hiki ni kikosi cha yanga kids chini ya kocha wao mzee kwala (shoto) ambaye sasa ni marehemu. wengi katika wachezaji hao waliibuka kuwa nyota wakubwa nchini katika kile ambacho wadau wanasema endapo kama mtindo huu wa kulea vipaji toka awali ungeendelea bongo tungekuwa mbali sana. wenye data za enzi hii pamoja na majina ya hao yosso msaada tutani. mie naanza kwa kumtambua gordian mapango (wa nne kulia mbele) na saidi mmanga (shoto mbele)
Home
Unlabelled
yanga kids enzi za mwalimu
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
nami naongezea Adolph Rishard wanne kutoka kushoto
ReplyDeleteDuuh sio mchezo watoto walikuwa wanakipiga hawa. mimi niliowatambua ni adolf rishad wanne toka shoto waliokaa. mohamedi mkweche wa tatu toka shoto waliosimama na wakwanza toka kulia ni juma pondamali mensha
ReplyDeletemdau
kisiju pwani
Duh kweli tumetoka mbali . Michuzi kwa kusaidia tu mimi nimekuona wewe hapo wa kwanza waliochuchumaa kutoka kulia hahahahahaha.
ReplyDeletemkweche wa tatu ,kassim manara wa tano waliosimama, wa kwanza kulia juma pondamali. waliokaa wapili kulia ni marehemu mwarami mohamed shemeji wa jumanne hassan masumenti. nawakilisha mdau wa dom
ReplyDeleteJamaa Ana Convers ya nguvu. Vijana wa Sunderland wapo wapi?
ReplyDeletewa tatu chini toka kulia ni, Jafari Abdulahamani
ReplyDeletekweli Tanzania kichwa cha mwendawazimu hii program ilifanikiwa ile mbaya hawa jamaa walikuwa tishio africa namaanisha waliweza kupambana na timu yoyote ile katika africa ilikuwa tunakwenda kuangalia mpira kifua mbele na matumaini makubwa ya ushindi lakini kilichotukuta mpaka leo tumekuwa nyuma kimpira mungu anajua watu wanakwenda mbele sisi tunarudi nyuma hata mtu akitaka kubisha mfano hai huo hapo juu nakumbuka tulikuwa tunamzomea juma pondamali akipita kuelekea jangwani saa saba mchana wewe jua kali saa hizi mpira utakuua akaja kuwa mmoja kati ya makipa mashuhuri nchini haihitaji mambo ya ajabu vile vile alivyofanya coach victor mtu mwingine afanye miaka mitano au kumi na sisi tutaonekana kwenye world cup
ReplyDeleteEh bwana eh! Huyu Wa pili (Walio simama kutoka kushoto)anafanana na Mohamed Saidi Sululu (ARUSHA), Mapango, Jaffari Abdurahman,Mkweche, na Pondamali.
ReplyDeleteDah kweli nimewakubali wa enzi hizo,mimi hapo hata sina dalili ya kuzaliwa.ila nimefurahi nimemuona kocha wangu wa timu yangu ya mtaani care boyz pale kinondoni DSM Gordian Mapango.Yanga endelezni huo mpango wa yosso!!!!!!!!!mdau Uk
ReplyDelete