Muimbaji wa nyimbo za injili wa jijini Mwanza,Esther Tindosi Kusekwaanatarajia kuzindua albamu yake mpya itakayoitwa Faraja kwa yatima nawajane, mnamo Agosti 29 katika uwanja wa Kambarage,mjini Shinyanga naAgosti 30 katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwaza.

Uzinduzi huo ambao unaratibiwa na kampuni ya Flora TalentPromotions,chini ya Mkurugenzi wake Bi.Flora Lauwo ,utakuwa ni wapekee na wenye kuwasisimua wapenzi wa muziki huo wa kiroho ambao kwasasa umekuwa ukikubalika na kupendwa kwa kiasi kikubwa.

Bi.Flora alisema kuwa albamu itakayoziduliwa itakuwa na jummla yanyimbo nane, ambazo kwa kuzitaja chache ni Faraja kwa yatima na wajaneuliobeba albamu nzima,nagalolela ambao umeimbwa kwa lugha yakisukuma,Kemea,Ole wao,Akina mama,Dhambi,Nimechoka na nyinginezo.

"Watakaousindikiza uzinduzi huo atakuwepo muimbaji mahiri wa muziki wakiroho kama vile Joseph Nyuki,Mchungaji Baru,Jerusalem Band,MathaRamadhani,Kwaya ya Vijana wa Bwiru, Kwaya ya AIC Makongoro bilakumsahau Bi Josephin anayetamba na wimbo wake wa mateso ya mwenyehaki, na band nzima ya Tabata ambao wanatamba na wimbo wao wa natembeakidogo kidogo, nikinyatanyata,Na wengine weeeeengi."amesema Flora.

Flora amesema kuwa katika suala la maandalizi kila kitu kinakwendasawa mpaka sasa,na kwamba kiingilio kimepangwa kuwa shilingi 1000/=kwa watoto na watu wazima kuwa ni shilingi 2000/=.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. dada esther tunakutakia kila heri katika uzinduzi wa album yako Mungu akubariki sana katika huduma hii ya uinjilisti kwa njia ya uimbaji kwani wengi wameokolewa na kuponya

    ReplyDelete
  2. hongera dada wa nyumbani kulitangaza neno,ila mgejaribu kuwa na tiketi ya familia yenye punguzo kidogo ili na wengine waweze kuingia na wake na watoto nao wapate neno kwani hapo utakuwa kweli umesaidia

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...