Na Mary Ayo.
Shirika lisilo la kiserikali lijulikanalo kwa jina la Springs of
Hope –Tanzania lenye makao yake makuu Mjini hapa limefanikiwa kuelimisha jumla ya watu 120 waishio kwenye mazingira magumu ikiwa ni pamoja na kuwajengea uwezo jinsi ya kuweza kuanzisha miradi midogomidogo ili kujikwamua na hali ngumu ya kimaisha waliyo nayo.
Kutolewa kwa elimu hiyo kunafanyika katika maeneo mbalimbali ya mkoani hapa, huku wakilenga zaidi jamii iishiyo katika mazingira magumu kutokana na kuwa wengi wao wakishindwa kuwasomesha watoto wao kutokana na ugumu wa maisha walio nao hivyo kuwaozesha ili kupunguza
gharama .
Akizungumza na mtandao huu , Kiongozi wa vikundi hivyo kutoka shirika hilo ,Linus Hokororo alisema kuwa mbali na kutoa elimu hiyo wameweza kuwaelimisha kuunda vikundi vya watu 30 kwa lengo la kuweza kukopeshana mikopo midogomidogo pamoja na kuwawezesha wao kuunda
mfuko wa jamii utakaowawezesha wao binafsi kujitatulia changamoto mbalimbali za maisha , ikiwa ni pamoja na kuwasaidia wao kuanzisha
saccos yao wenyewe bila kusaidiwa na mtu yeyote.
Alisema kuwa, baada ya elimu hiyo tayari jumla ya vikundi vinne vyenye idadi ya watu 120 vimekwisha undwa huku wakiweza kuchangishana fedha na kuanzisha miradi midogomidogo pamoja na kuweza kujiwekea akiba yao
kwa ajili ya kuwasomesha watoto wao ambao wengi wao wamekuwa wakibakia majumbani tu kutokana na ukosefu wa ada.
‘Sisi tulifikia uamuzi wa kufanya hivi baada ya kuona kuwa, jamii nyingi zimekuwa zikipata magonjwa mbalimbali ikiwemo ukimwi kutokana na kuwepo kwa umaskini, hali inayowapelekea kuingia kwenye vishawishi
mbalimbali, hivyo kwa kufanya hivi elimu hii imewawezesha kuwatoa kwenye mazingira magumu na kuweza kujiinua kuichumi kwa ujumla.’alisema .
Aliongeza kuwa, katika kufanikisha shughuli zao wamekuwa wakiwezeshwa na wahisani mbalimbali ikiwa ni pamoja na East Africa Adventure Safari company ambao waliwapatia masaada wa kiasi cha USD 360 kwa ajili ya kutoa elimu hiyo kwa jamii itokayo kwenye mazingira magumu.
Aidha alisema kuwa , elimu hiyo imewafikia watu waishio mazingira magumu kutoka kata ya Bwawani, Oldonyosambu, Muriet , kata ya Suye , Tengeru, Kimandolu na Sanawari.
Hokororo alisema kuwa, watu hao wametokea halmashauri ya Arusha vijijini, halmashauri ya Meru na manispaa ya Arusha huku wakiendelea kuongeza maeneo zaidi kulingana na watakavyoendelea kufanya uchunguzi na kubaini maeneo yenye uhitaji huo.
Aliongeza kuwa, lengo hasa la kutoa elimu hiyo ni kuwawezesha watu watokao mazingira hatarishi kuweza kujikimu kimaisha na kuondokana na hali ngumu ya maisha wanayokabiliana nayo kwa kujiwezesha wao wenyewe
baada ya kupatiwa elimu hiyo.
Mbali na kutoa elimu hiyo kwa jamii hiyo pia wameweza kuokoa jumla ya watoto 50 watokao mazingira hatarishi ambao waliwahi kuachishwa shule kwa kutaka kuozeshwa na wazazi wao, huku wengine wakishindwa kuendelea
na masomo kutokana na hali ngumu ya maisha ikiwa ni pamoja na wengine kupata mimba za utotoni.
Aidha wanafunzi hao wamekuwa wakisomeshwa bure na shirika hilo kuanzia kidato cha kwanza hadi chuo kikuu lengo ikiwa ni kuhakikisha watoto hao wameweza kujitegemea na kuondokana na hali ngumu waliyokuwa nayo .
Ambapo wameweza kuwalipia fedha kiasi cha milioni 15 kwa ajili ya kuwasaidia watoto hao katika kuwalipia ada na mahitaji mbalimbali waliyonayo huku wengi wa watoto hao wakiendelea kuongezeka na kuhitaji misaada zaidi.
Pia wameweza kuwapeleka Nursery watoto waishio mazingira magumu kwa kuwajengea shule yao iitwayo Make a Different Foundation ambapo hadi sasa hivi ina jumla ya watoto 36 wanaosomeshwa na shirika hilo huku wakiwalipia kiasi cha milioni 6 kwa mwaka.
Aidha shirika hilo, baada ya kutoa mafunzo kwa jamii hiyo iishiyo mazingira magumu na kuweza kujitegemea baadaye ndio wanatoa msaada wa kuwaongezea mitaji ili biashara zao ziweze kukua zaidi.
Naye mwezeshaji wa mafunzo hayo , Aisha Hussein alisema kuwa, amekuwa akiifundisha jamii hiyo itokayo kwenye mazingira magumu kwa muda mrefu sana huku akikumbana na changamoto mbalimbali ikiwemo ya wengi wao kuendelea kuwa maskini kutokana na kuwa hawana uwezo kwa kukopa banku kwani riba ni kubwa sana.
Ambapo hali hiyo imechangia kwa kiasi kikubwa sana jamii nyingi kuendelea kubakia maskini kwani hawana uwezo huo lakini kupitia mafunzo hayo wengi wao wameweza kuondokana na hali ngumu ya maisha na
kuweza kuanzisha miradi yao midogomidogo kwa kukopeshana wao kwa wao.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...