Ni watu maafuru katika tasnia ya Habari. Wengi wao majina yao yalikuwa yakisikika kila uchao redio ni au katika luninga, miaka ya 80 na 90 kwenye stesheni za ITV na Radio One Stereo enzi hizo.

Baadhi ninawafahamu kwa kuwaona kwenye luninga, wengine siwafahamu kabisa. Najaribu ila nitakwama: Na je wako wapi kwa sasa?

Waliosimama L-R: (?) Mike Mhagama, (?), (?), Vicky Msina (pengine), (?), (?), Sunday Shomari, Taji Liundi
Walioketi L-R: Charles Hilary, Mikidadi Mahmoud, (?), Anko J Julius Nyaisanga

Da'Subi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. Hapo Deogratias Mshigeni au mzee wa chombeza umemsahau.

    ReplyDelete
  2. Hawa walikanusha siku za nyuma na kusema hawajwahi kufanya na hawatarajii kufanya utafiti wa uchaguzi wa urais wa nchi yetu. Maajabu ni kwamba wameleta majibu ya utafiti.
    1. Watueleze wamefanya lini?
    2. Nimesoma hio ripoti ya utafiti ni mbovu na inaonekana imetengenezwa na mwanafunzi aliefeli elimu ya darasa la nne(miaka ya karibuni).
    3. Ripoti ina makosa ya uchapaji mengi kweli achilia mbali majedwali yaliyowekwa.
    4. Ukurasa wa 8 wanamtaja Jakaya Kikwete anakubalika 1% ( 0% sehemu za mijini) wakati Ukurasa wa 11 wanamtaja Jakaya Kikwete anakubalika 61%.
    Watueleze wamepikia wapi hio ripoti manake ni kichefuchefu tu, nasikitika nimepoteza muda wangu kuisoma.
    Hawa jamaa wasituletee za kuleta

    ReplyDelete
  3. Kwa kifupi wote wazee kwa sasa.Wamekula na "kuramba" chumvi nyingi.

    ReplyDelete
  4. Kabla ya Vicky Msina ni Flora Nducha na kabla ya Mike Mhagama ni Deo Mshigeni

    ReplyDelete
  5. Tunashukuru kwa picha hii nzuri ya kumbukumbu, hususani kwa wadau wa bongo.
    Kulekebisha tu kidogo, kusema kwamba walivuma miaka ya 80. Nadhani hapo ni kwa wale waliokuwa Radio ya Taifa(RTD) Mikidadi M,Julius N, na Charles H.
    ITV na Radio One havikuanza mpaka miaka ya 90'
    Na wadau wengi wakiwemo hao watatu niliowataja hapo juu walihamia huko.
    Ni marekenisho madogo tu

    Mdau Dar.

    NB: Usidandie gari kwa mbele, utagongwa...

    ReplyDelete
  6. waliosimama wa kwanza kutoka kushoto ni deo mshigeni. Yuko marekani siku hizi.

    ReplyDelete
  7. Hawa walikuwa watangazaji waanzailishi wa Radio One na MD wa kwanza wa ITV na Radio One.

    Waliosimama L-R; Deo Mshigeni,Mike Mhagama, Monica Mfumia, Flora Nducha, Vicky Msina, Aboubakar Liongo,Lilian Mbaga (Mrs Liundi), Sunday Shomari, Taji Liundi

    Na waliokaa L-R: Charles Hillary, Mikidadi Mahmoud, Mike Ross, Uncle J Julius Nyaisanga

    ReplyDelete
  8. Mikidadi Mahmood nimemwona juzi juzi tu, AFYA yake Du! anahitaji mazoezi sana, otherwise atapasuka sasa ivi!

    ReplyDelete
  9. Katika ninachomkumbuka zaidi Mikidadi Mahmoud ni alivyotangaza ile mechi bora kabisa ya kimataifa kuwahi kuchezwa katika ardhi ya Tanzania kati ya Simba Sports Club na vijana wa Atletico Sports Aviacao (ASA) kutoka Angola, hii ilikuwa ni nusu fainali ya kwanza ya kombe la CAF. Mzee mzima Mikidad Mahmoud ndio alikuwa mmoja kati ya watangazaji, hakika alikuwa mtangazaji bora sana. Kiukweli sijamsikia muda mrefu sasa na sijui anafanya kazi wapi tena. Kwa hakika ile mechi ilikuwa ni mechi kali sana, ASA wakiwa na kikosi bora kabisa kikiundwa na wachezaji kama golikipa Kanka Wemba, pia walikuwepo akina Keleke, Yanda wakati Simba kikosi chao kilikuwa na akina 1. Mohamed Mwameja (kipa bora kabisa katika historia ya Tanzania), 2. Kasongo Athumani 3. Deo Mkuki 4. Godwin Aswile 5. Geogre Masatu (Sentahafu bora kabisa) 6. Hussein Marsha (Kiungo bora kabisa ktk historia ya Tanzania)7. Geogre Lucas/ Abdul Ramadhan Mashine 8. Ramadhan Lenny 9. Edward Chumila "Edo Boy" 10. Malota Soma "Ball Jugler" 11. Thomas Kipese "Uncle Thom".
    Msimu huu Dua bin Said alikuwa hajasajiliwa kucheza mechi za kimataifa ila wadau wa Yanga wanamkumbuka vema. ASA walipokea goli tatu kwa moja, la kwanza likifungwa na "Ball Jugler" la pili likiwa la kujifunga na la tatu likipigwa na striker hatari kabisa "Edo Boy"

    Japokuwa ankal Michuzi wewe ni Yanga damu naomba basi ututafutie picha ya hiki kikosi ukiweke hapa kwenye bulogi yetu ya jamii.

    ReplyDelete
  10. Ujue kwamba siku hizi kuna technolojia mpya unaweza kwenda kwenye website km Facebook kuwatafuta na ukawapata, tumia technologia za siku hizi ndugu

    ReplyDelete
  11. umetaka maoni tumekupa maoni umeyachunia its either you or your subordinates,
    1. Unazeeka 2. wazembe mbona unakuwa hivyo au per diem ya campaign

    ReplyDelete
  12. Waliosimama from L-R ni Deo Mshigeni yupo Marekani,Mike Mhagama yupo Marekani,Monica Mfumia yupo UK, Flora Nducha yupo UN- Swahili Radio, Vicky Msina yupo Benki Kuu ya Tanzania ( BoT), Abou Liongo Yupo DW - German, Lilian Mbaga mke wa Taji,Sunday Shomari yupo VOA- USA, Taji liunsi wa TBC na waliokaa from L-R ni Charles Hillary wa BBC- London, Mikidad Mahmud wa Radio Uhuru, Mike Ross --/? Na Julius Nyaisanga hiyo picha ni ya mwaka 1997 au 98 hao jamaa walikuwa nyota wanavipaji si mchezo , sauti za vicky msina na florah ni bomba ile mbaya nawamiss sana hawa watu.

    ReplyDelete
  13. Watu wangine bwana wanaulizwa vitu vingine lkn wanajitungia maswali ya na majibu tofauti kabisa. We umeambiwa utaje hao ni kina na wako wapi na wala sio umri wao wala ripoti za nn sijui. Haya mkifeli mitihani mashuleni mnalalamikia elimu ya tz ni duni au hamujui Kiingreza kha

    ReplyDelete
  14. Sasa, kwani kuzeeka dhambi? Mijitu mingine bana! Kuzeeka ni Tunu na kunawafika wale tu wajaliwao Ndugu, si woote! Pole weeh!

    ReplyDelete
  15. VICKY MSINA YUKO BOT HQ NI PUBLIC RELATION OFFICER PALE OFISI YA GAVANA! YUKO VIZURI ILE MBAYA!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...