sehemu ya Nje ya  Jengo la Mradi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam.
 Ukumbi wa Kisasa wa Maonesho ya Jukwaani uliopo ndani ya Jengo la Mradi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam.
 Injinia mkuu wa CRJE Bw ZHANG XING akikabidhi Funguo na Document za Mradi  kwa Kahimu Mkurugenzi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Mama Christine Ngereza
 Artist Director wa VISA 2 DANCE Bw Aloyce Makonde nimmoja wa mashuhuda walio shuhudia Makabidhiano hayo kwani Tamasha la VISA 2 DANCE linatarajiwa kufanyika katika Ukumbi wa Kisasa wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar Es Salaam.
Kahimu Mkurugenzi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Mama Christina Ngereza akihojiwa na Waandishi wa Habari.

Na Mdau Sixmund J. Begashe wa Makumbusho Tanzania

Kampuni ya China Railway JianChang Engineering Co. (T) ltd (CRJE) imekabidhi rasmi majengo ya mradi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es salaam. Makabidhiano hayo yalifanywa kati ya  Kampuni hiyo ya Ujenzi ya nchini China na Uongozi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamani Dar es Salaam tarehe 8 Septemba, 2011  katika eneo husika la Makumbusho hiyo.

Mshauri wa  Ujenzi wa Mradi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Arch. Chazi Rwakanadi, alisema kuwa Mradi umegharimu zaidi ya Bilioni 8 za Kitanzania, pesa zilizotolewa na Serikali ya Sweden na Serikali ya Tanzania na umechukua miaka mitatu hadi kukamilika. Arch. Rwakanadi amesema kuwa walishirikiana vyema na Kampuni ya Ujenzi katika kuhakikisha ubora uliokusudiwa wa jengo hilo unafikiwa.

Akipokea majengo hayo kwaniaba ya Mkurugenzi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Mama Christine Ngereza, aliipongeza Kampuni hiyo kwa kazi nzuri ya ujenzi wa majengo hayo. Mama Ngereza ametoa wito kwa watanzania kujitokeza sasa kutumia mradi huu kwani unatoa nafasi kwa kila mmoja na hasa watoto, vijana na wasanii kwani wana nafasi kubwa ya kujifunza na hata kukuza vipaji vyao kwa kupitia studio ya kurekodi Muziki, Ukumbi wa Kisasa wa Maonesho ya Jukwaani, Studio kwa ajili ya mafunzo ya Dance, Chumba cha Masimulizi ya Watoto na kile cha Sanaa za Ufundi.

Mama Ngereza ameutaja mradi huu kama moja ya mafanikio makubwa ya Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni tangu Nchi yetu kupata Uhuru, hivyo mradi huu mkubwa utafunguliwa rasmi mwezi Desemba, 2011 kama  sehemu ya maadhimisho ya Sherehe za  miaka 50 ya Uhuru wa Nchi ya Tanzania Bara.

Mradi huu wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam una sehemu za Ofisi, Chumba mahususi kwa ajili ya Mikusanyo Nyeti, Bohari za mikusanyo, Kumbi za Maonesho, Seheumu za watoto za kujifunzia kazi mbali mbali za sanaa, Ukumbi wa kisasa wa sanaa za maonyesho ya Jukwaani, Studio ya Kurekodia Muziki, Maktaba ya Kisasa, Kumbi za Mikutano na Sherehe mbali mbali, Duka la Zawadi, Migahawa na viwanja vya wazi kwa ajili ya shughuli mbali mbali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Safi sana Mama Ngereza!! Wanawake tunaweza, wenye wivu wajinyonge.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...