Rogers Mtagwa
Bondia Rogers Mtagwa anayeishi Marekani atapanda ulingoni Januari 23, 2010 na kupambana na bondia Yuriorkis Gamboa katika piagno la raundi 12 litakalofanyika Madison Square Garden jijini New York katika pambano la ubingwa linalotambuliwa na HBO katika uzito wa Unyoya (Feather weight).
Rekodi ya Mtagwa inaonesha keshazipiga mapambano 26, kashinda kushinda 13 kwa pointi, kupoteza mawili na kushinda kwa KO 18.
Gamboa amecheza mapambano 16 na kushinda kwa KO 14, mawili kwa pointi na hajapoteza hata pambano moja.
Aidha, mbali ya pambano hilo pia kutakuwa na pambano la uzito kama huo ambalo litamshirikisha Juan Manuel Lopez atakayezichapa na Steven Luevano.
Pambano jingine linalotarajiwa kufanyika siku hiyo jijini Pasay nchini Philippines, Donnie Nietes atazipiga na Ivan Meneses.
Chanzo cha habari hii
mwaha alikosa techniques tu mpambano uliopita na kama ingeongezwa raundi 1 nyingine basi mtagwa alikuwa anamaliza kwa ko.
ReplyDeletenatumai sasa ameshapata techns na atashinda. kila laheri/lakheri/raheli/rakheli? kiswahili kigumu jamani
Mcuba with Olympic gold medal basi iko kazi. Technically Roger hataweza kumshinda Mcuba huyu kama ni ushindi itakuwa ni kumvizia achoke round za mwisho. Natabiri Mcuba atashinda kwa knockout!
ReplyDeleteWatuchungie tuu kijana wetu wasimpambanishe na mijitu iliomzidi uwezo kwa Tamaa zao za madola!Youtube mapambano ya Roger utagundua jamaa ni kama boxing bag anauwezo mkumbwa wakuvumilia makonde mazito raundi zote kumi na mbili lakini side effect za hao makonde hasa kichwani ni kubwa..
ReplyDeleteBwana Michuzi nimecheki fights kama tano za Mtagwa, this Guy is a piece of boxing art!!jamaa anaongeza maujuzi kila fight, kuna promoter maarufu wa Philly alikiri kwamba amekuwa kwenye bizness hiyo kwa miaka mingi,anaamini Rogers yupo Top Ten yake ya vifaa!!ukicheki mpambano alioupiga Madison na ya nyuma,ni tofauti kabisa, anazidi kuwa mzuri,tumuombee ndugu yetu huyu!!
ReplyDeletefeather weight= uzito wa unyoya hahaha kweli kiswahili kitamu....hiyo nimeipenda sana mie....anyway GOODLUCK KAKA MTAGWA
ReplyDeleteJana niliangalia ngumi kati ya kijana wa kitanzania(obote umeme) na veto sijui wa wapi.yaniii,nimesikitika sana mtanzania alivyokuwa anapigwa masumbwi,pia nilijisikia huruma sanaa kwani alijiona inferior sana kwenye ulingo,anakinga ngumi saba anarusha moja,sita zinamtandika.huruma sanaa,hakuna techniques,pia hata water bottle,wanatumia chupa ya kawaida nyumbani na kikombe cha plastiki.poa baada,Watanzania jamani,msitusikitishe
ReplyDeletemdau uk
Wewe mwandishi wa hii stori hesabu yako haiko sawasawa, amecheza 26, ameshinda 13 na kupoteza 2, what happened to the other 11 fights? Niliwahi kuona enzi za GTV Mtagwa ana record mbaya sana, idadi ya mapambano aliyoshindwa ni kubwa sana, sio kama hivyo unavyosema. Kama alivyosema mdau mmoja hapo, wasimtumie tu kama njia ya kuwapandisha mabondia wao, mi namuonaga picha zake ni kama analazimishwa vile kupigana halafu kama hatibiwi majeraha anayoyapata, anagalia tofauti ya sura kati yake na bondia atakayepambana nae, uso wake umevimba chini ya macho kabla hata ya pambano, ni nani sijui anaangalia maslahi ya Rogers huko!
ReplyDelete