Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi Ramadhan Khijjah (kushoto) akibadilishana hati ya makubaliano ya mkopo wa shilingi bilioni 173.8 na Balozi wa Jamhuri ya Korea hapa nchini Mheshimiwa Young-hoon Kim jana jijini Dar es salaam.Fedha hizo zitasaidia miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa Chuo Kikuu cha Muhimbili na usambazaji maji katika Manispaa ya Dodoma. Habari na Picha na Tiganya Vincent - MAELEZO

Jamhuri ya Korea imetiliana saini na Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania ya kuikopesha shilingi bilioni 173.8 ( Dola la Kimarekani milioni 124) kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mitatu ya maendeleo hapa nchini.

Sherehe hizo zilifanyika jana jijini Dar es salaam na kuwakilishwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi Ramadhan Khijjah kwa niaba ya Tanzania na Balozi wa Jamhuri ya Korea hapa nchini Mheshimiwa Young-hoon Kim.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi Khijjah, fedha hizo zitasaidia ujenzi wa upanuzi wa Chuo Kikuu cha Tiba na Afya Muhimbili(MUHAS) katika eneo la Mloganzila, usambazaji wa umeme katika mikoa ya Arusha na Kilimanjaro na usambazaji wa maji katika Manispaa ya Dodoma.

Alisema kuwa katika mradi wa maji katika Manispaa ya Dodoma utagharimu shilingi bilioni 69.5 na utahusisha ujenzi wa vyanzo vya maji , ukarabati wa matenki ya kuhifadhia maji na ujenzi wa matenki mapya.

Khijjah alisema kuwa kwa upande wa upanuzi wa MUHAS jumla ya shilingi bilioni 69.3 zitatumika kwa ajili ya ujenzi wa kufundishia na eneo la kutolewa matibabu.

Pia mkataba huo unalenga kusaidia kuboresha huduma ya umeme katika baadhi ya eneo la mkoa wa Kilimanjaro na Arusha ambapo mradi huo utagharmu shilingi bilioni 35.

Aliongeza kuwa Dola milioni 18 zitasaidia vituo vya ufundi stadi katika katika mikoa ya Dar es aalaam , Pwani, Lindi na Manyara na Dola milioni 25 zitasaidia ujenzi wa daraja la Maragarasi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. KingangitiAugust 06, 2010

    Vipi wadau tuchangie na haya ya fedha a.k.a taswira nzima ya uchumi wetu tehe! tehe! toba dola inaogelea 1500+ tsh.Ah ndo mambo yetu hayo fedha inakopwa na plani ishawekwa vizuri kabisa tehe!utekelezaji toba wee!! tehe! tehe! mwe wacha muchezo bwana.Mungu tusaidie.

    ReplyDelete
  2. Waawaaa!! hizo hizo hizoo.. zimekuja, na zitakuja nying sana ..wapinzania mtakoma.

    Nyie piganeni na porojo porojo, Sisi kuilainiii tunazikusanya tu za kununulia kura za watu wenu, na zingine hamtaziona kwenye media! mmmmh, huku raha..utamuu!

    CCM oyeeeee!!!

    ReplyDelete
  3. chonde chonde zisiende kwenye uchaguzi puleeez, manake ni mkopo huu zatakiwa kurudishwa ati..

    ReplyDelete
  4. zitatafunwa hizo!!

    Mdau Paris

    ReplyDelete
  5. ENDELEENI TU KUKOPA MZIPELEKE PIA VISIWANI TU HIZO SIO WAKATI WA KULIPA WALIPE TANZANIA NZIMA

    ReplyDelete
  6. Hadithi ndefu juu ya miradi itakayosaidiwa na fedha hizi, lakini maelezo ya mipango ya kuzilipa hizi hela yako wapi?

    ReplyDelete
  7. MAMBO HAYA SIJUI YATAISHA LINI YA KUKOPESHWA KWA RIBA, INA MAANA HAWA VIONGOZI HAWAJUI KAMA ISLAMIC BANKING INAKOPESHA BILA RIBA?

    ReplyDelete
  8. korea zipo mbili. ni korea ipi iliyotoa hizo pesa?

    ReplyDelete
  9. itasaidia sana kwenye kampeni

    ReplyDelete
  10. sio ya bure hiyo,lazima they want something na si tunawapa...Tanzania bwana!!!

    ReplyDelete
  11. baba tume pata chakula,tutashiba auvipi

    ReplyDelete
  12. Mmmh huu mkopo usije ukatutokea puani tuu, Maana kama kawa ya Nchi yetu hapao watu binafsi watateremsha majumba na kuendesha magari ya fahari na hiyo miradi iliyolengwa haitafika kokote, then mkorea atakuja kudai deni lake hela hatuna hapo ndio atakapo taka tumpe uranium za kutengenezea nukes na tumuuzi mjomba usa! patamu hapo .......

    ReplyDelete
  13. Which Korea are you referring too Michuzi? North Korea or South Korea?

    ReplyDelete
  14. Mimi binafsi ningependa kuona hawa kina Tigana Vincent na wenzake wana ripoti specifics za hii mikopo. Riba, duration N.K. na pia kuripoti Serikali ina ahidi kulipia vipi hii mikopo, Mambo ya kutuwekea picha tuu za watu wanacheka sio uandishi wa habari. Binafsi siamini kama unaweza kurudisha huu mkopo kama utatumia hizi hela kujenga shule, au kusambaza maji na umeme kwa wananchi ambao hawana uwezo wa kulipia hii huduma. Ila unaweza kutumia hii hela kufanyia biashara ya tofauti itayo ingiza hela halafu ukatumia faidi ku sambaza hizi hudumu muhimu.

    ReplyDelete
  15. Maisha bora kwa kila Mtanzania. Madeni hayo nani atabeba mzigo? Walipa kodi?

    Jamani hatujifunzi toka kwa Mheshimiwa Mkapa kukusanya kodi hapa hapa tutaendelea tu. Lakini hiyo mikopo MMMMmmmmmmmmmmmm?

    ReplyDelete
  16. hiyo ni south korea kwani hamuoni bendera hiyo toeni tinted hizo na mnajuwa north korea ni masikini hawawezi tupa misaada pesayao yote wanaipeleka kwa miradi ya kutengeneza mabomu ya nuclear ni wajamaa hao bado nchinzima wanafvaa uniform

    ReplyDelete
  17. WAKATI UGANDA WANAENJOY MIKOPO ISIYO NA RIBA KUTOKA IOC SISI UDINI NDIO UNATUFANYA TUKOSE MIKOPO YA AINA HIYO, HUKO UGANDA WAISLAM NI ASILIMIA CHACHE SANA NA WATU WALIPOANZA KUPIGA KELELE M7 AKAWAAMBIA NIPENI ALTERNATIVE AMBAKO TUTAPEWA MIKOPO BILA RIBA NA MISAADA (INAYOTOKANA NA ZAKA ZA MATAJIRI WA MAFUTA) BILA MASHARTI NITAJITOA OIC.

    KAMA MAMBO YA KULIPA RIBA TUNAYATAKA WENYEWE KWA WOGA NA UDINI WETU

    ReplyDelete
  18. Tutahitaji vx kama 15 yakusimamiya hizo miradi na poso na per diem.hazitoshi

    ReplyDelete
  19. UCHUMI WETU UTAONEKANA UNAKUWA LAKINI "HAPO MBELENI NI KIZAZAA" TUNAMADENI KUPITA KIASI LAKINI HAWASEMI YATALIPIKA VIPI NA NI TRILION NGAPI(KUNAMADENI TULIYOKWISHA KULILIPA HAPO NYUMA "WANAJIFANYA WAMESAHAU" NA TULILIPA ZAIDI X3 YA MKOPO WENYEWE..... BILA FAIDA YOYOTE).WAWEKE HADHARANI NA "INTEREST YA MADENI YOTE". HAKUNA "CHOMBO BINAFSI" KINACHOFUATILIA HAYA MADENI TUANZE KUYAFANYIA KAZI SISI WANANCHI KWASABABU SISI NDIO WALIPAJI.

    ReplyDelete
  20. CCM o yeee kama tunaria

    ReplyDelete
  21. wewe unaye uliza which korea kwa kutaka kuonyesha una jua sana but unaonekana kweli darasa limepita pembeni !1 kwani huoni bendera hapo ni bendera ya korea hipi! wewe umeona tangu lini NOrth kerea wakatoa msaada wao wenyewe msaada

    ReplyDelete
  22. Hivi nyie wadau mnaosema tuchukue mikopo OIC bila riba MNAMAANA GANI? Vya BURE VINAUA. Kama wanania ya kuondoa umkaskini basi UGANDA INGEKUWA WALAU NI DUNIA YA PILI Lakini ni maskini tu ka sie.

    Swala si kuchukua mikopo OIC bali ni kujiuliza sisi wenyewe tutajikwamuaje na umaskini? Nchi ya Ethipi ilishawahi kutoa misaada ya vgyakula kwa nchi kama Sweden n.k Lakini sasa Sweden ni first world na Ethiopia imebaki palepale.

    TUJIULIZE Jinsi ya kujikwamua na Umaskini. We unadhani Marekani walichukua mikopo OIC?

    Tujipange kuuinua uchumi- nchi na si kuwaza vya bure.

    Wakupe cha bure wanakupenda sana au? Wanachi wengi wa Africa walioko kwa nchi za OIC wanataabika sana mbona hatuoni OIC kugusia hilo?

    Tuyaache hayo tuchape kazi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...