Mwaka mpya, na mambo mapya. CRDB inakuja na droo zitazotokana na Manunuzi ya Bidhaa na huduma kwa kutumia TemboCardVisa, ambapo walengwa ni wateja wote wa Benki ya CRDB na watumiaji POS za Benki ya CRDB.

Benki ya CRDB Imeendelea kukusikiliza wewe mteja wake kwa kukupa huduma bora na za kiwango cha juu kabisa.
Kama hilo halitoshi, Benki ya CRDB sasa inakupa nafasi ya kutimiza ndoto yako ya kujishindia safari ya kwenda Afrika Kusini kushuhudia Fainali za Kombe la Dunia live na Zawadi nyingine kem kem kama Luninga plasma ilionginishwa na DSTV, Fulana, miamvuli, kofia n.k

Unachotakiwa kufanya ni
kutumia kadi yako ya TemboCardVisa kufanya malipo ya zaidi ya Shilingi 50,000/= kupitia mashine za malipo za Benki ya CRDB (Point of sales)
kila ununuapo bidhaa au kupata huduma kwenye Maduka, Migahawa, Supermarket, Malls, Maduka ya Dawa, Vituo vya mafuta, ulipiapo mbuga za wanyama (TANAPA) au ukilipa kodi (TRA) ili uweze kuingia kwenye draw na kujitengenezea nafasi ya kushinda.

Zawadi zote zitapatikana katika draw kubwa mbili ambapo:

Draw ya mwezi wa kwanza na wa pili:

Mshindi mmoja, atajishindia safari, chakula, malazi na Ticket ya kushuhudia live mechi ya kombe la Dunia Afrika kusini

Mshindi wa Pili na Watatu watajishindia Luninga ya SONY bapa (Plasma) inchi 32 zilizounganishwa na kulipiwa DSTV kwa mwezi mzima wa mashindano!

Wasindi wengine watano watajishindia zawadi kem kem ikiwamo T-shirts, Mipira, miamvuli nk.

Draw ya mwezi wa tatu:

Washindi watatu wa mwanzo, kila mmoja atajishindia safari, chakula, malazi na Ticket ya kushuhudia live mechi ya kombe la Dunia Afrika kusini.

Mshindi wa nne na watano,watajishindia Luninga za SONY bapa (Plasma) inchi 32 zilizounganishwa na kulipiwa DSTV kwa mwezi mzima wa mashindano!

Mfanyabiashara ambaye POS zake zitakuwa na miamala mingi nae atajishindia tiketi ya kwenda kushuhudia fainali hizi. Pia, wafanyakazi wa sehemu za biashara zenye miamala mingi pia watajishindia pesa taslimu kuanzia shilingi 100,000 mpaka shilingi 250,000

Anza sasa kufanya malipo kwa kutumia kadi yako ya TemboCardVisa na uwe mshindi!

CRDB Bank
Benki inayomsikiliza mteja


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Bernard Membe akikata utepe kuzindua huduma za ATM za kwenye magari wakati wa sherehe hizo.

Mh. Membe akibofya kwenye moja ya kompyuta za kwenye magari ya ATM baada ya kuzindua. Nyuma yake ni Mkurugenzi Mkuu wa CRDB Dr. Charles Kimei na maafisa wengine.

Mh. Membe akiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya CRDB Bw. Martin Mmari, Mkurugenzi Mkuu wa , CDRB Bank Dk. Charles Kimei na Mkurugenzi wa Masoko na Utafuti wa CRDB Bi. Tully Esther Mwambapa wakati wa uzinduzi wa huduma ya matumizi ya TemboCardVisa
Mh. Membe akiwa na viongozi wakuu wa CRDB pamoja na mwakilishi toka ubalozi wa Afrika Kusini Carol Rath wakati wa uzinduzi huo.
Mh. Membe akiwa na uongozi wa CRDB Bank na watendaji kitengo cha TemboCardVisa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Bravo CRDB. You started as a local bank for the poor - probably long before Tulli Mwambapa was born - and who would have thought then, that you would gear up to such success within a few decades. Julius Nyerere would surely be very proud of your achievement.

    I find your provision of mobile banking particularly exciting. Given our socio-economic structure, economic empowerment and security issues need be addressed alongside technical and logistical innovations. That way, it will be a win-win situation and, surely, the government and the entire business community must sperhead these efforts. The potential risks of socio-techno incompatibility are well documented and some not far from us.

    ReplyDelete
  2. hongera sana kwa kubuni huduma na bidhaa mpya kwa wateja wenu. Ila natoa ushauri mkazanie kuboresha vitu vidogo na rahisi (basics) kwanza kama foleni, ATM services nk.

    ReplyDelete
  3. hongera sana kwa kubuni huduma na bidhaa mpya kwa wateja wenu. Ila natoa ushauri mkazanie kuboresha vitu vidogo na rahisi (basics) kwanza kama foleni, ATM services nk.

    ReplyDelete
  4. mi nafikiri mkazanie kuongeza idadi ya ATM hizo gari ina maana itabidi tuzisubiri sio? na sio zitungoje? sasa nani mfalme? Mteja au moving ATM? Naomba muangalie hilo!

    ReplyDelete
  5. "TANZANIANS DREAM"

    ....At last,after many years of dreams,strugling & patiance finaly our dreams has come to reality.....
    Surely,baba wa Taifa would have been very proud of this outcome of his seeds planted for generation to come.
    I have no doubt this will be huge succes and there`s nothing to fear
    about the service,with such wise head of the Bank & well trained team of staffs,Tanzanians as well as foreigners will be given good investments advice and promt better service.
    ....Should`nt we say this is a start of better life for all......

    Mickey Jones Amos
    Denmark

    ReplyDelete
  6. Dr. Kimei is one of the greatest CEOs in Tanzania.

    Mzee huyu ni mchapa kazi na very innovative.

    (US Blogger)

    ReplyDelete
  7. Good one CRDB Bank!
    Mimi nafikiri its right time kwa watanzania kuacha kutumia cash kwenye manunuzi na kuanza kutumia TemboCardVisa kwa ajili ya urahisi na usalama.Hatuna sababu ya kujiongeza risk kwa kubeba mazigo ya cash wakati huduma hii inatupa uwezo wa kufanya malipo na maununuzi popote duniani bila kuhitaji kubeba cash.CRDB Bank should be praised for this initiative......Bravo CRDB,BRAVO Dr.Kimei na timu nzima!

    ReplyDelete
  8. Kimei ni mashine

    mimi nina shares zangu crdb na niko na confidence na investment yangu alimradhi kimei yuko pale. siku atapotoka... sijui

    ReplyDelete
  9. JK tafadhali mkabidhi Dr.Kimei TANESCO ili upuuzi wa kukosa umeme uishe.

    (US Blogger)

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...