Dardanus Mfalme

Tanzania inaporuhusu uraia wa nchi mbili (dual citezenship) ina maana pia inafungua milango kwa raia wa nchi nyingine yeyote kuwa raia wa Tanzania huku akiwa anashikilia uraia wa nchi yake huko alikotokea, au 'mzunguko boya' unakuja pale raia wa nchi nyingine kuja kuchukua uraia wa Tanzania kwanza kisha kurudia uraia wa nchi yake ya awali ama kuchagua nchi nyingine yeyote inayoruhuru uraia wa nchi mbili.

Kwa maono ya Kifalme, athari kubwa ya uraia wa nchi mbili ambayo watu wengi ikiwemo wanasiasa hawaioni ni:
* Watanzania tutarudi katika ukoloni (ukoloni wa kisasa) kwa kasi kubwa sana.
Mfano;
-Mtu kama Bill Gates anaweza kuja Tanzania kuchukua uraia wa Tanzania huku akiwa anashikilia uraia wa nchi yake ya awali (Marekani) na akanunua viwanda vyote vya Tanzania kwa pesa zake na kuviendesha anavyotaka yeye.
-Au Wachina na mataifa mengine ya Asia ambayo pia ni wawindaji wakubwa wa rasilimalii za Tanzania, wanaweza wakaja kuchukua uraia wa Tanzania huku wakiwa wanashikilia uraia wa nchi zao husika na wakanunua migodi yote kama Watanzania na kuiendesha wanavyotaka wao.
-Waarabu wanaweza kuja na kununua nyumba zote za Kariakoo ama kwengineko kwa pesa zao huku wakiwa wanashikilia uraia wa nchi walizotoka.
hii ni mifano tu, sekta nyingi ikiwemo ya afya, nishati na nyinginezo zinaweza zikachukuliwa namna hii. Na tusijaribu kusema kwamba Serikali itawadhibiti raia hao namna ya kuendesha miradi watakayoifanya kwa sababu kama Serikali inashindwa kuwadhibiti wenye vijisenti, itawezaje kuwadhibiti wenye majisenti?

Sisi Watanzania wengi tuliokuwa nchi za nje ambao tumekuwa ndio wapigaji makelele wakubwa kushinikiza uraia wa nchi mbili kwa manufaa yetu binafsi, mchango wetu kimaendeleo katika Tanzania mara uraia wa nchi mbili utakapuidhinishwa, ni mdogo sana kulinganisha na ubepari utakaofanywa na raia wa nchi nyingine watakaokuja kuchukua uraia wa Tanzania huku bado wakiwa raia wa nchi zao za awali.
Mara nyingi michango yetu kwa Tanzania imekuwa ni kupeleka magari, kujenga nyumba, kuanzisha biashara ndogondogo, ama kutuma dola mia mbili tatu kwa familia zetu huko Tanzania. Mchango huu ni mdogo sana ukilinganisha na athari zitakazofanywa na mabepari watakaokuja kututawala kwa pesa zao huku wakiwa wamevaa uraia wa Tanzania. Na hili si la kujificha, kwani hivi sasa hakuna uraia wa nchi mbili lakini kila ninapozunguka Tanzania hadi huko vijijini ndanindani ambako hata CCM haijafika, huwa ninakutana na haswa Wachina ama Wakorea wakiwa wanawinda rasilimali hasa migodi na kujaribu kuweka 'mikataba kenge' na wamiliki wa migodi hiyo. Je hatuoni kwamba athari hii ya uraia wa nchi mbili itaturudisha kwenye ukoloni wa kisasa haraka sana?

Kwa mtazamo wa kifalme naomba wazee wote Tanzania, wazee wote wa Usalama wa Taifa na wahusika wote, muendelee kusema 'HAPANA' kwa uraia wa nchi mbili mpaka pale Watanzania tulio nchi za nje tuwe na uwezo wa kuja nyumbani na kumiliki na kuendesha miradi yote mikubwa ambayo mabepari wanaivizia hadi leo kama vile migodi, uvuvi wa kisasa wa baharini na maziwani, sekta ya afya, viwanda, nakadhalika.

Kama mtu kweli ana uchungu na Tanzania basi arudi kuijenga Tanzania lakini kama sivyo tubebe boksi mpaka tuwe na uwezo wa kushindana na hao mabepari kwenye umiliki wa rasilimali zetu.
Mungu Ibariki Tanzania, Amen

Dardanus Mfalme
www.mfalme.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 42 mpaka sasa

  1. Acha ubaguzi kwanza nani ana haja ya kuja kuishi Tanzania mwenye pesa zake kumejaa mbu malaria haikubaliki kwa mzungu na mwenye pesa.

    ReplyDelete
  2. Pumba head,mbinafsi roho chafu,sasa hivi huoni kama hao wageni ndio wanapata maslah kulikoni wewe unaebeba box!Serikali inakubana hata kununua kiwanja kwa familia yako?unabanwa sehemu zote na umekwenda kutafuta maisha sbb ulikotoka hukupata ajira 90% hakuna kazi!Afadhali
    nchi iko na sura kidogo ya majengo sbb watanzania wako nje wanawajengea ndugu zao!Ikiwa dual watu watashirikiana zaidi na kuijenga tanzania!Nafikiri ulilala chooni wakati unaandika wakala hii!

    ReplyDelete
  3. tatizo liko wapi kama watkuja kujenga Tanzania na kurudi kwenye nji zao au wakinunua migodi? mpaka sahivi tu migodi karibia yote ipo mikononi mwao what difference will it make huko badae wakiruhusiwa kuwa raia. i think wat is needed is good govt policies to control hizo sector na sio kuzuia dual citizenship.

    ReplyDelete
  4. Jamani si sahihi kumtusi mtu anapotoa mawazo yake eti kwa vile hukubaliani nayo. Tupo wengi tunaoungana na mtoa mada kupinga uraia wa nchi mbili kwani una athari nyingi kuliko faida. Inawezekana wachangiaji wawili wa mwanzo mna maslahi mnayotarajia kuyapata kwa kuwa na uraia wa nchi mbili. Yachujeni hayo maslahi mnayotarajia mtuambie kama yana faida kwa kizazi cha leo na cha kesho. Mtoa mada ameainisha matatizo ya mfumo huo. Nilitarajia na ninyi mje na mawazo imara yanayoonesha faida za uraia pacha ambazo zinazidi hasara zake. Alichosema huyo ndugu ni kweli kabisa. Tanzania inmezewa mate na watu wa mataifa mengi na kila kukicha mbinu mbalimbali zinatumika kuhakikisha Tanzania inabadili sheria zake ili watu hao waje kiurahisi.
    Bila shaka wanaomezea mate Tanzania wameona kuna maslahi makubwa. Lakini ili uyapate ni lazime uwe raia. Je ni kwanini wasichukue uraia wa Tz kwa mfumo uliopo bila kufikiria kurudi makwao? Ni wazi kwamba wanataka maslahi watakayoyapata wayarudishe kwao. Kumbukeni bado tuko maskini. Hatuna uwezo wa kushindana na wenye pesa. Tungekuwa na huo uwezo tungefurahia uraia pacha kwani hata sisi tungeenda kuwekeza nchi zingine na kurudisha pesa nyumbani. Mimi nafikiri in the long run uraia pacha kwa stage tulipo utakuwa ni hasara tupu. Na watakaoumia ni watanzania wenyewe. Hata kama serikali itaweka sheria kali, bado usimamizi wa sheria nchi hii ni kitendawili. Angalieni tu wawekezaji wachache walioko nchini jinsi mbavyo wameanza kuwa pasua kichwa.

    Hata hivyo jambo likishakuwa ni la kidunia hatutakuwa na uwezo wa kupingana na dunia. itabidi tukubali tu. Hivyo ningeshauri kama ndio mfumo dunia inataka, Tz isubiri kwanza tuone mafanikio kwa hizo nchi walizofuata mfumo huo. Sasa hivi tunalia maisha magumu na tunayemlaumu ni JK wa watu. Kumbe wala si JK ni mfumo wa utandawazi ambao unafanya maisha yanakuwa magumu hasa kwa watu wasio na uwezo wa kushindana. Wewe unapandishiwa bei ya bidhaa kila kikicha lakini wewe huna cha kuuza ili na wewe ufidie ulivyolanguliwa. Unadhani maisha yataacha kuwa magumu kwako? Fikirini kwanza msikurupuke tu kutukana watu. Eti mnamuita mchoyo! Mmeenda nchi gani mkaona mtu mweusi akithaminiwa hata kama ana uraia wa nchi ile? Huo si ni uchoyo?

    ReplyDelete
  5. MZEE MFALME, ALL I CAN SAY IS THAT YOU HAVE A LONG WAY TO GO MAAN NAWAACHIA WADAU WAKUPE KWAMBA NINA MAANA GANI..GOOD LUCKY TO YOU BUT TRUST ME KAMA UNA MAKARATASI YA USA RUDI SHULE KAKA

    ReplyDelete
  6. Nadhani yule aliyeandika ujumbe ule anaweza kuwa anachangia jambo moja muhimu sana kwa vizazi vijavyo.lakini kwakuwa wengi tunataka kwa maslahi binafsi basi tunaona ni sawa.Wengine kwa maslahi tu unajua nina uraia wa marekani na tanzania,wengine ndo njia ya kutishia watu na wanawake.Na mimi nipo nje ya nchi naungana na mtoa mada hiyo.Kutakuwa na faida ndogo sana ya kuwa na dual citizenship kuliko hasara.

    Kama nchi inajali haitafanya maamuzi hayo,na kama haijali ikajali maslahi binafsi ya wachache na watoto wa viongozi kwa hilo watakuwa wamefanya kosa kubwa.

    Je nchi ambazo hazina dual citizenship zimepata hasara gani ? na zile ambazo wanahuo uraia wa nchi mbili wamepata faida kaisi gani kama nchi ?

    Hii ni sehemu ya maoni na siyo sehemu ya kutoa emotions jenga hoja yako kama unatetea hilo na wengine watachangia hoja yako.Kutakuwa na watu wanapenda huo uraia wa nchi 2 lakini mimi kwangu sivyo.kwahiyo pengine wengine wanaweza kuwa na hoja na nikapanuka kuona wnegine wanaadika nini ndo kujifunza.

    ReplyDelete
  7. ...Je kama tajiri tu nyumbani akihodhi ardhi na maeneo makubwa tunapiga kelele na kuchukia na kuweka uhasama mkb.je itakuwaje kwa mgeni atakayekuja kuhodhi maeneo yetu...fikiria

    ReplyDelete
  8. Polepole tutafika tu.

    ReplyDelete
  9. Hiyo ni dhana potofu darda king ikiwa sisi wazawa tumeikimbia nchi yetu sidhani wala sifikirii kama kuna watu wanataka kuhamia huko nchi iliyojaa kila aina ya uhalifu,labda watakuja wahamiaji kutoka congo na burundi.

    ReplyDelete
  10. hahahahahahahahah, is this guy for real?? hahahahahah what a way to start of a day. For a minute thought it was 1st of April. Mfalme of nonsense!

    ReplyDelete
  11. Huenda hizi zikawa ni hekima na busara ukizingatia taratibu za sheria hiyo ya urai 2. Lakini mbona tayari munayo hawa wachina/japan/type hiyo hiyo korea ..... wameingia mpaka mitaani unajua wanalengo gani? Baada ya miaka 10 au 20 ijayo tutakuwa na wazawa wakichina au kijapani je hawatakuwa na uraia na je hawataweza kutumia nafasi hii kufanya chochote cha kuidhuru nchi yetu? Unajua hata Nyerere aliona mbali alipoweka mwenge ulisababisha kuondoa ukabila. Basi hata wenzetu wanania na mbinu katika hilo. Tuinusuru nchi yetu.

    ReplyDelete
  12. Tunajua kuna wabongo walioharibu pasport zao ili wawe wakimbizi nchi za watu. Sasa wameona kugumu kule waliko na kurudi nyumbani ni ngumu pia hivyo wanaona labda uraia pacha ndo utakuwa mkombozi wao. Jitahidini kuisukuma serikali msamehewe ili mrudi nyumbani.

    Kimsing uraia pacha kwa raia maskini kama walivyo wa Tanzania una hasara nyingi kuliko faida. Lakini naungana na mchangiaji mmoja aliyesema kwamba kama litakuwa ni jambo la kidunia, hatutakuwa na uwezo wa kupingana na dunia. Ni Nyerere tu ndiye aliyepingana na dunia hasa pale alipoona mifumo inayoletwa na dunia ina hasara kuliko faida kwa wananchi wake.

    ReplyDelete
  13. Mimi binafsi naungana na mtoa mada ni kweli ukiaangalia asilimia chache sana ya watu ambao wanataka uraia wa nchi mbili hususani wale ambao hawajakuwa na msimamo wapi kwake.

    Katika mada hii kwa upande wangu napata funzo kwamba wanayetaka uraia wa nchi mbili ni kwamba wanaona Tanzania ni maskini kwa hiyo wakichukua uraia wa Marekani watapata unafuu. La msingi hapa turudi nyumbani tuibadilishe nchi yetu. Hivi kweli Wamarekani wangapi watataka uraia wa bongo? Kwa hiyo wadau turudi bongo tuijenge nchi yetu na kama hautaki basi chukua uraia wa nchi hiyo uliyoipenda.

    ReplyDelete
  14. duh nimesoma sentensi chache tu zako na nimeona niwache kusoma na kukujibu kwa ufupi tu. kwanza huelewi unachosema. Point yako ya kuwa tutarudi kwenye ukoloni ni potofu mno. Unadhani Tanzania ndio inakuwa nchi ya kwanza kuruhusu uraia wa nchi mbili? Kuna nchi tele zimeruhusu hili miaka tele na hakuna hata nchi moja iliyorudi kuwa koloni la nchi nyengine. hebu toa mfano wa nchi hizo zilizorudi katika ukoloni?

    pia umeonyesha ni kiasi gani hujui ni vipi mtu atapata uraia wa nchi. Mfano wako wa Bill Gate ni ishara moja ya hayo ninayoyasema. Kwa aikili zako unadhani uraia utakuwa unapatikana kama vile kwenda sokoni na unanunua unachotaka. kwa hivyo na uraia wa nchi huwa unapatikana namna hiyo.

    Ukweli mtu kupata uraia wa nchi sio rahisi hivyo, unatakiwa, mbali ya mambo mengine, uwe umeishi katika nchi hiyo kwa miaka mengi (kila nchi ina idadi yake), uwe umeishi muda wote kihalali na mengi mengineyo. Ni masharti kama hayo Tanzania wataweka kwa wasio watanzania wanapotaka kuwa raia wa nchi yetu.

    ReplyDelete
  15. Anonymous 10:15 AM
    Nafikiri wewe si mtanzania nimrundi unaetaka sisi watanzania tuliokuwa nje tusipewe haki zetu hata zakufungua Acount ili wewe upewe nafasi sbb wewe nirahisi kujichanganya kuliko wazungu!
    kunafaida nyingi sana ya dual kama hujui uchumi wa nchi unakuwa haswa kwa upande wa bank na tax!pili huyo mzungu unaesema akitaka uraia atapata kwa njia yakuowa ama permenent permit akitaka kuiba mali ya watnzania kupeleka kwao atafanya kama sisi tunaofanya kazi huku nakupeleka kwetu na wao huwa wanafundishwa na nchi zao kutowa nje kuleta nyumbani lakini sisi tunabanwa kila pembe!ninakuhakikishia kenya ipe mwaka itakuwa nchi iliokomaa kidemocrasia na maendeleo sbb ya hiki kitu!lakini sisi tunaangalia choyo na ubinafsi sbb mtt wafulani anajenga ama anailetea familia yake pesa yakula!ambapo kuna wawekezaji wa nje hapo hawalipi hata tax sisi ukileta kigari unabanwa!kaa chini fikiri ujue huyo ambae atapewa uraia wa nchi mbili ni mtanzania alizaliwa tanzania kama wewe alikwenda nje sbb ya ugumu wa maisha nikama mama akafanya umalaya kwa ajili yakumpa chakula mtt wake! na tatizo hili nikwamba nchi ni maskini na ubovu wa viongozi wetu!We wil be there Tanzania we love u forever

    ReplyDelete
  16. Mi navyojua dual citizenship ni kwa watanzania tu. Inatakiwa iwe hivyo

    ReplyDelete
  17. Wote watoa maoni mmesikilizwa sasa ngojeni: Mimi ni mbongo wa damu kufa na kupona na ninaishi majuu kama msemavyo, tena majuu ya kiuhakika, nchi ambayo inalipa social security (unemployment benefit) zaidi ya mbeba box wa huko USA. Mimi sikubaliani na hio mada hata kidogo eti mtu awe na uraia wa nchi 2, akili kweli mnazo? Kawaida mtu hupati uraia wa nchi uliyohamia kama ni UK,GERMANY,SWEDEN,HOLLAND,FINLAND ,DENMARK,NORWAY,BELGIUM, FRANCE, Hata uko ushenzini UGIRIKI. Kawaida kabla hujapewa uraia wa kwao kwanza unawakilisha certificate ya kuukana utanzania, na wengi wamefanya hivyo na kupata walichokitaka uraia wa nchi hizo,sasa imekuaje ghafla mnautaka tena ubongo? Kuurudia UTANZANIA haukatazwi lakini ukane tena huo uraia uliopewa na inchi hio uliohamia halafu omba tena UTANZANIA ni rahisi na Tanzania ni Democracy itapokea tu ombi lako bila tatizo.

    KWA NINI ULIUKANA utanzania na sasa unautaka tena wewe umechemsha nini huko ulikokimbilia? Msilete mchezo na sheria.Wewe ukorofishe huko halafu ukimbilie bongo ati wewe mtanzania, au uharibu bongo ukimbilie Sweden kwa sababu una uraia wa nchi mbili?Msituletee fujo katika maendeleo yetu na WAZAZI NA WANANCHI WOTE WA TZ MSIKUBALI HAYA MAONI YA WATU WALIOKWISHA CHEMSHA HUKO MAJUU SASA WANATAKA VURUGU KATIKA HARAKATI ZETU ZA MAENDELEO. HILO SWALA LIFIKIRIWE TENA LABDA BAADA YA MIAKA MINGINE 50 KUANZIA 9 DEC 2011, Ninyi mnaotaka uraia wa nchi mbili kitu gani mnaweza kuwekeza Tanzania? wakati wote huko sawa na walala hoi BOX usiku na mchana. Kama umempata tajiri anataka wekeza bongo fanya mpango na ndugu zako ili na wewe uwepo katika share na ndugu yako bongo apate hisa kwani ndio sheria za nyumbani mgeni hafungui biashara unless mzawa anahusika vilevile,(for your own tip, if you dont know!)HIVI WEWE UNAZO KWELI? UWE MSWEISH HALAFU NI MTANZANIA HAPO HAPO, WEWE MMAREKANI NA MBONGO VILE VILE?
    UTAMCHAGUA NANI KAMA KIONGOZI WAKO ? KIKWETE UA BARAK OBAMA? KAMA BIA ZENU ZA SUPER MARKET ZIMEWAZIDIA msikurupuke na maoni wakati mmelewa bia zenu za cent kumi kumi.MTANZANIA NI MTANZANIA KAMA WEWE UNA UMAREKANI KAA HUKO HUKO; BONGO UNAKARIBISHWA KUTEMBEA MAMA YAKO NA DADA YAKO WAKO BONGO KAMA UNATAKA WEKEZA MUHUSISHE NDUGU YAKO.

    NA UKIJA BONGO KUMBUKA UWE NA VISA YA UHAKIKA UKI OVERSTAY UNAPIGWA BOMBA KURUDI HUKO KWENU ULIKOCHUKUA PASSPORT NA CONDITIO USIFIKE TENA TANZANIA KWA MUDA WA MIAKA 3 SIO MINGI.

    LONG LIVE TANZANIA!

    ReplyDelete
  18. mm namuhunga nkono uyo mfalme tusiangalie nchi ngapi wamejiunga tuangalie upande wetu si kumuiga mtu au nchi fulani kumbuka nikwelikupata uraia si jambo ndogo na si rahisi ila kwa nchi zilizoendelea si kma nchi changa kma tanzania na ni nchi yenye kujaa rushwa watu wapapewa uraia kwa njia za rushwa adi itakuwa furugu kuna mchangiaji mmoja anasema nitajiri gani atakae kubari kuchukua uraia wa tz ww unaishi dunia ya ngapi?matajiri wte wa nchi zilizoendelea wanataka kwnda nchi masikini wakaishi wakawekeze angalia tailand leo kulivyo na ngono za wtt wadogo kuazia miaka 12 tu na nio matajiri walioamia na kuekeza ndio wanaofanya mambo ayo kwa ajili ya pesa zao na tz kma tz ukizichukua nchi za africa znye mali basi lazima tz utaiweka sasa kwnn wasije kuishi ili wapole mali ztu ila tuombe uzima tutayaona

    ReplyDelete
  19. Uraia wa nchi mbili hautatusaidia chochoteee tusidanganyinge!!!!!!!!

    ReplyDelete
  20. Huyo mtoa mada ni mbumbumbu. Inawezekana ubongo umebondeka kwa sababu ya kubeba maboksi huko ughaibuni. Hii sheria tunayodai ni kwa mtanzania kuweza kuwa na fursa ya kuwa na uraia wa nchi mbili. Na siyo kweli kuwa mtu ambaye ni raia wa Marekani au nchi nyingine atakuja Tanzania siku moja tu na kudai kupatiwa uraia wa Tanzania.

    Nafikiri kama sheria ikiwa makini, itawapa fursa tu watanzania kutopoteza uraia wa Tanzania pale watakapopata uraia wa nchi nyingine. Sasa kwa wananchi wa nchi nyingine, itategemea na sheria ya huko wanakotoka. Maana najua kuwa kwa sasa Tanzania kuna wageni wengi toka nchi jirani na nchi za mbali ambao wamepewa uraia wa Tanzania, lakini sijui kama kwa kufanya hivyo wamepoteza uraia wa kule wanakotoka!!! Kila mtu ana haki ya kuishi mahali popote na pia kuomba uraia wa hapo, muhimu atimize vigezo.

    Kama miaka ya kuishi nchini, yaweza kuwa miaka nane au kumi au miaka yoyote ile kulingana na sheria itakavyokuwa, kabla ya mtu kupata uraia wa Tz.

    ReplyDelete
  21. Huyu jamaa kabla hujaandika issue, na "make a fool out of yourself" fanya research. Kama mdau alivyokwambia rudi shule, learn to do research halafu andika idea zako. Ngoja kunieleweze ni low level of your understanding. Mdau hapo juu amekwambia kuna masharti, sio tu unakuja kusema nataka uraia wa America unapewa. Ngoja ni-list few:-
    1. Uwe umekaa kwende hiyo nchi kwa kipindi fulani
    2. Huna kosa la jinai
    3. Umeoa au kuolewa na raia wa nchi hiyo ambaye anafanya kazi na kulipa kodi (na ndoa ni ya kweli sio ya kisanii)
    I don't know about other countries, but in America you get permanent resident (green card) first; it like probation period before you get a citizenship. And get this they can revoke your green card/citizenship anytime when they feel you're danger to society.


    Licha ya hiyo kama umezaliwa Tanzania na wazazi wa kigeni unakuwa kama una dual citizenship anyway (Rostam Aziz) or other way around Kama wewe ni mtanzania na una watoto wamezaliwa abroad wakienda bongo wanagongewa muhuri wa kuingia na kutoka na kufanya mambo mengine kama mtanzania.


    Vile vile dual citizenship tunanyimwa sisi watanzania ambao hatuko tayari kuhonga ili kupata hiyo dual citizenship. Lakini watu wenye pesa zao kutoka nchi za nje wana-invest anyway. Na wanawanyanyasa watanzania wenzetu kila siku. Jaribu kufanya uchunguzi (research) kwenye migodi, usikilize malalamiko ya watanzania wenzako (na mmiliki sio dual citizen), he/she hang out with Mkapa, Msekwa, Kikwete etc. To me, una-sound like "If I can have, nobody can", with or without dual citizenship, people with money will dominate Africa continent Period. Maraisi/Viongozi wenu ndio wanaowauza, sio dual citizenship. By the way, where did you get that stupid idea that "hakuna mtu mweusi anayethaminiwa abroad".

    Nini maana ya kudhaminiwa? Watanzania wangapi wanathaminiwa Tanzania? umeme wa mgao, kukosa mafuta..nk. I don't know what country you reside...but probably you are better off wherever you're than been back home Ikwiriri.

    Little advice, go to the library and learn how to make an argument, and defend it with points.

    ReplyDelete
  22. KWELI MIMI NAPINGA;AKILI SI NYWELE;HUYU JAMAA ANAZO NYWELE ZA KUTOSHA MPAKA ZINADONDOKEA MGONGONI NYINGINE LAKINI AKILI YA KUCHAMBUA MAMBO RAHISI KAMA HAYA HAIPO?ALIYESEMA URUDI DARASANI NAMSIFU SANA. PUMBA;PUMBA; PUMBA. POLE;ILA HUO NDIO UKWELI.
    RESEARCH KABLA YA KUANDIKA; SOMA JOURNALS;NA HISTORIA ZA WATU MAARUFU WALIOFANIKIWA KWENYE NCHI ZA MBALI; NA WANAFANYA NINI NCHINI MWAO WALIKOZALIWA.ANGALIA UCHUMI WA NCHI KAMA GHANA; INDIA; BRAZIL; NK; UCHUMI WAO UNAKUA KWA KASI; NA MCHANGO WA DIASPORA NI MKUBWA SANA NYUMBANI. ELIMIKA ; SIJUI MFALME WA WAPI......

    ReplyDelete
  23. KWANI PAPERS ZIMEGOMA NINI? NAONA UMETOLEWA NJE NA UNAONA HII NDIO NJIA YA KUSEMA' SIZITAKI MBICHI HIZI'; KWA WALE MLIOSOMA KITABU CHA SUNGURA MJANJA.
    POLE NDUGU;UKIKWAMA RUDI KIMYA KIMYA NA SIYO KWA KUBWEKA. KAMA MAMBO YAMEGOMA; KUOZA SI OPTION; TARATIIIIBU; JIRUDIE; KIMYA KIMYA; SIYO UTUTANGAZIE .POLE;NDIO MAISHA

    ReplyDelete
  24. First of all nenda shule kwanza, what is citezenship? its citizenship? Mtu yeyoye akija Tanzania kuwekeza it good for our country, nchi zote duniani zinataka watu wawekeze kwenye nchi zao. Unafikiria USA, inajengwa na wamarekani tuu? watu wa nchi nyingine ndio mgongo wa USA, bro funga mdomo tuu.

    ReplyDelete
  25. Nyinyi watanzania mnajifanya wajuaji sana.Wote mnaoweka comment zenu,mbona majina yenu mnayaficha?yeye kama mtanzania ameongea,pia ni mtazamo wake kwa masilahi ya taifa.
    Mtu kuwa na mtazamo tofauti haimaanishi kubishana au kutukanana,kuzalilishana.Bali nikuelmishana katika mtazamo mwingine,na siamini kwamba hana point,or yuko nje ya hali halisi ya mambo.
    Tanzania haitaka kuendelea kama ndo hivi debate inakuwaga.Mashaka,anaongea vitu vingi tu vizuri na maana watu wanamtukana.Sembuse Mfalme?ride on brothers,michango yenu ni powa sana.we listening.

    MIchuzi,please umesema hapa "usijeruhi hisia za mtu/watu"hii nini sasa?

    Kido
    bay area-california.

    ReplyDelete
  26. yatakuwa yale yale ya MUGABE NA WAZUNGU.watch people,leo huyu mtu mnamwona mjinga sio?think

    ReplyDelete
  27. we mfalme endelea na uvuvi wako kama mambo hufahamu usiyaingilie

    ReplyDelete
  28. MMMMHHHHH! Kasheshe tena la mzee Sheshe!

    ReplyDelete
  29. Mfalme,

    Nakusihi urudi shule kaka so that you can be an asset to your country. Hata hao raia wa Tanzania wenye pesa zao wanakimbia nchi kuishi ughaibuni, do your homework you'll find out. Hata hao raia, viongozi wetu, ndio mafisadi wakubwa wa hizo rasilimali.

    Lazima tuelewe na kukubali we're not the only resource rich country in the world, and also we also need outside help exploit our resources for our own benefits. We simply cannot afford ourselves because we're too poor. Kazi ya serikali ni kulinda rasilimali za nchi zisitumiwe vibaya na wananchi au wageni.

    Sijui hata nianze wapi kukuelimisha, ushauri wangu wa bure kwako ni kwamba unahitaji elimu zaidi haraka iwezekanavyo ndugu raia mwenzangu.

    Chonde chonde,

    Raia mwenza

    ReplyDelete
  30. Huyu mtoa mada ameongea mambo muhimu na ya msingi sana. Mimi binafsi namuunga mkono. Wengine wamemshambulia kwa matusi kwa sababu hawana hoja. Huu uraia wa nchi mbili unaweza ukawa na manufaa kwa watanzania wasiozidi asilimia moja ambao wanaishi maisha yao hivi sasa. Lakini hili swala la uraia wa nchi mbili halitakuwa na faida yoyote kwa asilimia takribani 99 ya watanzania wanaoishi hivi sasa, na pia suala hili likuwa na madhara kwa watanzania karibu wote wa vizazi vijavyo. Mifano ipo hai. Zimbabwe na South Afrika ni mifano sahihi. Kila siku tunashuhudia migogoro mipya ya ardhi kupokonywa wananchi na kupewa wawekezaji ambao ni wageni. Sasa hawa wawekezaji wakishautwaa utanzania wa pasipoti, basi wananchi wa sehemu kama vile mbalali, mwana kerege, na tuwangoma watakuwa wamekwisha na hawatakuwa na haki tena. Mkae mkijua kwamba watoto wenu watapigana kwa vizazi na vizazi na ili tuu na wao wakubalike kama watanzania ndani ya Tanzania. Na haya ndiyo madhara ya usomi pasipo kuelimika. Watanzania wenye uwezo wa kumiliki uraia wa kigeni hawazidi asilimia moja ya watanzania wote. Lakini hao hao asilia moja kwa ubinafsi, tamaa, akili fupi na ujinga, wapo kuiweka nchi rehani kwa faida zao binafsi, bila ya kuwajali watanzania walio wengi ambao uraia wa nchi mbili hautawasaidia chochote.

    ReplyDelete
  31. Naongezea. Na ndiyo maana wapumbavu wote wanaopingana na huyu mtoa mada, kutokana na kutokujiamini kwa hoja zao, basi hawaandiki majina yao humu.

    ReplyDelete
  32. Completelty ILITERATE! Waulize waafrika wote hata Nigeria kwenye mafuta wanafhukua dual citizenship. Tanzania kuna nini cha kukimbilia tumejaa hapa washigton D.C kama hatuna akili nzuri? Why tumekimbia urasimu ukiritimba na mazongo ya bongo. Hapa you have your elimu na karatasi hata Ikulu utapata kazi bila kuhonga au kuwa na mjomba. Nilimaliza shule miaka mingi na nikatuma maombi ya kazi kwenye makampuni na sasa ninafanya kazi takribani miaka 10 kwenye maabara poaaaaaaaa napulizwa na kiyoyozi na dola zangu zinaingia sina uncle wala mjomba ninayemjua kila nikigeuka niko na wazungu na wananisikiliza. BONGO NEED TO CHANGE THIS MENTALITY NA WEE MPUUZI UNAHITAJI KUTOKA NJE KIDOGO UTAONA KIASI GANI UMEDUMAZWA KIALILI NA FIKRA. POLE WEEEEEEEEEEEEEE

    ReplyDelete
  33. Mdau Mfalme pole sana kwa maoni yako mazuri. Nakumbuka mimi nilipomaliza F6 niliambiwa kuwa nchi za ulaya zinampango wa kufungua vyuo vikuu Africa ili waafrika wasiende kusoma ulaya na kujichimbia. Nilipinga sana hiyo fikira ya wazungu kwani nilikuwa naamini na mimi nipate scholarship niingie ughaibuni nitajirike. Baada ya miaka kadhaa mada imerudi tena lakini kivyengine. Sasa watu wanaoona uraia miwili dili kwao wanapinga vikali wasiotaka uraia miwili kuwepo TZ. Nafikiri vijana msiwe na jazba, cha muhimu Mfalme ametoa sbb anazohisi kuwa faida ni ndogo kuliko hasara ya kuwa na uraia miwili. Tuwe waastaarabu vijana najua hata mimi nilipokuwa umri wenu nilikuwa na jazba kwa mambo yanayonipatia mimi maslahi yangu. Wengi wenu mnaonyesha mpo ughaibuni na mna elimu ya kutosha ya kujua kuwa sasa TZ kuna demokrasia na kwenye demokrasia wengi wape. Je fikira zenu nyinyi ikipigwa kura ya sheria hii unafikiri wepi watashinda? Raia wote wa TZ ambao wapo nje hawafiki hata laki 3. Kati ya hao wanaukuja TZ vacation hawazidi hata nusu laki. Uraia miwili itasaidia nini ikiwa hata huko TZ haendi? Wangapi kati ya waTZ walioko nje wana akiba ya zaidi ya $50,000? WaTZ halisi hawatafaidika na uraia miwili maana wengi wao hawana uwezo wa kuutumia huo uraia wa TZ, moja katika sheria ya uraia maana yake uweze kulipa kodi hiyo nchi uliyo na uraia. Sasa wewe upo ughaibuni tax utalipa vipi? Wengi wenu hamjui lakini raia wa ki-British ambaye hajakaa UK/EU zaidi ya miaka miwili huwa hana haki yoyote ile zaidi ya hiyo passport. Hawezi kupata benefit, fee za shule atalipa sawa na mbongo na mengineyo. Anachoambulia yeye ni kufanyakazi bila ya kibali. Kuwa raia wa nchi maana yake uwe unalipia kodi hiyo nchi na siyo hivyo mnavyofikiri nyinyi. KODI NDIO INAYOKUFANYA UWE RAIA. Hii iwe ndio moto yetu sasa, sio jitu limekaa USA miaka 30 halikulipa kodi hata siku moja halafu tumpe uraia na cheo juu, ujinga huo hatuutaki. MLIPA KODI WA TANZANIA HOYEEEEEEEEEEEEEEEEEE!!!

    ReplyDelete
  34. Wabongo: Tunapoongea dual citizen ni MTANZANIA (mimi na wewe bila kujali tuko wapi) kuwa na right ya kupata uraia wa pili. Yule aliyeishaukana utanzania hayupo hapa kabisa. Mbali ya hayo: kupata PP ya TZ ni sawa na kumsukuma mlevi. Asieamini kalaga bao. kwa TSh laki moja(!!!) unapata ganda, na watu wala hawaangalii wewe ni nani. Pia, iwapo nimezaliwa TZ na kusaliti PP huko ugaibuni, Je kuna sheria inayonikataza mie kwenda kijijini na kuishi kama waTZ wengine. Nani ataniuliza wapi nilikuwa miaka 10 iliyopita? Sio siri, kuishi TZ bila ID yoyote inawezekana. Juu ya wageni kuja, hivi ni nini kinawazuia? Amini usiamini, rushwa watoazo sasa ndo hizo hizo watakazotozwa tukiwa na dual citizenship! Kwa mie, hii sheria inatubana sie WATANZANIA tunaoshindwa kuchukua uraia wa pili kwa kipengele kuwa inabidi tuukane ubongo, kwani serikali yetu haituruhusu kuwa na PP mbili.
    Then: sheria inakuwa na vipengele na masharti tofauti:A) Iwapo wewe ni Mbongo na unataka kupata uraia mwingine au B) wewe ni mgeni na unataka kupata uraia wetu. Blackmpingo

    ReplyDelete
  35. Tanzania Tanzania!!!Elimu muhimu, tembea uone, uelimike, wewe ni mfano mmoja wa watanzania, hisia zako binafsi na kuna watu wanakuunga mkono. Ndugu yangu kama unasubiri tujifunze kwa wengine waliotangulia ndio maana ya kuzidi kuachwa, by the time Kenya na Uganda, Burundi ziko mbali ndio unafikiria tulete uraia wa nchi mbili is too late. Muwe careful kabla ya kuandika hizi mada, inasikitisha kuona in East Africa Kenya, Uganda ziko ahead of Tanzania kimaendeleo na hizi nchi zina dual citizenship, ukienda west Africa angalia Ghana na Nigeria zinavyoyoyoma.Bila ya dual citizenship tu tayari wabepari washachukua nchi futhermore hutaki ndugu zako waliotembea wakaona dunia wasirudi nyumbani kuja kuchangia maendeleo!! Inasikitisha! Shule muhimu! Nahisi huyu jamaa alinyimwa visa sasa anatoa dukuduku lake. Ule umasikini jeuri jamani tuuache umepitwa na wakati.Mungu tusaidie tufike.

    ReplyDelete
  36. Hii ndio maana mtanzania anasoma hadi anapata masters degree university Tanzania lakini hapati kazi kwasababu ya upeo mfupi kama huu, wakenya wanakuja wanachukua kazi zenu mnalalamika muwe mnaona mbali si mnashindia kikorosho na mawazo potofu. Mdau mada hii usilete tena au ukileta tena uandike vitu vya maana. Bill Gates!!!!! huna hata mifano ya kusapoti idea yako. Poleni Watanzania Mmelala

    ReplyDelete
  37. KWA TAARIFA YENU NINYI MLIOKUWA NA URAIA WA NCHI INGINE DHIDI YA

    TANZANIA. KAMA WEWE ULIKUWA MTANZANIA UKENDA ISHI HUKO NJE MPAKA

    UMEPATA URAIA WA HUKO , WEWE SIO TENA MTANZANIA! MIMI BINAFSI NI

    MTANZANIA WA BABA NA MAMA NA NILIKUJA KUISHI NJE MPAKA NIMEPATA URAIA

    HAPA UJERUMANI NAENDA TEMBEA NYUMBANI KWA BABA NA MAMA KILA MWAKA NA

    NINAKWENDA KWA VIZA KAMA MGENI MWINGINE ANAEINGIA TANZANIA, SIWEZI

    WALA SIONI SABABU TENA YA KUOMBA TENA URAIA WA TANZANIA WAKATI

    NILIIISHA UKANA,SASA MIMI NITAITWAJE? HAO WARUNDI NA WAZAIRE WANAKUJA

    NA KUOMBA URAIA WA TZ KAMA WAKIFAULU SIFA ZOTE BASI WANAPEWA LAKINI

    WAKIBAINIKA BADO WANA URAIA WA KWAO WANANYANGWANYWA NA HATA JELA.

    KUMBUKENI URAIA INA MAANA UNAHAKI ZOTE KAMA MWANANCHI MWINGINE WA NCHI HIYO, HATA URAIS UNARUHUSIWA KUGOMBEA. SASA NIGOMBEE URAIS HUKU UJERUMANI NIKISHINDWA NIENDE NIKAGOMBEE URAIS TANZANIA? ETI KWA SABABU NINA URAIA WA NCHI 20? NINYI MNAOMWAMBIA HUYO MTU ALIELETA MADA

    HII AENDE SHULE NINYI NDIO KWANZA MNGEENDA KWANZA KU REFRESH NAONA MABOX YAMEWAZIBUA

    HAIWEZEKANI WALA LISITOKEE BALAA KAMA HILO ,NCHI YA TANZANIA NI MASKINI ITAHARIBIKA TOFAUTI NA ILIVYO HIVI SASA

    MIMI ALLY WA FRANKFURT

    ReplyDelete
  38. the author of this article should read up on the subject before writing such ignorant comments on dual citizenship

    ReplyDelete
  39. Mfalme una point, watanzania wa kweli wanaliona hilo, ila walioenda kiuzamiaji na punguani wa uzalendo ndio wanaopinga bila kujali taadhari muhimu ulizotoa. asante kwa angalizo hope wenye mamlaka watazingatia point zako wanapotoa maamuzi. point unayo

    ReplyDelete
  40. Ushauri,

    Hapa tuko wote kueleweshana,tubishe kwa kutoa hoja ama tuchangie kwa kuongezea hoja itasaidia hata kwa wale ambao hawajui vizuri wakaelewa nini maana ya dual citizenship.

    Wapinga mada inawezeka mnahoja nzuri zaidi,tupeni maelezo zaidi,ambayo yatamwelewesha mtoa mada na kumbadilisha huko aliko na hata siye wengine tunaofuatilia lakni siyo kutoa maneno makali nayaita yakuonyeshana nani anajua zaidi ya mwenzake.

    wanaounga mada mje na hoja zaidi kukandamizia hiyo hoja iliyotolewa.

    Matusi hayamjengi mtu bali huleta mafarakano zaidi.

    ReplyDelete
  41. Woote mnaounga mkono uraia pacha ni wababa box mloko nje ambao hamna msaada wowote kwa maisha ya kesho ya mtanzania. Mna maslahi binafsi. Mngeona mbali msingeongea mambo ya uraia pacha kwa nchi masikini kama Tz. Una faida kwa nchi ambazo watu wake wameelimika wote na wote wana uwezo wa kuingia kwenye ushindani.

    After all, mpo nje ya nchi lakini mmeshindwa hata kuiba teknolojia mkaleta nyumbani ili na sisi tuweze kutengeneza vitu. Huko tunajua mnaosha magari halafu mnajifanya ninyi ndio mnajua sana kuliko watanzania wengine. Bakini hukohuko kama utanzania umewashinda. Kama hamna uzalenda hatuna haja na ninyi. Kwanza mkija huku mnaongeza foleni tu na joto.

    ReplyDelete
  42. Oya naona wengine humu wamekuwa kama vifuu,yaani wanashindwa kuwa great thinkers.

    Uraia wa nchi mbili ambao umependekezwa huko bungeni sio kwa kila mtu,huu umekuja baada ya wanzania kutaka kupewa fursa nchini kwao tanzania na zanzibar kuwa raia pia,kwani ukiangalia hao wapiga box na hizo biashara ndogo ndogo ndio wachangiaji wakubwa kwa pato la nchi.

    whatever munaona ni mchango mdogo,kujenga nyumba,kutuma pesa dola mia mbili,lakini inafahamika kuwa ni mchango mkubwa,sana,mbona serikali imeshindwa kumjengea mwananchi kajumba aishi nae katika living standard ?

    Lazima tukubali ukweli Mfalme,mchango wa watu wa ughaibu ni kubwa sana kwa serikali.

    Ushauri kwa serikali.

    Serikali kama inapitisha azimio wa uraia wa nchi mbili basi uwaguse watanzania na wazanzibari tu waliko nje walibeba uraia huko nje kukubalika nchini kwao hapo tz na znz.

    Mfalme wakati mwengine unaonea pumba wakati huo huo unaongea kweli,nafikiria huwa zinangia toka,au ulikuwa na stim,hahahahhaha

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...