Ankal Salam na pole na majukumu,
Mimi naandaika kama tahadhari kwa TFF na hii ni baada ya kuona kuwa tahadhari yangu haiwagusi ipasavyo wakuu wa TFF, nayo ni kuhusu utaratibu wa ukaaji pale Uwanja wa Taifa. Mara kadhaa nimeshuhudia na mimi mwenyewe nikiwa muhanga wa jambo hili, unakuta mtu kalipa kiasi cha fedha cha kukaa VIP B au C, cha ajabu anakuta pameshajaaa, analazimika kukaa kwenye ngazi, matokeo yake na hatari zaidi ikiwa kumetokea tatizo lolote wale wote waliokaa kwenye ngazi ndo watafanywa ngazi. Hili nilishawai mimi personaly kumueleza Rais wa TFF Leonard Tenga wakati wa mechi ya Kombe la Kagame baina ya Simba na Yanga, na nikampa business card yangu kuwa kama ana nia njema basi atanitafuta nitoe ushauri wangu.

Inatokeaje: Kuna watu wanalipa kiingilio cha kati ya Tsh 3,000/- hadi  7,000/=, wanakuja pale geti la kuingilia VIP B au C wameshika tiketi na shilingi elfu mbili mkononi, 'wanawashikisha' wale sijui ni walinzi au askari, haooo wanachoma ndani. Wewe uliyelipa kwa mfano elfu ishirini unakuta sehemu unayostahili kukaa imeshajaa, unalazimika ama kukaa katika ngazi au ukakae kule kwa aliyelipa shilingi elfu tano, wengi wanaona kuwa huu ni 'ujanja' ni kweli kiasi fulani ni 'ujanja' kwa wasio wastaarabu. 

Madhara: Madhara yake ni kuwa siku ambapo kunatokea janga kama la moto au kitu chochote, wale waliojazana VIP B na C watashindwa kuwa 'evacuated', mana kwenye ngazi kumejaa, wengine wako juu kule kwenye mabomba. Mambo haya yanatokea sana, madhara si mpaka mashabiki watwangane kama kule Misri. Sina nia mbaya na hao wanaoratibu hii michezo hivi sasa Kampuni ya Prime Time Promotion, lakini na wao walitazame hili, maana kwa heshima waliyojijengea katika kuratibu shughuli za aina hii, itakapotokea dosari na wao itawachafulia jina, haipendezi unamuuliza mmoja wa watendaji wao kuwa nikae wapi na sehemu imejaa, unaambiwa 'oohoo kaka yangu kuna watu wamekuja toka saa nne asubuhi' hivi kweli huna kazi uje kuwahi kiti saa nne asubuhi zama hizi? 

Ipo haja ya watu wenyewe kuwa wastaarabu lakini kwa kuwa wapo wanaotumia nafasi hiyo kujinufaisha uwekwe utaratibu ambao aliyelipia Tsh 20,000/= akae panapomstahili, na wa Tsh 5,000/= vivyo hivyo akae panapomstahili nk. Vinginevyo wastaarabu wengi wataacha kwenda mpirani.
Mdau- Mtu ni Utu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Shukran sana mdau kwa kuliona hili,nilidhani niko peke yangu,nimejaribu sana kuwasiliana na watu wa media walipigie kelele hili lakini naona kimya.Tatizo hapa ni RUSHWA tu,hakuna kingine,askari wanaokaa pale geti la VIP B Na C ndiyo wanafanya kuwa mtaji wao wa maisha.Tena kuna wengine wakiona unaingia wanafanya kukuita ili uwadakishe then uingie.Siku likiibuka la kuibuka ndiyo wakubwa wataamka na kutoa matamko yao maana hapa TZ viongozi wanaonekana wakali likitokea jambo la kuwachafua.MUNGU AEPUSIE MBALA MADHARA ULIYOTAJA

    ReplyDelete
  2. nyinyi kwa nini mlipe 20000 kila siku wakati mnajua hamtakaa huko VIP lipeni hio buku tatu harafu mkae kwenye hizo gazi kama mlivyokua mkikalshwa siku zote, then kunakua hakuna malalamiko tena maisha yenyewe yako wapi serikali yenyewe haina utaratibu tenga hana utaratibu mpaka kwenye familia yake sasa unategemea ataweka utaratibu kwa ajili yako achakujipa stress bana.

    ReplyDelete
  3. Mdau nakubaliana na wewe ni kitu cha kushangaza sana hasa wanaokaa kwenye mageti kuwa wababaishaji;unamruhusu vipi mtu mwenye teiketi isiyo ya mahala pake akakae pale.

    TFF msiwe wababaishaji jaribuni krekebisha hili ili watu wapende kwenda mpirani

    ReplyDelete
  4. hivi suala la uwanja ni la TFF?

    ReplyDelete
  5. Wadau wa soka
    Mkitaka hili la kuchakuchua liishie ni ticket ziwe zinawekwa namba hapo kila kitu kitakua sawa lazima tubadilike tuweke utaratibu wetu wenyewe kwamfano ticket za VIPB R1K1 maana yake ni kuwa ticket yako ni vip b row ya kwanza kiti namba 1 hapo kutakuwa na wepesi kwasababu namba yako ya ticket itakuwa sahihi yaani hapon unaweza hata uza ticketi za msimu..

    Pili hao tff wenyewe ni njaa kabisa unaweza kuta wanauza ticket mara mbili mbili

    ReplyDelete
  6. Wadau wenzangu wa mpira wa miguu hasas mnaotumia uwanja wa mpira nawapa pole na pongezi. mimi nilishajitoa siku kwenda national. mdau wa kwanza umeeleza vizuri sana na umechukua hatua kama mtanzania mwenzetu mwenye ufahamu na moyo wakutusaidia. kwanza napenda kuwaarifu kuwa ajali kutokea na kutokuwa katika hali ya kujiandaa sio swala la mungu. mimi naona kumlaumu Tenga kuhusu 'hongo' tunakosea sana...ingawaje mdau wa kwanza sawa kabisa kwani Tenga alikudharau na uzembe unaendelea. Hongo kwa nchi hii ni kitu kimekuwa sehemu ya maiisha au kugawiana hela. nitajie mahali ambapo wafanyakazi hawajaribu kwa njia zote ili wapate hela ya zaidi kwa kupata hongo?? polisi, hospital, car park, petrol stations, mashuleni, vyuoni, airport, muhimbili. UCHAGUZI,..hata ukimhamisha Tenga hongo itaendelea pale pale,..sasa niambie kwanini askari wa uwanja wa mpira wao wasichukue hongo????.. hapa ushauri wangu ni kuwa kama kuna mtu anajiona anachukia hongo...ajitokeze kupiga kura ya kupinga hongo...change the leadership.

    ReplyDelete
  7. SASA MTOA MADA WEWE UNASEMA UMEWAHI HATA KUMFAHAMISHA KITU HIKI RAIS WA TFF LEONARD TENGA ! NAONA KAMA UNACHEKESHA WATANZANIA WALIOKUWA THEATER KUONA MCHEZO WA KUIGIZA. HUYO MWENYEWE TENGA NDIO MOST CORRUPTED PERSON KATIKA JAMII YA HIVI SASA TANZANIA , NI KAMA VILE MSEMO USEMAO :KESI YA NYANI UKAMSHITAKIE TUMBILI, KWELI SI ATAKUONA KAMA UNA WAZIMU?

    ReplyDelete
  8. Wadau hata mimi hili suala nimektana nalo mara nyingi, I think soln kama alivyoandika mdau tupate seat number. kama nimekata ticketi hata nikienda kipindi cha pili nitakuta kiti changu kiko wazi.

    ReplyDelete
  9. Mdau mtoa mada, na wengi mliochangia kuna jambo hamuelewi kuwa TFF wanafumbia macho swala hilo, ili wachakachue na kutangaza figure yeyote, na mnajikuta hamna chakubisha.Viti vikipewa namba, na tiketi zikipewa namba, inamaanisha hawatoweza kuiba.

    Tenga yupo pale na wenzie kwajili yao binafsi kujineemesha lakini siyo kwa maendeleo ya soka nchini. Pia hata hayo mapato ya getini yana makato kibao, mara drfa, mara frat, tff, bmt, uwanja n.k matoke yake timu zinaambulia kiduchu na wachezaji waliyo vuja jasho ndiyo ndogo kabisaaaa. Kwa hali hii nani atataka mwanaye acheze soka kama hanufaiki?

    1. Nataka watanzania tuelimishwe, hizo 2.1milion wanazolipwa wachina kila mechi ni kwa ajili gani?
    2. Kwanini hadi leo uwanja haujamaliziwa na kukabidhiwa rasmi?
    3. Kwanini wadhamini wa ligi kama VodaCom wasifanye mikataba na vilabu moja kwa moja bila ya TFF kuwa mtu kati, yaani tff kuwa agent?
    4. Kwanini wachezaji waliochezea Taifa Stars hadi idadi fulani za mechi (caps) wasipewe upendeleo maalumu wa kadi za kuingia uwanja wa taifa bure? Na kila mechi ya ligi au/na taifa stars zinapochezwa 2% ya kiingilio iende kwenye mfuko wa bima ya afya kwa ajili ya wachezaji hao na familia zao?
    5. Kwanini uwanja wa taifa hadi leo hauna CCTV camera kwaajili ya usalama? Na hata waliong'oa viti picha zinge
    Kibanga Msese

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...