Ndugu Wadau wa Globu ya Jamii,
Mimi ni mwanamke mwenye familia ya watoto 3 naipenda familia yangu na ninaipenda jamii pia. Imefika kipindi sasa nataka kusaidia wanaohitaji msaada hapa namaanisha wale ambao imeshindikana kabisa kujimudu kimatibabu kimalazi na kwa lishe pia.
Najua wengi watanishangaa sina maana sijui pa kwenda hapana huwa napita vituo vya kulea watoto yatima na hata wazee na kutoa baadhi ya mahitaji ila hizo sehemu haswa kwa hapa mjini zinatembelewa na wengi, shida yangu nataka kwenda sehemu zilizojificha na hazijulikani sana au hazitambuliki yani msaada kwao kuupata ni neema.
Wadau naomba maoni yenu, mwenye kujua sehemu ambayo kweli imesahaulika kabisa au kijiji fulani hapa dar kinachotaabika sana na mambo muhimu kwa binadamu tafadhali naomba maoni yako.Watanzania kutoa na moyo na kila mtu ana uhuru wa kutoa kadri awezavyo tujitoe kwa moyo ili tusaidiane kuwa na maisha bora sote kwa pamoja.Mungu ni mwema tuzidi kumtegemea na kumtanguliza katika yote tuyafanyayo.
Mimi Mdau Emy

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. Samahani, Ila sijaelewa kabisa sasa unataka msaada wa unga, maharage au mchele au kitu gani?? Ebu fafanua kidogo.
    Asante sana.

    ReplyDelete
  2. We anon wa kwanza kabisa hapo juu... kichwa chako kizito sana eh?

    Mbona mdau Emy amejieleza vya kutosha. Hebu tulia soma maelezo ya Emy vizuri halafu utapata jibu la swali lako.

    ReplyDelete
  3. We anon wa kwanza kabisa hapo juu... kichwa chako kizito sana eh?

    Mbona mdau Emy amejieleza vya kutosha. Hebu tulia soma maelezo ya Emy vizuri halafu utapata jibu la swali lako.

    ReplyDelete
  4. Msema kweliApril 30, 2010

    Kama unaishi Dar, sehemu ya karibu ya wewe kwenda na kusaida wenye shida, ambapo watu hawajiwezi kimalazi, lishe na shule ni :

    - Vitongoji vya Mkuranga wala sio mbali na ukipita barabara kuu utaona nymba za mbavu za mbwa!

    -Vitingoji vya Bagamoyo kama Mkuranga, ni kiasi cha wewe kutaka kusaidia kwa kuingia ndani ndani kabisa.

    -Bunju B, ndani ndani, Manzese, Mburahati, Kigogo, Gongo la mboto, Chanika, Kisarawe vijijini.

    Dada sehemu ni nying, ni wewe tu, amua wapi ni karibu na mbali na wewe, na ni kiasi gani unataka kusaidia.

    Msema kweli

    ReplyDelete
  5. mimi sina sehemu ninayoijuwa hapo dar isiyo kuwa na shida ni kalibia kila mahali uswahilini watu wanashida, japokuwa si wote.

    kwamfano niliona video ile ya uwanja wa fisi nafikili pale asilimmia kubwa ya watu wanaitaji msaada.

    umu kwani hata ukienda mwananyamara watu wanaoteseka ni wengi tu. yaani kwa ujumla watu wengine wanashinda na njaa na unapishana nao hata kule keko. kuna watu kibao hawana hata ile hela ya kununulia panadol japo wanaumwa. watu hawa utawapata ktk hospital za selekali utawaona kinamama na watoto hawana hata sabuni ya kufuwa nguo zao na watoto,watoto hawana uji mambo haya yako kila kona ya dar hata mimi yalinikuta ila mwenyezi mungu ni mwema sasa wanangu wamekuwa na naweza hata kuigusa kibord ya computer ambayo sikuwahi kuota nitaigusa ila mafisadi moto wa jehanamu unawasubili

    ReplyDelete
  6. Wazo na nia ni nzuri, lakini kuna vitu hujaviweka sawa. Mfano watu watakupataje ili wakuambie shida zao? na unataka kutoa msaada wa kiwango gani, yaani chakula, malazi, maradhi, nguo, elimu, au katika nini? Uwezo wako unaishia wapi? Fafanua

    ReplyDelete
  7. ni ushauri tu, badala ya kwenda kwenye hivyo vituo ambao utawapa ubwabwa kwa leo halafu kesho hawajui wataupata wapi, ni bora utafute familia yenye shida, uanze kuisaidia kujiinua mpaka ikae sawa, i mean kama watoto waende shule pamoja na hayo matibabu au kama mzazi msaidie jinsi ya kupata kitu cha kuendesha maisha yake.
    kuliko kwenda kwenye vituo ambavyo vinaendeshwa na watu binafsi ambao ni selfish, unaacha mchele wa kilo 5, anawapa watoto kilo 1 na nne zilizobaki anapeleka kwake.
    i will do the same in the future mambo yakikaa kwenye mstari.

    ReplyDelete
  8. Ushauri wangu ni kuwa uende hospitalini ambako watu wengi wanashindwa kujimudu hata kununua paracetamol, na pia wamama wajawazito ambao hushindwa hata kumudu gharama za kupata vitamins, chakula bora na mavazi kwa vichanga vyao.na pia ukienda sehem kama tandale manzese,tandika mbagala huko utaona watoto wanavyopata tabu. mungu akubari kwa moyo huo.

    ReplyDelete
  9. Mume Wangu, safarini Ohio, U S AApril 30, 2010

    Mdau Emy, hongera kwa ujasiri na ari ya kuwasaidia wenye shida hapo nyumbani.
    Fanya hima utembelee vijiji vya kule PEMBA, nilikuwa huko hivi karibuni na kukuta hali mbaya kuliko upeo wa fikra zetu. Vijiji nilivyovitembelea ni pamoja na Shungi, Kiziwani,Mgelema,Tandani, Tasini na Kungumoga vilivyoko katika Wilaya ya Chake Chake.

    ReplyDelete
  10. Samaha ni Emy kwa kama nitwakuwa nimekukwaza! Msaada wako una lenga kwa jiji la Dar na vitongoji vyake? Lakini kama msaada kuna sehemu nyingi tu unaweza kwenda kutoa nyumba za pale jangwani za mbavu za umbwa wanahitaji msaada wa hali na mali. Hata unako toka kijijini kwenu iwe kwa baba ako au kwa mama ako nina uhakika sehemu hizo hakuna mwenyewe uwezo kwa 100% nako unaweza kuwapelekea msaada ukaanzia kwa ndugu zako na kisha ukasambaa kijiji kizima wao wazungu wanasema "Charity begins at home" kama umemaliza kuwasaidia wote kijijini kwenu kwa hapa Dar we tembelea wenye viti wa mitaa wa maeneo ya Mbagala, Kigogo, Mburahati, Manzese, Buguruni, Vingunguti watakwambia au watakuelekeza ni famili zipi hazijimudu.
    Ni mm mlopokaji.

    ReplyDelete
  11. Ushauri wangu kwa emy. Nenda pale Temeke au mwananyamala au amana hospitali, omba kwa utawala wakupe desk/meza na waambie kuwa unataka kuanzisha ka-kituo ka msaada ndani hapo kwa wamama wazazi, watoto na wagonjwa wengine wanaoshindwa kugharimia baadhi ya mahitaji hapo hospitali.

    Nadhani njia hii itakuwezesha kusaidia wengi.

    ReplyDelete
  12. Nakubaliana na mdau hapo juu.
    Watu wasema mtu akitaka samaki "dont give him fish buu teach him how to fish".
    Maana kwa misaada kama ya chakula nk ni misaada ya siku moja.
    Utamsaidia mtu lakini kesho atashinda njaa.Wewe utaenda kusaidia mwingine,yule ulomsaidia jana atalaa njaa.
    Kwa hiyo ni busara sana kama alivosema mmoja wetu hapa,kua tafuta familia fulani hata ikiwa familia moja.Lets say familia hiyo ina mtoto alie na uwezo kiakilia lakini haendi shule.Unaweza kujitolea kumsomesha huyo mtoto,kumlipia mahitaji yote ya shule na kufatilia maendeleo yake.
    Akiweza kufika chuo kikuu ,tayari kama atakua amefaulu vizuri serikali itamkopesha asome.Asipofaulu vizuri bado akimaliza kidato cha nne anaweza kwenda kozi kama ualimu miaka 2 na upesi anaanza kazi.Mwalimu wa shule ya msingi kwa familia ambayo ni fukara,bado ni msaada mkubwa kwa familia yake.Wakati huo huo ukimsomesha huyo,unaweza lets say mama yake ukampa kimradi fulani.
    Kwa kufanyaa hivyo you will make a difference ambayo kila siku utajivunia.Na familia hii haiwezi kukusahau kamwe.Tofauti na mtu ukimpa kila 3 za mchele,kesho akishina njaa hawezi kukukumbuka.
    Familia za aina hii hii nyingi sana.Ukitaka nikuunganishie na familia ambazo kweli wamepigika,mama mmoja,kijana kafaulu darasa la saba shule kashindwa mana hata daftari hawezi kununua,Akienda shule akirudi home analala njaa, niambie nikuunganishe,Hii ni jirani yangu maeneo ya kibamba.Mwanzoni nilijitahidi kusaidia lakini hata mimi nilishindwa maana hata mimi nina ndugu kibao wa damu ambao ninawasaidia.
    Naomba kuwakilisha.
    THE SON OF AFRICA

    ReplyDelete
  13. Dada--
    Mimi naomba utembelee kila hospitali ya wilaya na Mkoa vile vile Dispensaries za Serikali. Hali ni mbaya sana na inatisha. hapo utaweza kufanikisha nia yako njema.
    Mungu akubariki.
    Kama kila MTANZANIA mwenye nacho akifanya hivyo we wont need the basket fund na tutafika mbali sana.

    Mdau
    Regent Estate.

    ReplyDelete
  14. Fungua kituo ambacho kitasaidia watu wenye shida. Lakini hakikisha unafanya background check ya kila anayekuja na unachagua wale wanaohitaji msaada kweli. Fungua kituo chako sehemu za uswahilini ndio utapata watu wengi. Especially watoto, hao ndio wanaohitaji saana misaada. I wish you all the best, na Mungu atakusaidia.
    NB: Muombe Mungu akuongoze kwenye hilo kabla haujafanya chochote.

    ReplyDelete
  15. Naomba tuwasiliane na mimi nilikuwa na wazo kama lako ili tu join hands... naomba email address yako au namba yako ya simu
    Mdau

    ReplyDelete
  16. Emmy, nakupa big up sana tu tena sana.

    BUt nataka nikuambie kuwa CHARITY BEGINS AT HOME.
    K wa kuanza hivyo naomba nikuulize mwenzetu sijui unatokea familia ya aina gani? Namaanisha kuwa katika uafrika tuna extended family saa je, ktk family yake je wote mko maisha mazuri au kuna wanohitaji msaada kama unotaka kuutoa ka wengine? Je umeshawaattend? Hata hivyo najua wakati mwingine ni vigumu sana kusaidia ndugu kuliko mtu baki.
    Ningependa uanzie katika extended family yako na mume wako.

    Kama hizo mbili ziko shwari basi, nakushauri usiangalie Dar es salaam pekee. Tembelea hata mikoani kwani you will be getting the chance kuvinjari katika mkoa husika na wakati huohuo unatoa msaada.

    Waweza kwenda kwa wazee waishio na ukoma kule Ngomeni-Muheza , Tanga au wa kule Sokomahewa, Singida. Utalia na ukatuwa unarudi kila siku kuwacheki. Hali ni mbaya.

    Mara nyinhi mikoani ni vigumu sana kupata watu wanaotoa misaada kama ilivyo hapa bongo ambapo population ni kubwa kiasi chake.

    Nihayo tu.........

    ReplyDelete
  17. Mimi sijakuelewa ina maana huko unakokusema kumebanana na ukitoa hutaonekana kuwa umetoa kitu au jina halitasikika...

    Kutoa ni moyo na wala huchagui mahali...popote moyo wako unakokutuma uanaweza ukatoa msaada wako...Hapo Dar hao homeless na ombaomba...msaidie mmoja atoke kwenye maisha hayo...mchukue mmoja...mtafutie mahali pa kukaa na kazi au mpeleke shule ya ufundi na kama ni kijana mdogo mpeleke shule na uwe mentor wake...tukisaidia mmoja mmoja kila siku tutapunguza umasikini. Kwavile hujui ukimsaidia huyo mmoja atawasaidiaje ndugu zake huko kwao....Hizo no moja ya sehemu ambazo wenye hela hawajakumbuka kuzipitia kwa vile hazina photo op.

    Mi mambo ya kutoa mchicha hapa, matunda pale, nguo hapa wala siyafagilii.....

    ReplyDelete
  18. Dada Mungu akubariki kwa moyo wako, kuna kituo pale kimara suka
    kinaitwa friends of don of donbosco hakina mfaddhili yeyote hilo jina aliekianzisha ni kwa sababu tu alipenda mawazo ya donbosco watoto wengi wanahitaji ada za shule kama unahitaji mawasiliano nijibu humu kwenye comment ili niweze kukupatia

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...