Mkuu wa Chuo Kikuu kishiriki cha  Elimu (DUCE), Mama Salome Misana akiwaonyesha waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo ukumbi wa mihadhara wa Chuoo hicho unaoweza kuchukua idadi ya wanafunzi 1000. Kushoto ni Naibu Mkuu wa Chuo Utawala, Bi. Natu Msuya. Hii ni mojawapo ya mikakati kabambe ya Serikali ya awamu ya nne kuendeleza sekta ya elimu ambapo DUCE na vyuo vingine kadhaa vya elimu vitatoa waalimu wenye shahada 13,000, ambapo kabla ya mwaka 2005 ni waalimu wenye stashahada wasiozidi 1000 walikuwa wanapatikana kwa mwaka. Waalimu wote hao 13,000 wameshahkikishiwa ajira ya moja kwa moja ambapo kuanzia mwaka huu kila shule ya sekondari ya kata imepagiwa kupewa walimu watano wenye shahada.
 Mkuu wa Chuo Kikuu kishiriki cha  Elimu (DUCE), Mama Salome Misana akiwaonyesha waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo ukumbi wa mihadhara wa Chuoo hicho unaoweza kuchukua idadi ya wanafunzi 1000. Kushoto ni Naibu Mkuu wa Chuo Utawala, Natu Msuya
 Muonekano wa ukumbi kwa nje
Mkuu wa Chuo Kikuu kishiriki cha  Elimu (DUCE), Mama Salome Misana akifafanua jambo jijini Dar es Salaam leo kuhusu uzinduzi wa jengo la mihadhara Chuoni hapo, pamoja na kuzindua michakato ya kuchangia ujenzi wa jengo la maabara na madarasa katika shule ya sekondari ya Mazoezi Chang’ombe ambayo inamilikiwa na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu (DUCE). Kushoto ni Naibu Mkuu wa Chuo Taaluma, Prof. Ernest Mallya.


Na Francis Dande
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kinatimiza miaka 50 mwaka huu tangu kianzishwe mwaka 1961, katika kusherehekea kumbukumbu ya kuanzishwa kwa chuo hicho sambamba na miaka 50 ya Uhuru, Chuo Kikuu cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) ambacho ni Chuo Kikuu Kishiriki cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kimejipanga kufanya ufunguzi rasmi wa jengo la kisasa la mihadhara lililojengwa kwa fedha za serikali.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. Mkuu wa Chuo Kikuu kishiriki cha Elimu (DUCE) Salome Misana amesema kuwa uzinduzi wa mchakato wa uchangiaji wa ujenzi  wa jengo la maabara katika shule ya mazoezi ya Sekondari ya Chang’ombe.

Alisema kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dk. Mohamed Gharib Bilal  atakuwa mgeni rasmi katika sherehe za kufungua jengo hili la mihadhara na kuzindua uchangiaji wa ujenzi wa maabara hizi za sekondari tarehe 13/9/2011 ambapo kauli mbiu itakuwa ni Tuinue Sayansi na Teknolojia Mashuleni na Vyuoni iwe Chachu ya Maendeleo ya Kiuchumi Tanzania.

Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam kilianzishwa mwaka 2005 kwa lengo la kuzalisha walimu wa shule za sekondari na wataalamu wa elimu nchini. Kuanzishwa kwake kulitokana na uwingi wa shule za sekondari zilizokuwa zimeanzishwa nchini na uhaba wa walimu katika shule hizi. Tangu Chuo hiki kianzishwe hadi kufikia mwaka 2010, kimeweza kuzalisha walimu wapatao 3092, na mwaka huu tunategemea kutoa walimu wasiopungua 700, hivyo kupunguza pengo la walimu mashuleni.

“Kumbi zilizojengwa zinatumia teknolojia ya kisasa katika kufundishia. Kumbi hizi pia zinaweza kutumika kwa ajili ya mikutano inayohusisha watu wengi. Ni jambo la kujivunia kupata kumbi hizi na ndiyo maana tumeona tuzifungue rasmi, kama ishara ya kuishukuru Serikali kwa kutuwezesha na pia kuzitangaza kumbi hizi za kisasa”.

Sambamba na ufunguzi huo, Makamu wa Rais pia atazindua mchakato wa uchangiaji wa ujenzi wa maabara katika Shule ya Mazoezi ya Sekondari ya Chang’ombe. Wakati Chuo hiki kilipoanzishwa, pamoja na kurithi majengo yaliyokuwepo pia kilirithi shule 3 za mazoezi – Shule ya Awali, Shule ya Msingi ya Chang’ombe na Shule ya Sekondari ya Chang’ombe. Sule hii ya Sekondari kwa sasa ina kidato cha 1 hadi 6 na ina wanafunzi wapatao 616, kati yao 382 wanachukua masomo ya sayansi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...