Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dk. Mohamed Gharib Bilal akiangalia simu yake baada ya kutumiwa ujumbe unaomkaribisha katika Jamhuri ya Kenya, wakati alipotembelea kwenye Mpaka wa Tanzania na Kenya uliopo katika Hifadhi ya Taifa ya Mbuga za Wanyama kati ya Serengeti na Loliondo leo. kulia Mama Zakia Bilal, kulia Mama Aisha Bilal.
Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mbuga za Wanyama ya Serengeti Bw. Mtango G.G. Mtahiko, akimuonesha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dk. Mohamed Gharib Bilal, Mpaka wa Tanzania na Kenya wakati Makamu wa Rais alipotembelea eneo hilo liliopo kwenye Hifadhi ya Taifa ya Mbuga za Wanyama kati ya Serengeti na Loliondo leo. kulia Mama Aisha Bilal, kushoto Mama Zakia Bilal.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Mohamed Gharib Bilal wa pili kushoto na Familia yake wakiangalia Mamba na Viboko, walipotembelea moja ya Mito iliyomo kwenye Hifadhi ya Taifa ya Mbuga za Wanyama Serengeti leo. Makamu wa Rais yupo Serengeti kwa mapumziko mafupi.picha na Amour Nassor - VPO.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Kumbe ana wake waili? safi sana dini inaruhusu hongereni kwa kuwa watalii wa ndani mfano bora,

    ReplyDelete
  2. Sio dini tu hata Uafrika unaruhusu.Mimi ni mkristo lakini sioni ubaya na dhambi ya kuwa na wake wawili.Tangu enzi za enzi Waafrika walikuwa wanaowa kati ya mke mmoja au zaidi as long as una uwezo wa kuhudumia.Haya mambo ya kuowa mke mmoja ni ya western ambao hata wenyewe wanayapiga chenga kwa kuwa na vimada nje.

    ReplyDelete
  3. Sioni ubaya uko wapi wa kuwa na wake wawili.Mimi ni mwanamke na nasapoti suala hili kwani tupo wengi duniani kama hatukuolewa wawili wawili wengine watakosa nafasi ya kuolewa na puta nafasi ya kupa watoto.Jee upo tayari kumuona dada yako au mtoto wako wa kike anakuletea ujauzito bila ya kuolewa?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...