Ajali ya ndege namba 9J-BIO SESINA 206, imetokea leo asubuhi majira ya saa tatu eneo la Nanenane Uyole jijini Mbeya na abiria wanne wanusurika kifo na hakuna aliyefariki.

Abiria walionusurika kifo ni pamoja JVER WAAK Umri wa Miaka 49 ambaye alikuwa Rubani, Raia wa Afrika Kusini, Bwana CHRISTIAN BASIL MMASI umri miaka 30, Ambaye ni Afisa Utawala wa mashamba ya Kapunga wilaya ya Mbarali, Balozi MOHAMMED RAMIA kabula leke ni Mmakua mwenye umri wa miaka 64, mkazi wa Masaki jijini Dar es Salaam ambaye ni mfanyakazi EXPORT TRADING na Bwana SUNNY TAYIR mwenye umri wa miaka 50 ambaye ni Mhindi na ni mfanyakazi wa EXPORT TRADING.

Na chanzo cha ajali hiyo hakijafahamiaka mpaka sasa.

Imetolewa na Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya Bwana ANACLET MALIMBISA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Poleni kwa ajali.. tell us the cause of the accident when u gt to know!

    ReplyDelete
  2. Pole kwa waathirika wa ajali.
    Angalizo:
    9J-BIO ni registration ya ndege na Cessna 206 ndiyo aina ya ndege, kwa uelewa wangu mdogo.

    ReplyDelete
  3. Poleni sana wandugu, M/mungu atawaokoa sikuzote 'Amin'

    ReplyDelete
  4. michuzi aina ya ndege ni CESSNA, model 206 na namba za usajili ni 9J-BIO, ikiwa na utambulisho kwamba 9J ni Zambia na BIO ndio namba ya hiyo ndege, hivyo ni ndege iliyosajliwa zambia (9J) kwa usajili namba BIO, najua mnajua lakini ni vizuri kujua zaidi.

    Brain

    ReplyDelete
  5. Tunasikitika kwa ajali hii, poleni sana majeruhi. Bwana Michuzi kuna sababu gani ya kutaja kabila la Bwana Mohammed Ramia (kuwa ni mmakua) kusema kuwa ni raia wa Tanzania inatosha sielewi kabisa sababu ya kutaja kabila la mtu.

    ReplyDelete
  6. Poleni sana na Mumshukuru sana Mungu kwa kuanusuru katika ajali hoyo
    Please let us know the cause of the accident when you got to know

    ReplyDelete
  7. Sunny Tayir,Mtanzania mwenye asili ya kihindi. Sunny Tayir Mhindi inaleta maana mbaya

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...