kaimu mkurugenzi mtendaji wa manispaa ya Bukoba Robert Kwela akipongezana na rais wa klabu ya rotary ya Bukoba mara baada ya kukabidhiwa mabembea yaliyojengwa na klabu hiyo kwenye ufukwe wa ziwa victoria yaliyogharimu zaidi ya shilingi milioni 18.1.
Rais wa klabu ya rotary ya Bukoba,Elias Mashasi akisoma taarifa ya mradi wa mabembea kwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa manispaa ya Bukoba,Robert Kwela ambao ulitekelezwa na klabu hiyo kwa fedha za wahisani na baadae kukabidhi kwa manispaa hiyo kwa ajili ya kuuendesha.
baadhi ya wanachama wa klabu ya rotary ya Bukoba wakicheza kwenye mambembea waliyoyajenga baada ya kuyakabidhi kwa uongozi wa manispaa ya Bukoba, aliyesimama nyuma ya wanachama hao ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa manispaa ya Bukoba, Robert Kwela.Picha na Audax Mutiganzi,Bukoba.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Haya sasa tukutaka tutoe dukuduku Mithupu anabania,ila ushauri wangu tu hivi hawa Rottery Club hawatambui kwamba Bukoba kuna tatizo kubwa la madawa mahospitalini?hiv wanashindwa kweli kwenda kugawa dawa au kujenga kazahanati ka macho kenye thamani ya M 18 na ikawasaidia watu au kununua zile ambulance ndogo za Townace zenye kugharimu M 15 badala ya kujenga bembea tena mbaya zaidi kwenye ufukwe wa ziwa na kisha wanamualika kaimu mkurugenzi aje kusherehekea wakati wanaharibu mazingira...ah Michuzi we ibanie hii ila ujumbe utafika sio kila kitu kifanywe na serikali tu.

    ReplyDelete
  2. Sasa nyie mtavunja bembea. Hizo ni za watoto hebu acheni.

    ReplyDelete
  3. SASA HIZI NI ZA WAZEE AU WATOTO? KAMA ZA WATOTO MBONA HAWAONEKANI KWENYE PICHA?

    ReplyDelete
  4. ha ha haaa mdau hao wanaobembea ndo watoto kwani hukuona picha ya juzi wale waliokwenda kwenye michezo india ? zilikuwa za mawaziri na maofisa ubalozi za wana michezo marufuku, kila kitu uzandiki tuuuuuuu!!!!! wamesema bembea za watoto baba zao wanabembea kaazi kwelikweli!!

    ReplyDelete
  5. Michuzi tunaomba ututmie hii picha baada ya mwaka au miezi michache. Mdau hapo juu ni kwamba watoto wanahaki ya kucheza pia kila mahali ambapo pako wazi. Tunashukuru kwa wachache kujuwa umuhimu wa watoto na viwanja vya kuchezea, na siyo kucheza kwenye vibambaza vya nyumba tu. Offisi za arith ziliuza kila mahalia kwenye miji hakuna plan tena ya watoto, watoto siyo taifa kwa mawazo yao. Taifa ni kwa watu wazima wanaohitaji mahali pa kujenga tu.

    ReplyDelete
  6. Kubembea wazee si hoja; kwani hizo bembea hazijaundwa kwa uzito wa watoto wa shule za chekechea! Wacha nao wajikumbushe utoto wao - ala; after all wao ndio wamejitolea inabidi wa-test kama zinafanya kazi.

    Wasix2 wangu tu ni kwamba, wananchi hawaridhiki na hii misaada. Majuzi haox2 Rotarry Club wametoa vyandarua kwa wazee, maeneo ya Mwanza; wazee wakadai vitanda - eti watalalaje na kutumia vyandarua wakati hawana vitanda.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...