Eneo la mbele la Jengo la Utawala la Chuo cha Elimu ya Biashara kampasi ya Dar es salaam. Chuo hicho kimeanzisha sera ya mavazi kwa wanafunzi wawapo chuoni hapo ambayo imeanza kutumika rasmi kwa kuwataka kuvaa mavazi ya heshima na wale wanaokaidi kuchuliwa hatua za kinidhamu.
 Kaimu mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam Bw. Athman Ally Ahmed akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu kuanza kutumika kwa sera ya mavazi chuoni hapo yenye lengo kupiga vita mavazi yasiyo ya heshima kufuatia kukithiri kwa vitendo vya uvaaji wa mavazi yasiyokuwa na staha vinavyofanywa na wanafunzi  

Baadhi ya wanafunzi wa la Chuo cha Elimu ya Biashara kampasi ya Dar es salaam wakiwa darasani. Picha na Habari na Aron Msigwa -MAELEZO
Uongozi wa Chuo cha elimu ya biashara (CBE) kampasi ya Dar es salaam umesema kuwa hautasita kumchukulia hatua mwanafunzi au mfanyakazi  yeyote atakayefika chuoni hapo akiwa amevaa mavazi yasiyo ya heshima huku ukitoa wito kwa wananchi kuunga mkono kampeni hiyo yenye manufaa katika kujenga taifa lenye maadili mazuri.
Akizugumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Kaimu mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam Bw. Athman Ally Ahmed amesema chuo hicho kimefikia uamuzi huo kufuatia kukithiri kwa vitendo vya uvaaji wa mavazi yasiyokuwa na staha vinavyofanywa na wanafunzi  wa kike na wale wa kiume wawapo chuoni hapo hali inayosababisha udhalilishaji wa utu wa wanafunzi ndani na nje ya chuo.
Amesema wanafunzi ambao wengi wao ni vijana chuoni hapo wamekuwa mstari wa mbele katika kuiga kila aina ya vazi kutoka tamaduni za watu wa magharibi hali ambayo ameielezea kuwa ni ukiukaji wa mila , desturi na tamaduni za mtanzania .
“Mtindo huu wa kuiga tamaduni za magharibi pasipokuangalia wapi tunakwenda haukubaliki hata kidogo,ukiangalia katika vyuo vingi vya elimu hapa nchini wanafunzi wamekuwa wakivaa mavazi ya ajabu na yasiyofaa kabisa katika maeneo ya chuo” amesema.
Amesema kuwa Chuo hicho  kimekaa na kubuni sera  ili kuyaondoa mavazi ambayo hayaruhusiwi kuvaliwa katika maeneo ya chuo  na kubuni sera ya mavazi kwa ajili ya wanafunzi  hali itakayowajengea  nidhamu wasomi  hao  wa fani mbalimbali pindi watakapomaliza masomo yao chuoni hapo.
Amefafanua kuwa  adhabu mbalimbali zitatolewa kwa wanafunzi watakaokiuka agizo la uvaaji wa mavazi yenye heshima amabazo ni pamoja na kuzuiliwa kupita getini kwa mwanafunzi husika kuingia katika eneo la chuo kwa wale wanaotoka nje ya hosteli na wale wanaoishi ndani ya eneo la chuo hawatapewa huduma yoyote kama vile kuingia darasani,kantini , maktaba au ofisi yoyote ya chuo.
Aidha amefafanua kuwa wanafunzi  ambao  hawatakua  tayari kufuata utaratibu huo watafikishwa mbele ya kamati ya nidhamu huku akibainisha kuwa adhabu itakayotolewa ni mwanafunzi kusimamishwa  chuo kwa  muda wa miezi mitatu.
Kwa upande wake makamu mkuu wa chuo hicho ambaye pia ni mkurugenzi wa mafunzo Bi. Bertha Kipillimba amesisitiza kuwa zoezi hilo litawahusu wafanyakazi wote wa kampasi ya Dar es salaam na wanafunzi  zaidi ya 6000 wa chuo hicho.
Amesema hivi sasa taratibu hizo za uvaaji wa mavazi yenye staha zimeingizwa kwenye kanuni za chuo  na kuongezwa kwenye masharti ya fomu za kujiunga na chuo hicho huku akifafanua kuwa tayari wametoa kipindi cha wiki mbili kwa utekelezwaji wa kanuni hizo na watakaokiuka kuadhibiwa kwa mujibu wa kanuni hizo.
Naye mlezi wa wanafunzi wa hicho (Dean of Students) Bw. Faustin China amefafanua kuwa umefika wakati wa wanafunzi hao kujitambua huku akisisitiza kuwa kwa muda mrefu wamekuwa wakinyoshewa vidole na jamii kuhusu suala la uvaaji na mienendo ya wanafunzi chuoni hapo.
“Tumesemwa vibaya kwa muda mrefu hatuwezi kuachia suala hili likaendelea, tunataka wanafunzi wetu wavae vizuri kwa mujibu wa kanuni tulizojiwekea ili kujenga heshima ya chuo” amesema.
Kwa upande wao baadhi ya wanafunzi wamekuwa na maoni tofauti kuhusiana na uanzishawaji wa sera ya mavazi chuoni hapo wakieleza kuwa inaingilia uhuru wao wa kuamua huku wengine wakiupongeza uongozi wa chuo hicho kwa kuliona suala hilo na kulichukulia hatua ili kuleta na kulinda heshima ya chuo hicho.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 40 mpaka sasa

  1. safi sana. natamani na vyuo vingine vifuate hiyo sera............. ukweli wanafunzi wanajidhalilisha sana na mavazi yao, mimi wananiudhi sana. ina maana ukivaa kistaarabu hutaelewa? au ndo kujitafutia degree bila kutumia msuli?

    ReplyDelete
  2. SAWA KABISAAAAAA MM NAUNGA MKONO 10000%

    ReplyDelete
  3. How do you enforce this? Vazi lenye staha litathibitishwa na nani?Linaweza kumridhisha dean of students; ukifika kwa makamu mkuu wa chuo anamwambia mwanafunzi kuwa vazi halifai. Uniform ndio njia pekee ya kukabili tatizo kama hili;lakini huwezi kuanza kuwaambia watu wazima waliotoka makazini waanze kuvaa sare.Hii italeta taabu kidogo;kwani kitakachoonekana sawa kwa mmoja;kinaweza kikawa hakifai kwa mwingine.Nadhani si vibaya jamii ikaelimishwa;ila ktk hili;kutakuwa na taabu kidogo.

    ReplyDelete
  4. Adhabu ya miezi mitatu!!!! Hii ni kwa wafanyakazi tu, wanafunzi tu, au wote kwa pamoja???? Maana nijuavyo mimi mwaka wa masomo kwa vyuo vya elimu ya juu vimegawanyika kwa 'terms' au 'semesters'. Na mwanafunzi kuweza kufanya mtihani mwa mwisho wa semester inatakiwa awe amehudhuria 'lectures' kwa somo husika kwa asilimia kuanzia 80%. Muda wa kufundisha kwa Semester moja ni takribani wiki 15, sawa na miezi mitatu na kitu. Sasa huyo mwanafunzi atakayesimamishwa kwa miezi mitatu itakuwaje? Mimi nadhani adhabu ibadilishwe, badala ya adhabu ya miezi mitatu iwe adhabu ya mwaka mzima wa masomo.

    ReplyDelete
  5. anon wa tatu, tunaposema nguo isiyofaa ina maana moja kwa kila mtu, labda asiyefaa mwenzake

    ReplyDelete
  6. Fanyeni hivi na kwa wanamuzika kurudisha culture ya Africa,

    ReplyDelete
  7. Big up! Hii 'policy' iwekwe kwa vyuo vyote. Maana mimi nimewahi kuwa mhadhiri wa chuo fulani, kwa kweli wahadhiri wa kiume tunapata vishawishi sana toka kwa wanafunzi wa kike wasiopenda kujisomea, na wanaotaka kutumia uzuri wao kupata vyeti kirahisi. Wakati mwingine mdada unaingia ofisini kujieleza kwa nini umefeli, huku umevaa kimini, tena trasparent, chenye kujimwaga kidogo. Kinarembua macho, mara kinajifanya kudondosha kalamu, kikiinama kuiokota, kimini kinapeperukia mgongoni, unaona mpaka 'chupi' kama ukibahatika akawa ameivaa. Maana kwa Dar es Salaam, sababu ya joto, kuna wasichana ambao hawajui hata bei ya chupi.

    Ila sasa naungana na mchangiaji wa Wed Mar 28, 09:27 PM, kuwa muda wa adhabu inawezekana, uongozi umekurupuka. Maana miezi mitatu haiwezekani, kutokana na taratibu za chuo, hasahasa NACTE, maana najua wazi kuwa CBE iko chini ya NACTE. Adhabu inayowezekana kwa mwanafunzi kusimamishwa ni mwaka mzima wa masomo.

    Pia vyuo vingine viige mfano huu wa CBE. Ili kukwepa hao watoto KUTEGA wauume za watu. Najua sheria inawahusu hata wavulana, lakini najua walengwa ni wasichana, maana wao ndo mavazi yao yanatosha.

    BIG UP 'CBE'

    ReplyDelete
  8. unajua mie watanzania wananifurahisha sana.leo hii unapokataza mavazi na kusema si ya maadili kwa dunia ipi?basi watembee barabarani kubadilisha watu pia.chuoni kuna watu wazima wanajua wanachokifanya na si watoto kwamba uwafundishe wavaaje. kikubwa ni kuboresha ufundishaji coz at the end of the day kufaulu kwa mwanafunzi si mavazi

    ReplyDelete
  9. This is right, hii siyo shule but college ni watu wazima and they have a right to wear whatever they choose as long as sheria za nchi hazijavunjwa. Nawashauri hizo sheria wawapelekee watoto wa shule maana pale CBE ni mijimama na mijibaba inayoishi life yao japo kuna viserengeti vilevile. Leave them alone period ulokole na ujahidina ni huko huko maana Tanzania is secular state. Asanteni

    ReplyDelete
  10. Watanzania waliowengi hawajui nini wanachokifanya wengine wanaiga nguo wanazovaa akina Rihana barabarani basi wao wakiona kwenye Tv wanafikiri zinavaliwa tu kila mahali mbona hao wazungu tunasoma nao huku madarasani hakuna upuuzi kama huo msijifanye kuwatetea na nyinyi ndio wale wale mnaposema dunia ya leo dunia ya wapi? kuna vyuo huku ukishaingia chuoni sijui umevaa kofia au upuuzi wanakutimua msitake kupotosha watu nyie wachangiaji wa juu hapo mnaotetea watanzania mnajifanya kujua saana kumbe wengi watujui ni maneno maneno tu njoo huko mnakowaiga halafu uone kama darasani wanavaa huo upuuzi

    ReplyDelete
  11. VIZURI SANA !!!!!!!


    MKUU WA CHUO BW. ATHMAN ALLY AHMED UNASTAHILI PONGEZI KWA MSIMAMO WAKO HUU NA NI MUHIMU UUNGWE MKONO KWA NGUVU ZOTE::::::::::::::::::::

    SASA BASI IMETOSHA, KILICHOBAKI NI MASOMO KWA BIDII NA HESHIMA !

    HAIWEZEKANI CHUO MUHIMU SANA KWA TAALUMA KIWE KAMA KILABU CHA STAREHE ZA USIKU( NIGHT CLUB)!

    HAINGIII AKILINI MAMENEJA,WAHASIBU,MAOFISA, MAKARANI NA WAKAGUZI WA MAHESABU WA BAADAE WATOKEE KTK KILABU CHA USIKU KAMA ILIVYO CBE KWA SASA !

    ITAKUWA NI AIBU KUBWA KUFAHAMU KUWA MWANA TAALUMA MAHIRI KABISA BAADAE ALITOKEA CBE KWA MUONEKANO WAKE WA SASA KULINGANA NA MIENENDO NA HULKA YA MAVAZI YA WANAFUNZI WAKE !

    TUJARIBU KUANGALIA HADI SASA CHUO KIMEZALISHA WATU MAHIRI SANA AMBAO WANAITUMIKIA NCHI KTK SEKTA MBALI MBALI HIVYO HATUWEZI KIKIACHA CHUO KIUZWE KWA BEI YA MKOPO WA HASARA KUTOKANA NA WAKOROFI WACHACHE WANAFUNZI !

    ReplyDelete
  12. Assalama Leko zako Mkuu wa Chuo Bw. Athuman Ally Ahmed,

    Kweli kazi umeifanya hapo CBE kwa kuwa kama wewe ni Rijali kamili uwe mpita njia tu au mwanafunzi au Mwalimu huwezi kusoma au kudumu ktk mazingira haya huku unastarehe kwa macho kuona 'nusu uchi' na 'mikao ya kihasara hasara' hasa kwa Mabinti !

    ReplyDelete
  13. Shibe na afya vina mchezo ?

    Hata ukipewa kazi ya Kufundisha ewe Mwanaume ukiwa na afya na shibe zako kamili huku senti haikupigi chenga hapo CBE utapata Mtihani kwa Mabinti unaweza yakakukuta yale yale wa Babu Seya !

    ReplyDelete
  14. Yaliyowahi kumkuta mwaka 1988-89Fundi Cherehani wa Shule ya Msingi Mtendeni Dar Es Salaam Bw. ATHUMANI MAUMBA yanatokana na mkao wa 'kihasara hasara' wa Wanafunzi wa KIKE !

    Kwa Mwanaume aliye kamili ni vigumu kustahamili kashi kashi za Mabinti au Wanafunzi wa Kike wakorofi hasa ktk mwenendo wao na mavazi !

    ReplyDelete
  15. Zaidi zaidi walengwa ni Mabinti Wanafunzi CBE ni muhimu waelewe kuwa Masomo kwanza halafu Mapenzi baadae baada ya Kuhitimu Masomo !

    ReplyDelete
  16. Jamani zoo ikifungwa tutaenda wapi sie maana tulikua tukienda hapo kupata burudani ya macho!

    ReplyDelete
  17. Hawa Wanafunzi wa Kike pale CBE kwa mavazi yao ya kihuni wanawaadhibu watu wengi sana Wanaume kamili hata wapita njia wakiwa kwa miguu au ktk magari njiani Barabara ya Bibi Titi/ Ally Hassan Mwinyi!

    ReplyDelete
  18. tupo kwenye utandawazi kila mtu ana haki ya kuvaa atakavyo ili mradi asimbuguzi mtu. wanaume mnapata vishawishi kwani kipi msichokijua? zamani kabla ya ukoloni watu walikuwa hawavai nguo lakini ubakaji haukuwepo ilikuwaje? Dunia inabadilika inabidi watu wabadilike sio kurdi kwenye ujima. Wazungu wanavaa vichupi mmeshasikia wanabakana?

    ReplyDelete
  19. Big up!Anonymous Thu Mar 29, 08:13:00 AM 2012. Wape ukweli. Namimi naongezea kama ni uhuru wa mtu basi kubalini na ukamiruni ili muolewe.

    ReplyDelete
  20. Ni kweli kabisa, huku ugaibuni hakuna kabisa mwanafunzi anayevaa upuuzi mnaovaa huko Bongo. Wanafunzi wanavaa nguo nzuri tena za heshima sana, kwa ajili ya baridi tunavaa suruali lakini sio kama vijisuruali mnavyovaa huko, sasa jamani sijui mnaiga wapi upuuzi huo. Huku bwana huwezi ukaingia darasani umevaa nguo maziwa yanachungulia nje au vichipi mbele za malecturer au watumishi wengine hapa chuoni,jamani badirikeni,lindeni utamaduni wetu,juweni vazi gani linatakiwa kuvaliwa kwa wakati gani sio vazi la ufukweni linavaliwa darasani. Kweli huo uongozi wa CBE nawapongeza sana tena sana, naomba hata chuo kikuu cha Dar es Salaam sehemu ya mlimani kiige mfano huo maana huko ndio kuna uozo mkubwa katika uvaaji hasa wasichana. Prof.Mukandala angalia mavazi ya wanachuo wako wape sheria nao wabadilike tujenge kizazi sasa chenye maadili tukianzia katika mavazi na elimu kwa ujumla.

    ReplyDelete
  21. wanaotetea nadhani hawajui maana ya dress code hata kama ni watu wazima ni lazima wajue vazi gani livaliwe wapi, kuna nchi moja ughaibuni nilikwenda disco nilistaajabu kuwa eti watu hawaruhusiwi kuvaa neekers huku tumezoea rabamotonin Jeans na kama ni jeans basi iwe ni nyeusi sasa hebu fikiria hapo ni disco na mwenye umri chini ya 18 haruhusiwi, si watu wazima hao mbona kuna masharti? askari wa kizungu kagoma samahani haturuhusu uvaaji huu tulikua wa3 ilibidi wote tuondoke. sasa kwa wanotetea watu wazima waje basi wamevaa chupi kichwani nasi tuone sawa.

    ReplyDelete
  22. Chuo cha mipango Dodoma wanaifanya hii, huruhusiwi suruali kabisaa, unarudishiwa getini na sketi lazima ivuke magoti.. afadhali maana tulikuwa tunadhalilika sana, unamtizama msichana nguo alovaa unaona aibu wewe.

    ReplyDelete
  23. kuwa na viwango kwa kila chuo ndo heshma yake.mimi nawapongeza sana CBE ,kwani huo ni ujasiri wa kutosha. Kuna vyuo nje ya nchi uko uataratibu uingii darasani kama hujavaa tai kwa wanaume,na wanawake pia hgo zenye staha km vile suruali na blauzi zinazofunika sehemu tamnishi.CBEwwww wasikatishwe na waosha vinywa ,kazeni puti,mnakamua jipu watapona tu.BG UP!

    ReplyDelete
  24. Haki ya kuchagua vazi gani uvae kwa wanafunzi "wakubwa" iko pale pale: Vaa utakavyo ila mavazi yako yasiwe kero au kishawishi kwa wengine (Distraction to cocentartion)Kumbuka CBE ni mahala pa elimu!nani ataamua vazi la "Staha"? Ni jamii na wewe mwenyewe.Bahati nzuri ipo miongozo kwa jambo hili. Nimesoma Chuo Kikuu UK nawahakikishia wanavaa nguo za staha. Hii ni pamoja na wafanyakazi: Secretaries kwa mfano ni lazima wavae blouse nyeupe na skirt nyeusi ndefu na si vinginevyo.
    Anonymous

    ReplyDelete
  25. Naupongeza uongozi wa Chuo kwa angalau kuonyesha nia ya kuchukua hatua.

    Chuo ni mahala pa heshima na tunategemea wanaokwenda hapo wanakwenda kuchukua utaalamu ili wachukue nafasi mbalimbali katika jamii yetu.

    Kama ni shida ya kwenda kuonyesha mavazi basi tafuta mahali pake na kama ni shida ya kutangaza biashara zako tafuta sehemu muafaka.

    Hongera Kwa uongozi wa chuo. Nategenea na vyuo vingine wataiga.

    ReplyDelete
  26. ACHENI USHAMBA WA MIKA YA KINA KAWAWA NA NGUO FUPI ! HAYO MAMBO YALIISHWA PITA SANA ZAMANI. KITU GANI CHA AJABU KWEA MSICHANA ASIVAE NGUO ZINAZOMFURAHISHA MOYO ? KAMA HAMTAKI NENDENI KWA HAO DISIGNERS WA NGUO MUWAAMBIWE WASITOE NGUO KAMA HIZO HIO NDIO ITAKUWA MWISHO NA KAMA DUNIA ITAKUPENI SUPPORT, LAKINIO ULIMWENGU WOTE WATAKUONENI KAMA MNA WAZIMU ETI WATU WASIVAE SEX HUO NI UAFRIKA ULIOKITHIRI NA HAUJAENDA SHULE. WAKATI WENGINE WANAENDELEA NINYI MNATAKA KURUDISHA MAENDELEO NYUMA ,KAMA HAMTAKI BASI NENDENI MKAISHI SAUDI ARABIA NDIO ROHO ZENU ZITULIE SWAIN WAKUBWA. NYIE KAMA WEWE MUISLAM USIVAE WALA HULAZIMISHWI. KITU GANI CHA AJABU HAPO ? HAO SIO WATOTO WADOGO NI WANAWAKE WANAAKILI ZAO BILA HIVYO WATAMPATA MWANAUME GANI DUNIA HII KAMA HAWANA MVUTO?

    HIO MIAKA YA KINA NYERERE NA OPARATION NGUO FUPI ZIISHWA PITA!!!!!

    MDAU MBEZI BEACH

    ReplyDelete
  27. Sasa hao kina Rihanna sio watu au sisi watanzania tuna ubora gani zaidi ya kina Rihanna au Beyonce? Au ni njaa ndio inatusumbua mpaka tumechanganyikiwa? Hawana njaa wale kama wasipoiigwa nani atawaiga ? Tukumbuke wao ni RAW MODE lazima watu wataiga, muziki ,mavazi,nastyle zote zitazokuja duniani. sasa wakivaa hivyo ndio wameua watu?

    VAENI VILEMBA BASI NA KANZU KAMA WAARABU WA YEMEN BASI,AU SAUDIA KAMA WAO NDIO MMEWAONA WANAVAA VUZURI NA POMBE IKATAZWE TANZANIA KWA SABABU NI HARAM shenzitaip

    ReplyDelete
  28. They should spend this effort and resources on improving the quality of education provided, not on such quick fix "look at me now" kinda policies. I don't think whosoever thought of such a policy really sat down and thought this through. I mean seriously we live in a world were the media is constantly bombarding us with messages of freedom of choice and all the rest of it, and yet somehow some guy in his office thinks grown ups in his institutions will follow such a useless policy. I pray to God that we start concentrating on things that really matter. I mean in the end, what a person wears is a PERSONAL choice (Well unless one is in PRISON. Or are they?)

    ReplyDelete
  29. Hayo mavazi ya kutega yana mahali pale. Kama weekend unatoka kuelekea 'beach' sawa. Au usiku unaenda 'club' pia sawa. Au uko nyumbani kwako na mwenzi wako, hivyo unataka kum-attract ili mrushane roho sawa. Lakini si mavazi ya kuvaa hadharani, hasahasa mahali kama vyuoni, au maofisini.

    Lakini pia ni vigumu kufuatilia uvaazi wa mavazi ya heshima, maana 'mavazi ya heshima' ndo nini? Vazi unaloliona wewe kuwa ni la heshima, mimi naweza kuliona silo. Muhimu ni kuweka utaratibu wa 'uniform', au kama si uniform, sheria iseme aina ya material, pamoja na size ya vazi linalotakiwa.

    ReplyDelete
  30. Big up CBE hata wanafunzi wenyewe wanakwazika kwa jinsi wengine wanavyovaa. Habari ndiyo hiyo kama unataka kukaa uchi huko huko mitaani sio eneo la watu wanapochukua taaluma period.

    ReplyDelete
  31. JAMANI TUACHE UTANI KWELI HIVYO VUO MTU ANAENDA NA TRANSPARENT CLOTHES?

    ReplyDelete
  32. Anon wa pili nguo isiyofaa ukiiona tu hutajiuliza mara 2, iko wazi kabisa. Kadhalika inayofaa inafaa mbele ya macho ya wote.

    ReplyDelete
  33. Masomo hayawezi kupanda kwa kutegwa kwa MATAMANIO !

    Iwe Mwanamke au Mwanaume :

    MFANO:

    1.Matamanio kwa Mwanamke:::::::
    Kama kijana Mvualana akivaa fulana au shati inabana kifua wazi 'bustani ya mahaba' nje nje inaonekana kifuani,,,mwanamke hajategeka hapa?

    Au kijana amevaa Suruali imebana sana hadi 'silaha' yake kiunoni inaonekana japo ipo ndani ya suruali mfano ikipata msisimko utunaji wake haumshitui Mwanamke kweli ?

    2.Matamanio kwa Mwanaume:::::::
    Haya ni mengi mno kwa jinsi Ma binti wanavyowatega Wanaume hapo CBE kwa waliowahi kufika pale wanajua...

    -Mabinti wamefikia pabaya hawavai nguo za ndani, je ni vipi hapa ?

    -Mabinti wanatongoza watu kwa macho 'wanarembua macho' vipi hapa?

    -Hali ni mbaya je hakuna ushawishi watu na akili zao wakahujumiwa ?

    ReplyDelete
  34. Pana tofatui kati ya TAASISI YA MASOMO KAMA C.B.E na KLABU YA USIKU !!!

    ReplyDelete
  35. Walianza St. Augustine Mwanza na sasa CBE naomba Mungu na Muhimbili nao wapige marufuku, mtu anavaa skin tight darasani anakuja na wodini kwa mafunzo kwa vitendo kisa kwenda na wakati, wakati gani huo. Chuo cha Diplomasia Kurasini ni marufuku na unapojiunga tu unapewa muongozo wa dress code, na walinzi getini ndo wa kwanza kukurudisha kama umevaa nguo zako za mitego. SAFI SANA

    ReplyDelete
  36. inaonyesha ni jinsi gani watanzania tunawaza ngono zaidi kuliko mambo mengine. hao wanaume wanaosema wanategwa kwani wana mioyo ya namna gani,cant u control urself? wachangiaji wengi wanasema eti wanashindwa kuvumilia wanategwa sana na kina dada,kweli kama mtu mzima unawaza mambo muhimu na ya maendeleo na si ngono muda mwingi vazi halikuchanganyi hata kidogo.leo hii hao wanafunzi wakavalishwa kama wanavyotaka inawafaidisha nini kama elimu ndo inazidi kudorora au madai yao kiwango cha ufaulu kitaongezeka? jamani watanzania hebu tuamke na tuwe na mawazo endelevu na si kuwaza kuwavalisha watu ili hali elimu inazidi kudorora na tuna mambo mengi muhimu ya kutilia maanani na mkazo

    ReplyDelete
  37. NAFIKIRI WANAOSEMA KUVAA NUSU UCHI NI KWENDA NA WAKATI WANAKOSEA KWANI HAWAJASEMA NI WAKATI GANI TUNAOENDA NAO. ULE WA ZAMANI AMBAPO WATU WALIKUWA HAWAVAI NGUO AMA WALIKUWA WANAVAA VINGOZI TU VYA KUFUNIKA SEHEMU ZA SIRI AU MNAONGELEA WAKATI HUU AMBAPO MAVAZI YA HESHIMA YAMESHAPATIKANA? KAMA MNAONGELEA WAKATI HUU BASI MJUE KUVAA NUSU UCHI NDO MNATURUDISHA ENZI ZA UJIMA AMBAPO WATU WALIVAA VILE KWA SABABU KULIKUWA HAKUNA VIWANDA VYA NGUO.

    ReplyDelete
  38. Acheni kina dada wakae uchi kadiri watakavyo. Maisha ni magumu. Kukaa uchi ni njia mojawapo ya kuwavuta wenye tamaa ili waachie pesa walizo nazo. BIG UP MADADA KUKAA UCHI!

    CBE mmechemsha sana.

    ReplyDelete
  39. KUKAA UCHI NI KUTANGAZA BIASHARA. malaya ndo wanakaa uchi ili watamaniwe na wapate wateja wengi. Mtu mwenye staha zake hawezi kuvaa nguo za uchi.

    ReplyDelete
  40. hizo nguo fup zao wavae wakiwa wanaenda kwa mabwana zao na ndio maana kuna hadi nguo za kulalia kwann hawaji na night dress darasan wanakuja na vimin?

    muda unafika wavulana turuhusiwe tuwe tunawavua nina uhakika wataacha huu upuuzi wao

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...