Habari kutoka ukweni Kampala, Uganda, zinatahanabisha kwamba mwanamuziki maarufu wa Uganda, Jose Chameleon, amesilimu dini kutoka ukristo wa madhehebu ya Kikatoliki na kuwa Mwislamu katika hafla iliyofanyika leo mchana msikiti wa Kibuli jijini Kampala. Mwanamuziki huyo (pichani juu kushoto baada ya kutiwa maji wakati wa Swala ya Ijumaa) sasa amebadili jina na kujiita Gaddafi Chameleon, kwa mujibu wa gazeti la udaku la nchini humo la Red Pepper.
Kwa picha zaidi na stori kamili

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 24 mpaka sasa

  1. Mashallah mwenyezi mungu akujaalie imani na kuwa mfano mzuri kwa wengine.Alhamdulillah

    ReplyDelete
  2. Wahuu Mabrouq Ghadaffi Chameleon!Insha'Allah Mwenyezi Mungu akuongoze kama alivyokuongoa bado uko kijana famous ukaikubali Dini ya Haki kiwazi wazi!Endelea kuwasaidia kina Jamillah watulie katila Ndoa zao!Ramadhan Maqbour
    Ahlam UU!!!!

    ReplyDelete
  3. Takbir!!!

    Ndiyo nusura imekuja na watu wanaiingia dini ya kweli.

    Vitu vya kutarajia ni kwamba watu hawatakukubali na utaona kuwa utapoteza marafiki na wateja, hii imekuwepo tangu kwa akina Nuhu hadi kwa Muhammad (SAW).

    ReplyDelete
  4. Kwani Gaddaffi ndiye muislamu safi?

    ReplyDelete
  5. kijana kachanganyikiwa,mambo ya yaliyomkuta michael jackson,jamani dini ni kumwamini mwenyezi mungu,sio tu ukristo tu au uislaam

    ReplyDelete
  6. "Chameleon!!!!!" Sifa za kinyonga ni???????????????????????

    ReplyDelete
  7. Kubadili dini sawa, jina tu ndilo limenikwaza! Tuseme amekuwa muislam au amekuwa Gaddafi? Kinachomvutia ni dini au personality ya Gaddafi? Nampongeza ila namnasihi ashike dini yake mpya aachane na mambo ya Gaddafi!

    ReplyDelete
  8. Hata hilo jina poa tu, mbona kuna wakristo wamejiita Winston Churchill, William Wilberforce, Bill Clinton etc? Namkumbuka mchezaji maarufu wa Kenya miaka ya 1980's akiitwa Wilberforce Mulamba. Na nilishaona watu wanabatiza watoto wao kanisani kwa majina ya Diana, Madonna, Tyson na mengine. Ndiyo ulimbukeni uliotupata waafrika.

    ReplyDelete
  9. ....Celebrate the praises of your Lord
    and pray for His forgiveness:for He is
    Oft-Returning(in grace and mercy)

    Quraan 110

    Check it out
    Wakatabahu

    ReplyDelete
  10. Uyu kweli ni msanii! Masheikh na walimu wa dini mnisaidie Quaran inasemaje kuhusu mwanaume kusuka nywele?

    ReplyDelete
  11. Karibu sana katika dini yenye kumwamini na kumwabudu Mungu mmoja tu Aliyeumba kila kitu na mwenye uwezo juu ya kila kitu.

    ReplyDelete
  12. safi chamelion kwa kujua wajibu na kuingia din ya ukweli....nyie mnahoji why kajiita gaddafi ni jina tu hilo mboan nyie mnajiita bill cliton au william acheni ulimbukeni nyie
    MDAU NORWAY

    ReplyDelete
  13. MIMI PIA NAUPENDA UISILAMU TATIZO NAOGOPA FAMILIA NA JAMII KARIBU YA MIMI ITANITENGA NINFANYEJE WADAU MSAADA KWENYE TUTA

    ReplyDelete
  14. dini za uongo ni zipi? toeni kashfa zenu mpeni hongera zake ati dini ya ukweli, ni binadamu gani alienda mbinguni kuongea na Mungu ni dini ipi iko sahihi?

    ReplyDelete
  15. Karibu ktk uislamu ila tu hatutaki hizo rasta zako,uende ukanyoe haraka,uislamu hauruhusu kusuka rasta kamwe.Usipotoa tutakusilimisha kwa lazima.

    ReplyDelete
  16. Islam is defined around the Holy Quraan and teachings and examples of what the Prophet did and said. Hivyo basi nawaomba hao wanaokerewa na usukaji wa nywele wanipe aya na sura inayokataza kusuka nywele.Waswahili wasema ni kipenda roho kama vile kusuka au kunyoa,mie ningesuka nywele mzee wangu angenicheka tu na pengine angeniambia...you look like Asha.

    ReplyDelete
  17. JAMANI KWANZA TUMPONGEZE KWA HATUA KUBWA ALIYOICHUKUA NA SIO KUHUSU JINA AU KUSUKA NYWELE HAYO YATAKUJA BAADAE KILA ATAKAPO JIFUNZA DINI NA MAAMRISHO YAKE.KUNA WAISILAMU WANGAPI WANAOSUKA NYWELE NA HATA KUFUNGA HAWAFUNGI ITAKUWA HUYU AMBAE NDIO KWANZA KAIKUBALI DINI YA HAKI?
    ANOY 13:0214:00
    KAMA UMEIPENDA NA UNAAMINI UISILAMU NDIO DINI YA HAKI BASI HILO TU NDIO MUHIMU KWANI WAKO WALIO SILIMU NA BAADAE WAKAWASHAWISHI FAMILIA ZAO NA KUWASILIMISHA.KIKUBWA ZAIDI NI KUMUAMINI MUNGU NA KUMUOGOPA MUNGU NA NDIO ITAKUFANYA UWE NA BIDII YA KUWASHAWISHI FAMILIA YAKO NA KUWAELEZA NA KUWAONYESHA HOTUBA ZINAZO ZUNGUMZIA UISILAMU NA DINI TOFAUTI KAMA UPO KTK UKRISTO ZIPO NYINGI AMBAZO ZINAONYESHA TOFAUTI YAKE NA VITABU MBALI MBALI VYA KUJISOMEA MPAKA NA WAO WATAUJUA UKWELI ULIPO.NAKUTAKIA KILA LA KHERI KTK UAMUZI WAKO SAHIHI.

    ReplyDelete
  18. huyo kachanganyikiwa kama zinga mpeni pole soon atatafuta msosi jalalani

    ReplyDelete
  19. MDAU WA NORWAY PLEASE NAOMBA KUKUFAHAMU MAANA NA MIMI NIPO NORWAY NA HUWA NATUMIA MDAU NORWAY NINAPOCOMMENT KWENYE BLOG ZETU HIZI.NITAFUTE KWA NO HII 96724552. UKINICHEKI NA SIMU YA NORWAY HATA KWA MESSAGE TUTAWASILIANA ZAIDI.

    ReplyDelete
  20. very controversial. Religion....? I'm not judging anyone. But how do we know whether we are suppose to stick with our religion.... or just do good to one another and to the world, dont be judgemental that way we can love one another and make the world a better place.

    ReplyDelete
  21. One thing I know God accept you the way you are. Human being looks from the outward(rasta) but God looks us from inside. We are justfied by faith not bye works.
    Nobody is perfect, nobody will ever be in this follen world. Judgement in God's works not ours.
    Thanks.

    ReplyDelete
  22. Nani anajua dini ya ukweli na ya uwongo bwanaa wote tumezaliwa tumekuta dini hizi tukaaminishwa tukafuata baada ya kufika 18 kujua mema na mabaya ndipo tunapoamini na kuona yanayotutokea yanatufariji na imani tulio nayo ndio tunaona ukweli hapo msilete za kuleta hapa na dini ya kweli na uwongo.......Mungu pekee ataahukumu kuchagua nani mkweli wote hapa tunaamini tuu...it's all about what u believe and that's it.

    ReplyDelete
  23. Masha-Allah! Mwanzo mzuri. Hongera sana Jose Chameleon. Mwenyezi Mungu akuongoze daima.

    ReplyDelete
  24. Anonymous hapo juu dini ya Islam imekataza wanaume kujiweka mapambo ya kike,k.m vito vya gold,silver etc, cheni, bracelet vitu kama hivyo vyote ni HARAM.
    Thanx.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...