Ankal habari za kazi

Nipo Kigoma kikazi tangu J4. Jana katika kupiga stori na wenyeji kwenye kijiwe fulani cha nyama choma niliipata hii ya kutisha.

Mji wa Kigoma na vitongoji vyake kwa takribani wiki mbili tatu sasa umevamiwa na kundi la vibaka wa kutisha wanaotumia nondo kujeruhi na kupora watu chochote, simu pesa n.k. Kundi hilo uvinjali kuanzia saa 2 usiku na kuendela.

Mji kwa sasa una matatizo ya umeme na baadhi ya vitongoji vya mji wakazi wamepanda mahindi hivyo giza utawala. Wakazi kwa sasa utembea kwa teksi kutoka sehemu moja kwenda nyingine ifikapo usiku japo jamaa wameshamliza mtu kwa kumwekea jiwe kubwa njiani kisha wakampora wa kumpiga nondo baada ya kumchomoa kwenye gari.

Wametoka wapi vibaka hawa ghafla bin vuu!? Nimejulisha kuwa kutokana na kusitishwa kwa safari za treni kuja Kigoma kundi la wezi wote wa mizigo ya abiria wa treni lipo JOBLESS na ukabaji ndio imekuwa 'kazi' yao mbadala!
Kigoma wafa jamani Polisi wa doria wamezidiwa na vibaka hawa.
Mdau GBK

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. ILIKUAJE UKAKUBALI TRANSFER YA KIGOMA!!HIYO NI ZAIDI YA ADHABU!!!Huoni ZITO KABWE Anashinda DAR.
    ILA VUMILIA TU,UTA ADJUST LIFESTYLE TU, NAKUANZA KUWA MBISHI!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...