Nafasi ya Biashara

Tunapenda kuwatangazia wa-Tanzania wafanyabiashara na wanaopenda kufanya biashara kwamba kuna nafasi za kushirikiana katika biashara kati ya USA na Tanzania.

Tunakaribisha wale ambao wangependa kufanya biashara kutuandikia ili tuweze kuweka makubaliano.

Biashara itakuwa inalenga zaidi katika ku export electronics, nguo, vipodozi, jewelry, accesories na bidhaa nyinginezo kutoka USA.

Tunakaribisha wafanyabiashara kutoka mikoa yote ya Tanzania na sio Dar es Salaam peke yake. Wafanyabiashara watakaoteuliwa watajulishwa na baadhi ya wafanyabiashara walio Tanzania ambao tayari wameanza uhusiano nasi kwa lengo la kubadilishana mawazo.

Tutashukuru kupata mawasiliano kutoka kwa wale walio serious tu ili tusipotezeane muda .

Kila la heri katika shughuli zenu.

Wasiliana nasi kupitia:

tztrader@gmail.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. MliakuvanaMarch 10, 2010

    Ukiangalia haraka haraka inaonekana ni initiative nzuri. Ila hakuna information yeyote kuhusu nyie ni akina nani in terms of kampuny, au watu gani etc.

    Vilevile mnasema tuwaandikie - sasa tuwaandikie nini? Proposal, letter of introduction, company profile etc etc?

    More information would be great, don't you think?

    ReplyDelete
  2. gmail contacts???

    ReplyDelete
  3. Kama ni kuexport vitu bongo si una ndugu zako huku? kwanini usiwatumie vitu wakakuuzia? ungekua wewe sio mtanzania ningesema unatafuta partners lakini wewe mbongo kabisa.

    Wenzio siku hizi wakitaka bidhaa zao wanakuja huko na kuchukua kwa container na kurisha mali zao. Mambo ya kulanguana yameishapitwa na wakati na emails za google.

    ReplyDelete
  4. HAYA WAJINGA NDIO WALIWAO,HAPA SIONI BIASHARA YEYOTE YA MAANA,KWANZA HAWA JAMAA WANA gmail MMMMMH KUNA WALAKINI,ANYWAY KAMA KWELI NYINYI NI WAFANYA BIASHARA WA UHAKIKA TUPENI CONTACTS ZENU ZA UHAKIKA PLIZ,HAKUNA KAMPUNI HATA MOJA NINAYO IJUA DUNIANI INATUMIA EMAIL KAMA YENU,KAMPUNI ILIYOKAMILIKA KWANZA INA SITE YAKE NA EMAIL ADDRESS ZINAZOENDANA NA HIYO SITE,SIO TU HILO KAMA HATUTAKI KUWAANDIKIA TUNATAKA KUWAONA ANA KWA ANA MNAPATIKANA WAPI? HAPA WATU WAMESHAONA WATANZANIA WAPUMBAVU UNAWEZA KUWALA FASTER..TZ AMKA NA WEWE ANKAL WATU KAMA HAWA WANAOLETA MATANGAZO YASIOKAMILIKA TUPA KAPUNI TU.

    ReplyDelete
  5. Sidhani ....

    ReplyDelete
  6. TEGO HILO....hali ngumu jamani kwa wabeba box....
    wacha tupete na bongo yetu tambarare ukizingatia huu ni mwaka wa uchaguzi....

    ReplyDelete
  7. hapa piga ua baada ya makubaliano watataka uwatumie hela za kununua na kusafirisha bidhaa na ndio hapo sasa chezo la WFP linapoanza

    ReplyDelete
  8. Hata kama itakuwa ni biashara ya ukweli , kwa nini wabongo tumekalia ku-import tu mavitu hayo hatufikirii kuanzisha viwanda tukatengeneza wenyewe? Mambo ya ku-import yanarudisha sana maendeleo ya jamii, hakuna creation ya ajira etc, tuige mfano wa China, India etc Ndio maana tuna-import mpaka Tooth picks, Viberiti nk Hii ni aibu!

    ReplyDelete
  9. Kuna tatizo la kizungu hapo, unasema unataka kuexport electronics kutoka USA? nadhani ulitaka kusema kuimport, kwa maantiki hiyo hujui hata lugha ya biashara yenyewe? hao wamarekani unawasiliana nao vipi??...

    ReplyDelete
  10. Yani nyie bado mna promote biashara ya kutoa bidhaa nchi za nnje kwenda kuuza tanzania! Hivi mpaka sasa hamjajua mathara ya biashara za namna hiyo kwa uchumi wa nchi yetu? Badala ya kutafuta mbinu na njia za ku export bidhaa kutoka Tanzania ambapo bado tuna ile program ya kuuza bidhaa USA bila ushuru chini ya mkataba wa AGOA kama sijakosea. Nadhani watanzania tunatakiwa tuachane na biashara za aina hii la sivyo uchumi wa nchi zetu za kiafrika utabakia hapohapo.Afrika tumekukuwa CONSUMERS na IMPORTERS kwa miaka mingi sana! nadhani umefika wakati ambao tunatakiwa tuanze kuwa MANUFUCTURERS la sivyo ni kiama kwetu milele. Angalia China kwa mfano tangu wameanza mageuzi ya kilimo na viwanda. Tizama ukuwaji wa uchumi wao, tizama kenya wanavyouza, tizama south afrika n.k
    MDAU UK

    ReplyDelete
  11. Khaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaah
    kweli bongo tambarareeeeeeeeeeeee
    wajinga ndio waliwao

    ReplyDelete
  12. wadau wa tz traders msikatishwe tamaa na hawa wachimba chumvi walionyimwa visa. Lakini ni kweli mnahitaji credible contact information. Wafanya biashara wenye akili bongo wapo wengi tu ambao wanaweza kutumia service zenu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...