Wadau kama ilivyokwishafahamika Madaktari Tanzania wapo mbioni KUGOMA. Takwimu zisizothibitishwa zinaonyesha watanzania (wagonjwa) zaidi ya 1,500 wanakufa mahospitalini nchi nzima kwa wiki na hii haihusishi ajali mbaya za mabarabarani zinazotokea. Wagonjwa 2,000+ ikiwa ajali zinahusishwa. Wadau, Idadi ya wananchi wanaokufa wakati madaktari wanapogoma inatisha.
 
Watanzania na madaktari !!!! HAKUNA UMUHIMU WA KUWA NA TAIFA IKIWA WANANCHI WAKE HAWATHAMINI  UHAI NA MAISHA  YAO.
 
MASWALI: Madaktari wanapogoma wanataka kupeleka ujumbe gani kwa watanzania wengi wanaowategemea
                   kuokoa maisha yao? Je wanataka watanzania wafe wakijiona? Kwa hakika madaktari wetu ni wataalamu wa kulaumiwa
                   lakini nani ni chanzo cha mtafaruku huu wote? Taasisi zinazoangalia posho za wataalamu hawa wapo wapi na
                   kwa nini wasijadili nao kulikoni hili?
 NYONGEZA: Watanzania thamani yetu ipo wapi kama hatuthamini hata uhai na maisha ya wenzetu wanaotuzunguuka?
 
Ushauri wangu kwa madaktari, wagonjwa hawana makosa nanyi, ikiwezekana mtoe matakwa yenu na wananchi watachanga kuwapa
posho au mishahara minono mnayotaka kuliko kuwaacha watanzania kufa wakijiona bila matumaini.
Tafadhali elekeza majibu yako sehemu ya maoni. Tuanzie hapo kupata ufumbuziwa kurekebisha mwelekeo wetu.
Katika Tanzania ya sasa blogs zinaweza kufahamisha, kuelimisha na kukosoa jamii zaidi kuliko radio na tvs.
 
Ni kweli kabisa; WAPIGANAPO MAFAHARI WAWILI ZIUMIAZO NI NYASI Mengine nakuachia wewe Ankal na wadau.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 23, 2012

    asante kwa hoja nzuri.nimesikiliza radio immani 104.4 FM ya mjini morogoro leo asubuhi (mimi niko zanz, kuna watu wametoa maoni yao mablimbali. wachache sana wameunga mkono mgomo huu kama sikosei ni watatu tu ndio waliounga mkono.lakn pia kuna watu wametoa maoni yao ambayo mimi binafsi nayakubali...sisi wananchi kwa hakika lazima na ni lazima watanzania wenzange tuanze utaratibu wa kuwawajibisha wote wanaoleta mzaha, vinginevyo tutalia sana mda si mrefu..njia ni rahisi tu, wananchi wagome waingie barabarani na mabango ya namna mbili
    1.kuwalaani,kuwaonya na kuwataka madaktari mara moja waache/wasitishe mchezo wao wa kugoma wakati wanajua kabisa madhara yake ni makubwa kuliko hicho wanachokililia serikalini.
    2.kuilaani, kuishutumu, kuilalamikia, kuishinikiza (weka neno lolote tu linalofaa kuonya) serikali kwa kuwa bingwa wa kukaidi na kupiga siasa sehemu zote ambazo hazihitaji siasa. (madaktari, waalimu, waislam, wanavyuo,wazee wa EAC,na wale wote ambao wameshapeleka malalamiko yao serikalini lakini kwa kiburi tu serikali inaamua kupuuza huku wabunge wakineemeka na kujilimbikizia wenyewe na posho za ajabu ajabu serikalini na wananchi wanajua kila kitu).ukiona moshi unatokea pahali kuelekea angani unatakiwa uwahi mara moja kuuthibiti na kuzima cheche inayosababisha huo moshi vinginevyo ukija kuwaka moto hapo kazi utakuwa nayo kubwa ya kuuzima..

    naomba niishie hapa maana yapo mengi ya kusema ila wtanzania wenzangu narudia tena tuano uwezo wa kufanya haya,tuache woga...tuwawajibishe wazembe wa kila namna.

    ahsnte ankal na mdau pia.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 23, 2012

    Mtoa mada, mimi sina nia ya kuchochea wananchi wawaadabishe ha wa madokta wetu lakini ikibidi wafanye hivyo. Madokta wanasababisha wananchi wawachukie bila sababu za msingi. Ujumbe kwa madokta wetu ni kwamba hatutajali mna bifu na serikali juu ya posho zenu, ila mkae mkijua kabla ya sisi kuangaika na kufa mahospitalini itabidi tuanze na ninyi ama kwa kuwawekea makalantini majumbani kwenu au namna nyingine yeyote itakayowafanya muonje joto walau linalokaribiana na wagonjwa watakaokufa ama kuteseka. Mgomo unakusaidia nini wewe dokta? Maana ya utaalamu wako upo wapi? Hata kama una damu baridi, kama Mtanzania utajivunia nini katika uzalendo wako kwa kuwaacha wananchi wenzako, ambao kwa namna moja ama nyingine wameshiriki kugharamia(Wamelipa kodi kusudi upate mkopo chuoni) kupata utaalamu ulionao. Ama kweli kuna kusoma, na kusoma kuelimika. Inasikitisha kuona wasomi wetu wana-act kama wahuni wa mitaani. Tafuteni njia mbadala ya kudai posho zenu njia hii mnayotumia siyo sahihi(wrong). Kwa mfano kama alivyosema mtoa mada, mnaweza kuwataharifu wananchi kuwa, serikali haijali kazi yenu kwani haikumbuki posho na mishahara yenu. Kwa hivyo kulikoni ninyi kugoma basi wananchi wawachangie chochote kitakachokukuongezeni maslahi yenu. Naamini mtafanya hivyo badala ya kugoma.

    Kwa upende mwingine wahusika wanaoshughulikia posho za wataalamu hawa tafadhali jaribuni kutatua tatizo hili, msiache wananchi kuteseka na wakafa mahospitalini safari hii tena kama safari zilizopita. Hakuna anayejua madhara ya kugoma wataalamu hawa ila ni mwenyezi Mungu peke yake.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 23, 2012

    Mdau wa kwanza una point kidooogo lakini muhimu. Ila kumbuka serikali ya Tz inatumia ubabe hasa kwa kuwatumia polisi. Uandamane bila kibali mwishowe uishie kupigwa risasi manake nini? Bora tu hao madaktari wagome. Mimi nawaunga mkono.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 23, 2012

    Watanzania hatuna uwezo wa kuwwajibisha viongozi wanao kosea kwanza ukisema watu watakuletea utamaduni kiongozi akisemwa umemkosea adabu ndiya maana hata mimi siwalaumu Madaktari kwanza katika nchi za kiafrica madaktari wetu ni first class kwa ubinadamu ukilinganisha na jins serikali inavyo wadhalilisha. Nchi nyingine ukiende hospitali hata uwe mahututi vipi watakuambia kwanza utoe pese ndio waanze kazi kama huna daktari anakuabia there is nothing I can do kabla hujalaumu jaribu kufikiria kama wewe ungkuwa daktari kwa situation hii ungefanyaje kufanya kazi katika mazingira maguma hakuna hata vitendea kazi

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 23, 2012

    Madaktari wagome tu. Serikali imezoea kupunja baadhi ya watu katika sekta zao huku wengine wanapewa mijipesa chungu mzima. Mfano watu wa TRA, BOT, wanasheria na wanasiasa wanalipwa fedha nyingi sana wakati hakuna kazi ya ziada wanayofanya ukilinganisha na watu wa sekta zingine. Jambo la msingi ni kujua kwamba uchumi wetu kama ulivyo (kama tujiite tumeendelea au hatujaendelea) unachangiwa na watu wa sekta nyingi wakiwemo madaktari. Kitendo cha kuwapa mishahara mikubwa baadhi huku wengine wanateseka ni makosa. Kwa hiyo unayepinga mgomo wa madaktari unepinga kwanza mishahara mikuba na posho kubwa za mawaziri na hao niliowataja.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...