Mkuu wa kaya pole na mihangaiko ya kampeni naona imepamba moto kweli kweli ! Uzuri ni kwamba libeneke bado linaendelea kama kawa hivyo lazima nikupongeze sana kwa hilo !

Sasa pamoja na kwamba nchi nzima iko kwenye harakati za uchaguzi ,mambo mengine lazima yaendelee kama kawa na hivyo nimeona ni vyema nikawajulisha watanzania wenzangu nini kinachoendelea kwenye soko letu la ajira tokea tufungue milango ya soko huru julai mosi mwaka huu.

Ikumbukwe kwamba lengo la soko huru lilikuwa ni kufungua milango ya uwekezaji na ufanyaji kazi kwenye eneo letu la Afrika Mashariki kwa kuondoa vikwazo visivyo vya lazima na mpaka sasa makubaliano ni kwamba wananchama wa nchi 5 za Afrika Mashariki wanaweza kufanya kazi kwenye nchi yoyote ila kwa hapa kwetu wageni lazima waombe vibali vya kufanyia kazi wanapopata kazi hapa kwa muda wa miaka 5 ijayo ambapo vitaondolewa kabisa.

Hivyo Mkenya, Mganda,Mrundi,au Mrwanda akija hapa akipata kazi kihalali ataomba kibali uhamiaji . Ikumbukwe kuwa wenzetu Wakenya walianza ubepari zamani hivyo si ajabu ni nchi ya 2 kufanya biashara kwa wingi na Tanzania baada ya Uingereza hivyo pia tunategemea wakenya wengi wawepo kufanya kazi Tanzania lakini kwa kushindanishwa na wazalendo .

Cha ajabu mzee ni kwamba hawa wenzetu badala ya kutumia ushindanishi unaotakiwa sokoni kwa kuangalia vigezo na uwezo wa mtu wao wameanza kutumia propaganda,mizengwe na mbinu nyingine chafu za kuwaondoa watanzania kwenye nafasi zao na kuwapa wakenya.

Utakuta mtu anapewa kazi kwenye kampuni ya kikenya then anapigwa zengwe kuwa utendaji wake ni mbovu na kesho yake analetwa mkenya hata kama mtanzania ni mzuri kwa vigezo vyote au pia kuna kazi zinahitaji training wao hawatakupa hiyo training kwa makusudi ili ionekane huwezi kazi wamlete mkenya!

Mbinu nyingine wanayotumia wanakupeleka training kwao Nairobi labda mwezi mzima na huku nyuma wanamleta mkenya anafanya kazi zako kisha wewe ukimaliza training unaambiwa hukufikia vigezo wanavyotaka hivyo ujiuzuru au wakufukuze kazi au watakutafutia kisa chochote tu hata cha maisha yako binafsi yasiyohusiana na kazi yako halafu unatishiwa kuwa watakufukuza au ujiuzuru nwenyewe! Kisha wanaenda uhamiaji kumwombea kibali mkenya wao wakitoa sababu kuwa mtanzania waliyemweka ameshindwa kufikia vigezo wananvyotaka!

Wadau hizi ni baadhi ya mbinu tu wanazotumia hawa wenzetu kunyakua kazi wa watanzania kwa nguvu ! Kuna mifano mingi na watu wengi wameathirika na hizi mbinu chafu za wakenya hivyo naona muda muafaka umefika wa mamlaka husika kufanyia kazi hili jambo!

Tunaelewa kuwa Kenya maisha ni magumu sana ndo maana wanakimbilia huku kutafuata kazi wakati hakuna watanzania waliofanikiwa kupata kazi Kenya kwa kuomba tu kwenye makampuni ya Kikenya ukiacha wanaopelekwa na makampuni nya kimataifa yaliyopo Tanzania . Hii ni kwasababu Wakenya wana dharau sana (Kenyans are very arrogant) kwa mataifa mengine ya Afrika Mashariki na wanajiona wao wanajua kila kitu. Hii imesababisha hata wao kwa wao wabaguane kimakabila hivyo kampuni ya Mkikuyu huwezi kumkuta Mjaluo au Mkamba ! hiki ndo chanzo cha wao kuuana mwaka juzi baada ya uchaguzi wao maake kule kwao wanaishi kwa mbinu za msituni (survival of the fittest) .



Hata hapa kwetu wafanyakazi wengi walio chini ya mabosi wakenya wanadharauliwa na kunyanyaswa kisa ni watanzania hata kama wana uwezo kuwazidi hao wakenya !

WATANZANIA TUFANYEJE

Ningependa kuwashauri wadau wanapokutana na hali hii wasikae kimya na kusubiri mungu awasaidie . wajue kwamba huu ni mpango maalum ambao wenzetu wamekuja hapa kupokonya ajira za watanzania hivyo tuchukue hatua madhubuti ambazo ni pamoja nazifuatazo:

-hakikisha kila unapofanya kitu kizuri ofisini kwako bosi wako anajua .Hii itakusaidia sana wakati wa kureview performance yako kazini . wenzetu wanaijua sana kuitumia mbinu hii inayoitwa corporate politics! Akifanya jambo dogo tu lazima amwambie bosi wake hivyo kujilinda pakitokea tatizo baadaye.

Watanzania tusikae kimya kusubiri bosi wako aone mwenyewe kuwa wewe unafanya kazi vizuri sana ! mfuate bosi mweleze mafanikio yako kazini na sio kujificha bosi akipita koridoni oooh utakula wa chuya !

Pili tuhakikishe tunazijua sheria za kazi vizuri na sio kutishiwa tishiwa tu na hawa wakenya wakati nchi ni yetu bwana ! tujenge utamaduni wa kusoma haki zenu ndani ya sheria ya kazi ili likitokea jambo tuweze kujitetea ipasavyo. Japokuwa sheria zenyewe zina mapungufu kwa mfano mwajiri anapewa uhuru wa kuchagua akurudishe kazini au akuachishe kazi na kukulipa mshahara wa miezi 12 tu ! sheria ibadilishwe hii !

Tatu tujifunze bargaining skills wakati wa kuomba kazi maake utakuta wengi wetu mishahara ni midogo sana kwani wakati wa kuomba kazi tunamwachia mwajiri ajipangie mshahara wa kukulipa matokeo yake hata ukimpeleka mahakamani atakulipa vijisenti vya miezi 12 na kukufukuza kazi huku nafasi yako akipewa Mkenya na kulipwa kama expatriate.

Nne tungependa vyombo vinavyohusika na kutoa vibali vya kazi kwa wageni (hasa wizara ya mambo ya ndani, wizara ya kazi na professional bodies ) vijiridhishe kweli hakuna Mtanzania mwenye uwezo wa kufanya kazi ambayo kibali kinaombwa. Hivi kweli jamani hatuna wahasibu wa kutosha mpaka Mkenya aje awe management account (mhasibu wa ndani) au financial controller (mhasibu mkuu ) hapa Tanzania wakati NBAA wanatoa CPA mara 2 kwa mwaka ! hawa vijana wanaomaliza hizi qualification watafanya kazi gani sasa ? Tuachane na njaa za muda na utamaduni wa kuabudu wageni ! Tuamini wazalendo na kuwajengea uwezo wa kufanya kazi .



Tano watanzania tubadilike tujenge attitude ya kujituma kazini maake soko la kibepari ndo linavyotaka ! ukiwa mvivu kazini wakenya watazidi kuja na kuchukua nafasi zetu nasisi tutaishia kulalamika tu ! hivi sasa mabenki makubwa 3 madirector wao ni Wakenya ! mshahara wa director mmoja tu unatosha kuwalipa watanzania zaidi ya 20 wa ngazi za chini na hapo bado hujazungumzia wenzao waliowaleta toka Kenya na vitu wanavyonunua kwa makampuni yaliyo Nairobi hata kama kuna makampuni ya Tanzania yanazalisha kitu hicho hicho maake bosi ndo mwamuzi !

Naomba kuwakilisha

Mdau aliyetendwa na wakenya !!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 23 mpaka sasa

  1. kitendo chakuakaribisha wakenya hakuna rangi tutaacha ona hawa watu wanaroho mbaya sana na wanaugonwa mmbaya sana ya ukabili yaani kukaribisha hawa manyangau nikosa kubwa sana sasa hivi ujambazi utashabiri tena hawa watu sio wenzetu wanakila aina ya ubaya wabinafsi sana watanazania tuliozoea amani hapa tutaula wa chuta kwa uvivu wakuchambua hawa sio watu wakushirikiana nao

    ReplyDelete
  2. Tuna big excuse kwamba wakenya wanajua sana english ndio maana wanastahili kupata top posts Tanzania.

    This is never true. World statistics from wikipedia zinaonesha 9% ya watanzania wanajua english na 7% ya wakenya wanajua english. Only that kila mkenya anajitahidi kuongea "some english" ambayo sio good english-Find a link below
    List of countries speaking english
    http://en.wikipedia.org/wiki/List_of_countries_by_English-speaking_population

    Shida yetu ni unyonge na kujiweka nyuma na kuwa tayari kuonewa-Nidhamu ya woga.

    ReplyDelete
  3. Maendeleo hayaji kwa kujua English nina mifano mingi ya nchi zilizoendelea ambazo wananchi wake wengi hawaongei Engliosh lakini zimepiga hatua kimaendeleo katika nyaja zote. Angalia China, na Japan sio wamendelea na wanakuwa maleader kiuchumi duniani lakini lugha ya taifa sio English mbona wameendelea?????? la msingi sisi watanzani we dont have confidency for everything halafu Education needs to be restructured kwendana na mabadiliko ya IT la sivyo tutakuwa tunalalama hapa kila siku na kupigwa bao na hao wakenya simply tu Gov imeshindwa kubadilisha mfumo mzima wa Elimu nchin. Wachangiaji wa kwanza wamejaribu just kutoa lawama bila kutoa solution nakaribisha mjadara uendelee kuhusu Elimu yetu ya Bongo. Nashukuru kwa mtoa mada hii maana Blog nayo ilikuwa imeeegemea upande mmoja tu wa CCM na hata hiyo CCM wenyewe hawataki DEbates ambapo tutapata majibu ambayo hatuwezi kuuliza kwenye Hotuba zao.
    www.opulukwa.blogspot.com

    ReplyDelete
  4. Huyu mdau aliyetoa haya binafsi naona anachuki binafsi. Kwanza anaanza kwa kuwajumuisha wakenya wote (Wabaya na Wazuri). Sisemi kwamba hamna makampuni mabaya Kenya bali si kweli kwamba makampuni yote ya Kenya ni mabaya. Pia Huwezi kusema makampuni yote ya Kitanzania ni mazuri. Hapo tutakuwa tunadanganyana. Huyu hapa angetuelezea kwamba ni kampuni gani ya Kenya anayosema inabagua basi atoe mfano na naamini kwamba kampuni husika itatoa maelezo. Kama hana mifano basi hana haki ya kuzungumza kisichokua na msingi. Tusitumie kigezo cha uraia kufikia azimio binafsi ya kuleta kutoelewana baina ya taifa jirani. Tupe mifano na siyo wakenya hivi.. wakenya vile.

    ReplyDelete
  5. Jamani Mzee Mkapa alishatuambia kuwa sie Watanzania ni WAVIVU. Sasa wewe unasema mabank 3 hapa Bongo Directors wake ni Wakenya, je wamiliki wa hizo Bank ni Wakenya pia? Je hakuna Human Resource hapo kazini kwenu kama unaonewa? Tuache kuona tunaonewa na kugangamara sio kuanza ooh wakenya...Haka akipata Mtanzania mtaanza Ohh jamaa ni mchagga anawaleta wachagga tu au ooh jamaa ni mhaya kazi kupendelea wahay tu. Tuache UVIVU!!

    ReplyDelete
  6. Tatizo letu watanzania sisi ni wavivu, wadokozi na wazembe kazini, hilo tusikatae. Na ndio maana wanakuja wakenya wanatutawala na hatimae wanatudharau. Sio kwamba hatuna ujuzi ila hatutaki kujituma hata kidogo wala kujishughulisha na ndio maana anakuja mkenya japo hana ujuzi lakini kwa sababu anajituma.

    Leo ukifanya utafiti basi makampuni makubwa yana wakenya na hii siku zote inaongezeka tuuu.. mdau umetoa nasaha nzuri za kujirekebisha sisi watanzania lakini bado tuna kazi ya kufanya. Mkenya ana ubinafsi, ni mshenzi na ana dharau lakini mchapakazi. Tunashindwa nini sisi pia kuwa wachapakazi tuuu? Leo rwanda imepiga hatua na baada ya miaka kumi watatuachia vumbi tu... tanzania itaitwa kenya baada ya muda mfupi

    tuendelee kufanya mzaha tuuu

    ReplyDelete
  7. Haya ndio mambo wapigakura wanatakiwa kumuuliza mgombea. Maana serikali inasema tunatengeneza mazingira ya uwekezaji amabayo yataleta kazi, lakini kama hizi kazi ni kwaajili ya wageni, mzawa utakula wapi. Mi ndio maana nilikuwa nampenda sana Mtikila. Ukikaa nje ya nchi ndio utajua kwamba kubaguliwa kukoje, hata uwe na sifa zinazotafutwa na mwajiri, kitu cha kwanza wenzetu wanaangalia ni je wewe ni raia?

    CCM iko wapi?!

    ReplyDelete
  8. You guys stop this nonsense. Fanyeni kazi. Na tumieni akili, za darasani na za kuzaliwa.

    Pia msirizike haraka. Unakuta kijana akijenga nyumba na kununua kaToyota anarelax anaona amefiiiika!

    ReplyDelete
  9. Ebwana, umetoa mada muhimu saana. Yaani sisi sijui tumerogwa na nani na kisha akafa, tego alotuwekea hadi huyo jamaa afufuke. Hawa jamaa wa nchi jirani hawafai. Kuna jamaa yangu weshamfanyia kitu mbaya. Yalokutokea ndo yalomtokea na huyo jamaaangu. Hivi kweli, kweli hatuna vijana WANAOJUA KAZI hadi tuwaite hawa jamaa!!!

    Mimi nimesoma na hawa jamaa ughaibuni, wanajua kiinglish japo sio cha sana, wakawa wanatudharau wa Tz, nikawaambia jamaa zangu hakuna haja ya kushindana nao. Wanataka wao waonekane the best, imagine kwaa level ya Masters mtu bado anaficha anachoandika. Tulipomaliza course work hapo ndo walijua wabongo nuksi. Yaani hangare hangare za vyuo vyetu tunajifunza mengi sana. Kuandika thesis imewachukua mwaka na nusu na kiinglish chao kibovu ili hali ilitakiwa six months only. Wabongo wote tulimaliza kwa wakati wao hata cha kufanya hawajui kabisa. NB: thesis ilikuwa inabeba zaidi ya 3/4 ya course yote. Tuliwacheka tukawa tunawaambia "AMA KARA KARARIO AMAKORO" Ni kikikuyu maana yake mtachekea chooni.

    Hawa jamaa mpaka leo wanatujeshimu na huwa nachati nao kwenye face book yangu wanakubali wabongo!!!!xciXCHWIIIIIN!
    wABONGO TUSIDANGANYIKE NA KIINGEREZA CHAO. vYUO VYA BONGO BADO ELIMU IPO JUU SANA NDUGUZANGUNI.

    ReplyDelete
  10. Mtoto wa CoastSeptember 30, 2010

    Mdau imebidi nikupe heko kwa andiko lako.

    Hata hivyo lazima tusisitize pia jambo moja kuwa suala la uwajibikaji bora ni la mtu binafsi kama ilivyo wokovu!

    Yaani hakuna cha kusema kuna ubora kwa Watz zaidi ya WaKenya au zaidi ya Waganda n.k.
    Utendaji unapimwa kwa mtu mwenyewe binafsi momoja mmoja hivyo ndg. zangu WaTz tujitahidi kuchapa kazi kwa ubunifu na kwa ufanisi. Tujiamini na tunaweza sana.

    ReplyDelete
  11. Well said!! Natumaini watu wenye kushughulikia hayo mambo watapitia na kuona na kuelewa hii njama na kujua ni nini kinaendelea.

    Inasikitisha kuona wanaokula nchi ni watu wa nje na wazawa wanakufa njaa.

    Culture yetu imetukuza vibaya sana na hii inaanzia majumbani kwetu. Nakumbuka tukiwa wadogo mgeni akija nyumbani watoto mnampisha mgeni chumbani nyie mnalazwa sebuleni kila siku. Hata kama huyo mgeni anakaa miezi mitatu hapo nyumbani kwenu. Nenda uwe mgeni hizi nchi zilizoendelea utalala sebuleni mpaka siku unayoondoka. Kwanza utakua uncomfortable mwenyewe ukatishe safari yako mapema. Ninamaanisha kuwa mfumo wa nchi yetu na ukarimu wetu ndio unaotumaliza. Hao wazazi waliotulaza sebuleni ndio hao wanaofanya kazi na kuingiza wazungu na foreigners na kusahau watoto wao. Well, unaweza kuwa mkarimu lakini usifanye kwa kiwango cha kusahau watoto wako, ndugu zako etc etc kwa mgeni anayepita njia. Culture yetu kuwaona watu wa nje ya nchi ni bora kuliko sisi ndio inayotuumbua na imepitwa na wakati. Wao wanajali kwanza raia wao halafu wewe ndio uwe wa pili.

    Halafu tunatakiwa kuwafundisha watoto kuweza kujieleza tokea nyumbani. Hii kitu ya baba ndio mwenye last saying ndio inawaharibu watoto au ilituharibu sana. Hivyo sisi tusiendeleze hii kitu kwa watoto wetu. Tuwafundishe watoto uhuru wa kujieleza toka wakiwa wadogo. Siye tumekuwa wakubwa na waoga waoga tu. Mwanzoni nilivyokuja huku nilikua naogopa walimu, kazini naogopa maboss. Kumbe hiyo ndio inatupotezea bahati. Boss na mwalimu sio watu wakuogopwa mpe heshinma yake lakini pale unapotaka kumweleza kitu usiogope. Bosses ni kama watu wengine hawajui kila kitu na ukiwaeleza kitu 90% ni cha muhimu na cha kuongezea company faida. Sio unakaa kimya halafu akifanya mwingine unasema I knew that lakini niliona nikisema itakua soo. Kwa vile nyumbani kwetu huwezi kumwambia baba umekosea. Wabongo wengi ni yes sir yes sir always...Tumekuwa suppressed so much kwa hiyo hatuwezi kueleza nini tunachofikiria na maboss wanatumia hii advantages ya kutunyakulia kazi kuwapa watu wenye uwezo wa kujieleza na kuchangia mawazo katika kampuni. Sisi kwetu mwalimu na boss ni adui yako ukimwona unakimbia na kujificha...

    Pia watanzania we are lucky of confidence a lot...tunabelieve on white people or foreigners sana tu. Ukisema tu mtu fulani kaoa/kaolewa swali la kwanza unaulizwa kaolea/kuolewa na mzungu au mkenya?? It is sad sana inayoonyesha mpaka leo mawazo ya watu wa Tanzania wanavyofikiwa watu wao wenyewe. Hivi mzungu au foreigners wanatuzidi nini? Mwingine anaweza kuajiri mzungu/mkenay tu hata kama hana ujuzi just because na yeye aseme kampuni yake ina mzungu. Ukumbuke hata wewe ni foreigner kwenye nchi ya nyingine. Lakini jiulize wewe ukienda kwao watakutreat the same you do when they come into your country?

    Mwisho tujifunze kuchapa kazi. Mambo ya kuingia na kulala kazini usubiri saa kumi utoke uende nyumbani, kuingia kazini upost updates on facebook, sijui kuangalia mablog ukiwa kazini, sijui chat halafu utegemee kulipwa vizuri kwa vile unakadgree kako ka mlimani yamepitwa na wakati. Degree sio miguu siku hizi ya kukupeleka kokote. Jinsi unavyoitumia hiyo degree yako ndio miguu yako. Hata kama huna degree unachapa kazi vizuri utaheshimika na utafika mbali sana.

    ReplyDelete
  12. Well said, natumaini wenye kushughulikia haya mambo watafuatilia na kujua nini kinachoendelea.

    It is sad kuona kuwa wageni ndio wanakula nchi wakati wazawa wanakufa na njaa.

    Culture yetu inatuharibu na inaanzia hata nyumbani. Nakumbuka tukiwa wadogo ilikua mgeni akija watoto tunalazwa sebuleni na mgeni hutumia chumba mpaka siku anayoondoka. Nenda kwa wenzetu ukawe mgeni uone utakapolazwa. Ukarimu wetu ndio unautuponza na kuona mgeni ni mtu muhimu kuliko sisi. Ndio ile mgeni njoo mwenyeji apone…Why??? Na hao hao wazazi wenye tabia hizo nyumbani ndio wanaopeleka mpaka makazini. Watu wengi huajiri mzungu/mkenya hata kama hana qualifications zinazohitajika ili mradi tu na yeye aonekane ana mzungu/mkenya anafanya kwenye office yake.

    Pia tuongeze confidence ya watu wetu. Watu wanathamini sana wazungu au foreigners. Ujue na wewe ni foreigners kwenye nchi nyingine lakini jiulize ukienda kwao watakutreat the same way unavyo treat them? Hawasahau watu wao na hawaput watu wako mbele zaidi ya wakwao. It is sad nikiongea na old school mates zangu na kuwaambia fulani kaoa/kaolewa swali la kwanza unaloulizwa kaoa/kaolewa na mzungu? Inaonyesha jinsi fikira zetu zilivyo duni mpaka leo. Mtu akiolewa/akioa na foreigner basi anaonekana yuko kwenye class nyingine…It is very sad

    ReplyDelete
  13. Pia tunatakiwa kuwafundisha watoto uhuru wa kujieleza na kuwa friendly na watoto wako. Ukiwaachia watoto waweze kujieleza pia wanakua more creative. Wazazi wetu walitufanya tuwaogope sana na kuwaachia wao ndio wawe wanasema kila kitu na final saying is always from them. Hata kama unaidea nzuri huwezi kujieleza. Na hiyo tabia tukafundishwa mashuleni. Tumekuzwa siye mwalimu umwogope na kusikiliza tu. Hamna kujadili hata kama unajua kuna mahali kakosea au unataka kuongezea nini unachojua. Na ukitoka shuleni where are you going? Kufanya kazi!!!! Unapeleka yote yale uliyofundishwa toka nyumbani uoga, muted na lack of confidence. Na tunasubiri bosses watwambie nini cha kufanya na ujue boss ni kama mtu mwingine. Hawajui kila kitu na ukiongea unaweza kuta 99% ya kile kitu kinasaidia mchango katika kampuni yako. Na maboss wanapenda hiyo kwa vile wanachoka kuwaeeleza watu kila kitu cha kufanya. Siye tumezoea kuapply tu kile tulichofundishwa. Hatuwi creative kwa vile tumezoea baba kusema nini tufanye kila siku. Sio ukae tu halafu akifanya mtu mwingine ambaye ni foreigners unasema I knew that. Aliyesema au kufanya kitu fulani ataongezwa cheo wewe ubaki pale pale. Sio tumezoea kuomba kazi na kusema najua hiki najua kile …Kazi sio kuapply tu kile unachokijua. Kazi ni kuonyesha nini ulikifanya huko ulikopita? Hicho unachokijua ulikitumiaje kuaccomplish something?

    Ila yote hayo hayatawezekana kama na siye watanzania hatutajifunza kuchapa kazi. Mambo ya kuingia kazini asubuhi cha kwanza ni kucheck updates za facebook, post updates, sijui soma blogs ndio yanatuharibia. Wewe ukikaa sijui kwenye office ukizania kamaster kako ndio katakushika hapo sahau. Sio elimu e itayokupeleka mahali ni jinsi unavyotumia hiyo elimu kuchapa kazi. Juhudi zako ndio zitakuongezea sio elimu ya kukaa darasani tu. …

    ReplyDelete
  14. nakubaliana na mtoa mada jamani yani mahotelin ndo usiseme mimi mwenyewe muathirika alipozidi kunisumbua nikaita migration kumbe hakua na work permit akatimuliwa,yaai sasa hv nmekomaaa kinyama mkenya hanisumbui hata kwa dawa.

    ReplyDelete
  15. Majibu ya elimu yapo hapahapa nchini kwani wiki iliyopita na wiki hii wataalamu wametoa ushahidi kuonesha kiwango cha elimu yetu, pia upo ushahidi halisi wa Zain University Challange ambapo tangu mashindano haoy ya vyuo vikuu Kenya na Uganda wamekuwa wakitushinda; ubishi hautatusaidia kitu bali suluhisho ni kujiendeleza na tuondokane na uchakachuaji wa mitihani. Watanzania tuanjulikana sana kwa ulalamishi usioisha kila kukicha sababu sababu tu.

    ReplyDelete
  16. Kenyans are working for Kenyans in order to improve their lives. Kenyans are not here to coperate with Tanzanian they are here to make sure that all of Tanzanian are going to loose everything. Take an example of EAc. All Senior positions are for Kenyans. Your guys we have to resist this condition. This is our country we have to benefit from our country we cannot to slaves within our country. Nina hasira sana ni hii situation.

    ReplyDelete
  17. Nani iliyaua makampuni yetu? Nani aliiua Bora? mbona Bata ya Kenya bado ipo wakati sisi tulitaifisha kiwanda cha Bata tukaiita Bora kisha tukaiba viatu vyote kupitia kwenye senyenge? TanBond iko wapi? mbona Blue Band bado ipo licha ya kuanzishwa miaka ya hasini? ATC ameila nani? haya ndiyo yakujiuliza na si kuwasingizia wakenya, matatizo kwenye makampuni yetu ni makubwa sana, Kenya Bus bado ipo KAMATA kwishna na ilitokana na OTC na Kenya Bus. Visingizio haviwezi kutufanya tuajiriwe hata kama hatutaki kufanya kazi ndiyo maana makampuni ya simu na mengine yanaleta bahati nasibu ambazo yanavuna kiulaini sisi tukiamini utapata pesa kiulaini!Kudadadeki.

    ReplyDelete
  18. Mdau nakupongeza kwa comments zako. Lakini wachangiaji wengine huwa hawajui kilichosemwa na wanarukia kuponda kilichomo bila kujua au kwa makusudi. Hata hivyo huwezi kuwalaumu sababu sio kila mtu anajua kila kitu, hata kama mtu huyo amesoma mpaka PHd. kwanza kadri unavyosoma elimu ya juu ndio upeo wako wa mambo au field nyingine unapungua sababu unakuwa unajikita katika eneo lako zaidi la elimu.

    Kwanza mkubali mkatae ni ukweli usiopingika kuwa wakenya wengi wana dharau dhidi ya Watanzania na Raia wengine wa Afrika Mashariki. Kama vile mnavyolaumu Watanzania kuwaogapa wakenya kama ni ujinga au uoga basi wakenya nao inawezekana ni ujinga au tabia yao ilivyojijenga..

    Pili Wakenya wengi ni wabaguzi aidha wa Utaifa, Ukabila, Umajimbo na hata udini. Kama mtu anabisha hilo aende Kenya atagundua na hata Uchaguzi wao uliopita ulithibitisha hilo, labda ni mpumbavu tu ataendelea kubisha.

    Tatu, ni kwa sababu mbili za hapo juu basi huhitaji kuwa mtaalamu au Mwanasayansi wa roketi kuthibitisha nini kitatokea endapo hawa watu wana tabia hizo.

    Ukimkimbiza Mwizi kimya kimya ni vema zaidi sababu anajua ukimshika utamuua hivyo atanyoosha mikono juu ajisalimishe, ndio nnachosema waacheni watudharau lakini takwimu na ukweli halisi ndio vitawaumbua. Kwa mujibu wa Wikipedia Tanzania inaongoza kwa kuwa na raia wengi wanaozungumza kiingereza ambao ni Milioni & sawa na 9.89%,Kenya Raia Millioni 2.7 saswa na 7.19% na Uganda Millioni 2.5 sawa na 8.9%, hii nikweli kabisa sababu pamoja na kuwa watoto wa Kitanzania wamejaa katika shule zao na Vyuo vikuu vyao (Kenya na Uganda)bado sasa hivi kuna shule nyingi na vyuo vinatoa elimu bora hapa nchini lakini pia hazina raia wa Nchi hizo, hivyo basi tunawashambulia kutoka pande zote.

    Ni suala la muda tu tutawashika kila mahali.

    ReplyDelete
  19. Haya ni majungu tuu hakuna lolote,story ya kutunga tuu,kama kweli toa jina la kampuni na issue nzima waliyofanya sio kuandika tuu wakenya wabaya,hizi point tumesikia sana kwa wale wasiopenda hii EA tangu zamani..acheni majungu na kusikiliza watu kama hawa wenye agenda zao,nia yao ni kufanya watu wachukie wakenya/wageni

    ReplyDelete
  20. Pole sana kama ni kweli ulitendwa!!

    Hapa Bongo kuna ugonjwa mkubwa, mmoja wapo ni kulalama kwa kila kitu badala ya kufanya kazi na ku-focus.

    Sijui tatizo ni nini, hata Raisi wetu alishawahi kusema hajui tatizo, na Waziri Mkuu (kutoka Sumbawanga) akajiuliza kuwa nchi imerogwa na nani?? Kwani tulishindwa kuendesha hata bishara ya Bia (TBL)na sigara(TCC)!!

    Tukijua kinachotufanya kushindwa kuendesha biashara raisi kama hizo itakuwa ni hatua mojawapo kujua kinachoendelea sasa hivi.

    Utendaji wa Wakenya haujaletwa na upepari, kwani wajamaa wa China ndio wanafanya kazi kama mchwa. Tutafute tatizo jingine.

    Waethiopia na matatizo ya ukame na vita lakini wanaendesha makampuni yao wenyewe wazawa!! Ethiopian Airlines inapeta (ATCL iko wapi??).

    Mchawi hayuko Kenya wala China wala Burundi, mchawi ni sisi wenyewe Wa-TZ!! Rejea hotuba ya Raisi Mkapa mwezi January 2005 (nafikiri aliona baadhi ya matatizo ya TZ).

    Yeyote akikudharau au kukunyanyasa, hiyo inaonesha insecurity aliyonayo dhidi yako, wewe kaza uzi, hakuna kulipiza wala kumchukia. Msamehe tu!!

    Wewe chapa kazi, na sio kwa kujionesha, chapa kazi, output zitaonekana, kama hazitambuliwi anza mbele, itafika pahala ambapo utavuna jasho lako. Wanasema kwa kawaida "cream" hatimaye ujitokeza juu ya "naji", keep working comrade!!

    ReplyDelete
  21. Kaka Michuzi
    Kuna msoba umetokea leo hii hapa Botswana kwa mjasiria Mali mkuu wa Teknohama kwa jina la Andrew Dachi/Druu Dachi /Adam Dachi maiti inasubiriwa toka Botswana kwa mazishi kwao Dar Es Salaam, Kigamboni tafadhali turushie na ufuatile habari hizi

    ReplyDelete
  22. Watanzania acheni Pombe, na Rushwa, na tutumie muda huo kuangalia haki za binadamu na jamii zetu kwa ujumla. Saheria zipo lakini ni sawa na hakuna sheria. Inatia uchungu sana wakati kuan viongozi ambao ni hawataki kujuwa wananchi wanshida gani.Huo ndiyo mfano mzuri kaka umetuletea, na bado hatujaona kitu bado, wataanza kuowa dada zetu, na wakishawazalisha watakimbia na kuacha watoto hapo nyumbani bila baba. Wafundisheni dada zetu waiswapapatikie hao jamaa hawana chochote. Well sikilizeni UBAGUZI ni mbaya sana kwa nini kama mmoja akifukuzwa watanzania wote mnagoma manakwenda offisi za kazi mnawatimuwa huko offisini wakaangalie ni utaratibu gani wa kazi unafanyika hapo?

    ReplyDelete
  23. bora mie nauza karanga zangu sokoni kariakoo, kazi kwenu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...