nimeombwa kuurudisha tena mjadala wa lebozzzzzz.
je ujumbe huo hapo juu ni sahihi? maana kila mnuso
nakuta wadau wametinga na malebozzzzzz

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. kiukweli mie kwa mtazo wangu japo sijafika huko ulaya hiyo lebo ingetolewa tu, kwa sababu inaoneka kama uchafu, kinachokela zaidi mtu mwingine hata kama imebanduka yupo tayari kuishosha hata kwa mkono eti waone kama inatoka huko italiano mie nakasirika basi tu, hata kwenye harusi bwana harusi unakuta na lilebo lake hapo aaah, inachefua sana. Tunaomba watu wanaojua maana ya hiyo lebo na ifanywe nini watuambie maana wengie=ne tuna watu wabishi sana kuhusiana na hizo lebo.
    nawakilisha.

    ReplyDelete
  2. Sasa weweeee!!! watu watajuaje kama hiyo suti ni mpya! mimi naziacha lebo zote, hata ile inayoning'inia kwenye mfuko wa suti! I am free to do anything that pleases me and is not against the law!!!
    kwa kwa kwa

    ReplyDelete
  3. mi naona label zinabaki ni kama urembo.Ni mtazamo tu.

    ReplyDelete
  4. Mbona ukinunua BWM haubandui nembo?
    Mbona ukinywa Coca Cola haubandui nembo?
    Si mambo ya quality jamani au?
    Kama wangetaka ibanduliwe si wangeining'iza...
    Au kama haitakiwi kuonekana si wangeshonea ndani?

    We toa sababu za msingi kwa nini lebo itolewe.. halafu sisi tutachuja hoja

    ReplyDelete
  5. michuzi hii mijadala mingine inatuchosha,sisi huku ulaya tutapata wapi muda wa kubandua label-time is money,huko kwenye mavumbi bandueni label maana you people got lot of time.Sasa hivi tunavaa disposable suit,unavaa mara mmoja na kutupa,hakuna muda wa kufua

    ReplyDelete
  6. Hahahahahah jamaa mmoja leo kanifurahisha Suti kuvaa na kutupa Ahsante nimekubaliiiiiiiiiiiiiiiiiiii. Ila Lebo ukitowa kweli mbona BMW Nembo hamtowi watajuwaji kama unaendesha Skoda au BMW au Corola?

    ReplyDelete
  7. haya jamani wabeba mabox msokua na muda wa kubandua lebo maan mko busy, inachukua masaa mangapi kubandua lebo jamani. watu kwa mbwembwe.

    ReplyDelete
  8. achana na miutamaduni ya watu. ebu tubuni suti ya kwetu ambayo hatimaye tutakuwa 'masters'. hii ya ulaya tutaendelea kuelekezwa ni ni cha kufanya, nk.

    ReplyDelete
  9. Kuziacha hizo lebos ni ushamba wa hali ya juu. Siyo siri mimi ninapokutana na mtu kaivaa huwa nashindwa kujizuia huwa namasaidia kumfahamisha. Akikasirika shauri yake. Tena wengine waheshimiwa kweli kweli. Jamani huo ni ushamba ushamba ushamaba

    ReplyDelete
  10. Jamani lebo ni muundo mpya ambao umeletwa na designers kwa makusudi ili kutambulisha product yake. Ni sawa na kusema unataka kutoa lebo ya kwenye Collar ambayo mathalani imeandikwa Adidas au Mark and Spencer. Kwa vile sasa hivi watu wanakwenda na wakati na kwa kujitangaza zaidi ndio maana kwa makusudi ya watengenezaji wakaona basi ni vyema wakatafuta sehemu nyingine mbali na kwenye Collar ambapo wengi wanaamini huwa hazionekani wakaamua kuziweka kwenye mikono kwa makusudi ili kutangaza bidhaa zao na majina ya kwa ujumla wake.

    Kwahiyo kuiacha lebo ama kutoa ni uamuzi wa mvaaji au mwenye kumiliki bidhaa hiyo lakini kwa upande wa watengenezaji wangependa sana lebo hiyo ikabakia

    Yaani ni sawa na mimi sasa hivi kusema kwamba naondoa lebo ya AIG kwenye uzi wa Man Utd au Liverpool ambao wanakuja na uzi wa Standard Chartered au Emirate kwa Arsenal na Samsung kwa Chelsea nafikiri haitaleta ladha ya vazi lenyewe kwa ujumla wake.

    Mdau Davey

    ReplyDelete
  11. suti zote zenye akili uwa zina lebo, ni hiyo misuti yenu ya kina kanumba ambayo haina lebo.kwani nyinyi wala vumbi hapo bongo ni wajanja kuliko kina armani,versace,dolce &cabana,hawa wakali wa kudizaini wameona poa kuweka lebo na huku viwanja watu hawamind.basi totoe na tiki kwenye nike.wabongo bwana mbona mnavaa mivulana yenu yenye majina kama kanga,muambieni basi na jamaa awache kuweka mipasho kwente t-shirt.pumbavzzz

    ReplyDelete
  12. Kwa kweli mie naboreka nikiona mtu kavaa suti na lebo kwenye mkono! It doesnt look good to be honest inaonekana kama ushamba fulani. Ni sahihi kabisa lebo zitolewe mkononi kabla ya kuvaa suti.

    ReplyDelete
  13. Haaaa haaaa.Waaambie hao Michuzi!Wamezidi!

    Na wewe ndugu Tarehe Wed Sep 16, 06:10:00 PM, Mtoa Maoni: Anonymous

    Mbona ukinunua BWM haubandui nembo?
    Mbona ukinywa Coca Cola haubandui nembo?
    Si mambo ya quality jamani au?
    Kama wangetaka ibanduliwe si wangeining'iza...
    Au kama haitakiwi kuonekana si wangeshonea ndani?

    We toa sababu za msingi kwa nini lebo itolewe.. halafu sisi tutachuja hoja

    ACHA USHAMBA....YALE NI MAGARI...NA HIZI NI NGUO...KAMA UNA JEURI YA KUACHA LEBO MBONA PRICR TAG UNAIONDOA??
    UKWELI NI KWMBA...MLALAHOI WEWE UMEJIKUNG'UTA UMEWEZA NUNUA SUIT YA DUKANI BASI HADI KILE MTU AJUE...KEEE.WENYE KUJUA DESIGNER SUIT HAWAHITAJI KUONA LABEL KUIJUA KAMA HIYO NI DESIGNER SUIT.KAMA UNA UWEZO WA KUINUNUA SUIT...KWANINI USIIBEBE HADHI YAKE BASI...HEBU WATAZAME WENYE SENTI ZAO...HATA SIKU MOJA UMESHAWAHI ONA MTU KA SEAN JOHN COMBS AKA P.DIDDY ANAVAA SUIT NA LABEL?NA MBWEMBWE ZAKE ZOTE....KWENYE LABEL SIJAONA...NI USHAMBA!PERIOD!

    ReplyDelete
  14. Sijawahi kufikiri hata siku moja juu ya lebo mpaka nilipoona kwenye haya maoni.
    Sioni shida ikibaki au ukiondoa, niuamuzi wa mtu.
    Tuache kuitana washamba kwa vionjo vyetu.
    Na baada ya kusoma maoni tofauti tofauti bado sijaona kama kunasababu ya kutoa au kuacha.
    Anayetoa ni sawa kwake na anayeacha ni sawa kwake.
    Kwa wale wanaokereka "pilipili ya shamba inawawashia nini?"

    ReplyDelete
  15. dah lakini ukiangalia kwa ukweli zaidi ni ushamba wa aina fulani kwanini mtu uvae lebo iko nje.uamuzi wa busara kni kuto kuvaa tu suti za namna hiyo kushonesha ndiyo dili

    ReplyDelete
  16. Jamani mimi ni mfanyabiashara wa suti ughaibuni hizo label HAZITAKIWI ZITOLEWE na ndio maana zimeshonewa. Zinazotakiwa kutolewa zote ziko loosely msiharibu suti zenu bure.

    ReplyDelete
  17. Huku USA kuna kitu wanaita "Return Policy".iankuruhusu kurudisha nguo within 90 days toka siku uliponunua. Mimi kama nataka tu kuazima nguo...huwa nanunua navaa kwenye okeshini yangu...kisha narudisha...sasa hapo ndo utanikuta na Labels...ha ha ha..!!! Ila jamani tuongee ukweli...Labels ni "Ushamba wa hali ya Juu"...yaani inaudhi sana kuona watu wamevaaa suits an labels sijui wanatafuta nini? Acheni jamani huo ushamba..mnatuchosha wenzio..!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...