Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Mh. Reginald Mengi akizindua kitabu cha historia ya maisha ya aliyekuwa Gavana wa kwanza wa Benki Kuu Tanzania Mzee Edwin Mtei anayeonekana na mai waifu wake Johara Mtei. Kitabu hicho kinaitwa "Kutoka Uchungaji wa Mbuzi kwenda Gavana". Hafla hiyo ilifanyika Dar usiku kuamkia leo.
----------------------------------------
The new book from GOATHERD to GOVERNOR:
The Autobiography of EDWIN MTEI is now available
in Google Book, you can read and get some gist on it.
Wishing you all nice reading.

Adam Jackson Foya
P.O.Box 42329 Dar Es Salaam,
As much as you are critical, be constructive"

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. "Mchunga mbuzi mpaka gavana", rekebisha jina la kitabu.

    ReplyDelete
  2. Nakubali na hoja ya kwanza. Jina la kitabu sio zuri. Abadilishe kama inawezekana.

    ReplyDelete
  3. Jina la kitabu ni baya baya mno; kwa hadhi yake anatakiwa akipe jina zuri na bora (Jina lajiuza lenyewe!kwa jina hilo hamna mtu na akili zake timamu atae nunua)!

    ReplyDelete
  4. Wadau naomba kueleweshwa Edwin Mtei ana uhusiano na haya mabasi ya mtei bus service? mengi yake yakifanya safari kati ya arusha,manyara,singida na machache dar?vilevile nyumba za kulala wageni nyingi zenye jina stereo hapa arusha na hoteli ya kisasa ya stereo karibu na A.M hotel(1988)ya arusha?je mali hizo zinauhusiano na gavana huyu wa zamani?au ni ndugu zake?

    ReplyDelete
  5. Jina kweli Baya, abadili.

    Huyu Mtei ni Gavana wa kawanza TZ, alikuwa hapatani sana na Mwalimu, Akaanzisha CHADEMA, Mtoto wake kaolewa na Mh. Mbowe wa CHADEMA, sio mwenye mabasi, labda ndugu yake.

    ReplyDelete
  6. Mmeshaambiwa kuwa kitabu kinahusu maisha yake ninyi wasomi waleo mnataka abadili jina la kitabu kinawahusu nini? kwani maana ya maisha ya binafsi ya mtu ninini? acheni ushamba na kuiga mambo msiyoyajua. jina la kitabu chake limesimama vizuri na kwa maana ya maisha yake yupo sahihi, sasa ninyi kama amtanunua ni kwa sababu zenu. sisi tunaoelewa maana ya maisha ya mtu tutanunua kwa maana inasisimua sana.

    ReplyDelete
  7. Ni za kwake na ndio maana Nyerere hakumpenda. kuwa na mali ni disqualification kwa nyerere. Wivu tu na uvivu umejaa kwenye fikra zenu kuwa mtu hawezi kuwa na mali. basi endeleenu kukumbatia umasikini.

    ReplyDelete
  8. Nyinyi wote mnaosema abadili jina la hicho kitabu mbona hamsemi aandike jina gani?

    Na pili hamjui mnachoongea. Na inaelekea hamjui sanaa ya kutengeneza jina la kitabu.

    Hilo jina liko safi sana, na naamini litavutia walengwa kununua hicho kitabu.

    Jina linaonesha hicho ni kitabu cha "motivation" Mtei anajaribu kutoa mwanga kwa wengine ambao wako chini na wanataka kwenda juu ... ndio maana halisi ya kuweka "Mchunga mbuzi" katika title.

    ReplyDelete
  9. Jina la kitabu ni zuri sana,
    kwa ajili linasema alikotokea na mpaka kilele cha kazi yake.

    nyinyi mnaoona jina baya, Jina sio baya bali nyinyi akili zenu ndio mbaya na hamna hulka ya kusoma vitabu.

    ReplyDelete
  10. Mwl Nyerere alitofautiana na Mtei si kwa sababu ya utajiri ila ni kutokana na Mtei kumshauri Mwl kuingia mikataba na WORLD BANK na IMF,vitu ambavyo Mwl hakutaku kabisa. Mdau hapo juu Nyerere hakuchukia watu walopata mali kiuhalali bali watu waliopata mali kwa njia ya ufisadi au wizi.

    ReplyDelete
  11. BABA MKWE WA MBOWE HUYO NA MWENYEKITI WA KWANZA WA CHADEMA.... JINA LA KITABU NI HIARI YAKE KUTAFUTA LAKINI HALINA MVUTO KABISA ....

    ReplyDelete
  12. Kitabu kinaelezea maisha yake Mzee Mtei.

    Kabla hajaanza shule ya msingi alikuwa mchunga mbuzi kama waafrika wengi. Wengine ni Baba yake Obama pia alichunga mbuzi kabla ya kuanza shule, Mwalimu Nyerere pia alichunga mbuzi kabla ya shule.

    Mwl. Nyerere baada ya kutofautiana mawazo ya kisera na Mzee Edwin Mtei hakumchukia, ndiyo maana anampigia debe, kumkingia kifua na kumpatia baraka zote akapata ajira IMF/WB kama mkurugenzi huko Marekani.

    Nyie watoto wa Ocean Road pia mlikuwa mnawinda sungura mapori ya kwa 'Pipino' na Msasani/Masaki Dar-es-Salaam, vilevile mlikuwa mnapopoa ukwaju, embe ngongo na ubuyu pia- kila mtu kufuatana na mazingira yake kabla hamjaanza shule na pia wakati wa likizo.

    Mdau
    Gerezani DSM

    ReplyDelete
  13. Kama hamelewi Mchungaji wa Kondoo/ mbuzi ni mtu muhimu sana Afrika, Mashariki ya Kati, Ulaya na hata Marekani(Cowboys).

    Ukiwa katika majiji ya ulaya utakuta majina Shepherd Bush (London) n.k.

    Mchungaji mbuzi/kondoo pia huja kuwa kiongozi mzuri wa watu, chama (Chadema/Tanu), tembeeni duniani muone.

    Mdau
    Athens, Ugiriki

    ReplyDelete
  14. Mtei, ni muasisi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), katika kitabu chake licha ya historia yake ndefu kutoka mchunga mbuzi hadi Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), ameelezea jinsi Kenya ilivyoshiriki kuvunja iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) mwaka 1977.

    Awali, Mwenyekiti wa Bodi ya Uhariri wa Gazeti la Raia Mwema, Jenerali Ulimwengu, alisema ingawa wengi wanabeza wasifu wa mtu akiandika mwenyewe kutokana na kujipamba, lakini Mtei ameeleza ukweli kwenye kitabu hicho.

    Ulimwengu alisema Mtei akiwa na umri wa miaka 33 alipewa jukumu la kuanzisha BoT na kazi ya ujenzi aliipa Kampuni ya Mecco (Kampuni ya Kitanzania)na kuongeza kuwa, iwapo viongozi waliopo wangefuata uzalendo huo, kasi ya maendeleo ingekuwa kubwa.

    Alisema licha ya mwaka 1979 kuondoka serikalini baada ya kutoafikiana na Mwalimu Julius Nyerere kuhusu sera za uchumi, bado aliendelea kukubali umahiri wa kiongozi huyo.

    Mtei alisema kati ya mambo ambayo anajivunia aliyoanzisha na kuendesha ni BoT na Chadema na kwamba, Mwalimu Nyerere licha ya kutofautina kisera bado amekufa akimuita gavana.
    www.ippmedia.com

    ReplyDelete
  15. it was not personal. ilikuwa ni mtu na bosi wake kutofautiana kimtizamo ktk kazi. hilo likapelekea Mtei kuandika barua ya kujiuzulu na Mwalimu alikubali uamuzi huo.

    Mtei aliendelea kuwa na mahusiano na Nyerere. baadaye Nyerere alikubaliana na mawazo ya Mtei na akaruhusu majadiliano na IMF yaendelee. Mtei alitoa ushirikiano mkubwa ktk majadiliano hayo ambayo yalianza wakati wa Mwalimu, lakini yalipamba moto wakati wa utawala wa Ali Mwinyi.

    Mtei alikwenda IMF akiwa na baraka za serikali ya Nyerere. aliporudi Tanzania, Raisi Mwinyi alimteua kuwa Mwenyekiti wa Tume ya kurekebisha mfumo wa kodi. Ripoti ya Tume ya Mtei ndiyo iliyopelekea kuanzishwa kwa Tanzania Revenue Authority.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...