Rais wa Miss Utalii Tanzania, Gideon Chipungahelo akifafanua jambo kwa washiriki wa Miss Utalii Tanzania 2010-11 wakati walipotembelea mradi wa chumvi wa Nunge,uliopo Bagamoyo Mkoani Pwani leo.
Baadhi ya Washiriki Miss Tourism wakiwekachumvi katika vifurushi, Nunge Bagamoyo Pwani,Wakati wa ziara ya Washiriki hao walipotembelea mradi wa chumvi wa Nunge,Bagamoyo Mkoani Pwani leo.
Washiriki Miss Tourism wakitazama jinsi chumvi inavyopakiwa katika vifurushi, Nunge Bagamoyo Pwani,Wakati wa ziara yao leo.
Washiriki Miss Tanapa -Tourisim Tanzania 2010-11 katika picha ya pamoja.

Warembo wa Tanapa-Miss Utalii Tanzania 2011, jana walitembelea maeneo mbalimbali ya vivutio vya Utalii ikiwa ni katika mchakato wa kujifunza masuala mbalimbali yanayohusian na Utalii wa Ndani wa Tanzania, katika mkoa wa Pwani Bagamoyo.

Katika matembezi hayo warembo waliweza kujifunza namna Uzalishwaji wa Chumvi unavyotengenezwa kutokana na mabwawa ya maji kutoka bahari ya Hindi(Maji chumvi).

Akizungumzia Mradi huo wa Chumvi, Meneja wa Mradi, Nicolaus Meliha, alisema kuwa Chumvi hiyo inatengenezwa kutokana na mabwawa yatokanayo na maji chumvi yanayopatikana kutoka bahari ya Hindi.

“kiujumla mradi wetu huu ndiyo unaozalisha chumvi nyingi hapa nchini pamoja na kwamba pia zipo sehemu zingine kama Mikoa ya Lindi na Zanziba, lakini hapa kwetu chumvi zaidi ya tani mia kwa wiki huku soko la ajira kwa wakazi wa mkoa wakiendelea kunufaika na mradi huu, ila kwenu washiriki wa shindano hili mkiwa kama mabarozi mnapaswa kuutangaza kama moja ya kivutio cha Utalii kutokana na kwamba upo maeneo ya kale ya kihistoria”alisema Meliha

Na kuongeza kwamba hadi chumvi inapatikana inatokana na kukaushwa kwa maji chumvi yatokanayo na maji ya bahari ya hindi, ikiwa ni baada ya kukaa eneo moja lisilorusu maji kutoka na pia inategemeana sana na jua ili maji kukauka ba baada ya hapo chumvi upatikana.

Fainali za mwaka huu zitarushwa moja kwa moja (live) na kituo bora kabisa cha runinga StarTV cha jijini Mwanza. Zitafanyika Februari 5, 2011 ambapo wasichana zaidi ya arobaini watakuwa wakimsaka mmoja anayestahili kuvikwa taji la umalkia wa taifa wa Utalii nchini ambaye pamoja na kuwa balozi wa kimataifa wa utalii wetu pia atapata mkataba wenye thamani ya shilingi milioni mia moja na hamsini.

Kambi ya warembo hawa iliyopo hoteli ya Kiromo View Resort, imekuwa gumzo kubwa la jiji la Dar sasa kutokana na ukweli kuwa, utulivu, umakini na madhari ya hoteli hii vimekuwa kielelezo tosha cha kufanya ushindani uwe mkubwa miongoni mwa washiriki ambapo pia watawania tuzo (awards) zingine zaidi ya ishirini na nane zitakazowawezesha kushiriki mashindano mengine ya kimataifa na kuwakilisha mikoa au maeneo yao vema.

Kauli mbiu ya mashindano ya Miss Utalii mwaka huu ni “Ewe Mtanzania tembelea na tangaza hifadhi za taifa, utalii ni maisha na utamaduni uhai” ambayo kimsingi ndicho kielelezo yakini cha shindano kikilenga kuhamasisha utalii wa ndani miongoni mwa Watanzania ambaio wengi wao hawajui kabisa maana vivutio vya kitalii na kitamaduni vilivyopo nchini.

Hoteli ya Kiromo ambako Shindano hili litafanyika ni ya kitalii na yenye hadhi ya nyota tatu na iko umbali wa kilometa kumi tu toka mjini Bagamoyo. Kadhalika, inatoa Huduma zote za kisasa kwa umakini na ustadi mkubwa.

Aidha, wadhamini wakuu wa shindano ni Kiromo View Resort na Sahara Media Group inayomiliki kituo cha runinga cha StarTV, Radio Free Africa, Kiss FM na gazeti la Msanii Afrika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. ...jamani watoto wazuri hivi kwa nini mnataka kuwachubua ngozi na machumvi yenu jamani!haya ni maua muumba ametupa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...