Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mh. Lazaro Nyalandu akikata utepe kuzindua moja ya ndege mbili za Bold Air leo katika uwanja wa ndeeg wa Julius Nyerere jijini Dar. Kulia ni mmiliki wa kampuni hiyo Bw. John Ndunguru, Mtanzania anayeishi Marekani ambaye kaja kuwekeza nyumbani
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara,
Mh. Lazaro Nyalandu akitesti ndege hiyo
Mh. Nyalandu akishuka. Chini akiongea na waandishi

Watanzania wametakiwa kuacha kuogopa usafiri wa ndege kw akuwa zaidi ya jkuwa wa haraka lakini ni salama kuliko usafiri wa aina nyingine.

Akizindua Kampuni ya Ndege ya Bold Air leo, Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mh. Lazaro Nyalandu alisema wakati wa sasa usafiri huo inatakiwa uwe wa kila mtu na si anasa kama watu wengi wanavyodhani.

"Kuna watu wanaogopa ndege; yaani kuna baadhi ya waheshimiwa watatukiwa Dodoma ukimwambia kuna ndege atakwambia 'Hapana ntadrive tutakutana Dar'

Bold Air ni kampuni inayomilikiwa na kijana wa kitanzania aishie Marekani, John Nduguru ambaye ameanza kwa ndege mbili ambazo zitakuwa zikienda sehemu mbalimbali nchini.

Mh. Nyalandu aliwataka watanzania zaidi walioko nje ya nchi kuwekeza katika sekta mbalimbali nchini ili kuleta ajira kwa watanzania na kuinua uchumi wa nchi.

Alisema serikali imeweka mazingira mazuri na taarifa nzuri kupitia kituo cha Uwekezaji (TIC) lakini wengi wamekuwa hawafuatilii na kuendelea kulaumu nchi haina mazingira mazuri kwa wawekezaji wazawa.

"TIC si kwa ajili ya wageni tu bali wawekezaji wa aina zote wanahudumiwa<>

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 30 mpaka sasa

  1. Sio kama tunaogopa fare ikiwa poa tutapanda

    ReplyDelete
  2. wow. This is amazing. I would like to hear from other Tanzanians who are living in foreign countries to comment about this and have to tell us what about them? This is a pilot example for sure.

    Big up Ndunguru.Keep it up.

    ReplyDelete
  3. hatuogopi kupanda ndege ila ni gali mno, kwenda moshi dola 200, wakati basi ni elfu 30 wapi na wapi! ebo! mutapanda wenyewe lol

    ReplyDelete
  4. Hongera sana Shirima wa Precision alianza hivyo hivyo na kindege kidogo sasa ni milionea.

    Basi na uhakikishe kuwa hizo ndege zina Comprehensive Insurance sio tena mambo ya third party policy na premium iwe imelipiwe kabisa. Pia ziwe air worth.
    Alexbura, Dar

    ReplyDelete
  5. Waziri does not get it....si kwamba tunaogopa, hatuna uwezo. Nauli ya basi inatushinda...itakuwa ndege?

    ReplyDelete
  6. Hongera kaka. Ni hatua kubwa na wazo zuri. Wengine tunaogopa kuwekeza huko kutokana na rushwa iliyokithiri. Kuna wakati nilituma gari huko, pale bandarini jamaa zangu waliolipokea walizungushwa mno, wakalipishwa ushuru usio halali, pamoja na kutoa rushwa. Sasa ndugu waziri, tutaweza vipi kuendelea wakati watu walioajiriwa pale TRA ndio kikwazo? Kwa maana nyingine, adui wa kuwekeza huku kwa sisi tulio U.S. au popote pale, ni TRA pale bandarini. Waziri husika asafishe hii TRA ili tuwe na imani.

    ReplyDelete
  7. Waziri Nyalandu- tunataka kuwekeza sana lakini adui yetu ni bandarini- tukituma magari yetu au vifaa vyetu vinachargiwa ghali kuliko bei tuliyonunulia...hakuna mahali kwenye rusha kama bandarini na Brela( waandikaji wa makampuni) hebu paangalia hapo.
    Mdau

    Uk

    ReplyDelete
  8. Ndunguru huyu ni APEX Iringa au Mwakaleli Sec.

    ReplyDelete
  9. Reply to Anonymous 6:13
    You sound educated, but yet enough. Not all Tanzanians living abroad are required to invest or have businesses abroad or Tanzania. What if most people are happily satisfied with just regular jobs just like the majority of workers in Tanzania?? Do not let your mentality judge your character my friend, better yet; do not let your desires speak for others, better yet; do not just type just because you have fingers and a computer!

    My hope is that all planes passes all the security measures and be checked with people who qualify which is not typical in Tanzania, hence Precision and ATC. Does Tanzania have standard requirement for inspection of commercial air crafts? I am talking about people’s lives here.

    If the proper inspection was not performed, I hope you’ll do the right thing Mr Ndunguru. Make sure it’s done and set an example.

    If all this was conducted and approved, I would like to congratulate and wish you success on you business.

    ReplyDelete
  10. Mimi nataka basi hiyo wizara iweke form za maombi ya vitu vingi online...Tuko huku mbali kwa mtaji wa kubeba box kila kitu mpaka nikachukue form huko? Tuwekeeni easy way ya kuanzisha legal business nyumbani kwa kutumia mitanao...Final detail na process ndio mtu aje kumalizia nyumbani.....Hii nenda rudi nenda rudi si tutamaliza mtaji kwa kutumia nauli...

    Tunakatishwa tamaa saana na mambo madogo madogo ambayo yangeweza kumalizwa online mtu mpaka aende huko offisini. na ukienda unaambiwa boss katoka..Sijui ni rushwa inatakiwa hata kupata form na maelekezo? Kwanini form nyingi msiziweke online tukaapply na kuprocess online....

    Mkitaka tuwekeze honesty kwanza
    1. Msafishe bandarini
    2. Wafanayakzi wenu wapewe elimu ya kuelewa (wafanyakazi wengi hawajui kweli nini wanachofanya) Ukienda kutafuta kitu utasumbuliwa, nenda huku rudi huku huo muda nani anao...

    Mimi niligive up kabla hata sijaanza....Likizo yangu iliisha bila kupata information zozote za maana nilizokua nataka...Kila siku nenda huku nenda kule...Kuwekeza tunaweza sana huku twaishi kwa credit ...with good credit tunaweza leta ndege nyingi sana tu lakini hayo maudhi ya kusumbua watu bila sababu yataisha lini?

    Na pia mkumbuke kuwa mtu akiwa anaanza kuwekeza sio kuwa ni millionea tayari sasa mkianza kumchmoa hata kabla ya kupata faida not good my dear

    ReplyDelete
  11. HUYU NDO YULE NDUNGURU ATUPAYE SCHEDULLE HAPA DC...AU MWINGINE...SAFI SANA MTU WANGU..UNATULINDA HATA HAPA AMERICA PIA KWA KUTUWEZESHA KUTUPATIA VIBABU NA VIBIBI VYA KUVIHUDIMIA

    ReplyDelete
  12. This is what I'm talking about. Wakati Wamarekani wanalalamika uchumi mmbaya 'The worst econimic impact since the great depression'. Mtanzania anadondosha ndege nyumbani,safi sana, Keep it up man, We are behind you Bro.
    Nyalandu clean the corruption and I promiss to drop six new planes next year from the great state of Texas.

    ReplyDelete
  13. We anonymous wa 11:46 pm. Sijui wewe huko nchi ipi. Lakini kwa hapa U.S., hata uwe na excellent credit history, huwezi kupeleka chochote nje ya nchi kama bado una ki finance(gari au ndege). Bank au financial institution iliyokupa loan inashikilia title(lien holder) mpaka hapo utakapomaliza malipo(pay off). Kwa hiyo huwezi peleka gari au ndege au piki piki nje ya U.S. kama bado hujamaliza malipo ya mkopo hata kama pale bandarini wameacha kula rushwa.

    ReplyDelete
  14. US Blogger na Mashaka munaona mambo haya?

    ReplyDelete
  15. To anonymous of 10:46 pm. I don't know if it was a typing error or not. But in english grammar, there is no such a word like "aircrafts". To be correct, you should have said "aircraft" because the word aircraft doesn't have a plural form, just like the word "milk". There's no such a thing like "milks".

    ReplyDelete
  16. SASA WABONGO TUSIJARIBU CHAKACHUA MAFUTA YA NDEGE PALE DEMAND YAKE INAPOANZA KUONGEZEKA. TUTAWAFUKUZA WATU WENYE NIA NJEMA...

    ReplyDelete
  17. wenzetu wanaongelea airbus a380 sisi ndio kwanza waziri mzima anazindua hako kammbu!!!! we have a long way to go...

    ReplyDelete
  18. Nauli ya kwenda Bukoba na kurudi dar ni Laki 6 mtu mmoja. Watanzania wangapi tua uwezo huo.Basi kwenda na kurudi ni Laki 1.Hatuogopi ndege ni uwezo nauli za ndege ziko juu mhe.

    ReplyDelete
  19. na mwingine anazungumzia english grammar.
    yale yale...

    ReplyDelete
  20. We Thomas uliyeongelea Airbus nina uhakika ukipimwa lazima utakutwa kama siyo na minyoo basi na kifaduro, hovyoooo!!

    ReplyDelete
  21. we uliyezungumzia grammar umechemsha ,hapa si mahali pake kabisa.Mbona watukuza sana kizungu!!!!mada hapa ni mwenzetu kuwekeza,na matatizo yanayo wapata n a kuwakatisha tamaa wawekezaji.Siyo kizungu.kama unajua kuzungu njoo ufungue shule tutaleta watoto wetu,lakini siyo hapa.

    ReplyDelete
  22. Du wabongo nuksiiiii.nimecheka mpaka mbavu nazikanda yaani hauna shukrani jamaa moyo umemuuma hadi anakaita ka MBU.hizo ndo roho mbaya tulizojaliwa sisis wabongo ndo maana hatuendi popote.

    ReplyDelete
  23. wewe annoy wa hapo chini ndio una minyoo na kifaduro inaelekea hata airbus a 380 huijui, mimi nilikuwa namaanisha kwamba wakati wenzetu wanakimbia sisi ndio kwanza tunatambaa baada ya kutembea!!!! sasa huelewi nini?

    ReplyDelete
  24. Piga schedule ya box, and then save.
    Boksi halimtupi mtu!!

    ReplyDelete
  25. HATA DR REMMY ALIWAHI KUWEKA MANENO KWENYE GARI LAKE KUWA" BABA YAKO ANALO"

    ReplyDelete
  26. mwenzenu mnamuana mjinga...hapo lazima kuna niche market yake.. simjinga kupeleka ndge ndogo kama hizo. na naamini hatotegema abiria wa kitanzania walio ndani ya bongo. na uhakika asilimia 90%.

    ReplyDelete
  27. Tanzania inashindwaje kuweka utaratibu wakusajili makampuni online?
    Mbona Rwanda wameweza? Kama kusajili kampuni Tanzania ni shida pamoja nakupa vibali TIC kuna longolongo kwanini tusifungue makampuni Delaware, Uk, Bahama na sehemu nyingine ambapo ni ndani ya masaa 3 umepata kampuni na certificate yako -tena popote ulipo duniani.

    Watanzania wekezeni popote, msisahau uli usemi wa Chuma ulete.. kwa kuchuma ni popote.

    Mkifungua milango Tanzania tutawekeza pia, fedha inatafutwa popote!
    Hongera mdau kwa kufanikiwa kuwekeza Tanzania.

    Mdau,

    Norway

    ReplyDelete
  28. Anony wa kukosoa English za watu Wed Dec 08, 03:05:00 AM

    It is sad to see that the only thing that interested you is English grammar. Shame shame shame.

    Ndunguru mwanzo mzuri sana kaka, ila namuunga mkono Anony wa 10:46, Safety Safety Safety comes first. Hata kama we mwenyewe unania na kutenga fungu la ukaguzi wa ndege kila inapohitajika, watanzania watu wa ajabu sana, pesa kwanza then maisha ya mtu second. Angalia Tanesco mpaka leo tabu. Nna wasi na usimamizi haswa kama we mwenyewe unarudi kula bata USA!

    Ni hayo tu!

    ReplyDelete
  29. mhhh watanzania kwa kuchakachua ndio wenyewe, ikiwa waliweza kuchakachua mafuta yaliyowekwa kwenye magari ya msafara wa rais iweje washindwe kuchakachua mafuta ya ndege? mmiliki wa ndege hiyo jihadhari, wakichakachua huko angani hakutakalika!! akha mwee mimi sipandi ndege za tanzania afadhali nipande afghanistan airline au air somalia ahahahaaa!!!!

    ReplyDelete
  30. Wewe unayezungumzia bank kuhold tittles sijui USA amka ndugu yangu watu tumenunue nyumba nje ya nchi kwa mkopo wa marekani...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...