NDUGU MICHUZI NAKUOMBA UNIWEKEE HILI LIFUATALO KUSUDI WADAU WA BLOG YETU PENDWA WAPATE KUNISHAURI.
MIMI NIMEFANIKIWA KUPATA UFADHILI WA KWENDA KUSOMA NCHINI ITALIA SHAHADA YA KWANZA (FIRST DEGREE). NDUGU WADAU NI SOME MASOMO GANI HUKO ITALIA AMBAYO MITAALA YAKE INASHABIHIANA NA YA KWETU? {MFANO NILITAMANI SHERIA, WENGI WAKASEMA SISI HAPA TZ TUNATUMIA MFUMO WA KIINGEREZA AMBAO NI TOFAUTI NA WAKIITALIANO}.
SHAHADA YA PILI (MASTERS) NATEGEMEA KUSOMA HAPA NYUMBANI; SITOPENDA NITAKAPORUDI HAPA NIAMBIWE NIMESOMA KITU TOFAUTI NA HAPA.
WADAU NISAIDIENI MDOGO WENU KWANI NAKARIBIA KUONDOKA KUELEKEA HUKO.
MTANZANIA MWENZENU
DAR ES SALAAM
somea mapishi, yako sawa huko na hapa.
ReplyDeleteform six mzima hujui kuangalia mbele.
unafikiri hawa wabongo walioko italia wamesoma.
Acha uzushi kwani wakati unaomba ulipanga ukasome nini?Ungeomba ushauri kabla ya kuomba.
ReplyDeleteHongera kwa kupata scholarship, huko Italy waweza soma journalism ambayo internationally misingi haitofautiani kuliko sheria itakusumbua kidogo. Fani ya journalism nchini bado inakua taratibu kwahyo hutotaabika sana kupata kazi. Kama chaguo lako moyoni ni sheria waweza isoma hapo baadae hata Tanzania kikubwa ni nia tu pia huwezi jua hao waliokupatai scholarship bdae unaweza kuwaomba scholarship ya masters ufanye media law. Kila lakheri
ReplyDeleteSafi sana kwa kuwa na mwamko wa kusoma hasa nje ya nchi. Kiukweli sidhani kusoma sheria nje ya nchi ni vizuri, hapana kabisa. Sababu moja ni kwamba kama unataka kuja kufanya kazi Tz we tafuta chuo hapahapa nyumbani kwani kuna vyuo vingi vinatoa degree ya sheria. Ila unaweza soma mambo ya International Relations hata nje ya nchi na ukawin. Please usikimbilie nje kumbuka kuna TCU.
ReplyDeleteGoodluck...
Mdau hapo juu si amesema alitaka kusoma sheria ila amaembiwa itakula kwake akirudi nyumbani. Wewe ndo inaonyesha hujaenda shule unashindwa hata kusoma meseji na kuelewa. Mimi sina cha kukushauri mdogo wangu. Ngoja waje wadau wengine
ReplyDeleteAma bingo dogo, ufadhili bila kujua usomacho? Ngoja waitaliano waje wakushauri wengine born here die here...
ReplyDeletekijana hujasema a-level ulisomea masomo gani. jee ulisomea sayansi? au sanaa? masomo yako ya a-level ndio yatakayoamua ni kozi gani uchukue. lkn nachukulia umesomea sayansi na hivyo kukushauri kama ifuatavyo:
ReplyDeletesoma uhasibu ndugu. dunia nzima uhasibu upo sawa hakuna cha italy wala marekani wala uingereza. masuala ya kifedha ni sawa tu.
pia unaweza kusomea udaktari ambao pia dunia nzima ni sawa bila ya kujali nchi na nchi.
Hiyo University unayokwenda wanaoffer masomo gani kwanza? Somea Human Resource ambayo itakupa uwezo wakujiendeleza kusomea Masters ya sheria baadaye.
ReplyDeletesoma technology iwe coz yeyote ya Tech.
ReplyDeleteEwe Kijana kasome pale Tursia University, Viterbo. Ukisomea hapa Engeniere (Engineering) au Forestale miaka Minne unapewa Degree ya Udokta au Dr. Italy Economia husomewa kwa Kiingerezakwa mfumo wa UK nayo poa. Kwa mtanao wa sasa utakubalika kufanya kazi za Kimataifa au hukohuko kama Dr. Tanzania ukirudi wameze wateme utakubalika kwenye Ma NGOS nk. Ciao e Auguri. Richardo Mazingira
ReplyDeletemmmmh we umemaliza f6 kweli? hujui whats happening now? then hujasema una combination gani ya masomo,kasome wildife management haina tofauti dunia nzima
ReplyDeletesoma udakitari. utapeta sana sana popote pale!!!!
ReplyDeletewewe shule ni interest yako, ukiambiwa ufanye Engineering utaweza!! unasomea kitu ambacho una interest nacho na unaweza kuperfom vizuri, sio unauliza nisome nini. Naanza kuwa na wasiwasi na hata hiyo form six yako, maana mtu na akili zake hawezi uliza swali kama hilo.
ReplyDeleteKasomee ubunge au uwaziri, na make sure with specialsation of Tanzania. Ukirude utakuwa tajiri kabisa maana utakula hii nchi, kama kutakuwa kumebaki kitu cha kula!!! Nakutakia kila la heri.
ReplyDeleteKasome Engineering au medicine uje usaidie nchi,wanasheria tunao wengi wa kutosha
ReplyDeleteNafikiri ni vizuri ukaenda kusomea INTERNATIONAL LAW. ni nzuri sana, coz itapanua upatikanaji wa ajira kwako. ukiwa na hiyo nahisi unaweza kufanya kazi sehemu yoyote ile duniani. Good luck!
ReplyDeletekajifunze namna ya kuishi Tanzania au kuendesha taxi ughaibuni au kufagia vyoo
ReplyDeleteNafikiri ni vizuri ukaenda lusome INTERNATIONAL LAW. coz itapanua upatikanaji wa ajira kwako baadaye, ukiwa na iyo nahc unaweza kupata/kufanya kazi sehemu yoyote ile duniani. Good luck!
ReplyDeleteMfadhili gani huyo yuko tayari kutoa hela yake bila kujua unaenda kusomea nini!? Angalia kama ni ufadhili wa kujuana through intrenet utapigwa changa la macho! Kama ni mzazi kwa nini asikupeleke nchi nyingine zaidi ya Italia!
ReplyDeleteKukushauri ni ngumu maana hatujui a-level umesomea nini! lakini pia wewe interest yako ni nini?
Wewe ulivyoomba sponsership hukujua unaenda kusomea nini?
ReplyDeleteKwa ushauri wangu ni bora ungesomea hapo hapo nyumbani bongo kuliko kukimbilia huku. Italy ni ubabaishaji mtupu na jamaa ni wasanii ile mbaya. Huku ni kiitaliano kila kona. Maprofesa hawajui kiingereza ni zero kabisa halafu jamaa ni wabaguzi sana wanaona hii ngozi nyeusi haijui kitu kwa hiyo hapo pia ni shughuli nyingine. Kwa hiyo ndugu kama uko serious unataka kusoma shule ya uhakika bora au usome hapo hapo bongo au upate shule nyingine Nothern Europe kuliko hapa Italy. Ni ushauri wangu tu maana na mimi niko huku joto ya jiwe naipata. Usifikiri nakukatisha tamaa ila nakupa hali halisi ili ufanye informed decision. Halafu kama una ndoto za kuja huku na kufanya hiyo usahau kabisa maana kazi hazipatikani kwa urahisi na kama zipo priority ni kwa weupe wenzao. Hii ni tofauti na Northern Europe ambapo kazi zipo nje nje. Kwa hiyo usishangae unakuja huku unasoma unamaliza unnarudi bila chochote mfukoni. Kila la heri.
ReplyDeleteConsult TCU you will get what you need and will give you a variety of choices for more help TCU offices are located near Rose Garden Mikocheni.
ReplyDeleteWewe Mtanzania vipi bwana..Weka unachofikiria kwenda kusoma halafu uliza kama kinashabihiana na ya kwetu....lakini umeficha..Kama unatutega vile?.Ni Kushabihiana au kutambulika na vyuo vikuu vyetu?Kila la kheri.
ReplyDeleteDavid V
Mdau usihangaike bureeee,
ReplyDeleteItalia ndio Makao Makuu ya Ukatoliki, pia kulingana na mabadiliko ya kimaisha Sekta tatu (3) hizi, yaani Michezo, Siasa na Dini ndio SACCOS za kisasa hivyo usipoteze muda kufikiri Engineering, Business,Management, Law na mengine, kwanza inaonyesha Udhamini huo umepewa na Kanisa sasa unataka kuwageuka mapema(Dunia imefilisika ni vigumu kwa zama hizi kupata Sponsor) kwa namna ulivyopata wewe hata aina ya Masomo usijue?.
Italia nenda kasomee DINI YA KIKRISTO ili UPIGE BAO!
Nenda ofisi za TCU kwamsaada zaidi, ndio pekee wanaoweza kukupa muongozo mzuri ahsante.
ReplyDeleteUngeuliza mapema ningekwambia kwamba fanya bachelor nyumbani halafu ndo uende kwa masters na PhD nje. Huwa si vizuri sana kuanzia bachelor nje ukaja kufanya master TZ utakuwa frustrated na system ya elimu ya juu ya Bongo. Pia hujasema ni masomo gani ulifanya A-level. Pengine ungesema baadhi ya kozi unazotaka ukiondoa hiyo sheria ili ushauriwe kirahisi.
ReplyDeleteSomea photo editing
ReplyDeleteNENDA TU KAKA KITAELEWEKA HUKO HUKO.
ReplyDeletesomea umafia. ukirudi ukachanganya na ufisadi degree ya pili utatisha mwanangu
ReplyDeletesoma engineering like electrical, n.k kwa experience yangu ukimaliza vizuri unaweza pata ajira popote i.e duniani
ReplyDeleteKasomee ukocha wa mpira wa miguu
ReplyDeleteacha ushamba wewe!! umepataje scholarship hata hujitambui!! ndio mambo ya kuletewa driving licence kama zawadi ya birthday.unatakiwa kujitambua unataka uwe nani ufanye nn ndo uamue usome nn. umemuabisha sana hata aliekupa scholarship
ReplyDeleteNdugu yangu sijui ni ipi nikupe kwanza pole au hongera. Hongera kwa kupata ufadhili wa kusoma nje ya nchi, pole kwa kuwa hadi umemaliza form six hujui ni aina gani ya kazi ungelipenda kufanya/kusomea. Nashangazwa kuwa kuna mtu au kampuni imeweza kukupa ufadhili bila ya hata kujua ni fani gani ya masomo unataka kuchukua, au wewe ni moja katika watoto wa vigogo?
ReplyDeleteSomea udaktari.
ReplyDeleteMambo vipi?
ReplyDeletemimi ningeweza kukushauri, kwanza kabla ya kukushauri naomba nikuulize ulisoma masomo gani A-level? na pia nisingekushauri ukasome sheria as ulivyosema sisi tuko tofauti sheria yetu na hao Italy.
Pia ningekushauri kama ulisoma hesabu fanya accounting, finance, management au economics
au computer science au IT.
kama ulisoma Arts A-level,
Kuna environment field, its a coming field now all over the world and its very good, geology pia its good.
Napia kama ulisoma science kafanye science na usome chemistry, physics etc.engineering we need this people in TZ a lot.
Good luck.
Good luck.
Kasomee fani unayoimudu, then think beyond the nation borders. Si lazima ufanye kazi Tanzania. Nenda ukajenge skills zitakazokuwezesha kucompete internationally. Think of East Africa Community and beyond that! Kama hapa Tz watasema haimatch and so & so...bac skills zako zikuwezeshe kefanya kazi zako Sudan, Uganda, Zambia n.k. Nakutakia masomo mema
ReplyDeletemtoa maoni wa kwanza , wewe kiboko, nakupa 5 bila kupigwa . Yaani huyu jamaa bogasi kichizi, sijui na huyo aliyemlipia nauli kwenda Italia, hiyo pesa bora angelikaa kwa macheni akanywa bia. yaani watu kama hawa na vicheti vyao ndo wanaoshika madaraka hapa bongo ,na kutuvurundia kila wizara wanakopelekwa, hata hayo mapishi !!!! mmmm!!! sidhani asije akaua watu huko Kebbys hotel. Mimi naona abaki tu bongo au akienda basi asirudi. Zebedayo mna Nasa.
ReplyDeleteHivi kweli mpaka sasa hivi huna muelekeo wa maisha tu? Yaani inamaanisha mpaka sasa hujui unataka nini hii ni aibu kubwa sana mpaka unaanza chuo huna muelekeo. Usisome unachoambiwa na jua wewe unataka nini. Sasa Kama ukipokea ushauri zaidi ya tano si ndio tutakuchanganya kabisa. Acha hizo wewe hata ukipewa uongozi wa taifa utalipeleka kijingajinga hivyohivyo
ReplyDeleteWatu wengine bwana mwenzenu kaomba mssada mnatukana..
ReplyDeleteTechnology ni sawa kote Duniani
IT, Computer, Engineering, Economics, Finance etc
Ningekushauri kama unapenda lugha usomee communication aidha international communications au international relations. Itakusaidia hata utakapo tafuta stashahada ya pili kupata mambo ya relations au hiyo hiyo communications au ukiona vyote haviko sawa malizia na HR (Human Resources).Angalia mbali utaweza jikuta unachukuliwa hata na UN ukimaliza masomo kama hayo,au hata mashirika makubwa au ya kimarekani au italia hasa kwamba utakuwa umesoma kwao...Mdau
ReplyDeleteDegree ya law ambayo inajulikana kama LLM ninadhani kua ni moja dunian kwa maana ukisoma sheria popote basi umesoma sheria kitu labda cha kuwa na wasiwasi ni lugha inayotumiwa ktk masomo. I think if language problem is solved you shoul be fin, giv it try. thanks
ReplyDeleteDunia imegawanyika kwa fani kulingana na Taifa husika,
ReplyDeleteMifano ya nchi chache ikiwemo Italia unazoweza pata taaluma ikakusaidia ukiwa hapa Tanzania ukirudi:
1.Italia:-
Somea kati ya fani hizi:
-Udobi (kufua na kupiga pasi)
-Ukinyozi
-Uhudumu wa Baa au Migahawa
-Uchomaji wa Pizza (aina ya Chapati)
-Unenguaji ktk Klabu za Srarehe za Usiku (Kazi ambayo hata Waziri Mkuu Mstaafu wa Italia Bilionea Silvio Berlusconi aliwahi kuifanya kabla ya kupata Fedha, Madaraka na Umaarufu, tena yeye alifanya ktk Meli za Kifahari za Watalii matajiri)
2.Ujerumani:-
Somea kati ya fani hizi:
-Ufinyanzi (Hii ukiwa hodari itakupelekea hadi kuwa mbunifu ktk Viwanda vikubwa vya Mitambo na Magari kama Mecredes Benz,Audi,Opel,BMW n.k
-Uchoraji na Sanaa
-Ufundi wa mashine ndogondogo na matengenezo (micro mechanics)
3.Uholanzi:-
Somea kati ya fani hizi:
-Ukulima wa mbogamboga na matunda
-Biashara ndogo ndogo (kama Magenge)
-Usindikaji wa vyakula
-Utayarishaji wa Maziwa ya ng'ombe na mazao yake, Siagi,Jibini n.k
Ila kwa baadhi ya taaluma hapo ktk nchi hizo (3) utaona kama ninakubeza isipokuwa hiyo ni kweli.
Kazi kwako !
Hiyo "scholarship" uliipataje au ndio undugu?
ReplyDeleteNenda kasomee theolojia inalipa, uje kugombea urais na wewe
Ahhh,
ReplyDeleteWewe nenda kalitumike Kanisa tu!
Angalieni huyu jamaa, unapewa Udhamini kwa Masomo ya Dini unataka kuchomoka usomee mambo ya Kimaslahi sio?
Kila kitu kinaonyesha ya kuwa hiyo Sponsorship ni ya Kanisa,(Kwa sasa ni nadra sana mtu ukapata Udhamini kwa Mazingira haya labda uwe GENIUS (mwenye akili za ziada),au BABA YAKO AWE NI TAJIRI PIA),,,MARA NYINGI UDHAMINI WA AINA HII UNALENGA WATU WA TAALUMA YA DINI SIO TAALUMA ZA KIMASLAHI,,,sasa wewe huku pembeni unawatoka Maaskofu na Mapadri unataka kuchagua Kozi ya Fedha!
Ohoooo acha hizo!
Mpendwa mchangiaji wa kwanza unadhani usingechangia kungeharibika neno? Siyo kwamba hawezi bali ninadhani anahitaji kupewa mwelekeo na ndo maana kaomba kusaidiwa kumamanua hili.
ReplyDeleteKama umeshapata udahiri, jaribu kutembelea website ya chuo husika uchagua degree programme uipendayo au uwezayo kuimudu vizuri zaidi.
Engineering
ReplyDeleteBiashara
Mimi naona ukisoma masomo ya sayansi au biashara yanakubalika kila mahali.
Ungetuambia umesoma "combination" gani tungekuwa katika nafasi nzuri ya kukushauri.Kama umesoma sayansi ni vizuri ukasoma course za engineering(zipo nyingi),Geomatics(surveying)au zinazohusiana na afya kama umefanya PCM,PGM,PCB au CBG kwa sbabu zote zipo world wide.Kama umesoma arts ni bora ukasoma mambo ya utawala au internatinal relations kwa sababu hizo huwa zinashabihiana nchi zote.Sheria utaingia chaka manake sidhani kama mitaala ya Italy inafanana na hapa kwetu
ReplyDeleteMdau,
ReplyDeleteUshauri wangu ni kama ifuatavyo: Shahada ya kwanza inahitaji uwe na background ya masomo fulani ili ufanye vyema. Kwa mfano, shahada ya kwanza ya Uhandisi(Engineering) inahitaji umesoma A-level(Physics, Chemistry na Maths) au shahada ya Social science pengine itahitaji umesomea history, lugha au geography ili uweze kufanya vyema. Kwahiyo ni muhimu ujue umesomea A-level kitu gani ndipo uendeleze hiyo field shahada ya kwanza ama sivyo masomo yatakuwa magumu kwako.
Pili, ni muhimu ujue job market ya Tanzania inahitaji zaidi taaluma gani kwa sasa? Je wahandisi, Quantity Surveyors, Architects au Marketers n.k ili ukimaliza upate kazi kwa wepesi.
Haya mawili ni muhimu kuzingatia.
Kwanza ningependa kufahamu mtu uyo kasomea masomo gani A-level.Kama ni Arts ni vyema akasomea mambo ya International Relatioship(IR).Nahisi ni course itakayomfaa.Na kama amesoma science,basi ni vyema akisoma mambo ya ICT,atakubalika
ReplyDeleteungesema umesomea mambo gani huko labda mtu angepata picha akushauri nini...specify hiyo degree ya nini unakaribia kuipata...
ReplyDeletekuhusu sheria sikushauri kila nchi wanamfumo wao kama mimi nasoma uingereza nafanya business ila kunakitengo cha law as subject nimesoma ambapo tunafuata sheria za uk , waweza fanya business, science na vinginevyo
ReplyDeleteHuu ni mfano halisi ya watanzania wengi. Jitu linafika hatua ya kusoma chuo halijajua linataka kufanya nini huku duniani. Badala yake litakurupuka na kitu halafu likiirudi linabaki misifa ya kusoma italy tu huku haliwezi fanya chochote. Watanzania bwanaa!!!!!!!!!
ReplyDeleteJim, hilo ni tatizo la mfumo wa nchi yetu. Na tunawaza kuajiriwa zaidi. Ndo maana watu wanakimbia taalama zao na kukimbilia kwenye siasa!
ReplyDeletekapige book kaka hao wasikuzingue.
ReplyDelete