakwitwa 'ujasiri -character' pamoja na 'uchapakazi - work rate'..
    - kasheshe kwa sasa, ndugu mkuu wa nanihii, ni confidence ya timu..ndo ilowabeba saana mwaka jana (sababu wachezaji wenu ni wa kawaida sana)..na mechi ya jana pia, wachezaji hawakutaka kukubali kuwa yanaweza kuwatokea yale..ikianza kuwa 'kama kawa' basi mtaporomoka kupita hata maboga, matombo!

    ReplyDelete
  40. HAPA NDIO INAONESHA WATU HAWAJUI KUSOMA KICHWA CHA HABARI. MNAJIPENDEKEZA MMEULIZWA NYIE WENGINE SWALI KWA WADAU WA BWAWA LA MAINI TU. TAFUTENI BLOG ZENU ZA MICHEZO MWACHENI MICHUZI. GAME YA TATU TU WATU MINENO HIYO SUBIRINI BAADA GAME 15 au 20. CHELSEA ILICHUKUWA MIAKA 50 UBINGWA Man U Miaka 26. sasa leo Liverpool hii 19 tu makelele Liverpool itachukuwa muda ila 21 wanachukuwa MWaka jana ndio ulitakiwa kuwa wao isingekuwa Mirefa ya UK wangebeba. ila wasubiri baada ya Miaka 21.

    ReplyDelete
  41. sidhani kama tatizo ni rafa, nina shaka sana na wale wamarekani wezi. matatizo yaliletwa na mtu mmoja anaitwa souness miaka 19 iliyopita lakin ya wamarekani ni makubwa zaidi. wanunuliwe wachezaji wakubwa ndo tumlaumu mwalimu

    ReplyDelete
  42. ASTON VILLA OUTCLASSED LIVERPOOL.. TEH TEH TEH TEH TEH... KWI KWI KWI... MA.. YAMEWABANA NA BADO.

    ReplyDelete
  43. mbwegelembwegeleAugust 25, 2009

    Nadhani Rafa ni kocha mzuri sana, lakini si meneja mzuri.

    Timu haina depth kabisa, ok anaweza kupata first 11 nzuri, lakini si ya kutisha.

    striking force:Torres, hakuna mwingine wa maana, compare au chelski wana options gani.

    midfield: macherano na Steve, wengine bado sio top quality. ahkuna timu inayoweza kuchukua ubingwa na few options ktk midfield.

    Central defence: skirtel na carragher. hakureplace Hyppia on time, matokeo yaka imebidi anunue mgiriki kuziba pengo la majeruhi within days.

    To my opinion , no depth, no ubingwa. Tujipe matumaini kuwa wengine nao watateleza.

    What about team spirit ??

    ReplyDelete
  44. ni kweli bwana michuzi ..... hawa hawa fai

    ReplyDelete
  45. MKUU wa NANIHII,ndo kusema UMISUSA au nini,naona hakuna mupya leo zaidi ya hio ya KIBAJAJI cha tangu jana,isije ikawa mama yetu hajui namba za kuokolea watu,mwambie abonye 911 pls,bado tunakuhitaji mzee.

    ReplyDelete
  46. Mdau wa Bwawa la Maini, KigogoAugust 25, 2009

    UNAJUA WATANZANIA WENGI NI KAMA MBWA KOKO!!! ACHENI ULIMBUKENI...JUZI JUZI LIVERPOOL WALISHINDA...5, MIDOMO SHATU KUDADEKI..ACHENI KUWA KAMA MAJI YAFUATAYO MKONDO...SASA HII JANA KUFUNGWA TENA 3-1 MNAONA NI TATIZO...?? HELA WAPATE WENGINE VICHWA MUUMIZE WENGINE...NAONA WENGINE MUMEANZA HATA KUPANGA LIST...MUMEKUWA BENITEZ? SASA SI MKAOMBE KUIKOCHI LIVERPOOL? MECHI NDIO KWANZA ZIMEANZA...MECHI 3 TU..BADO MECHI 36.....SAFARI BADO SANA...KAMA MNKUMBUKA LIGI YA MWAKA JANA EPL, BOLTON WALINZA KWA MBWEMBWE TENA VIZURI SANA...NINI KILITOKEA???? WALIINGIA HATA 5 BORA????ACHENI ULIMBUKENI...BADO MAPEMA...

    ReplyDelete
  47. Waswahili wanapenda sana kusema kocha hafai mambo yakienda kombo kidogo tu, sijui kwa nini wanaendekeza knee jerk reactions. Stars wakitoka draw, Maximo hafai. Yanga wakitoka droo Kondic hafai. Simba wakishinda 1-0, Phiri hafai.
    Kama Rafa aliweza kutwaa Champion's League kwa kutumia wachezaji kama Vladmir Smicer huwezi kuniambia kwamba amepoteza uwezo wa kuikochi Liverpool baada ya mabadiliko mazuri ya msimu mzuri uliopita.
    Tatizo ni Wamarekani walioitwaa timu hawana hela, wako sawa na wawekezaji wanaokuja bongo. Alonso ameondoka Rafa amemleta majeruhi Aquilani. Aquilani hakuwa chaguo la kwanza. Wamarekani wangekuwa wametoa hela ya kueleweka angeweza kumpata Gareth Barry lakini ni Man City waliotoa dau kubwa zaidi.
    Mwenendo huu ukiendelea Liverpool itaanza kugombania wachezaji na Newcastle na Leeds.

    ReplyDelete
  48. msimu uliopita ulikuwa ndio msimu wenu,msimu mpya muwaachie chelsea na man u. chelsea kushinda champions league na premiaship na manu kushinda fa cup na carling cup. blue kamanda

    ReplyDelete
  49. NAONA WENGINE SASA WAMEANZA HATA KUPANGA MATOKEO KUWA NANI ATAKUWA BINGWA WA KOMBE GANI...DAH, BONGO FEDHEHA SANA..

    ReplyDelete
  50. NYIE MNAOTAKA BENITEZ AONDOKE LIVERPOOL NAFIKIRI MTAKUWA MMECHANGANYIKIWA, BINAFSI NAWEZA KUWAWEKA KWENYE KUNDI LA LIVERPOOL MAGOLI, HIVI KUFUNGWA GAME MBILI NI KITU CHA AJABU?? HAWA ASTON VILA SI TULIWAPIGA TANO SEASON ILIYOISHA MBONA HAMKUMTAKA KOCHA AONDOKE?? NI MAZURI MANGAPI AMETENDA KIASI KWAMBA MNATAKA AONDOKE KWA MECHI MBILI TU ALIZOFUNGWA MSIMU HUU?? MNAPASWA KUWA WANAMICHEZO ZAIDI SIO USHABIKI USIOKUWA NA MSINGI, BADO SAFARI NDO KWANZA IMEANZA NYIE MNAANZA KUPAYUKA PAYUKA OVYOOOO, AU MNATISHIKA NA KASI WALIYOANZA MADOH\GO ARSENAL?? PIA MNAPASWA KUFAHAMU KUWA HII ASTON VILLA SI TIMU YA KUBEZA MAANA NI TIMU AMBAYO ALWAYS INALETA USHINDANI HALISI IKIAMBATANA NA EVERTON AMBAO NAO WAMEPIGWA BAO 6 KWENYE GAME YA KWANZA,, PIA MWAPASWA KUITAMBUA KWAMBA HAO HAO ASTON VILA WALIKWISHA POTEZA MAECHI MBILI MFULULIZO HIVYO WALIKUWA WANAINGIA UWANJANI KAMA MBOGO ALIYEJERUHIWA NA LENGO LAO KUBWA LILIKUWA KUCHGEZA KWA BIDII NA KUHAKIKISHA HAWAPOTEZI MECHI YA TATU MFULULIZO HIVYO SI JAMBO LA AJABU SANA KWA MATOKEO YALE.

    KWANI HATUJACHUKUA UBINGWA KWA MIAKA MINGAPI SASA?? WALIKUWEPO AKINA ROY EVANS WAKAHSINDWA KUCHUKUA UBINGWA IWEJE MUMSHURUTISHE BENITEZ??

    NAWAOMBA WALE WOTE WANAOIPENDA LIVERPOOL KUTOKA MOYONI KUWA WATULIVU NA KUIOMBEA MEMA TIMU YAO.

    Willy UDSM

    ReplyDelete
  51. ENYI WAGALANZANIA MSIO NA AKILI, NI NANI ALIYEWALOGA NA KUWACHANGANYA AKILI NA KUZANIA KUWA NINYI NI WAINGEREZA? NATAKA KUJIFUNZA HILI KUTOKA KWENU. JEE HAMJUI KWAMBA LIVERPOOL NIMTIME YA WAINGEREZA? JEE MMEPOKEA UTUMWA KIROHO PAMOJA NA KIMATENDO? NI KWA NJIA YA AMANI TUU? HIVI KWANI HAPA BONGO HAKUNA TIMU? AU HAO MABWANA ZENU WA UENGREZA WANAPENDA TIMU ZA BONGO?

    ReplyDelete
  52. As ManUnited fun nina mambo ya kusema kuhusu hili saga la Liverpool.

    Kwanza ni mwanzo wa ligi huu,ManUnited last two seasons walitoka sare mechi tatu za mwanzo na wali pick up only 3 points.

    Pili,Liverppol kusema wamemkosa Alonso ndio sababu, ManUnited plays without CR7 na Tavez.

    Tatu,Liverpool ni team ina depend on Torres & gerald.Torres hawezi kucheza ligi yote, atacheza may be 60% mechi zote.Huwa anaumia,ndio history yake katika maisha yake ya mpira.Hii peke yake tunaweza kusema they are out.

    Nne,Chalsae ndio timu ambayo inaonyesha dalili ya kushinda,lakini Arsenal nafikiri wamo pia.

    Tano,Manunited wanaweza kuwin hii ligi kwa mara nne mfululizo.Why?Liverpool wame drop kimpira vibaya mno na chalsae still is not team to beat ManUnited all the time.Arsenal always run out the gas as ligi going o.

    yangu macho

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...