Maulid Ya Mtume Muhammad  (S.A.W) yalifanyika jana kama ilivyotangazwa, yalihudhuriwa na watoto na wakubwa kupelekea kufanikiwa kwa kiasi kikubwa. Wanafunzi wa Madrasatul Amin walionyesha uwezo wao kusoma na kufafanua quran tukufu.Shughulizi ziliongonzwa na Ustadh Abdullah Abubakar Mtawa na Ustadh Khalfan Abdullah. Maulid yalitayarishwa na madrasatul Al Amin jijini Toronto Canada.
 Sehemu ya wahudhuriaji kwenye Maulid hiyo
 Wanafunzi wa Madrasatul Amin
 Waliohudhuria
 Vijana na watoto walijitokeza kwa wingi
 Wanafunzi wa Madrasatul Amin wakionesha umahiri wao katika kusoma Quran Tukufu
 Ustadh Abdullah Abubakar Mtawa akihutubia
Ustadh Khalfan Abdullah akitoa mawaidha maridhawa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Ma'asha'Allah!ilikuwa ni Maulid kubwa sana na nzuri mno kwa picha.Nafurahi sana kuona watu wa nyumbani bado mnatilia mkazo wa kusheherekea Maulid Nabii!
    Huku watu wengi,hata waliotoka nyumbani wamefuata mila ya kutosheherekea Maulid ya Mtume wetu Muhammad (S.A.W),eti wanaita ni Bida'a....Bora baada ya kuuliza mimi kwa Masheikh wa nyumbani nikaambiwa kuwa kuna Bida'a nzuri na mbaya,,,Na kweli Bida'a ya kusherekea Mazao ya Kipenzi cha Mwenyezi Mungu,Kipenzi cheti,Mwalimu wetu!Ni bida'a nzuri,,Insha'Allah wenye kumpenda mtume wetu tusheherekee siku hii,mpaka mwisho wetu hapa Duniani!Taqbir,Allahu Aqbar!
    Wabillahi Tawfiq
    Ahlam ,,,Uk

    ReplyDelete
  2. Kwa niaba ya Madrasatul-Al-Amin napenda kuchukua fursa hii adhimu kukushukuru kaka issa michuzi pamoja na ndugu yetu Esmail kwa juhudi zenu kututangazia Maulid Nabii...Allah Izza islamu Wal-Muslimina. Jazaka Allahu Al-Kheiry.

    ReplyDelete
  3. MSWALIENI MTUME,,,,ALLAHU MASWALIA SALIMAAAAAAALEEEEEEEEE!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...