JK akihutubia wakati akizindua rasmi kampeni kabambe ya vita dhidi ya malaria kwenye viwanja vya Leaders Club jijini Dar usiku wa kuamkia leo
JK na Mama Salma Kikwete wakipozi na Bi. Kidude
JK katika picha ya pamoja na wadau mbalimbali wa makampuni, Taasisi na viongozi wa serikali yanayopambana na ugonjwa wa Malaria.
Meneja udhamini na mwasiliano wa Vodacom Tanzania George Rwehumbiza (shoto), Mkurugenzi wa Masoko Vodacom Tanzania Ephraim Mafuru (kati) na Naibu Mkurugenzi wa Shirika la PSI Mheshimiwa Romanus Ntung'e wakifurahia mafanikio ya tamasha hilo.
Mkurudgenzi wa Vodacom Foundation Mwamvita Makamba (wa pili kuumeni) akiwa na wadau wengine wa mapambano dhidi ya Malaria. Kulia ni Sofia Byanaku na Mange Kimambi (shoto)
Ray C alikuwa mmoja wa mastaa kibao waliotumbuiza

















Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. JK na vidolezzzzzzzzz!!!!

    ReplyDelete
  2. tanzania bila malaria inawezekana

    ReplyDelete
  3. TANZANIA TUACHE USANII, ZINDUKA ITAKUWA NI TAFRIJA KAMA NYINGINE ZILIZOPITA KWANI WANAOANDAA NDIO HAOHAO WANAOTAKA KUFANYA BIASHARA YA KUUZA VYANDARUA HAWAKO TAYARI KUONA MAZALIO YA MBU YANATOKOMEZWA. NI VIONGOZI HAOHAO WALIUA MRADI WA WAJAPANI AMBAO ULIONESHA MATUMAINI MAKUBWA SANA KUANGAMIZA MBU. WAKATI ZINDUKA IKIZINDULIWA WAKAZI WA DAR HAWANA HABARI YOYOTE KUHUSU KAMPENI HIYO! TUMESHINDWA KUONDOA TAKATAKA AMBAZO NI RAHISI KUZIONDOA TUTAWEZA MALARIA.

    ReplyDelete
  4. MAFISADI NI WENGI SN WANAJARIBU KUTOKA KILASIKU KWENYE MAGATETI KUSUDI TUWAONE WANASAIDIA KUMBE AMNA CHOCHOTE,MTAKUFA SIKU SIZENU NA KUZIKWA MAKABURI SI YENU MLY NYIE

    ReplyDelete
  5. Nakubaliana sana na mdau wa pili hapo juu. Haiwezekani kutokomeza malaria kwa vyandarua au Dawa Mseto bila kutokomeza mazalia ya mbu. Kampeni kubwa ingelenga katika kuboresha mazingira kuliko hii ya vyandarua. Nimeshangaa President kusema hiki ndicho kiwe kizazi cha mwisho kufa kwa malaria. Hii itakuwa ni ndoto kwani hao wafadhili kwao hakuna mbu wakati katika nchi za tropiki ni kitu kinachoishi nacho. Ile kampeni ya Wajapani ilikuwa ni positive katika kuangamiza mazalia ya mbu. Hata mara baada ya Uhuru kulikuwa na mtu mwenye cheo cha "African Malaria Officer", kazi yake ilikuwa ni ku-spray dawa kwenye vichaka karibu na makazi ya binadamu, vyooni na kwenye maji machafu, siku hizi hakuna. Huu mradi wa vyandarua vyenye dawa kweli tunauona ni mradi mkubwa uliofadhiliwa fedha nyingi lakini mafanikio yake yanaweza kuwa kidogo bila kwenda sambamba na utokemezaji wa mazalia ya mbu.

    ReplyDelete
  6. Duh kwanini tunakimbilia neti wakati kuna njia za kupunguza mazalia ya mbu!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...