WAZIRI WA FEDHA AKICHANGIA MJADALA KISERA KUHUSU WAJIBIKAJI NA UWAZI KATIKA USHIRIKIANO WA MAENDELEO; NAMNA YA KUJENGA USHIRIKIANO ULIO SAWA MIONGONI MWA WADAU MBALIMBALI. MJADALA HUO UMEFANYIKA MAKAO MAKUU YA UMOJA WA MATAIFA JIJINI NEW YORK.
NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA FEDHA NA UCHUMI, DK. SERVACIUS LIKWELILE AKIFUATILIA MAJADILIANO
WAZIRI MKULO AKIBADILISHANA MAWAZO NA WAJUMBE MBALIMBALI WA KIKAO CHA KILELE CHA KAMATI YA UCHUMI NA MAENDELEO YA JAMII YA BARAZA KUU LA UMOJA WA MATAIFA( ECOSOC

UWEZESHWAJI WA WABUNGE

NA MWANDISHI MAALUM
New York, 30/6/2010
Imeeleza kuwa, licha ya wabunge na taasisi za kijamii, kuwa na fursa na nafasi ya kushiriki katika ufuatilia wa upangaji na utekelezaji wa bajeti ya taifa, sera zinazohusiana na masuala ya fedha na misaada ya kimaendeleo kutoka kwa wahisani, imebainika uwezo wa vyombo hivyo kutimiza wajibu huo kikamilifu bado ni mdogo.

Waziri wa fedha na Uchumi, Mh. Mstafa Mkulo ameyasema hayo hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, jijini New York. Wakati wa majadiliano ya kisera kuhusu uwajibikaji na uwazi katika ushirikiano wa kimaendeleo; namna gani serikali zinaweza kujenga ushiriano ulio sawa kati yake na taasisi nyingine. Mjadala huo umefanyika ukiwa ni sehemu ya mkutano wa kilele wa Kamati ya Baraza Juu la Umoja wa Mataifa inayoshughulikia masuala ya Uchumi na Maendeleo ya Jamii. (ECOSOC).

Mh. Mkulo anayeongoza ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo, anasema "Ushiriki wenye nguvu wa wabunge na taasisi za kijamii katika masuala yahusuyo fedha ni jambo la muhimu sana kwa kuwa ni wawakilishi wa wananchi, lakini ni sehemu ya utekelezaji wa sera ya uwajibikaji na uwazi. Lakini uzoefu unaonyesha kuna udhaifu kwa upande wa wabunge na taasisi za kijamii".

Akabainisha kuwa udhaifu huo ndio unaolazimisha kuwapo kwa hitajio la kuzijengea uwezo zaidi taasisi hizo ili kuhakikisha kwamba ushiriki wao katika mijadala ya kitaifa na kimataifa kuhusu ubora wa misaada ya maendeleo unakuwa na tija.

Akisisitiza haja hiyo ya taaisi hizo kujengewa uwezo zaidi, Mkulo anasema, sera zinazohusu fedha na hasa zile zinazohusu misaada ya wafadhili ni ngumu na zenye vipengere vingi, ambavyo anasema vinahitaji mshiriki awe uwezo na upeo wa kutosha wa siyo tu wa kuvijadili bali pia kivielewa na kuwa na mbinu za kufuatilia.

Wanajopo wengine katika majadiliano huo walikuwa ni Bi. Irene Freudenshuss-Reichal kutoka serikali ya Austria, Michael Anderson kutoka serikali ya Uingereza na Bi. Ingrid Srinath kutoka Taasisi isiyo ya kiserikali ya CIVICUS.

Mh. Mkulo ambaye aliainisha hatua mbalimbali ambazo zimefanywa na serikali lipokuja suala la uwazi na uwajibikaji, amewaeleza washiriki wa mjadala huo, kwamba kwa kiasi kikubwa Tanzania imefanikiwa kuwa na uhusiano endelevu na wenye kuridhisha kati yake na wadau wa maendeleo.

“ Kwa kujiwekea sera, mipango na mikakati mbalimbali ambayo tumeshirikiana na wadau wetu wa maendeleo, wabunge na taasisi za kijamii, Tanzania imeweza kuongeza kiwango cha umiliki wa ajenda zake za maendeleo, kupanua wigo wa majadiliano kati yake na wafadhili , na wadau wengine.
"Na kwamba kiwango cha uwazi na uwajibikiaji kimeongezea katika uandaaji na utekelezaji wa bajeti ya taifa na sera zinazohusiana na masuala ya fedha na misaada kwa kuzingatia vipaumbele vya kitaifa” anasema Mh. Mkulo.
Hata hivyo anaeleza kuwa , dhana hiyo ya uwazi na wajibikaji bado inaelemea zaidi upande mmoja yaani upande ule unaopokea misaada ( serikali) kuliko upande wa pili yaani wafadhili.

“Suala hili la uwajibikaji kwa kweli kwa wafadhili bado halijawa na uzito wa kutosha. Mara kwa mara sisi nchi tunao pokea misaada ndio tunaolazimishwa kuwa wawazi na kuwajibika. Hii si haki kwa sababu inakwenda na kinyume na tamko la Paris la mwaka 2008 linalo sisitiza uwajibikaji wa pamoja”, ameongeza.

Katika hatua nyingine, Waziri wa Fedha na Uchumi anasema kuwa ujenzi wa ushirikiano endelevu na wenye tija kati ya serikali na wadau wengine, ni jambo linalohitaji kuaminiana, kujituma, uwazi katika majadiliano na kwamba litachukua muda mrefu.

Aidha anasema ili hilo liweze kutekelezeka, uwajibikaji wa kisiasa kati ya mfadhili na mfadhiliwa ni jambo la muhimu sana.Kwa sababu ndiko kutakako pelekea uwajibikaji wa pamoja kwa lengo la kuimarisha misingi ya uwajibikaji katika ngazi ya kitaifa na kimataifa.
Wakati wa majadala huo, baadhi ya wazungumzaji pamoja na kukubaliana na hoja ya uwezeshwaji zaidi wa wabunge na taasisi za kijamii hasa katika mataifa yanayoendelea, walitaka pia uwezeshaji huo ushuke mpaka kwenye vyombo vya habari, kwa kile walichosema kwamba nao ni wadau muhimu katika kufuatilia utendaji wa serikali.

Wengine waliainisha kwamba, linapokuja suala ya uwazi na uwajibikaji, basi lisiishie kwa serikali na wadau wa maendeleo, bali uwazi na uwajibikiaji huo uwepo pia kwa taasisi nyingine zikiwamo Bunge na vyama visivyo vya kiserikali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 30, 2010

    Ankal utafungwa bure rekebisha haraka Likwelile si naibu waziri bali ni naibu katibu mkuu. Toka lini waziri asiwe mbunge? Ina maana umesahau kwamba kateuliwa juzi tu toka kwenye ubosi wa TASAF?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 30, 2010

    Serikali yetu ndio maana inafilisika...yaaani kuna waziri, naibu waziri, katibu wa waziri, naibu wa katibu wa katibu...yaani ni titles tu...naibu katibu yupo huko katibu yuko wapi?


    Na hapo ujumlishe kila wizara ina hayo majambo...duh kazi ipo....

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 01, 2010

    Waziri na naibu na naibu na tena naibu msaidizi, hawa watu wote wa nini???
    Ni lazima serikali ijaribu kuangalia gharama na kitu wanachokileza kwenye huu mkutano. Ukiangalia hoja aliyotoa waziri ilikuwa haina manufaa yoyote kwa Tanzania na mtanzania wa kawaida.
    Maelezo yalikuwa ni njia gani itumike katika kuimarisha GLOBAL ECONOMY?? Naibu au naibu msaidizi au waziri yaani mmoja wao alikuwa anatosha kabisa kuiwakilisha TANZANIA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...