Mapacha watatu kati ya wanne katika onesho lao Kinondoni Stereo jijini Dar Jumatatu usiku. Toka shoto ni Khalid Chokoraa, Jose Mara na Kalala Junior. Pacha wa nne Chazz Baba hakuonekana baada ya kuingia mitini bila shaka kuogopa kupoteza ajira Twanga Pepeta.
Uzinduzi wa bendi ya mapacha wanne uliingia kwikiwi Jumatatu usiku baada ya pacha mmoja kujitoa kinyemela.
Bendi hiyo iliyokuwa izinduliwa na wanamuziki mahili hapa nchini ambao ni Khalid Chokora, Jose Mara, Kalala Junior na Chaaz Baba iliigia dosari baada ya Chaaz baba kujiengua kinyemela wakati wa onyesho,

Hata hivyo pamoja na kujitoa kwa mwanamuziki huyo uzinduzi ulifana na kuwafanya wapenzi waliojaa katika ukumbi wa Stereo uliopo Kindondoni kupata burudani ya aina yake. Hata hivyo mwanamuziki Chokoraa alisononeka sana kwa mwenzake Chaaz kuwa kigeugeu.

Bila shaka hii inafuatia mkwara mzito aliotoa mkurugenzi wa bendi ya Twanga Pepeta Da' Asha Baraka alipotangaza kuwa mwanamuziki anyefanya kazi katika bendi hiyo akionekana katika uzinduzi huo atafukuzwa kazi.
Tayari kuna minong'ono kwamba Chokoraa ameshasimamishwa kazi toka wiki iliyopita kwa kile kilichotajwa utovu wa nidhamu na uaminifu, na kwamba ajira ya Kalala Junior nayo imeshaota mbawa baada ya kushiriki kwenye onesho hilo.
Uchunguzi wa Globu ya Jamii umebaini kwamba wanamuziki hao watatu wa Twanga Pepeta hawakuwa na nia ya kuhama bendi na kuanzisha ya kwao, bali kutumia muda wa ziada wa kazi kwa kujiingizia kipato. Jumatatu ni siku ya mapumziko kwa bendi ya Twanga Pepeta.
Vile vile Redio Mbao zimedatisha kwamba Da'Asha, ambaye si mpenzi sana wa upinzani katika fani, machale yamemcheza kwa kile kilicoelezwa kwamba endapo Mapacha hao wanne wangefanikiwa wangemtoroka.

Wanamuziki nyota wa bendi mbalimbali wakiwemo wa Twanga walihudhuria onyesho, ambalo lilipambwa wenyeji wa onesho, Top Band ya TID.

Ila katika hali isiyokuwa ya kawaida habari zinadatisha kwamba baadhi ya wanamuziki wa bendi ya MAPACHA WANNE, akiwemo mpiga drums walikamatwa na polisi kwa sababu ambazo bado kuwekwa wazi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 24 mpaka sasa

  1. Ndio maana nasisitiza Wasanii wetu kwenda shule ili wanapoingia mikataba na watu kama Mh. Asha Baraka wajue wanaingia katika mazingira gani na pia kuelewa haki na wajibu wao.

    Vinginevyo wataendelea kuwa wa kubinywa chini ya mikataba wasioielewa vyema kama ambavyo baadhi ya Machifu wetu walivyouza utu wetu kwa 'peremende' toka kwa Wakoloni.

    Aidha hapa ndipo ule umoja wa Wasanii unapotakiwa kuingilia kati na kutetea haki za wanachama wake endapo kweli wameonewa.

    ReplyDelete
  2. maisha ni magumu acheni watoto wajiogezee vipato uzandiki tuu

    ReplyDelete
  3. jamni huyu da asha vipi...waache vijana watafute hela.. unafiriki kuna mtu anapenda kuajiriwa siku
    zote za maisha yake?kama vijana wameamua kujituma waache...big up mapacha wanne...just go on and just biliv in yourselves.

    ReplyDelete
  4. Naomba nichukue nafasi hii kuwapa moyo Chokoraa, Kalala Juniour na Jose Mara wasikatishwe tamaa na matukio machache yaliyotia dosari onyesho lao. Siku zote mwanzo ni mgumu na kama kweli wana nia na hicho walichokianzisha, iko siku watafanikiwa.

    Utafanya kazi kwa Asha hadi lini! Lazima wawe na mikakati ya kufanya kazi kivyao ili kujiongezea kipato na hatimaye kuwa na chao wenyewe!

    Watu kama Chaaz wapo katika jamii! Ni waoga wa maisha, ni waoga wa kujaribu! Wamuweke pembeni, wasonge
    mbele.

    ReplyDelete
  5. CHAMUDATA MKO WAPI??????????????

    Huyu Asha Baraka aache ujinga, hao

    vijana wameamua kutafuta extra

    income kimtindo then yeye anabana

    nini maana yake??

    Then Chalz baba, mbona umenianguasha ndugu yangu?? mi nakuaminia wewe ni kamanda then unatishika na huyo mrugaruga!

    Huyo ana ujanja kwenu, akiwatimua nyie watatu, ni sawa na yeye kuamua kuua Twanga Pepeta!

    Ashakum ci matusi: "Asha Baraka anatishia kujamba wakati anaarisha"

    Komaa Chalz, asiwatishe huyo

    (Michuzi pls usiibanie hii comment)

    K'dume

    ReplyDelete
  6. wadau naomba msaada kidogo hivi jose mara ameondoka fm academia?

    ReplyDelete
  7. Huyo mama hajui ushindani na ni roho mbaya, mbona FM hawajasema wakati Jose ni star kule? KtK ulimwengu wa sasa wa ushindani kujiamini muhimu, angefanya busara kama angeongeza donge nono kwa vijana ili waridhike.Big up Mapacha tutawa support mpk mwisho

    ReplyDelete
  8. Yaani wangejua wangeuchuna, mimi sasa week end ntakuwa busy na familia jumapili kazini, jumatatu MASAI CLUB kupata burudani ya Ukweli ya Mapacha watatu..Narudisha card yangu ya uanachama wa Twanga.

    ReplyDelete
  9. Mkata issue kwani hiyo mikataba yenyewe wanayo? wamiliki wa mabendi wanachojua ni kujinufaisha wanamuziki wanaishia kuwa ombaomba. sasa wakiamua kufanya ujasiliamali wanawabania. WATATUPOTEZA WASHABIKI.

    ReplyDelete
  10. huyo mwanamke ni tatizo la huo muziki wa bongo kwanza yeye ndio mwanzilishi wa kuua muziki wetu asilia na kuwashawishi watu kuimba kiswahili kwa mipigo ya kikongo na kama haitoshi alihakikisha kila bendi inayooanzishwa ife mifano ipo ,bambino,extra,dm nk bila kusahau kuwashakizia immigrations wacongo.sasa nataka kumwambia kuwa huwezi kumzuia artist maishani,na huyo chalz tatizo lake mario ila atapona tu.sasa kama kufanya kazi za ziada ni kosa mbona yeye hawajamfukuza bima.kenge kabisa

    ReplyDelete
  11. Mwacheni Dada Asha nyie mashabiki uchwara. Nyie hamuoni huko ni kunzisha bendi ndani ya bendi. Wao mapacha wanne sijui watano kama wana ubavu siwaache kazi kabisa waanzishe bendi yao. Utawatumikia je matajiri wawili wakati mmoja. Acheni kuingilia biashara za wenzenu kwa mambo msiyoyajua. Hata mngekuwa nyie msingekubali

    ReplyDelete
  12. Rais JK alivyotutembelea San Fransisco miezi kadhaa ilyopita alitoa joke moja kuhusu dual nationality. Alituambia watanzania wenzenu kule Bongo wanaonekana kuupinga huu mpango wa dual nationality. Wanasema nyie mnataka Kula Huku na Huku, chagueni upande mmoja.
    Sasa ndyo hayo ya hao Mapacha. Asha Baraka kisha waambia wana uhuru wakuchagua upande mmoja.

    ReplyDelete
  13. Aah kama ndvyo hivyo alivyofafanua mdau hapo juu kuhusu Kuruhusiwa kwao kuanzisha bendi yao sioni kama uongozi wa ASET una makosa. Kila mtu ana haki ya kulinda nembo yake ya biashara. Hao mapacha wametemgenezwa na ASET. NANI ALIKUWA ANAWAJUA KABLA. Waanzishe bendi yao wenyewe kama ni rahisi, na siyo kujimbaza kivulini huku wakivuta mishahara Twangapepeta

    ReplyDelete
  14. KWELI JAMBO USILOLIJUA SAWA NA USIKU WA GIZA. ASHA BARAKA HAJAWABANIA HAO MAPACHA, ISPOKUWA WANAMUZIKE WENZAO NDANI YA BENDI NDIYO WANAOWAGOMEA KWA HUO MPANGO WAO, KWA KUDAI KWAMBA NA WAO WAKIAMUA KUFANYA HIVYO THEN KUTAKUWA NA MPASUKO MKUBWA NDANI YA BENDI YAO, AMBAPO MAFANIKIO YAO HAPO WALIPO YAMETOKANA NA UMOJA WAO WA MUDA MREFU. SASA KWA NINI WENZAO WAJITENGE?. WANASEMA KAMA NI KUPIGA JUMATATU BASI WAPIGE WOTE, KWA NINI WAO WAJIBAGUE?. NANI ANGEWAJUA BILA KUPATA SUPPORT YAO?

    ReplyDelete
  15. Wadau mbona mnpenda sana kumsakama Da Asha?. Siyo kila maamuzi yanatolewa na Da Asha. Bendi ya Twangapepeta iko chini ya uongozi wa kampuni ya ASET anbayo ina Board yake ya Wakurugenzi na Management yake. So maamuzi mengine huwa si yake. Mwacheni huyo M NEC wa watu. Kwanza siku hizi anajishughulisha zaidi na mambo ya siasa. Utawala wa kila siku wa bendi upo chini ya wanamuziki wenyewe wakiongozwa na Abuu Semhamdo, Amigolas, Luiser Mbutu Chalz Baba na wengineo

    ReplyDelete
  16. Hakuna mwanamuziki aliyekamtwa, ispokuwa kuna wanamuziki wawili wa Dimond Musica mpiga solo na mpiga Bass wa Mapcha hao walikuwa wamefuatwa kwa ajili ya kuhojiwa uhalali wao wa kupiga katika kikundi hicho huku wakijua kuwa Working Permits zao wakiwa ni raia wa DRC haziwaruhusu kufanya kazi zaidi ya ile ya Diamond Musical KUTOKANA NA SHERIA za uhamiaji.

    ReplyDelete
  17. Mdau unayesema kuwa hawa wanamuziki hawana mikataba- hii si kweli, wana mikataba. Kampuni kama ASET itakuwa na mwanasheria ambaye anashirikishwa kwenye uaandaaji wa mikataba na ni obvious kuwa mikataba hiyo itakuwa na vipengele vinavyom favour mwajiri na kumbana msanii.

    Si lazima wasanii wetu waende shule kama mdau wa kwanza alivyosema lakini wasisite kutumia hela kidogo na wao ili wawe na watu wanaowashauri kwenye mambo ya kisheria. Mwajiri akikutela mkataba mezani usisaini hapohapo, uchukue ukaupitie, ujadiliane na mshauri wako wa mambo ya sheria- na kama una matakwa yako yaingizwe kwenye mkataba huo iwapo mwajiri atakubaliana na wewe. Haya ni mambo ya majadilianao na makubaliano baina ya pande mbili. 9 out of 10, kama una kipaji- mwajiri atakubaliana na masharti yako kwa kuwa anakuhitaji wewe zaidi ya unavyomuhitaji yeye. Lakini kwa kuwa wengi wa wasanii wetu hawana mipango endelevu ya muda mrefu wanaishia kuingia mikataba ambayo inawanyonya na kuwabana kwa muda mrefu bila hata wao kujua.

    Hawa mapacha wanne, kama wangekuwa wanaona mbali na hili wazo la kuungana pamoja zing zong wakati wa siku zao za off lingekuwa vichwani mwao, wangeweza kuliweka wazi kwa waajiri wao kupitia mikataba yao na wala kusingekuwa na tatizo.

    Sijafurahishwa na kitendo cha Da' Asha but I kind of see where she is coming from. Suala kubwa hapa ni conflict of interest kwa hawa wasanii, yeye angependa kuona tungo, ideas na nguvu za hao vijana wake zinaelekezwa kwenye bendi yake. Hata ingekuwa mimi, ingeniuma sana kama hawa vijana wangetoa nyimbo kali zika hit wakati kwenye ajira yao kuu wanaimba utumbo, and to be honest ningependa kuwaona wanapumzika siku yao ya off ili wakirejea kazini waweze kuperfom vizuri! Ndio yale yale- kwa kuwa mwalimu kaanzisha tuition, akiingia darasani analipualipua ili uende tuition yake, daktari kafungua dispensary ahamisha dawa zote toka hospitali ili wote muende huko, nk.
    Ni hayo tu machache, wadogo zangu msife moyo, mnaweza kusubiri hadi hiyo mikataba yenu ifikie kikomo then kabla hamjasani mipya, mchukue mapendekezo yangu hapo juu.

    Kila kheri
    Kana-Ka-Nsungu

    ReplyDelete
  18. Da'Asha Baraka,
    jaribu kufungua geti la upizani katika gemu la mziki,
    Mziki bila ya upizani sio mziki,tangu enzi za waenga tuliwaona akina Marehemu Mbaraka Mwishehe(RIP) wa Moro jazz na mpinzani wake Marehemu Juma Kilaza.
    Westen Jazz na Dar-es-salaam Jazz,Patric Balisidya na Afrosa na wapinzani wao Marjan Rajabu mwana manyema na Safari Tripers upo hapo?
    Leo Sikinde na msondo Ngoma wanaendeleza destuli na mila hiyo.
    Lakini upinza unapofika kwako Da Asha Baraka,basi lazima kutakuwa na kutishiana maisha! kama vile wewe ndiye mungu unayetoa ridhiki?
    Tumeshuhudia jinsi ulivyokuwa unazishimbia kaburi na kuzika zingali hai juhudi za wanamziki akina Ali Choki an Extra Bongo,Prince Muhmin na Mambo Mshike mshike Band(Double M),
    Da'Asha tusitafute mchawi wa mziki wa dansi wa Tanzania wewe ndiye kinara wao.
    Biashara ya mziki lazima kuwe na ushindani ndio mtego wa kuwanasa washabiki.

    ReplyDelete
  19. Mdau hapo juu uliyesma eti mbona FM Academia hawakumzuia Jose Mara akiwa kama star kwenye hiyo bendi ya Wana Ngwasuma,kama huna habari ujue mpango mzima wa hiyo group ya Mapacha wanne umesukwa na Bendi hiyo ya FM ikiwa ni moja ya mbinu za kuidhohofisha Twanga pepeta baada ya kugundua wamezidiwa kete vibaya sana katika kipindi cha hivi karibuni

    ReplyDelete
  20. Inawezekana anony wa 03.36pm uko sahihi, kwani hata matangazo ya onyesho lao hao mapcha siku ya jumatu, lile gari lao walofanyia P.A kwa ajili ya matangazo alilokuwa anazunguka nalo Chokoraa ni gari la FM Academia, kwani nililiona likiwa na maandishi ya FM Acdemia mbele na nyuma

    ReplyDelete
  21. Habari zilizozagaa mjini zinasema Mapacha wa nne ulikuwa ni mpango wa kuanzishwa kwa FM Academia B mbapo Jose Mara alikuwa awe Kiongozi wa Group hilo akisaidiwa na Kiomgozi Msaidzi Khalid Chokora, na taratibu za usajili wa bendi hiyo ya pili ya ngwasuma zilikuwa zikiendelea. Uongozi wa ASET wanaomiliki Twanga pepeta wameustukia mpango huo na inaelekea wamefanikiwa kuzima mapinduzi hayo

    ReplyDelete
  22. Jamani mbona mnatuchanganya sasa. Naanza kutaka kuaminiamini kuwepo kwa mkono wa Ngwasuma manake siku ile ya onyesho la mapacha wanne ambalo baadye likwa la mapacha watatu baada ya Chalz Baba wa kuwatosa wenziwe na mpiga Drums wa Twanga Pepeta James Kibosho kuingia mitini, ilibidi Pchu Mwamba wa FM ACADEMIA ndiyo apande stegini kucharaza Drums huku kukiwepo wanamziki wengi wa FM Academia wakiwapa support na wakishangilia mapacha hao kwa nguvu. Dah! kweli hapa kuna jambo limejificha

    ReplyDelete
  23. Jamani swala la upinzani si la mtu kupenda au kutokupenda. Competition is always there kwenye siko huria. So Unapokuwa kwenye game lazima ufanye juhudi za kuuzidi upinzani wa aina yoyote ili uendelee kuwa kwenye game, hiyo ndiyo siri ya mafanikio, na ndiyo kitu kinachofanywa na Da Asha na management yake ya ASET. Hongereni sana kwa kuwa mstari wa mbele always kama CCM

    ReplyDelete
  24. Mapacha watatu original yaani Kalala, Chokora na Chalz Baba jana waliungana pamoja na kundi zima la African Stars Band- Twanga Pepeta, baada ya Khalid Chokoraa kuonekana akishambulia jukwaa katika Ukumbi wa Bilicanas kama alivozoeleka kabla ya kusimamishwa na Uongozi wa ASET. Onyesho hilo la jana la usiku wa mwafrika= Club Bilicanas, lilitoa taswira inayoonyesha mpango wa watatu hao kujiunga na mwenzao Jose Mara wa FM Academia(Ngwasuma) katika kukamilisha uundwaji wa Bendi ya mapacha wanne sasa umeota mbawa. BRAVO TWANGAPEPETA. nawaaminia

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...