Habari Ankal,
Napenda kuwatangazia wadau wote na wananchi kwa ujumla kuwa mswada kwa ajili ya mabadiliko ya katiba sasa unapatikana kwenye tovuti ya Bunge ambayo ni www.parliament.go.tz.

wadau wanaweza kudownload mswada husika kwa kufuata link http://www.parliament.go.tz/bunge/docs/constituentreview.pdf na pia wanaweza kuchangia kwa kutoa maoni yao kuhusu muswada kwa kubofya mahali palipoandikwa "contribute" Wote wanakaribishwa kutoa maoni kwa lengo la kuboresha muswada husika.

Na
Mdau Owen Mwandumbya wa Bunge

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. MwananchiMay 04, 2011

    Bunge andaeni bandwidth ya kutosha sio wananchi tunafurika kwenye hiyo website inaanza kuleta kwikwi.

    Naamini bandwidth mnayotumia kila siku itachemsha, hivyo fanyeni mpango wa kupanua bandwidth kwa kipindi chote cha kupokea maoni ya katiba.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 04, 2011

    Mimi naomba kuuliza hivi lugha yetu ya taifa ni kingereza? Najua watu wengi hawatashiriki TZ kwa ajili ya lugha iliyotumika. Halafu madhumuni na sababu ndio wanaandika kwa kiswahili na kiingerezza. kwanini msitafsiri yote kwa kiswahili na kingereza au hiyo ya juu ni just copy and paste.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...