Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Shirika la Synavate Tanzania Jane Mahela(kushoto) akijibu maswali ya waandishi wa habari juu ya matokeo ya utafiti wa hali ya demokrasia ambao Rais Kikwete aliiogoza kwa kupata asilimia 75 ya wahojiwa kuwa watamchagua tena katika uchaguzi ujao. Kulia ni Meneja wa Utafiti wa Vyombo vya Habari na Umma kutoka Shirika lisilokuwa la Kiserikali la Synovate Tanzania Abdallah Gunda

Na Tiganya Vincent-MAELEZO

Asilimia 75 ya watanzania waliohojiwa na Shirika lisilokuwa la kiserikali linajihusisha na utafiti wa masuala ya siasa, uchumi na kijamii wameonyesha kuwa wangependa Rais Jakaya Mrisho Kikwete andelelee kuongoza Tanzania mara baada ya uchaguzi Mkuu mwisho mwa mwaka huu.

Hatua hiyo inafuatia watanzania 2000 waliohojiwa kutoka sehemu mbalimbali kumkubali kuwa Rais Kikwete anastahili kuchaguliwa tena kuwa Kiongozi Mkuu wa Tanzania.

Takwimu hizo zilitolewa jana jijini Dar es salaam na Meneja wa Utafiti wa Vyombo vya Habari na Umma kutoka Shirika lisilokuwa la Kiserikali la Synovate Tanzania Abdallah Gunda alipokuwa anatoa matokeo ya utafiti wa hali ya demokrasia hapa nchini.


Alisema kuwa asilimia hizo ni zaidi ya theluthi mbili ya Watanzania ambao walihojiwa kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania.


Katika utafiti huo Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) alipata asilimia 10 wakati Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi alipata asilimia 9.


Gunda aliongeza kuwa Mwenyekiti wa United Democratic Party (UDP) , Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe na Dkt Salim Ahmed Salim walipa asilimia moja kwa kila mmoja wao ya Watanzania wenye uwezo kupiga kura wakipenda kuwa wanafaa kuwa Rais.


Meneja huyo alisema kuwa katika utafiti wao asilimia mbili ya wahoojiwa wote walisema kuwa wasingependa kueleza nani wangependa awe Rais wakati asilimia mbili nyingine hawajui wa kumchagua.


Aidha katika utafiti huo Chama cha Mapinduzi kilioneka kuwa watu wengi walio karibu nacho kwa kuapa asilimia 70, CHADEMA asilimia 17, CUF asilimia 9, NCCR-Mageuzi kuwa na asilimia 2 huku TLP na UDP zikiwa na asilimia moja kila kimoja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 24 mpaka sasa

  1. Ankal

    Mimi binafsi sikubaliani na data hizi, walifanyia maeneo gani, wapi na wakati gani?

    walitaganza kwenye vyombo vipi vya habari kuwa kutakuwa na research ya namna hiyo?

    Walikuwa wanauliza masawali yepi?, tunaweza kuyapata ili tuyachambue?

    Hakika nakuambia research nyingine zipo kwa ajili ya kufagiliana na wala siyo chochote, katika hali kama hii, ufisadi, EPA, 82.15% ya wanafunzi kufeli na kupata divison four unatarajia nani asema hayo majibu ya research yapo sawa?

    kama walifanya Bagamiyo hapo sawa.

    ReplyDelete
  2. JK kiboko,anastahil kabisa,na uhakika atapata zaidi ya asilimia 80 kama chama cha cuf na chadema kila mtu akiweka mgombea wake.jk amefanya mambo mengi,sema magazeti ya bongo siku hizi udaku ndo dili,kazi kuripoti biff la lowasa na sita.wanaacha kuonesha vitu vya maendeleo,JK ameingia ikulu TRA wanakusanja 190 bilion kwa mwenzi,now inagonga 400 bilions.cha muhimu aondowe wazee wote serikali ijayo

    ReplyDelete
  3. kweli JK mtoto wa mjini,yani huwezi amini anavyokubalika kimataifa.jamaa wanamuona kama lulu.ukiangalia ata anapoingia kwenye mikutano ya africa union utaona viongozi wa africa wanavyopanga mstari kuongea naye.na uhakika jamaa anakubalika kimataifa kuliko ndani.

    ReplyDelete
  4. Hahahaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
    Naona kampeni zimeshaanza mapema,
    wapinzani wanapigwa bao kijanja

    ReplyDelete
  5. Hao wana mtandao wamekwisha aanza pilika zao he! he! he!. Hata hivyo, ukiangalia udhaifu wa vyama vyetu vya upinzani, uelewa wa wapiga kura kuhusu wajibu wa serikali na mifumo ya vyama, hususan chama tawala, ninakubaliana na matokeo ya utafiti huo.

    ReplyDelete
  6. KUFANYA UTAFITI KAMA HUU NI KUPOTEZA TU RESOURCES ZA WATU, MUDA NA FEDHA. HAWA WATAFITI WALITEGEMEA KUPATA JIBU TOFAUTI NA HILO HAPA TANZANIA? KWA UFUPI MTU KWA JINSI SIASA ZA TANZANIA ZILIVYO MTU YEYOTE ATAKAYEPITISHWA NA CCM KUGOMBEA NAFASI YA URAIS ATASHINDA TU. SASA JK NDIYE ANASHILIKIA KITI UNATEGEMEA WATASEMA ATOLEWE?

    ReplyDelete
  7. Mwaka wa mavuno huu. Kila mtu kwa nafasi yake atavuna ila kwa kukifagilia CCM. Alianza Sheikh Yahya, Wamekuja hawa wanaojiita pollstars wasio na uhusiano na mtu yoyote bali wana uhusiano na PESA ambazo tunajua ni nani anazo

    Tutasikia mengi sana ili mradi tu midomo ya watu iende kinywani. Kwani mimi CCM wakinipa Shs Million 10 ntakataa kuwafagilia?, ni mwehu tu maana Tanzania ya Leo hapendwi mtu wala chama bali ni maslahi binafsi tu.

    ReplyDelete
  8. Nyinyi mnaokubaliana na utafiti wa

    namna hii nyote ni misisiem!! watu tupo milioni 40 utafiti watu elfu 2 alafu ndio mnauita utafiti, hovyo kabisa!!!
    wewe unayesema kuwa hakuna chama, hivi unajiuliza maswali ya msingi!! hivi baba wa taifa nyerere na wenzie wangeambiwa kama hivyo wangekabidhiwa nchi? kila kitu kina mwanzo bwana, acheni hizo!!

    ReplyDelete
  9. CCM Oyeee! Mie mwenyewe niko nje ya nchi, sitaweza kupiga kura kumchagua Mbunge wangu kwanza sina hata interest ya kumchagua Mbunge. Lakini nawahakikishia nitasafiri kwenda Ubalozini kupiga kura ya kumpa JK, kama siye yeye sie wengine ambao ni wachovu watoto wetu, watoto wa ndugu zetu wasingeliona madarasa ya Sekondari.

    Hesabu na kura yangu ukijumlisha hapo utapata asilimia 71.

    Chama Cha Mapinduzi Juu!!!
    JK Juu!
    Pinda Juu
    Mwinyi Juu
    Karume Juu

    Mwenye wivu na ajinyonge!

    ReplyDelete
  10. kaka MICHUZI wewe CCM nini?!!!!
    mdau-UKEREWE.

    ReplyDelete
  11. Ndomana tunabaki na umasikini wetu kwa rushwa za kijinga. hunapo mpigia jeki mtu kama hivi kumbuka unaweza faidika wewe kwa leo je kesho kizazi chako kitafaidika nini? lini tutaamka ? we need good governors siyo .............

    ReplyDelete
  12. mmmmh kasheshe!!! imbombo inkafu!! kazi kweikwei!!!

    ReplyDelete
  13. Maskini nimemuona Marhum Bingu wa Mutharika....

    ReplyDelete
  14. Gosh.
    Yaani JK kashuka kutoka 80% hadi 75%? Nadhani hadi Oktoba atakuwa kwenye 35% au chini ya hapo, hakyanani vile.

    ReplyDelete
  15. Population sample yenu ili based kwenye makundi gani ya watu, jinsia, umri, kipato, mikoa gani?

    Je, maswali yenu yalikuwa ya design gani?

    Je, Pesa zenu kuendesha zoezi hilo zilitoka wapi?

    Je, nyie ni watakwimu makini, yaani mnauzoefu na mafunzo ya kutosha kuteleleza zoezi hili?

    Baada ya majibu, ndipo tutajua credibility ya POLLS zenu wakuu.

    Mdau
    Blogu Ya Jamii

    ReplyDelete
  16. zanzibar_mpyaFebruary 22, 2010

    Mhh utafiti huu haupaswi hata kuandikiwa report achilia mbali kuuwanika mbele ya watanzania! Ndani ya watu million 40, una hoji watu elfu 2, tena wa mkoa wa Dar, sababu nna hakika ndo waliohojiwa hawana ubavu wakwenda vijijini. Kisha unathubutu kuuita utafiti?! Ha ha ha watu elfu 2! Kwa utafiti huo, hata huyo Kikwete haukubali. At least ungehoji 10% ya watanzania wanaoweza kupiga kura, results zako zingekuwa reliable. Lakini huu ni kujifurahisha na kutaka kufurahisha mabwana zenu tu

    ReplyDelete
  17. ADILI NA NDUGUZEFebruary 22, 2010

    Kama noma na iwe noma. Nyumbani kwangu utafiti huo haukufika. Tupo wapiga kura 12 na sisi wote chaguo letu ni Jakaya Mrisho wa Kikwete. Haki ya mama sitanii.

    Nyie wengine msiopenda ukweli huo shauri yenu na ni haki yenu. Hivi pale Pangani baada ya kuahidiwa pantoni na JK kweli limefika na limeanza kazi.Unategemea anyimwe kura na wakazi wa Pangani? Hata Mbunge Rishad atapaonea kwa mgongo wa JK. Haya kule Loliondo alikoahidi AMbulance na sehemu nyingine mnafikiri atanyimwa kura? Nyie vipi?

    ReplyDelete
  18. Michu umeanza unazi wa JK, mambo ya conflict of interest.

    ReplyDelete
  19. Ninatafuta mtaji wa kutengeneza muvi itakayoitwa "Bongo tambarare". Sihitaji akina Kanumba kuicheza, matukio yanatengenezwa kila kuchapo kazi ni kuyakusanya na kuyaunganisha matukio haya haya tunayoletewa katika vyombo vya habari na picha itakuwa imekamilika. Kama kuna washirika wanataka tushirikiane tafadhali wasiliana nami

    mlalahoi

    kwa mfuga mafisadi, jirani na kwa mfuga mbwa.

    ReplyDelete
  20. Wabongo wacheni ujinga, at least hawa jamaa wanafanya matumizi ya statistics, wengi wamebekia na nadharia tu za mashuleni bila ya matumizi yake.

    Sasa jamaa wanakupeni polls za utafiti wao, nyinyi eti hooo hatuamini, nanyinyi msioamini fanyeni zenu na leteni majibu yenu hapa badala ya kulalama. Haya ndio yaleyale aliyosema Prof. Mbele, wabongo uvivu wa shule lakini kujifanya wanajua na kukandia kazi za watu namba moja.

    Hizi polls hata hapa Marekani zinafanywa hivyo hivyo. wanachukua sample ya watu, across the population, sana sana watu 1,500. Tena jamaa wamehoji watu wengi zaidi ...2,000, hivyo usahihi wa poll yao ni mkubwa zaidi.

    Ndugu tubishe kiutaalamu, na vitu unavyojua, sio kuja kuonyesha ujinga wako hapa. Polls ndizo zinazowapa watawala picha nzuri jinsi gani wananchi wanavyoiona serikali yao inavyoendesha nchi.

    Mimi ningeomba hawa jamaa kufanya polls za masuala tofauti yanayowagusa wananchi. Bila ya kusubiri hili la uchaguzi tuu. Labda huu ndio mwanzo.

    Mdau USA

    ReplyDelete
  21. marekani wana tea party na sie tuanzishe chai party tutashinda...hivyo vyama vingine ninamake the same mistakes kila siku CHAI PARTY mpoooooooooo

    I don't agree with those data

    ReplyDelete
  22. kama yanayoandikwa ni ya kweli basi Tanzania bado pana kazi kubwa.
    Inakuwaje JK anakubalika yeye kama chama chake ni kichafu?
    Hivi hatujui kuwa maamuzi ya chama ndo maamuzi ya JK? Hivi hatujui kuwa chama ndo kiliamua maamuzi ya mwisho ya Richmond?
    Hivi JK kama ni safi atawezaje kufanya kazi na watu wachafu na ameshindwa kuwachukulia hatua?
    JK amefanya nini mpaka aonekane anafaa? Ni JK aliyewateua akina Lowassa, Karamagi, Chenge kwenye baraza lake la mawaziri, mbona kuna kashfa kibao ameshindwa kuzifanyia kazi hadi leo. Ubora wake uko wapi?
    Mbona watu wameiba hela za EPA na hadi leo wanapeta mtaani na JK anawaangalia tu, huo uzuri upo wapi?
    Ni pesa ngapi za umma zinapotea na wezi wanajulikana lkn amekaa kimya.
    Naombeni hao watu walioojiwa waseme ni kipi kizuri cha JK tunakiona?
    Eti kuna mdau anasema amejenga shule watoto wa maskini wanasoma? Hivi shule ni majengo au walimu na vitabu kwanza? Kijijini kwetu pana shule lakini ina walimu wawili sasa hapo pana shule au?
    Watanzania gani walihojiwa mpaka wakasema JK anafaa kwa 75% au ndo maana ya REDET ya kipindi kile na leo Prof. Mukandala ni VC UDSM wakati hana hata chembe ya uongozi. Tumeona matokeo yake , migogoro kila siku mlimani tena ikiwa zaidi ni ya wafanyakazi wakati zamani ilikuwa ni ya wanafunzi pekee.
    Huo utafiti ulifanyika katika mikoa ipi? na waliohojiwa wanaelewa hali ya nchi hii ikoje?
    Tena jamaa mmoja yupo Marekani anasema ataenda ubalozi kumpigia kura JK, unajua matatizo ya hapa nchini au kisa unabeba boksi na kupata hela ya kuishi ndo unaona JK anafaa? Au kisa anakuja sana Ulaya na Amerika na kuwaandalia dinner ndo mnaona anafaa. JK anaweza mambo yasiyo ya msingi kama parties lakini si maamuzi mazito yanayoihusu nchi.
    Hata kama wapinzani hawafai lakini JK si mtu wa kuendelea kuongoza nchi hii maana ameshindwa kufanya vitu vya msingi vya kuisaidia nchi. Kila alichopanga kimeshindwa hadi leo, Kilimo kwanza, maisha bora n.k.
    JAMANI NAOMBA MWENYE HOJA ZA KUSEMA JK ANAFAA ATOE ILI NAMI NIONE KAMA NITAMPA KURA YANGU.

    ReplyDelete
  23. MICHUZI SORY MTU WANGU, HIVI MFANO CHAMA FULANI KIKAKUFUATA KIKAKUPA HATA EMTANO TUU UKIFAGILIE UTALAZA DAMU?

    ReplyDelete
  24. Nyie pigeni kelele tu ila JK anapeta, na atamaliza ngwe ya pili. Unaweza kubali hilo na kuishi kwenye uhalisia au kukataa na kuishi kwenye nadharia.

    Hapa Dar tu anapeta. Mradi wa maji wa wachina unampandisha chati.

    Kuna maeneo ya mbali na city center kama vile Ubungo walikuwa hawana ndoto ya kupata maji safi ya uhakika ya bomba.

    Sasa hivi wanaunganishwa kwa kasi ya ajabu tena kwa gharama nafuu mno ya Tshs. 50,000 tu! Unaunganishiwa maji ndani ya siku moja!

    Kwa kulinganisha tu sehemu ambako wachina hawapiti ukitaka maji toka DAWASCO utafuatilia hata miezi mitatu, na utakamuliwa si chini ya Tshs. 300,000/-

    Watu kama hao (wa Ubungo) sidhani kama watamtosa JK, pamoja na CCM yake.

    Hii naongezea tu kwa point ya mchangiaji mmoja hapo juu aliyoengelea zahanati na kivuko.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...