Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Abdillahi Jihad Hassan akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na maendeleo na Malengo ya wizara yake huko katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la zamani Kikwajuni kulia kwake ni Katibu Mkuu wa Wizara hio Ali Mwinyikai na kushoto ni Naibu katibu Mkuu Issa Mlingoti.
Mwenyekiti wa Kamati ya Wazazi Ali Hassan akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na suala zima la kufutiwa matokeo kwa Wanafunzi wa kidato cha nne Zanzibar kulia kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa D,C,P,M Najma M,Giga na kushoto yake ni Katibu wa kamati ya Wazazi Saleh mohd Saleh.
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakiuliza maswali katika mkutano wa Kamati ya Wazazi kuhusiana na tukio zima la kufutiwa matokeo kwa Wanafunzi wa kidato cha Nne Zanzibar.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Wazanzibar wavivu wa Masomo, wanataka kufaulu kwa kununua Mitihani badala ya kusoma.

    NECTA imefanya uamuzi sahihi kufuta matokeo baadaya kubaini uvujaji wa Mitihani.

    MASOMO YATAKA BIDII YA KUSOMA YAKHEE NA SIO KUGHUSHI MITIHANI!

    ReplyDelete
  2. Mtoa mada hapo juu wacha stihizai, mitaala ya masomo bara na visiwani ni tofauti sana hivyo kuwafanyisha mitihani sawa vijana wa sehemu hizo mbili tofauti si kuwatendea haki. Wizara ya elimu miaka michache iliyopita chini ya mh. Haroun Suleiman aliamua kuanzisha utaratibu wa mchepuo kwa vijana wa darasa la saba kuendelea Form 1 ili angalau kuendana na bara. Hata hivyo mfumo huu haujashika kasi kwa kuwa msingi wa elimu bado haujaanza kuendana na ule wa bara, waziri wa elimu wa sasa anatakiwa kuendelea pale alipoachia Mh. Haroun na inshallah Unguja na visiwani itakuwa nguvu sawa baadae.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...