Meneja Udhamini na Matukio wa Vodacom Tanzania Rukia Mtingwa akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wakati wa kutangaza njia(route)zitakazotumika wakati wa mbio za Vodacom Mwanza Cycle challenge zitakazotimua vumbi tarehe 12 na 13 jijini mwanza.Mwenyekiti wa kamati ya ufundi Taifa Godfrey Jax Mhagama(kushoto)akitangaza njia(route)zitakazotumika kwenye mbio za baiskeli za Vodacom Mwanza Cycle Challenge.(katikati) Meneja mauzo wa Pepsi Gastor Leo, na Meneja utawala wa knight support Loishiye Teveli.

Vodacom Tanzania ambao ni waandaaji wa Vodacom Mwanza Cycle Challenge wametangaza njia(route) zitakazotumika kwenye mashindano ya baiskeli ambayo yatafanyika Jijini Mwanza tarehe 12 na 13 mwezi huu yanayotarajiwa kugharimu zaidi ya shilingi milioni 50.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Jijini Mwanza leo, katika ofisi ya Vodacom kanda ya ziwa Meneja Udhamini na Matukio wa Vodacom Tanzania, Mwenye Rukia Mtingwa alisema kwamba mashindano ya mwaka huu yameboreshwa zaidi na kuwaomba waendesha baiskeli kujitokeza kwa wingi na kuwaomba wawe makini na utumiaji wa njia(route)ili waweze kupata ushindi wa halali na wenye manufaa kwao na wapenzi wa mchezo huu,alisema.

Nae Mwenyekiti wa Kamati ya ufundi Taifa Godfrey Jax Mhagama alizitaja njia(route)hizo alisema mbio za walemavu wanawake ambazo ni za kilometa 10 zitaanzia kiwanda cha soda cha Pepsi cha jijini Mwanza (SBC Company) na watageuzia eneo la Nyamangoro lililo umbali wa kilometa 5 toka Pepsi jirani na kituo cha kurushia matangazo cha Radio Free Africa (RFA) ambako kutakuwa na alama ya WWK:5KM.

Mhagama alisema kwa mbio hizo za walemavu wanawake hakutakuwa na kituo cha kuchukulia matunda na maji na badala yake yatawekwa kwenye baiskeli zao katika eneo watakaloanzia mbio hizo.

Aidha kwa upande wa mbio za kilometa 16 zitakazowashirikisha walemavu wanaume pia zitaanzia kiwanda cha soda cha Pepsi cha jijini humo (SBC Company) na watageuza baada ya kilometa 8 katika eneo la Kisesa karibu na mashine ya mchele ya Ndakila. (Ndakila Rice Mills) kutakapowekwa alama ya WWM: 8KM.

Hata hivyo eneo la kugeuzia limeongezwa kwa sababu ndani ya kilometa 7.5 linaangukia kwenye kona, kwa sababu za kiusalama na kiufundi imeonekana haitakuwa vizuri kuliacha eneo hilo likatumika kama ilivyokusudiwa. Hivyo basi njia hiyo itakuwa ya kilomita 16.

Kwa upande wa mbio za kilometa 80 kwa wanawake zitaanzia eneo la Nata na kuendelea kuelekea Bihayabyaga umbali wa kilometa 25 kutakapokuwa na alama inayoashiria mbio kufikia kilometa 25. Vilevile baada ya umbali wa kilometa 39 kutakuwa na kituo cha maji na matunda na zitageuzia eneo la Rugeya kutakapowekwa alama inayosomeka WWK 40KM.

Wakati wa kurudi alama za kuonesha kilometa zilizobaki kufikia kumaliza mbio zitawekwa ambapo bango la bado kilomita 20 litawekwa eneo la Sangito. Kuendelea hadi kufikia eneo la Nata kutawekwa tena bango linaloashiria bado kilometa 1 kwa washiriki kumaliza kufikia eneo la Bugando kutakapokuwa na kituo cha kupokelea washindi hao wa mbio hizo za wanawake.

“Mwenyekiti huyo wa kamati ya ufundi Taifa alisema kwa upande wa mbio za kilometa 196 wanaume zitaanzia eneo la Nata, kuelekea Bihayabyaga umbali wa kilometa 25, kupitia Bundilya zitakapofikia kilometa 50 ambako kutakuwa na kituo cha kwanza kwa washiriki kujipatia maji na matunda.

Baadae Mhagama alisema zitaendelea hadi eneo Kisamba/Magu umbali wa kilometa 70 kutoka Nata kutakapokuwa na kituo namba mbili cha vinywaji na matunda ambako pia bango la kuonesha umbali litawekwa na zitageuzia/kurudia eneo la Nyashimo kutakapokuwa na alama ya 97.5KM kuonesha eneo la kurudia.

Vilevile njiani zitawekwa alama zinazoonesha umbali uliobaki kumaliza mbio hususani katika eneo la Kisamba umbali wa kilometa 70 kutoka Nyashimbo kutakapokuwa na kituo cha tatu cha maji na matunda, aidha kituo cha nne kitakuwa eneo la Bundilya kilomita 50 kabla ya mbio kumalizika.

Vilevile aliongeza kuwa kituo cha tano kitakuwa eneo la Sangijo umbali wa kilometa 20 kabla ya mbio kumalizika wakati eneo la Nata kutawekwa bango litakalokuwa likionesha kwamba bado kilomita 1 tu mbio hizo kumalizika kwenye kituo chake cha mwisho ambacho ni Bugando na kufanya mbio kuwa za kilometa 196.

Aliyataja maeneo ya tahadhari kwa wakimbiaji kuwa ni Mabatini, Igoma na Kituo cha basi cha Buzuruga kutokana na hali yake ya kuwa na idadi kubwa ya watu na baiskeli kukatisha barabara katika maeneo hayo,Pia mashindano haya yamedhaminiwa na Alphatel, Knight support,SBC kupitia kinywaji chake cha Pepsi.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. issamichuzi mimi ni mpenzi sana ya glob yako asante kwa kazi nzuri ya kutuhabarisha yanayoendelea ubarikiwe sana mimi niko nje ya mada kidogo japo usiache kurusha wachangiaji wanijuze pls ninaswali moja ambayo inanisumbua kidogo ktk maandiko iwe ya kikristo au ya kiislamu maandiko yanasemaje kwa ndoa au wapenzi uapokuta mwanamke amemzidi mbwana au mpenzi nakama kuna anayejua mstari anijuze pls mimi ni mkikristo ni hayo tu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...