Na Mwandishi wetu,
Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi, Bw. Omari Nundu amemteua Bw. Paul T. Chizi  (pichani) kukaimu nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Ndege, ATCL.
Uteuzi huo ulianza tarehe 11 Agosti, 2011 na utaendelea hadi hapo Rais atakapouthibitisha au kuteua mtu mwingine.
Akiongea na mwandishi wa habari hizi jana, Bw. Chizi alisema kazi kubwa iliyoko mbele yake ni kuifufua ATCL.
Hivi sasa ndege za ATCL hazifanyi kazi lakini Bw. Chizi aliahidi kuwa ndege zitaanza kuruka hivi karibuni.  Hakutaka kutoa maelezo zaidi akisema ni mapema mno kutoa mikakati iliyopo.
Bw.  Chizi ni Mhandisi wa ndege mwenye uzoefu wa siku nyingi.  Ana Shahada ya Uzamili ya M.sc kutoka chuo cha Odessa Polytechnic katika Soviet Union. Pia ana shahada ya Uzamili ya MBA kutoka Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam (UDSM).

Alijiunga na lililokuwa Shirika la Ndege la Tanzania (ATC) mwaka 1979 kama Injinia wa Mipango na Matengenezo na akapanda hadi kufikia Unaibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika mwaka 2002.
Chizi alistaafu kwa hiari 2002, na kuanzisha Kampuni yake ya kutoa ushauri inayoitwa Customer Support Systems Ltd.  Ametoa ushauri wa kitaalam kwa mashirika yapatayo 60 (sitini) hapa nchini na nje ya nchi.

Kutoka 2007 hadi 2008 alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Community Airlines. Kutoka Machi, 2011 hadi alipoteuliwa na Waziri Nundu alikuwa Meneja Mkuu wa Jetlink Express (T) Ltd.
Bw. Chizi ana umri wa miaka 58, ameoa na ana watoto watano.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Jamani lakini hili sio Shirika la umma tena kama mnavyoonyesha kwenye habari hapo.

    Hii ni Limited Company iliyosajiliwa chini ya Sheria ya Makampuni Sura 212.

    Sasa the Companies Act inaruhusu utaratibu huo wa kuchaguana wakurugenzi kienyeji hivyo au wanateuliwa kwenye MEMBERS(SHAREHOLDERS) MEETING au ANNUAL GENERAL MEETING.

    AG yuko wapi? anashindwa kushauri hilo.
    Wenye ujuzi zaidi wa Company Laws hebu tuhabarisheni

    ReplyDelete
  2. Hongera Kwa Uteuzi. Una kazi Nzito Mheshimiwa wa kupeperusha Flag Carrier

    ReplyDelete
  3. Labda huyu atatuvusha
    lets wait n c

    ReplyDelete
  4. He he he heeee Chizi kapewa rungu!

    ReplyDelete
  5. Hili dubwashika linahitaji mtu 'chizi' kwelikweli, no pun intended!

    ReplyDelete
  6. wadau pole pole jamani acheni uchizi
    huyu chizi naona analijua shirika nje ndani kwa hiyo tutarajie habari njema

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...