Kaka michuzi naomba jamani msaada
Hivi hawa jamaa zetu wa usalama barabarani hapa TIOT Tabata hawapaoni jamani?
Juzi tu lori limesababisha ajali ya mpendwa wetu na kuchukua uhai wake.

Jamani leo asubuhi nimepita nikitoka Ubungo, haya malori jamani yamepaki kwenye njia iendayo Buguruni bila kiashiria chochote, mi sijui tatizo ni nini kwanini wasipaki jamani hata kwenye Service Road jamani, watatuulia wapendwa wetu mpaka lini?

Yaani ni jambo la kusikitisha sana na ni hatari kwa njia hii sana hasa hapa kuingia Ofisi za hii kampuni wanaita sijui AMI.

Tusaidieni jamani tunakufaaaaaaaaaa! Askari wa pikipiki acheni tu kushika jamaa ambao hawavai kofia ngumu piteni na hapa TIOT saa za jioni na usiku jamani.

Mdau Tabata

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Viwanja vya wazi vingesaidia kumaliza tatizo la malori lakini ndio hivyo tena wakubwa wenu chini ya cc? wameamua kuviuza na kula pesa na hakuna hatua yoyote tuliikia ya kuvirejesha. Malori yataendelea kupaki barabarani kwani hawana mahali pengine pa kupaki. Bongo tambarare kabisa.

    ReplyDelete
  2. BWANA MAGRI HAYO HASA MAROLI HAYAFUATI SHERIA POPOTE PALE LINA SIMAMA NA WAO MADEREVA HAWAPISHI MARANYINGI WANACHUKUA ROBO TATU YA BARABARA NDIYO MAANA MAROLI YANASABABISHA AJARI DAWA BWANA NYIE LAKUFANYA NIWAKIEGESHA TU SEHEMU ISIYO TAKIWA NIKUYATIA MOTO KIMYA KIMYA

    ReplyDelete
  3. Ndugu nakushukuru sana kwa kuliweka hili suala humu, mimi huwa linanikera na wala sijui nisemee wapi ili wahusika wanisikie na kurekebisha hii hali. Ni juzi juzi tu malori ya sehemu hiyo yamemuua aliyekuwa mwandishi hayati Mwakitereko na kama pakiendelea hivyo ni kwamba patapoteza maisha ya wengi.
    Mbali ya kupaki pembeni ya barabara bila alama, pia wakati yanakata kona kutokea njia ya buguruni kuingia hapo AMI, mida ya usiku lori halionekani sababu linakupa ubavu ambao hauna hata taa kwaiyo ni rahisi mtu kulivaa... Mungu atusaidie jamani. Natamani niwashauri wahusika wawape amri kuwa kupaki pale mwisho saa 12 jioni na hata magari mapya yasiingie pale zaidi ya muda huo becoz giza likishaingia ndo inakuwa mbaya sababu huoni mbali unalishtukia tu kwa ghafla na ni hatari sana. Tujaribu kulipigia kelele hili hadi wahusika walifanyie kazi.
    Ipyana

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...