Meneja wa benki ya CRDB tawi la Bukoba,Emmanuel Chaburuma akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Kagera,Mohamed Babu mfano wa hundi yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 990 iliyoitoa kama mkopo kwa chama cha akiba na mikopo cha Tumaini kilichopo wilayani misenyi kinachoundwa na wakulima wa miwa.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera,Mohamed Babu akimkabidhi mweka hazina wa kikundi cha akiba na mikopo cha Tumaini, Savelina Charles mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi zaidi ya bilioni 990.1 iliyotolewa na benki ya CRDB, mkuu huyo wa mkoa alikabidhi hundi hiyo kwenye viwanja vya maonyesho ya nanenane vilivyoko Kyakaibailabwa.

Na Audax Mutiganzi,Bukoba

BENKI ya CRDB imetoa mkopo wa zaidi ya shilingi zaidi ya milioni 990.1 kwa chama cha akiba na mikopo cha Tumaini chenye wanachama 409 kilichoko wilayani Misenyi kinachojihusisha na kilimo binafsi cha miwa.

Hundi ya mkopo kwa kikundi hicho ilikabidhiwa jana na meneja wa CRDB wa tawi la Bukoba Emmanuel Chaburuma kwa mkuu wa mkoa wa Kagera Mohamed Babu aliyemkabidhi mweka hazina wa Tumaini savelina Charles wakati wa kilele cha maadhimisho ya nanenane yaliyokuwa yanafanyika kwenye viwanja vya Kyakailabwa vilivyoko katika manispaa ya Bukoba.

Akiongea mara baada ya kukabidhi hundi hiyo Chaburuma alisema zaidi ya shilingi milioni 85 zitatumiwa na wana kikundi kupanua mashamba na zaidi ya shilingi milioni 914.1 zitatumika kuendeleza mashamba yaliyopo.

Alisema mkopo huo ni kwa ajili ya kuwasaidia wakulima wa miwa kupata pembejeo na mbegu pamoja mbolea ya kukuzia miwa yao, Chaburuma alisema benki hiyo itakuwa sambamba na wakulima hao na itahakikisha lengo lao la kuchukua mkopo katika taasisi hiyo linafanikiwa.

Chaburuma alivihimiza vikundi vingine vya akiba na mikopo vichangamkie fursa za mikopo zinazotolewa na CRDB ili vipate mitaji ya kuendeleza shughuli ambazo wanachama wanaunda vikundi hivyo za kuwaongezea kipato.

Meneja huyo huyo alisema CRDB inazi fursa nyingi za kuwawezesha wananchi wapaepukana na umaskini wa kipato unaowakabili, alisema CRDB ni benki inayowajali na kuwasikiliza wananchi.

Naye Mkuu wa mkoa wa Kagera aliwataka wananchi wachangamkie fursa zinazolenga kuwaondoa katika wimbi la umasikini, aliwashauri watumie zaidi taasisi za fedha ili waweze kupata mikopo itakayowawezesha kupata mitaji.

Aliishukuru benki ya CRDB kwa jitihada zake inazozifanya za kujali maslahi ya wananchi, aliitaka taasisi hiyo iendelee kufanya hiyo ili wananchi waendelee kujenga imani zaidi na benki hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. kaka...tafadhali rekebisha caption ya picha...inasomeka "bilioni" wakati ni "milioni"

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...