Kaka michuzi habari za asubuhi,
Tunaomba leo blog yetu ya jamii itoe nafasi kwa wadau kujadili haya malipo ya wabunge baada ya kukaa bungeni kwa miaka 5.
*Mshahara wa miaka 5....(1,921, 000 x 12 x 5)= 115,260,000
*40% ya mshahara wa miaka 5........... ......... ..... 46,104,000
*Jumla....... ......... ......... ......... ......... ......... ......... 161,364,000

KILA Mbunge ataondoka na zaidi ya Sh46milioni kama kiinua mgongo baada ya Rais Jakaya Kikwete kulivunja Bunge Julai mwaka huu.

Bunge hilo litavunjwa baada ya mkutano wa bajeti unaotarajiwa kumalizika mwishoni mwa Agosti mwaka huu kwa ajili ya kujiandaa uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba.Fedha hizo ni sawa na asilimia 40 ya mishahara ya miaka yote mitano ya utumishi bungeni ambapo mshahara wa kila mbunge kwa sasa anafikia jumla ya Sh1,921,000 kwa mwezi.Kwa mujibu wa Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashilillah, wabunge watalipwa fedha zao mara baada ya Bunge kuvunjwa.

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lina wabunge 325, kati yao 49 ni mawaziri na manaibu waziri. Ukiondoa mawaziri na manaibu wao ambao kinua mgongo chao hulipwa na serikali, hivyo watakao lipwa na Bunge ni 276. Kwa mantiki hiyo jumla ya Sh12,724,704, 000 zitalipwa kama kiinua mgongo kwa wabunge hao ukiondoa mawaziri.
Malipo ya wabunge hao, yatatolewa kwa mujibu wa sheria ya mafao ya viongozi wa kisiasa ya mwaka 1999 ambayo ilianza kutumika 2000.Kwa mujibu wa sheria hiyo, iliyotokana na marekebisho ya sheria ya awali ya mafao ya viongozi maalum wa kitaifa ya mwaka 1986, kila mbunge atalipwa asilimia 40 ya mshahara wake alioupokea kwa kipindi chote cha miaka mitano. Marekebisho ya mishahara ya viongozi wakuu wa nchi na viongozi wa kisiasa yaliyofanywa Julai mwaka jana, yameonyesha kuwa, mbunge anapokea Sh1,921,000 milioni kwa mwezi.
Mdau Usongo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. sasa unataka kutueleza nini? unalalamika nini unataka tujadili?

    mie sijakuelewa

    ReplyDelete
  2. mi nafikiri wangeongezewa kidogo hiyo %..kwa hali halisi ya maisha na kazi ngumu wanayoifanya...mfano kuzima mjadala wa Richmond nk siyo kazi lelemama

    ReplyDelete
  3. Nchi masikini?au raia maskini? Aibu nchi Kama tz kutumia billions kwa few elites! Govn't inatumbua tuu,hao wabunge tu,vipi kuhusu sector zingine Kama finance and security?don't go there!! They get paid by kilos? Halafu nchi za ulaya zikitia masharti kutusaidia yunapiga kelele wanatunyanyasa? Tax payer wao manavuja jasho sisi tunapata kwanja la dezo na viongozi wetu wananenepa:)

    case study: compare Ghana vs Malaysia. Same year of independence na Ghana walikuwa na reserve twice us much as Malaysia. Now where is Ghana and where is Malaysia? Same nightmare..we Africans loves luxury before our people;)

    ReplyDelete
  4. Mi naona mshahara wao ni mdogo sana, hata wabeba box tu wanawazidi, 1.9 Million per Month, Mmbunge..!!!!, du, bongo tambarare.

    ReplyDelete
  5. That amount is equivalent 4 BOT governer houses, it's really nothing considering their number.

    Hawa jamaa tuliwachagua sisi na soga wanalolipiga pale bungeni tunaona japo sio kwa kiwango cha matarajio ya wengi but they do something. They deserve it

    Five years, aah! hiyo pesa kidogo tu ndugu yangu unawananga tu bure.

    ReplyDelete
  6. Jamani tuangalie ukweli kwanza. Kwa Africa mashariki wabunge wa Tanzania ndio wanaolipwa mshahara kidogo kuliko wabunge wengine wote. majimbo yao na mategemeo ya watu wanaowawakilisha ni mengi mno kiasi kwamba wabunge hukimbia majimbo ili tu kupunguza gharama za kuhudumia jimbo kwa hizo hizo pesa wanazozipata. Kwa mtazamo wangu wangeongezwa zaidi hata mara mbili wanavyopata sasa. Hebu angalia mbunge akiupata uwaziri jimbo lake huwa linakuwa na maendeleo zaidi kwahiyo ni kweli kabisa kuwa wabunge wengi hutumia hizo hizo pesa kuendeleza jimbo lake na kiasi kwa yeye mwenyewe. tusione wivu usiokuwa na kichwa wala miguu kwa kazi wanafanya kazi lakini hapa cha kujiuliza ni kuwa kama wabunge wanafanya kazi nini kinakwamisha maendeleo? Kwa mtazamo wangu ni Uongozi wa serikali kwa kutotekeleza maazimio ya bunge ndio wa kulaumiwa lakini bunge limefanya kazi yake, mtazamo wangu pia ni kuwa wakulaumiwa ni Viongozi wachache wabinafsi waliomo kwenye chama tawala na ndio wenye madaraka ndio waadhibiwe ili tupate maendeleo lakini sio wabunge wametekeleza kazi yao lakini wanafiki wachache kwenye chama wanakitumia chama kuwanyamzisha sasa hapo lawama isije bungeni bali ni hao vigogo na wananchi tunawajua. nahitimisha kwa kusema wabunge wanafanya na wamefanya kazi yao na wanastahili zaidi ya wanachopewa.

    ReplyDelete
  7. And your point is? (Yaani hoja yako iko wapi?)

    ReplyDelete
  8. Mdau nashukuru kwa hayo mawazo yako. Wengi tulikuwa hatujui wawakilishi wetu tunawalipa kiasi gani! Kwa kazi ngumu wanayotakiwa kufanya kwa taifa letu hasa katika karne hii, ninaona hayo malipo yanatosha sana. Tatizo ni kwamba wengi wao hawatakiwi kupata hayo malipo kwani wao wanasubiri muda ufike ili wapate hayo malipo! Hakuna kinachofanywa ndani ya Bunge.

    Mimi ninaomba kwa Wabunge kama Mhs. Dr. Mwakyembe, Dr. Slaa, Mhs mama Malecella hayo malipo ni jasho lao kwani kazi inayofanywa imeonekana!
    Hayo mapato ya Waheshimiwa wabunge ningeomba hata wananchi wa vijijini wayajue ili walinganishe na performance ya Mbunge/Wabunge wao.
    Mgombeaji Mtegemewa kupitia CCM 2010.

    ReplyDelete
  9. Hapa tumeelezwa juu ya 'forma and statutory' payments. Tungeelezwa juu ya bahasha zinazopita pita, mbona tungezimia! Wenzetu wako juu bwana! 'BAHASHA' zaweza kuzidi malipo rasimi.

    ReplyDelete
  10. ADILI NA NDUGUZEFebruary 22, 2010

    Naungana na Anon wa 22 feb, 12:09:00 pm. Hivi umeweka suala hili hapa kama taarifa? Au kuwa wabunge hawastahili kulipwa hizo? Maoni ni kuwa kulipwa wabunge halihusiana na ufisadi hata kidogo. Hayo ni masharti ya kazi ya ubunge. Ni taratibu na kanuni zilizowekwa ambazo hata watumishi wengine wa serikali wanazo kuanzia mhudumu hadi Chief Secretary. Kwa lugha ya english zinaitwa terms of service.

    Kama unaona maya basi jitahidi na wewe mwaka huu ukagombee. Ukishinda ubunge ikifikia 2015 utalipwa. Ya wabunge yanakuuma. Ukisikia ya wakuu wa mikoa na wilaya je? Hii ni serkali ya utawala bora na utawala wa sheria. Mimi sioni cha kujadili hapo.

    ReplyDelete
  11. florian rweyemamuFebruary 22, 2010

    mtoa hoja, hata tukipiga kelele weeeeeeee, bado tatizo ni kwamba hatukemei uozo kwenye siasa zetu kuanzia chini.

    Ili tuwe makini zaidi, inabidi msukumo uanzie chini kabisa. Serikali za mitaa, madiwani wetu, kwenda juu. Tukishaondoa ufisadi huku chini, itakuwa rahisi kuung'oa wa huko juu. Tatizo ni kwamba hatuoni uozo wa chini ndio maana mitaa yetu ipo ovyo ovyo, mitaro michafu, shule mbovu nk nk

    Tuanze kupiga kelele kwenye 'grassroots' kwanza.

    Mtoa hoja, unalijua jina la mjumbe wa serikali za mitaa hapo mtaani kwako?

    ReplyDelete
  12. du jamaa mbona wanapewa pesa ndogo namna hiyo wakati mi nilikuwa nalpwa us dola 2500 barrick na malupulupu kibao total kwa mwez kama 3200 kabla hawajanileta apa canada kusoma

    ReplyDelete
  13. Mimi nakubaliana na wale wanaosema kiwango sio kikubwa cha hivyoo ukilinganisha na kazi wanayofanya pamoja na malipo ta taasisi nyengine nyeti za serikali ambapo mafao yao nimakubwa kwamfano kwani Gavana wa Bekni kuu analipwa mshahari kiasi gani na je maruporupu yake.Mimi kinachonikera ni KWA NINI WAO HAWALIPI KODI? hii ndio shida

    ReplyDelete
  14. dah hiyo ni hela ndogo sana....kuna wajinga wajinga wengi tu wanalipwa twice au three times ya hapo...na kazi yao haieleweki....Anon Feb 22,03:27:00 hata wakilipa kodi wewe itakusaidia nini?? jiulize kodi zoote zinazolipwa nchi hii wewe unafaidika na nini???

    ReplyDelete
  15. Duh, aisee, Bongo kweli maskini saaana, yaani kiinua mgongo cha wabunge 276 kwa miaka mitano ni sawa na mshahara wa Christiano Ronaldo kwa mwaka mmoja.

    Kaazi kweli kweli.

    ReplyDelete
  16. hakuna uhuru upatikanao bure na demokrasia ni bidhaa aghali sana. huo ni ukweli usiopingika na sasa unaweza kuelewa kwa nini wateule wetu hufikia kuvimbiana inapotokea dalili za kutiliana mchanga katika vitumbua vyao. mimi napendekeza mshahara wao uongezwe mara mbili!!

    ReplyDelete
  17. jamani mcmshambulie sn, roho inamuuma sn aligombea ubunge sasa kakosa anataka ku2shauri upuuzi hapa..kesho na kesho kutwa ataleta mishahra hata ya wakuu wa majeshi..Mkuu wa blog post kama hizi we minya tuu..khaaaaa (((((((

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...