Wakaazi wa Dar es salaam wakitembea baada ya barabara ya Morogoro road sehemu za Jangwani kufungwa kwa muda kutokana na mafuriko yaliyoikumba jiji hilo kwa siku mbili mfululizo na hadi sasa imefahamika kuwa watu 13 wamepoteza maisha yao. Picha zote na Francis Dande wa Globu ya Jamii
Boti kutoka feri likitelemshwa kusaidia zoezi la uokoaji
Askari wakiwa tayari kulinda usalama wa mali na watu
Mto Msimbazi ukifurika kuingia bahari ya Hindi
Daraja la Jangwani halipitiki
Askari wa JWTZ katika kuokoa wananchi
Boti za Fibre toka JWTZ zawasili kusaidia uokoaji
Mimi nilijua mafuriko ya kawaida lakini hizi picha zimenistua sana tu, Mwenyezi Mungu azipumzishe roho zao mahali pema waliofikwa na umauti
ReplyDeletesasa afande chacha kicho kirungu cha nini kwenye uokoaji tena unaonekana ukiwapigia watu mkwala.anyway poleni sana ndugu zangu wa dar.
ReplyDeletehii ni hatari kubwa.. poleni waathirika wote
ReplyDeleteHali inatisha inasikitisha mungu saidia watanzania
ReplyDeletejamani mungu waokoe wenzetu.
ReplyDeleteHata mimi nilikuwa nadhani kama miaka yote, kumbe hali siyo ya kawaida haijawahi kutoke hii, naona zimesombwa hata nyumba zilizo mbali na bonde la mzimbati, poleni sana, mambo kama haya mamlaka ya hali ya hewa, wenzao huku juu, wana shika vipaaza sauti kutangaza watu waondoke waondoke sasa haraka haraka na magari wakizunguka kabla ya mvua yenyewe kunyesha, sasa hawa jamaa wana subiri mpaka watu waathilike ndo waseme eti mvua hii haijaisha, mbona hata mimi naweza kutabiri hivi.
ReplyDeleteMwenyezi Mungu awalinde waja wake. Hii hali inastua sana
ReplyDeletePoleni waathirka wa mafuriko, na pia hameni mabondeni!
ReplyDeletepoleni sana ndugu zangu mana kweli hizi picha zinashtua inaonekana sio mafuriko ya kawaida, tutaomba watu wote tushirikiane kwenye kusaidiana katika janga hili tusisubiri tu serikali mana kutokea imeshatokea...
ReplyDeleteEee Mwenyezi Mungu tusaidie waja wako! Hizi picha zinatisha kwa kweli. Wakati mie nalalamika kuwa umeme umekatika kumbe sijui kuna binadamu sehemu nyingine wanateseka hivi! Mungu nisamehe!
ReplyDeleteMwenyezi Mungu atawasahilishia ndugu zetu na mitihani yake Allah. Na Mwenyezi Mungu atakupeni vilivyobora kuliko mlivyovikosa Insha'Allah. Kuweni waja wenye subra ndugu zangu.
ReplyDeleteMungu wanusuru ndg zetu na hili janga..dah poleni sana waTz
ReplyDeletepolen ndugu zangu wa dar jamani mungu awalinde ee mungu waone waja wako katika hiki kipindi kigumu
ReplyDeleteMamlaka ya hali ya hewa ilishatangaza siku nyingi ila wananchini wabishi.
ReplyDeleteKwa hapo hata siwezi walaumu serikali, walishaambiwa wahame kwenye mabonde miaka mingi sana, hawataki. Wanataka walipwe fidia na kupewa viwanja maeneo mengine kwani serikali ndio iliwapimia hapo mabondeni.
Waulize kama hata wana hati za hivyo viwanja adi kusema walipwe fidia..
Kutoka maisha ya nyumbani hadi makazi ya muda Darasani ktk Shule kwa wahanga wa mafuriko,,,kuyamudu mabadiliko kugumu, bahati watoto shule zimefungwa wapo likizo,,,ile kwaaa unatoka na taulo kiunoni kwenda kuoga watoto wapo ktk darasa wanasoma!
ReplyDeleteMADHARA YA BAADAE NI KIPINDUPINDU MAJI SIO SALAMA SERIKALI KAZI HIO.
ReplyDeletehivi sasa jamani walio bomokewa na nyumba zao,ndio tena watabaki mitaani au serikali hua inamipango ya kuwasaidia makazi mapya?maana kwa mtanzania wa kawaida aliye weza kujibana akajenga banda lake miaka hiyo,sidhani kama ni rahisi kurudia tena ujenzi miaka hii,maisha yenyewe miaka 50 ya uhuru mpaka chakula imekua ngumu kununua kwa bei zilivyo panda!! Poleni sana waathirika wa mafuriko,Mungu yu pamoja nanyi,kweli miaka 50 ya uhuru imekuja na mengi.
ReplyDeleteMdau wa 14 hapo juu, Duhh inakuwa ni kumbukumbu mfano mtu Mhanga wa mafuriko unapangiwa makazi ya muda ktk Darasa la Shule halisi uliyosoma miaka takribani 30 na ushee iliyopita huko nyuma????,,,tofauti inakuwa ni kuwa mwanafunzi wa umri mkubwa safari hii unakuwa na familia yako ahh ndio maisha,,, maiti haichagui KABURI!
ReplyDeleteHAPO HAPOOOO,,,,,,MBINU YA KUHAMISHA MAKAZI HARAMU MABONDENI, JANGWANI KIGOGO MTO MSIMBAZI NA KWINGINEKO!.
ReplyDeleteMuda huu hao wakazi haramu wakiwa ktk makazi ya muda ya Msaada wa Serikali ktk madarasa ya Shule, KABLA MAJI HAYAJATOKA HUKO MAKWAO, WASIJE WAKARUDI MAKWAO TENA,,,ILI WAPATE AKILI YA MAKAZI MAPYA YANAYOKUBALIKA,,,GREDA IPITISHWE HARAKA KUBOMOA!
TANZANIA NCHI YANGU NAKUPENDA KWA MOYO WOTE.....
ReplyDeleteTANZANIA BADO TUPO NYUMA SANA TUACHANE KABISA NA KUJISIFU ETI TUNA MAENDELEO
POLISI WANAFIKA ENEO LA TUKIO HUKU WAMESHIKA MABUNDUKI NA MABOMU YA MACHOZI ETI WANALINDA RAIA NA MALI ZAO
HAO PILISI WAMEFIKA SEHEMU KAMA HIYO INATAKIWA WAONYESHE UTU WAO NA SIO KUSHIKA MIBUNDUKI KAMA KUNA VITA
WANATAKIWA WASHIKE VIFAA VYA KUOKOLEA NA KAMA NI ULINZI BASI WAUFANYE KIUSTAARABU NA SIO KUJIONYESHA KAMA WANA UGOMVI NA RAIA
NJIA ZA MAJI TAKA NI NDOGO MNO KIASI KWAMBA LIKITOKEA LA KUTOKEA TUTAKUJA KUPOTEZA HIYO NCHI
NA WATU NI WENGI SANA HUKO MJINI KIASI KWAMBA INATISHIA HIVI KWELI WATU WANAOFIKA MJINI KILA SIKU NA KURUDI MAKWAO KILA JIONI NI KIASI KANA KWAMBA WANASHANGAZA
YOTE NI SERIKALI MBOVU AMBAYO IMEJENGA KILA HUDUMA YA KIJAMII KUPATIKANA MJINI WAMESHINDWA KUPANUA MJI KWA KUJENGA VITUO VYA HUDUMA YA JAMII KWENYE KILA KITONGOJI
NI WAKATI WA SERIKALI KUBADILIKA NA KUANZA UJENZI WA KISASA ILI KUPUNGUZA MSONGAMANO WA HUKO MJINI
MAGARI UTATESA HAYAENDI YAMEUNGANA UTASEMA NYORORO KUTOKANA NA MSONGAMANO WA MJINI
CHONDE CHONDE SERIKALI TUJENGEENI VITUO VYA HUDUMA KWA JAMII KWENYE VITONGOJI VYETU ILI TUWEZE KUPATA HUDUMA BILA KUFIKA MJINI.
POLENI SANA WAFIWA NA WALE WALIOPATWA NA SHIDA ZOTE ZA MAFULIKO HAYO.
MUNGU IBARIKI TANZNAIA DUMISHA AMANI NA UMOJA.
Mungu Baba, tunakuomba uinusuru nchi yetu Tanzania kwenye balaa hili la mafuriko hasa ukizingatia kwamba hatuna uzoefu wa maafa kama haya. Baba tunaziweka mikononi mwako roho za wahanga waliopoteza maisha yao kutokana na mafuriko haya na pia uwape hekima viongozi wetu kama ulivyompa Mfalme Solomon ili waweze kuwa na busara ya kulitatua tatizo hili kwa ufanisi na kuwajali kwa hali na mali wote waliopatwa na maafa haya, tukizidi kukuomba na kukushukuru kwa jina la mwanao Yesu Kristo. Amen.
ReplyDeleteNaona Ras Makunja juu ya farasi? kweli mambo yao sio mabaya
ReplyDeleteakina ras makunja wapo kazini sasa mbona magitaa kiunoni kulikoni?
ReplyDeleteMkiona watu wanakaa Mbagala mnawaona washamba na wakulima... haya sasa Msaada wa Serikali wa makazi ya muda kukaa maisha ya Shule ktk Madarasa uzeeni ndio ujanja?
ReplyDeleteHuyo farasi mpeni lishe
ReplyDeleteAskari mpaka mabomu ya machozi ya nini?. Je farasi analishwa kweli amekonda!
ReplyDeletetypical ya askari wetu wa Tanzania hata kwenye maafa haweajui kuongea kidiplomasia. Wao ni virungu na bunduki tu mkononi.
ReplyDeleteWatu wamefikwa na maafa, wamepoteza mali zao na hata ndugu zao, wanachihitaji ni msaada, uongozi na moyo wa huruma kutoka katika vyombo vya serikali. Hivi kweli kulikuwa na haja ya askari kuchukua bunduki na virungu? Ona picha hiyo boti inashushwa ni askari mmoja tu anaesaidia wengine wako wapi?
Na sio kama kumezuka wimbi la wizi, hasha!!!!!
Huyu afande na bunduki tena kulikoni jamani si mafuriko tuu?? I hate seeing these guns on people's hands! Watanzania hatujazoea vitu hivi sana sana mabomu ya machozi kaaaaaaaaaaaaa.
ReplyDeleteNi kweli walibaki mabondeni lakini adha ilipotokea tulikuwa tayari au tulibahatisha tu kama kawaida yetu? Tunahitaji kuwa na taratibu za kukabili majanga kwa haraka na kwa kutumia utaalamu unaojulikana unafanya kazi. Kila janga kwetu ni matatizo makubwa sana. Pia janga ndio linalotuonyesha wote sie ni binadamu ila kwa walionacho au wenye majina suluhu ni haraka na rahisi zaidi. NCHI YANGU TANZANIA je lipi lingine lifanyike?
ReplyDeletehii picha ya mwisho mi naogopa hii boti/mtumbwi ilivojaza watu. sasa hapo mtumbwi ungepinduka kati kati ya maji mengi si ndo ingekuwa shughuli nyingine!
ReplyDeletePOLENI NDUGU ZANGU WAFIWA NA WAANHGA KTK JANGA ILI,ILA NAPENDA KUITUPIA LAWAMA KIDOGO OFIC ZETU ZA IDARA YA HALI YA HEWA,HAWASEMI MAPEMA WANASUBIRI HARI ITOKEE NDIO WAPATE SABABU YA KUJIFANYA WAO NDIO WATAALAM WA KUTABIRI,HII SIO SAWA KWA KWELI.ALAFU NAITUPIA KIDOGO MAMLAKA HUSIKA YA UOKOAJI KWA KUCHELEWA KUFIKA ENEO LA TUKIO HADI KUSABABISHA ONGEZEKO LA VIFO.NDUGU ZANGU NI JAMBO LA KITAIFA HILI TUNAOMBA TUWE PAMOJA KWA KUWACHANGIA NDUGU ZETU WAISHI KAMA SISI KWA SASA KTK KIPINDI HIKI KIGUMU.
ReplyDeleteNi mimi Cloud John wa Ubungo DSM.
Mungu ibariki Tanzania.